TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU TOZO KWENYE SEKTA YA TEHAMA
Katika wiki ya pili ya Februari 2015,
baadhi ya watoa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi walianzisha
vifurushi vya mawasiliano na bei na kusabababisha malalamiko kutoka kwa
watumiaji na umma kwa ujumla. TCRA, kwa kuzingatia upeo wa shughuli
zake, imechambua hali hiyo na inapenda kutoa maelezo na maagizo ambayo
yatawezesha kuondoa sintofahamu iliyopo na kujenga mustakabali kwa siku
zijazo.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003, miongoni mwa kazi za TCRA ni
kufuatilia utoaji wa huduma katika sekta inazozisimamia kwa kuzingatia
kiwango cha upatikanaji wa huduma hizo, ubora na viwango vya huduma, bei
ya huduma na kuhimiza ushindani na ufanisi wa kiuchumi. Katika
kutelekeza majukumu yake, TCRA inawajibika kupitia na kuchambua, mara
kwa mara, utoaji wa huduma katika sekta na kuchukua hatua dhidi ya
chochote kinachotokea kwenye soko, kiwe chanya au hasi.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
inaongozwa na Sera za Kisekta, Sheria ya Mamlaka ya Mawasilioano
Tanzania ya 2003, Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA)
ya 2010, na Kanuni zake za mwaka 2011 zilizotungwa kwa kuzingatia
matakwa ya EPOCA. Kifungu 6(1) cha Sheria ya TCRA kinaitaka Mamlala
kufuatilia utoaji wa huduma unaofanywa na sekta inazozisimamia ikiwa ni
pamoja na upatikanaji, ubora na viwango vya huduma, gharama za huduma
hizo na kufanikisha ufumbuzi na utatuaji wa malalamiko na migogoro. Hivi
karibuni kumekuwa na malalamiko kuhusu tozo mpya zilizotangazwa na
makampuni ya simu za mkononi. Endelea kusoma taarifa yote hapa
0 comments:
Post a Comment