Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ametangaza kushusha kodi ya mapato ya Mshahara ( Pay as you Earn -PAYE ) kutoka asilimia 11 iliyopo sasa hadi asilimia 9.
Rais
amesema ameamua kuchukua umamuzi huo ili kutimiza ahadi yake aliyoitoa
wakati wa kampeni ya kuwapunguzia mizigo wafanyakazi kwa kuwaongezea
mishahara na kuwapunguzia kodi ya mapato ya mishahara.
Kuhusu kuwaongezea mishahara, Rais Magufuli ameomba wafanyakazi wamvumilie kwa kuwa hivi sasa yuko kuimarisha uchumi wa nchi kwa kuziba mianya yote ya Rushwa.
Kuhusu kuwaongezea mishahara, Rais Magufuli ameomba wafanyakazi wamvumilie kwa kuwa hivi sasa yuko kuimarisha uchumi wa nchi kwa kuziba mianya yote ya Rushwa.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amewataka waajiri wote nchini kuwapa wafanyakazi wao mikataba ya ajira na kupeleka makato yao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii bila kukosa
0 comments:
Post a Comment