Wednesday, 22 February 2017

WANAOSOMA CHINA KUISOMA NAMBA,SERIKALI YASISITIZA KUSITISHA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAFUNZI WANAOSOMA NCHINI CHINA

...
Serikali kupitia wizara ya elimu,sayansi na teknolojia imesisitiza kusitisha pesa za mikopo ya nauli za kwenda masomoni na malipo mengine yote yaliyokuwa yanatolewa kwa wanafunzi wanapata ufadhili wa masomo kutoka kwa nchi rafiki ikiwemo nchi ya China.
Kauli hiyo imetolewa kupitia barua(ya tarehe 7,February,2017) iliyoandikwa na wizara ya elimu ,sayansi na teknolojia kwenda ubalozi wa Tanzania chini China wakati wakijibu barua iliyoandikwa na wanafunzi wanaosoma nchini china kuomba serikali kuangalia vizuri maamuzi hayo.
Takribani miezi miwili iliyopita,Bodi ya mikopo (HESLB) iliauandikia barua ubalozi wa Tanzania nchini china kuueleza maamuzi ya serikali kusitisha utoaji wa fedha za nauli kwa wanafunzi hao.Lakini wanafunzi hao hawakuridhika na maamuzi hayo hivo kuamua kuiandikia barua wizara ya elimu kuangalia vizuri maamuzi hayo.
 
Kwa mujibu wa barua hii ,wanafunzi watatakiwa kujigharamia wenyewe gharama za kwenda na kurudi masomoni kitu ambapo awali walikuwa wanapatiwa na serikali ya Tanzania.
Hii hapa barua mpya uliyosisitiza kutotoa pesa hizo na nauli kwa wanafuni hao
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger