Sakata la dawa za kulevya katika jiji la dsm limeendelea kutikisa watu
maarufu,wakiwemo wafanyabiashara na wanasiasa Pamoja na Kiongozi maarufu
wa dini ambao wametakiwa kwenda kituo cha polisi cha kati siku ya
ijumaa kwa ajili ya mahojiano.
Mkuu wa Mkoa wa dsm Paul Makonda akizungumza na vyombo vya habari
ametangaza Orodha mpya ya watu 65 ambao wanadaiwa kujihusisha kwa namna
moja au nyingine katika kuuza au kusaidia kuingiza dawa za kulevya hapa
nchini au nje ya nchi.
Baadhi ya watu maarufu wanaotakiwa kuripoti kituo cha polisi cha kati
Siku ya Ijumaa ni pamoja na Mbunge mstaafu wa kinondoni Iddi
Azzan,Mfanyabiashara Yusuph manji,Mbunge wa hai Freeman Mbowe,mchungaji
Josephat Gwajima,huku wafanyabiashara maarufu akiwemo Hussein pamba kali
,mwinyi machapta pamoja na boss Chizenga wakazi wa kinondoni.
Aidha makonda amewataka wamiliki wa hotel wakiwemo Cassino sea
cliff,Parm beach casino,Sleep way ,Yatch Club pamoja na Viongozi wa
makampuni ya mafuta yakiwemo GBP,Tanga Petrolium,na Nas Hauleg nao
kujisalimisha Polisi siku ya ijumaa.
0 comments:
Post a Comment