Thursday 2 December 2021

BARRICK NORTH MARA YAWEZESHA MRADI WA AFYA KWA WANANCHI TARIME…WANAKIJIJI WAJITOKEZA


Wananchi wakipata huduma ya kupima afya zao wakati wa mradi wa afya kwa jamii uliofadhiliwa na Barrick North Mara

*****
Kampuni ya Madini Barrick kupitia mgodi wake wa North Mara, imefadhili mradi wa kuelimisha wananchi masuala ya afya na kupima magonjwa mbalimbali, kupata chanjo dhidi ya UVIKO-19 pia kujitolea kutoa damu, katika vijiji 11 vinavyozunguka mgodi huo uliopo wilayani Tarime mkoani Mara.

Mradi huo wa wiki 2 ulioanza Septemba 11 na kuhitimishwa Desemba 1,umetekelezwa kupitia Wizara ya Afya chini ya Mganga Mkuu wa wilaya ya Tarime,umewafikia wananchi zaidi ya 3,000 ambao wamejitokeza kupima magonjwa ya UKIMWI, Kifua kikuu, kupata chanjo ya UVIKO-19, na baadhi yao kujitolea kutoa damu kwa ajili ya Benki ya Damu pia wananchi walipata ushauri wa kiafya kuhusiana magonjwa mbalimbali kutoka kwa madaktari waliokuwa wanatekeleza mradi.

Akiongea kwa niaba ya wanakijiji wenzake kuhusiana na mradi huu, Nyamwiga Warioba, mkazi wa kijiji cha Nyamongo,alisema kuwa kupitia mradi huu wananchi wengi wengi wamepata fursa ya kupima afya zao na kupata elimu ya afya kuhusiana na maradhi mbalimbali,ameishukuru Barrick North mara kwa kufanya uwezeshaji unaolenga kuboresha afya za wananchi sambamba na kudhamini maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.

Kwa upande wake,mkazi wa kijiji cha Matongo,Maria Samweli,amesema yeye pamoja na wanawake wezake wamepata fursa ya kupima magonjwa mbalimbali na kupata ushauri kuhusiana na jinsi ya kukabiliana na magonjwa sugu yanayowasumbua Wanawake wengi na watoto ambapo pia baadhi yao wamepatiwa chanjo ya UVIKO 19.

Naye Julius Sospeter, mkazi wa kijiji cha Nyangoto amesema yeye na wanakijiji wenzake wamehamasika kujitolea kutoa damu kutokana na kupata taarifa kuwa wapo wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu. Aliomba wadau waliofanikisha zoezi hili kuhakikisha linakuwa endelevu na kufanyika mara kwa mara.

Pia aliipongeza Kampuni ya Barrick North Mara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuwasogezea wananchi vijijini huduma za afya kwa karibu.

Mganga Mkuu wa Barrick North Mara ,Dk.Nicholas Mboya, aliwashukuru wananchi kwa kuwa na mwamko mkubwa kushiriki zoezi hili la kupimwa afya zao na kupata ushauri wa afya kutoka kwa wataalamu ambalo limepata mafanikio makubwa.Aliishukuru Serikali na taasisi mbalimbali waliszoshirikiana nazo kufanikisha mradi huu ambao umewanufaisha wananchi wengi.
Wananchi wakipata huduma ya kupima afya zao wakati wa mradi wa afya kwa jamii uliofadhiliwa na Barrick North Mara
Zoezi la utoaji huduma ya kupima afya likiendelea
Wananchi wakisubiri kupata huduma ya kupima afya zao wakati wa mradi wa afya kwa jamii uliofadhiliwa na Barrick North Mara
Wananchi wakisubiri kupata huduma ya kupima afya zao wakati wa mradi wa afya kwa jamii uliofadhiliwa na Barrick North Mara
Wananchi wakipata huduma ya kupima afya zao wakati wa mradi wa afya kwa jamii uliofadhiliwa na Barrick North Mara
Share:

MSANII MUSOMA AACHIA WIMBO MPYA 'MALALAMIKO'... TAZAMA HAPA


Msanii Musoma

Na Dotto Kwilasa-Malunde 1 blog, Dodoma

MSANII wa Muziki wa Kizazi kipya Giraruma Yusuphu Kisheri maarufu kwa jina la Musoma ameachia wimbo uitwao Malalamiko ambao amemshirikisha Msanii mwenzake Coclyn huku akihidi kuendelea kutoa nyimbo zenye ujumbe na zinazowakonga watanzania.


Musoma ambaye anatamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo Umenichota aliomshikirisha Staa wa Bongo Star Search,Mesha Mazing,Miss Dom aliomshirikisha One Six na Njoo njoo na Zamu yetu.

Akizungumza na Malunde blog Desemba 1,2021,Msanii huyo ambaye ni mwalimu wa shule ya Msingi Amani ya Jijini Dodoma amesema wimbo wa Malalamiko umekuja kueleza kwa kina kuhusu usaliti ambao umekuwa ukitokea katika jamii.

Musoma amesema matarajio yake ni kuendelea kutoa nyimbo zenye kuelimisha,kuburudisha na kuonya jamii juu ya mambo mbalimbali huku akisisitiza watanzania wazidi kumuunga mkono.

Katika hatua nyingine, Msanii huyo amesema anatarajia hivi katibuni kutoa wimbo uitwao Yatima ambapo amedai atamshirikisha Msanii mwenye jina kubwa hapa nchini Linex.

Tazama Hapa Video : MUSOMA FEAT.COCLYN - MALALAMIKO
Share:

Project Management Officer at CVPeople Tanzania

Project Management Officer CVPeople Tanzania | Full time Dar Es Salaam , Tanzania Job Description MAIN PURPOSE OF THE JOB- (JOB SUMMARY)   The PMO Officer shall be responsible for the maintenance of defined project management framework to ensure the successful delivery of projects undertaken by Insurance Company of Tanzania Ltd – Medical through effective […]

This post Project Management Officer at CVPeople Tanzania has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

USHINDI WA BIKO WATUA KWA HASHIMU WA LUGOBA


Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akifurahia jambo na Hashimu Shabani wa Lugoba mkoani Pwani aliyeshinda fedha za bahati nasibu ya Biko sh milioni 10. Makabidhiano hayo yamefanyika Kibaha, mkoani Pwani. Picha na Mpiga picha wetu.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akifurahia jambo na Hashimu Shabani wa Lugoba mkoani Pwani aliyeshinda fedha za bahati nasibu ya Biko sh milioni 10. Makabidhiano hayo yamefanyika Kibaha, mkoani Pwani.
Balozi wa Biko Kajala Masanja akiwa na mshindi wa sh milioni 10 Hashimu Shabani wa Lugoba mkoani Pwani kushoto kwake. Wengine ni marafiki wa Hashimu waliokuwa wanampongeza kwa ushindi wake. 

***
Mwandishi Wetu, Chalinze

Mkazi wa Lugoba, wilayani Chalinze mkoani Pwani, Hashimu Shabani, amekabidhiwa fedha zake sh milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye droo kubwa ya bahati nasibu ya Biko inayoongoza kutoa washindi wengi sehemu mbalimbali za Tanzania wanaocheza kwa kuanzia sh 1000 na kuendelea.


Makabidhiano hayo yamefanyika mkoani Pwani na kuongozwa na balozi wa Biko Kajala Masanja na kusema biko ni mchezo unaosambaza mamilioni ya fedha kwa Watanzania wanaocheza live kwa njia ya mtandao www.biko.co.tz pamoja na wanaotumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu 2456 au neno biko.


Akizungumza katika makabidhiano hayo, Shabani alisema kuwa fedha zake hizo ataziingiza kwenye mradi wake wa kumiliki bodaboda ili ziweze kumsaidia katika maisha yake, akiamini kuwa bahati kama hiyo inaweza isijirudie tena.


“Namshukuru Mungu kwa kunipatia fursa hii ya kushinda zawadi nono ya Sh Milioni 10 kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko, hivyo wakati huu ambao maisha ni magumu mtaani, nimeamua kununua bodaboda nikiamini zinaweza kuniokoa.


“Siwezi kufanya makossa, maana Mungu mwenyewe ndiye anayejua kwanini ameamua kunipa ushindi wa Biko, ingawa nilicheza nikiwa na Imani kubwa kama kuna siku ningeweza kuibuka mshindi kama wanavyoshinda wengine,” Alisema.


Naye Balozi wa Biko, Kajala Masanja amesema kuwa wakati huu wa kuelekea kufunga mwaka 2011, Watanzania wote wanaocheza biko wana nafasii kubwa ya kushinda zawadi za papo kwa hapo pamoja na ofa kibao zikiwamo za mamilioni kila Jumapili.


Biko ni mchezo wa kubahatisha unaoongoza kutoa fedha nyingi kwa Watanzania, ambapo zwadi za papo kwa hapo zinatoka kila sekunde moja kuanzia sh 2500 hadi milioni 5 papo hapo bila kusahau kutoa zawadi ya hadi sh milioni 40 kila Jumapili ambapo mbali na kucheza kwa namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu 2456, pia watu wanaweza kucheza live kwa kuingia www.biko.co.tz.
Share:

WORLD GOLD COUNCIL REPORT UNDERSCORES BARRICK’S LEADING ROLE IN SHARING THE BENEFITS OF MINING


Barrick Gold Corporation (NYSE:GOLD) (TSX: ABX) welcomed the release of the World Gold Council’s report highlighting the role of its members in contributing to socio-economic development in the countries and communities in which they operate. According to the report, available at www.gold.org, this contribution amounted to almost $38 billion in 38 countries last year, in the form of payments to governments, employees and suppliers.

Barrick’s status as an industry leader in socio-economic development was underscored by the comparison between its performance and the industry wide figures reported by the World Gold Council:

97% of Barrick’s employees and contractors were host country nationals, compared to 95% reported cumulatively by the World Gold Council member companies;

Barrick paid $1.8 billion out of the total $7.6 billion reported in taxes, royalties and dividends to host governments;

$4.5 billion of the total $26 billion spent on goods and services was spent with local and national suppliers; and

Barrick’s total economic contributions amounted to $12.1 billion out of the total $37.9 billion contribution reported for the 2020 year.

Barrick president and chief executive Mark Bristow said that the company’s ability to share the benefits of mining was one of the key ways it measured its success. “We partner with our host communities and countries to transform their natural resources into tangible benefits and mutual prosperity. Additionally, we hire talented individuals from the communities closest to our mines and train them to world-class standards; we leverage our supply chain to facilitate the growth of thriving and self-sustaining businesses; and our taxes further contribute to the economic development of the countries and communities in which we operate,” he said.

“This all happened against the backdrop of the Covid-19 pandemic when our prompt and effective responses protected our businesses from the worst of the virus and provided a further opportunity for us to demonstrate our commitment to partnerships,” Bristow said.

Barrick spent more than $30 million on Covid-related community support measures in 2020 and prepaid more than $300 million in taxes and royalties. It also supported communities through a number of initiatives ranging from medical supply donations to local hospitals, loans to small businesses, setting up food banks and delivering food packages.
Share:

CAMFED YAUNGA MKONO SERIKALI KUWAREJESHA WANAFUNZI SHULENI


Mkurugenzi wa CAMFED Tanzania, Bi. Lydia Wilbard akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa mwisho wa mwaka wa watoto wasichana waliosomeshwa kwa msaada na Shirika la CAMFED, ambapo mkutano huo umeipongeza Serikali kwa kitendo cha kuwarejesha shuleni wanafunzi wote waliokatiza masomo kutokana na sababu mbalimbali wakiwemo wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shuleni.
Mkurugenzi wa CAMFED Tanzania, Bi. Lydia Wilbard akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa mwisho wa mwaka wa watoto wasichana waliosomeshwa kwa msaada na Shirika la CAMFED, ambapo mkutano huo umeipongeza Serikali kwa kitendo cha kuwarejesha shuleni wanafunzi wote waliokatiza masomo kutokana na sababu mbalimbali wakiwemo wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shuleni.
Sehemu ya washiriki Mkutano Mkuu wa mwisho wa mwaka wa watoto wasichana waliosomeshwa kwa msaada na Shirika la CAMFED, ambapo umeipongeza Serikali kwa kitendo cha kuwarejesha shuleni wanafunzi wote waliokatiza masomo kutokana na sababu mbalimbali wakiwemo wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shuleni.
Sehemu ya washiriki Mkutano Mkuu wa mwisho wa mwaka wa watoto wasichana waliosomeshwa kwa msaada na Shirika la CAMFED, ambapo umeipongeza Serikali kwa kitendo cha kuwarejesha shuleni wanafunzi wote waliokatiza masomo kutokana na sababu mbalimbali wakiwemo wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shuleni.
Sehemu ya washiriki Mkutano Mkuu wa mwisho wa mwaka wa watoto wasichana waliosomeshwa kwa msaada na Shirika la CAMFED, wakiwa katika majadiliano kuangalia kusaidia utekelezaji wa waraka no mbili wa Serikali.
Programu Meneja wa Shirika la CAMFED Tanzania, Anna Sawaki (kulia) akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Ukumbi wa Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.
Mwalimu Mshauri wa Wanafunzi Shule ya Sekondari Viwege Ilala, Bi. Ruth Saibull akizungumza na wanahabari mara baada ya mkutano huo kuchangia maoni yake kufuatia uamuzi wa Serikali.
Learnerguide wa CAMA, Bi. Mzizi Rashidi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano huo kuelezea namna watakavyoshiriki kusaidia utekelezaji wa agizo la Serikali.
Mkurugenzi wa CAMFED Tanzania, Bi. Lydia Wilbard (wa pili kulia) akifurahi pamoja na wasichana waliosomeshwa kwa msaada na Shirika la CAMFED, ambao kwa sasa wamepata shahada mbalimbali.
Mkurugenzi wa CAMFED Tanzania, Bi. Lydia Wilbard akizungumza nawanahabari mara baada ya Mkutano Mkuu wa mwisho wa mwaka wa watoto wasichana waliosomeshwa kwa msaada na Shirika la CAMFED, kuelezea namna watakavyoshiriki kusaidia utekelezaji wa Waraka No. 2 wa Serikali wa kuwarejesha shuleni wanafunzi wote waliokatiza masomo kutokana na sababu mbalimbali wakiwemo wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shuleni.

Na Joachim Mushi, Dar es salaam

SHIRIKA lisilo la kiserikali la CAMFED Tanzania limeipongeza Serikali na kuunga mkono uamuzi wa kuwarejesha shuleni wanafunzi wote waliokatiza masomo kutokana na sababu mbalimbali wakiwemo wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shuleni.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa CAMFED Tanzania, Bi. Lydia Wilbard kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa watoto wasichana waliosomeshwa na Shirika la CAMFED, alisema uamuzi wa Serikali ni mafanikio makubwa katika sekta ya elimu kwani umefungua fursa kwa kundi hilo la jamii kurejea shuleni na kupambania ndoto zao.

Alisema CAMFED inaamini kurejeshwa kwa wanafunzi hao shuleni kwenye mfumo rasmi ni mafanikio makubwa, kwani ni jambo ambalo lilikuwa kikwazo kikubwa hasa kwa wanafunzi wa kike ambao ndio waliokuwa waathiriwa wakubwa kwa sababuza kupata ujauzito.

"Sisi kwetu ni kitu kikubwa sana, unajua tumefanya michakato mingi, tumeshiriki katika mijadala mbalimbali kupambania hii fursa kupitia kwenye mtandao wetu wa elimu TEN/MET na pia kama CAMFED kwa kushirikiana na jamii tumejaribu kuonesha ni lini mtoto anapopata ujauzito na kuacha masomo jamii itaamini ni sababu za kutowajibika vema kwa jamii husika (watu wazima)," alieleza Bi. Lydia Wilbard katika mkutano huo.

Alisema CAMFED inaamini hatua ya Serikali inaonesha wazi kuwa changamoto zilizokatisha masomo ya wanafunzi hao zimechangiwa na jamii inayowazunguka kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo.

Aidha aliongeza kuwa uamuzi huo wa Serikali kurejesha kundi hilo la wanafunzi kwenye mfumo rasmi kumeongeza wigo kwa wanafunzi waliokubwa na vikwazo kwenye masomo kabla ya kukatizwa masomo hivyo wanapata fursa ya kuamua wenyewe kulingana na mazingira na pia ndoto zake kwamba arejee katika mfumo upi kati ya rasmi na usio rasmi kumalizia masomo yao.

Hata hivyo, amebainisha kuwa suala la Serikali kutoa tamko hilo ni moja, lakini utekelezaji wake ni eneo lingine ambapo wao kama wadau wanashiriki kuangalia ni nini cha kufanya ili kuhakikisha utekelezaji unafanikiwa na hatimaye wanafunzi hao wanarejea masomoni na kukamilisha ndoto zao kielimu.

"Mimi nafikiri sasa tujikite kwenye utekelezaji...Serikali, wanajamii, sisi wakereketwa wa elimu, wasichana wenyewe, vijana tuanze kujipanga ni namna gani tunatekeleza suala hili na lifanikiwe, tusikae madarasani kusubiri wanafunzi hao warejee wenyewe kwani hawata kuja," alisema Bi. Wilbard.

Wito wetu kama CAMFED kila mmoja wetu alichukulie suala hili kwa mtazamo chanya na kisha kushiriki katika utekelezaji wake, kila mmoja wetu afanye ni jukumu lake hivyo kuchukua hatua sehemu alipo.

"Mfano viongozi wa dini wapaze sauti kwenye nyumba za ibada kushawishi jamii kuunga mkono suala hilo kwa vitendo, wanasiasa nao walisemee suala hili kupitia majukwaa yao, viongozi wa shule nao walitangaze vizuri suala hili na pia kuangalia namna nzuri ya kudhibiti vitendo vya unyanyapaa kwa wanafunzi watakao rejea shuleni." Alisisitiza Mkurugenzi huyo wa CAMFED Tanzania.

Kwa mujibu wa tamko la Waraka namba 2 wa Mwaka 2021 Serikali hivi karibuni ililiridhia kuwarejesha shuleni wanafunzi wote waliokatiza masomo kutokana na sababu mbalimbali kama vile utoro, utovu wa nidhamu na kupata ujauzito.
Share:

KENANI KIHONGOSI AENDELEA KUWASHA MOTO JIMBO LA NGORONGORO


Na Imma Msumba Loliondo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi Uvccm Kennani Kihongosi ameendelea na kampeni za kumtafutia kura mgombea ubunge katika Jimbo la Ngorongoro Mkoani Arusha ambapo hii leo amefanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Kijiji cha Alailelai. katika Kata ya Alailelai Tarafa ya Ngorongoro.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Alailelai amewataka wananchi wa kata hiyo yenye vijiji vitatu kwenda kumchagua kwa kura nyingi kijana wao Emmanuel Ole Shangai ili aweze kuendelea kuchapa kazi na kwa kukamilisha miradi mbalimbali iliyoanzishwa na mtangulizi wake.

"Shangai ana uwezo na uweledi mkubwa katika kuwatumikia wananchi kama alivyokuwa olenasha,Rais samia ameona shangai anatosha kuleta maendeleo hapa ngorongoro na ndio maana amewaletea huyu nendeni mkampe kura zote za ndio ifikapo disemba 11", alisema Kihongosi

"Pia nafahamu hapa kwenye hii kata kuna changamoto mbalimbali ikiwemo za afya,barabara,maji na barabara na mnahitaji fedha za ukwamilishaji wa mabweni mawili katika shule ya msingi kwa sababu watoto wenu huwa wanaliwa na simba wanapoenda shule Rais Samia ameshatoa milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili ya shule hii lakini pia ameleta milioni 154 kwa ajili ya usambazaji wa maji katika kijiji cha Sendeu",alisema

Kwa upande wake mgombea Ubunge Emmanuel Shangai amesema kuwa, kama atapata ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo, atahakikisha kero zinazowakabili wananchi, zinapatiwa ufumbuzi wa haraka ili waendelea na shughuli za kila siku pasipo vikwazo ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Afya Kata,ukamilishwaji wa mabweni ya wananfunzi 88 ambayo yote ni viporo yatayogharimu milioni 80 katika shule ya msingi.

“Bado jimbo letu lina changamoto nyingi ambazo zinahitaji kutatuliwa, naombeni kura zenu ili niweze kuwatumikia, nawaahidi katika uongozi wangu, hakuna mwananchi wala mtumishi atakayenyanyaswa na mtu mwingine, nitawatumikia kwa weledi na uaminifu mkubwa" ,Ole Shangai
Share:

BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPENI YA “TISHA NA TEMBOCARD VISA,” WATEJA 4 KUPELEKWA KUSHUHUDIA AFCON 2022 NCHINI CAMEROON


Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (katikati) akionyesha aina mpya ya kadi za ‘TemboCard’ wakati wa hafla ya uzindunzi wa kampeni ya Tisha na TemboCardVisa ulioenda sambamba na uzinduzi wa kadi hizo uliofanyika leo katika Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Mkuu wa Idara wa Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda (Kulia) na Kaimu Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi wa Benki hiyo, Erica Mwaipopo.

===== ====== =====
Benki ya CRDB kwa kushirikiana na kampuni ya Visa international leo imezindua kampeni ya “Tisha na TemboCard Visa” inayolenga kuhamasisha wateja kujenga utamaduni wa kutumia kadi zao za TemboCardVisa huku wakijiwekea nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwamo kushuhudia kombe la mataifa ya afrika AFCON litakalofanyika nchini Cameroon mwakani 2022.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Wateja wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Rabala alisema zawadi zitatolewa kwa wateja ambao watafanya miamala mingi zaidi kupitia TemboCardVisa zao katika kipindi chote cha kampeni ambayo inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Machi 2022.
“Lengo letu ni kuona wateja na Watanzania wanajenga utamaduni wa kutumia kadi zao kufanya malipo ya manunuzi na kuachana na utaratibu wa kutumia pesa taslimu ambazo sio salama. Katika kipindi hiki cha kampeni tutatoa zawadi kwa washindi zaidi ya 80 ambapo kila mwezi tutao zawadi kwa washindi 20,” alisema Raballa.

Akielezea kuhusu zawadi zitakazotolewa katika kampeni hiyo, Raballa alisema wateja watapata zawadi mbalimbali ikiwamo kurudishiwa asilimia 5 ya kiasi walichotumia, kulipiwa bili ya malipo ya manunuzi, simu janja, tablet, televisheni, sofa set, home theatre, pamoja na safari ya kitalii kwenda Zanzibar au Serengeti. “Kubwa zaidi ni zawadi ya safari ya kwenda Cameroon kushuhudia michuano ya AFCON kwa wateja 4 ambao watakuwa na miamala mingi zaidi katika kipindi cha Desemba na Januari. Washindi wataruhusiswa kwenda na wenza au rafiki zao” alisema Rabala.

Raballa alitoa rai kwa wateja wa Benki hiyo na Watanzania kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika kampeni hiyo kwa kutumia kadi zao za TemboCardVisa kufanya malipo huku akiwasihi kuendelea na utamaduni huo hata baada ya kampeni kwani lengo ni kufanya matumizi ya kadi kuwa sehemu ya kawaida ya miamala ya malipo ikiwa ni mkakati wa kujenga jamii yenye matumizi machache ya pesa taslimu “cashless society”.

“Kwa wale ambao hawana akaunti niwashauri wafungue akaunti ili waweze kuunganishwa na TemboCardVisa na kuanza kufurahia huduma huku wakijiwekea nafasi ya kujishindia zawadi kemkem. Kama mnavyojua sasa hivi zoezi la kufungua akaunti tumelirahisisha sana…”

“…kama una simu janja unachotakiwa kufanya ni kupakua SimBanking App na kufuata hatua za kufungua akaunti kwa kutumia namba ya NIDA na kisha utaomba kupata TemboCard yako, kwa wale wa sio na simu janja wanaweza kutembelea kwa CRDB Wakala wakiwa na kitambulisho cha NIDA kufunguliwa akaunti na kupata TemboCardVisa kwa urahisi. Tunatamani kuona watu wengi zaidi wakishiriki ili kwa pamoja tuweze kufikia lengo,” aliongezea.

Awali akielezea namna ya kushiriki katika kampeni hiyo na kuibuka mshindi, Kaimu Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi Benki ya CRDB, Erica Mwaipopo alisema wateja wanatakiwa kutumia kadi zao za TemboCardVisa kulipia manunuzi na huduma katika maduka, supermarkets, migahawa, hoteli na vituo vya mafuta kupitia vifaa vya manunuzi (POS), pamoja na malipo ya mitandaoni ikiwamo kulipia tiketi za ndege au malipo ya kuagiza bidhaa nje ya nchi.

Uzinduzi huo wa kampeni hiyo ya “Tisha na TemboCardVisa” ulienda sambamba na uzinduzi na muonekano mpya wa kadi za Benki ya CRDB ‘TemboCard’ ambazo zimeboreshwa zaidi ili kuwapa wateja uzoefu bora zaidi pindi watumiapo kadi zao. Akielezea kuhusu ujio wa kadi hizo mpya za TemboCardVisa, Mkuu wa kitengo cha Masoko, Joseline Kamuhanda alisema kadi hizo zimetengenzwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa itakayowawezesha wateja kutumia kadi zao kwa urahisi kufanya malipo popote pale.

Benki ya CRDB ilikuwa benki ya kwanza kuanzisha huduma za kadi ‘TemboCard’ nchini mwaka 2002, ikilenga kuwapa wateja wake urahisi na unafuu wa upatikanaji wa huduma popote walipo. Mpaka sasa Benki ya CRDB imefanikiwa kutoa zaidi ya TemboCard milioni 3 ikiungana na mifumo ya malipo ya kimataifa ya Visa, MasterCard na Union Pay. Huduma za Tembocard zimechangia kwa kiasi kikubwa kusaidia jitihada za serikali katika kuimarisha mfumo wa malipo nchini na kuongeza ujumuishi wa kifedha “Financial Inclusion”.

--
Share:

Marketing Coordinator at CVPeople Tanzania

Marketing Coordinator   CVPeople Tanzania | Full time Job Description Main Purpose of the Job- (Job Summary) Brand officer oversee a wide array of business functions including branding, communication channels, product development, online and offline promotions, and market research. Also conduct various market research and survey for the company. Main Responsibilities   Responsible for brand […]

This post Marketing Coordinator at CVPeople Tanzania has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger