TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
WANAFUNZI WASIO NA SIFA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU
Tume ya Vyuo Vikuu
Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa zoezi la uhakiki wa sifa za wanafunzi
wanaondelea na masomo kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kwa mwaka 2016/2017
limekamilika katika baadhi ya vyuo. Katika kutekeleza zoezi hilo Tume imebaini
kuwa kuna wanafunzi ambao wamedahiliwa katika programu ambazo hawana sifa.
Orodha ya wanafunzi
wasio na sifa imeshawasilishwa kwenye vyuo husika. Hivyo, wanafunzi wote
wanaondelea na masomo kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu nchini wanaweza kutazama
matokeo ya uhakiki wao kupitia kiunganisho (link) (Bonyeza Uhakiki wa Sifa za Udahili).
Tume inawaarifu
wanafunzi wote ambao majina yao yameorodheshwa wawasiliane na vyuo vyao ili
kuthibitisha sifa zao kabla ya tarehe 28 Februari 2017. Wanafunzi ambao
hawatafanya hivyo hawatatambuliwa na Tume na hivyo kukosa sifa za uanafunzi.
TCU inatoa rai kwa
wanafunzi wote kutembelea tovuti ya Tume (www.tcu.go.tz) mara kwa mara ili
kupata taarifa mpya kuhusu uhakiki wa sifa za wanafunzi.
Imetolewa na
Katibu
Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
20/02/2017
0 comments:
Post a Comment