Wednesday 25 November 2020

Halima Mdee na Wenzake Waitwa Kujieleza CHADEMA


Katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika amesisitiza kuwa chama hicho hakikufanya uteuzi wa wanachama wao 19 ambao jana Jumanne Novemba 24, 2020 waliapishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwa wabunge wa viti maalum.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Novemba 25, 2020, Mnyika amesema chama hicho hakijateua wabunge hao wala kupeleka orodha ya majina Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), huku akitoa wito wa kuwataka wabunge hao kufika katika ofisi za chama hicho  keshokutwa Ijumaa, Novemba 27, ili kuhojiwa na Kamati Kuu ya Chama kutokana na kitendo walichokifanya.

“Tumewaita kuwaeleza kwamba Chadema hakijateua wabunge wa viti maalum wala hakijawasilisha orodha yoyote Tume Uchaguzi ya uteuzi wa wabunge wa viti maalum. Kwa katiba ya Chadema mamlaka ya uteuzi wa wabunge yako kwa kamati kuu ya chama, na kamati kuu ya chama haijawahi kufanya kikao cha uteuzi wa majina ya wabunge wa viti maalum na mimi Katibu Mkuu sijawahi kuwasilisha orodha yoyote Tume ya Uchaguzi.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilituandikia barua Novemba 10, 2020 kutueleza haijapokea majina ya wabunge wa viti maalum na kutuomba kuyawasilisha ikiwemo fomu namba 8D inayopaswa kuwa na idhini ya katibu mkuu wa chama na mimi sijajaza yoyote. Niliiandika baada ya Mkurugenzi wa NEC kunukuliwa na vyombo vya habari kwamba Chadema imewasilisha orodha ya wabunge wa viti maalum na yeye amekwishaipeleka bungeni.

“Mimi kama Katibu Mkuu hakuna fomu yoyote niliyowahi kuijaza popote kuthibitisha uteuzi wa yeyote, hii fomu pia ina sehemu ya kiapo cha hakimu, kwa tafsiri nyepesi kilichofanyika ni  kughushi na wameenda kuapishwa bila baraka ya chama.

“Tumeitisha kikao cha kamati kuu Ijumaa, Novemba 27, 2020, Dar es Salaam, na tutawaandikia wahusika ili kisitokee kisingizio hakupata taarifa, natangaza wito kwa wanachama wetu 19 walioshiriki kuapishwa kufika makao makuu Kinondoni Ijumaa saa 2:00 asubuhi,” alisema Mnyika.

Aidha, amesema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ataongoza kikao cha kuwahoji wanachama walioapishwa kuwa wabunge wa viti maalum akiongeza kwamba si mara ya kwanza wao kufanya vikao vya kinidhamu na walioapishwa wameshiriki kukihujumu chama.


Share:

Idara Ya Utamaduni Yaagizwa Kufanya Maandalizi Ya Uzinduzi Wa Bodi Ya Mfuko Wa Utamaduni Na Sanaa

 Na Shamimu Nyaki – WHUSM, Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi ameiagiza Idara ya Maendeleo ya Utamaduni ya Wizara hiyo kuanza maandalizi ya kuzindua Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa.

Katibu Mkuu Dkt.Abbasi ametoa maagizo hayo Novemba 24, Jijini Dodoma katika kikao chake na Idara hiyo.

Dkt.Abbasi ameiagiza Idara hiyo kusimamia vyema Taasisi zilizo chini yake hasa inayohusika na kukuza na kuendeleza Lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi.

Aidha, Dkt. Abbasi ameitaka Idara hiyo kuratibu matamasha mbalimbali huku akieleza nia ya kuwa na tamasha la Singeli Festival mwishoni mwa mwezi Desemba, 2020.

MWISHO.


Share:

TAKUKURU yamkamata Meneja wa fedha wakampuni ya vinywaji vikali BEVCO


Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) imemkamata Rwegasira Samson kijiji cha Kinang’weli, Itimila Mkoani Simiyu

Rwegasira alijificha baada ya TAKUKURU kutangaza kuwa inamtafuta ili kumjumuisha kwenye kesi ya Uhujumu Uchumi namba ECC 87/2020 iliyokuwa na washtakiwa wengine watatu

Kesi hiyo inahusu makosa ya Rushwa, Ubadhirifu, Utakatishaji fedha na Ukwepaji kodi unaohusisha zaidi ya Tsh Bilioni 1.6

Rwegasira alikuwa ni Meneja wa Fedha wa Kampuni ya BEVCO limited inayojihusisha na uagizaji na uuzaji wa vinywaji vikali kutoka nje ya nchi.


 


Share:

Wizara Ya Ardhi Yaanza Upimaji Na Umilikishaji Vitongoji 14 Kata Ya Chamwino Dodoma


 Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza zoezi la kupanga, kupima na kumilikisha ardhi katika vitongoji 14 vilivyopo katika kata ya Chamwino mkoani Dodoma.

Zoezi hilo limeanza rasmi tarehe 24 Novemba 2020 kwa timu kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi chini ya Mkurugenzi Msaidizi wa Upimaji na Ramani Bi. Elizabeth Mrema kukutana na wananchi wa vitongoji vyote 14 vya Kata ya Chamwino ili kuangalia namna bora ya kuendesha zoezi hilo.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Usanifu Miji na Mipango Kabambe Wizara ya Ardhi Bi. Immaculate Senje aliwataka wananchi wa vitongoji vya Chamwino kuhakikisha wanamaliza tofauti za  migogoro midogomidogo ya ardhi katika maeneo yao kabla ya wataalamu hawajafika uwandani ili kurahisisha kazi ya upangaji, upimaji na umilikishaji ardhi kwa wananchi.

Alisema, iwapo wananchi wa maeneo husika watashindwa kumaliza tofauti zao za migogoro ya ardhi mapema basi wataalamu watakapofika watashindwa kuendelea na zoezi mpaka pale utatuzi wa mgogoro uikapomalizika.

‘’Zoezi la upimaji katika eneo la Chamwino hapa Dodoma linalenga pia kupata maeneo ya miundombinu ikiwemo barabara na zoezi litazingatia njia za awali na kuepuka kugusa nyumba za wananchi’’ alisema Bi Senje.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Upimaji na Ramani Elizabeth Mrema aliwatoa hofu wananchi wa maeneo ya vitongoji vya Chamwino kuhusiana zoezi hilo ambapo aliwataka kuwapa ushirikiano wataalamu wa wizara ya ardhi watakaokuwa wakifanya kazi hiyo.

Alisema, hofu ya wananchi kuwa wanaweza kudhulumiwa maeneo yao kupitia zoezi hilo siyo za kweli na kusisitiza kuwa Wizara imeamua kuboresha vitongoji vya kata ya Chamwino ili kuwawezesha wananchi kuwa na nyaraka za umiliki wa maeneo yao.

Kwa mujibu wa Bi. Mrema, zoezi la kupanga, kupima na kumilikisha ardhi Chamwino litaanza na vitongoji vitano na baadaye kuendelea na vitongoji viingine hadi kufikia 14. Alivitaja vitongoji vitano ambavyo zoezi hilo litaanza kuwa ni Sokoine, Ukombozi, Kambarage, Umoja na Azimio.

Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma Letare Shoo aliwaambia wananchi wa Chamwino katika mkutano huo kuwa, kazi ya upangaji, upimaji na umilikishaji maeneo katika vitongoji vya Chamwino umegawanyika katika makundi makuuu mawili aliyoyaeleza kuwa ni urasimishaji au uboreshaji maeneo yaliyojengwa bila kufuata taratibu na pili ni kupima mashamba makubwa kwa kuanisha matumizi yake ikiwemo viwanja.

Hata hivyo, Afisa Ardhi huyo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino alisema, tofauti na maeneo menfine wananchi wa Chamwino watapata unafuu katika gharama wakati wa zoezi hilo ambapo badala ya kulipia 150,000 wao watalipia shilingi 50,000 kwa kila kiwanja.

‘’Halmashauri ya Manispaa ya Chamwino ina jumla ya vijiji 107 lakini kijiji cha Chamwino kimepata upendeleo wa kipekee kupimiwa na wataalamu wa Wizara ya Ardhi’’ alisema Shoo.

Mmoja wa wananchi wa kitongoji cha Talama katika kata ya Chamwino Dikson Mchiwa mbali na kuipongeza Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa uamuzi wa kupanga, kupima na kumilikisha maeneo Chamwino alitaka wizara kuhakikisha zoezi hilo linatakelezwa hasa ikizingatiwa kumekuwa na kugeugeua chakuelezwa upimaji utafanyika halafu haufanyiki..


Share:

Tanzania Yateuliwa Umoja Wa Mataifa


 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya hati za utambulisho ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN Credentials Committee) New York Marekani kwa mwaka 2020/2021.

Hii ni mara ya kwanza katika Historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushika nafasi ya kuongoza kamati hiyo nyeti ya Umoja wa Mataifa ambapo uteuzi wake ulipendekezwa na Ofisi ya Rais wa Baraka Kuu la Umoja wa Mataifa na kuidhinishwa kwa kauli moja na wajumbe wote tisa wa Kamati hiyo.

Wajumbe hao ni Marekani,China,Urusi,Cameroon,Uruguay Iceland Papua Guinea na Trinidad na Tobagona na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza mara baada ya uteuzi huo Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Prof. Kenedy Gaston amesema kuwa uteuzi huo ni muhimu sana na ni ishara ya namna Tanzania inakubalika katika uso wa Jumuiya ya Kimataifa kutokana na uongozi thabiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli halikadhalika sera zake za mambo ya nje.

Balozi Prof. Kenedy Gaston ameongeza kuwa kwa mara ya kwana tangu uteuzi huo Tanzania imeongoza kikao chake cha kwanza cha kamati hiyo Kikao kilichofanyika New York,Marekani.


Share:

Wafanyabaishara Mkoani Tabora Wakubaliana Faida Ya Mfuko Mmoja Wa Saruji Isizidi Shilingi 500/=


NA TIGANYA VINCENT
UONGOZI wa Mkoa wa Tabora umekutana na wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi na saruji na kukubaliana faida wanayopata katika kila mfuko mmoja wanayouza isizidi shilingi 500/= baada ya kuondoa gharama mbalimbali wazizotumia ili kutowaumizi wananchi wanyonge.

Wamefikia uamuzi huo  katika Mkutano ambao uliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt.Philemon Sengati kwa lengo la kutafuta muafaka wa kutatua tatizo la bei ya saruji kupanda.

Akifungua mkutano huo Mkuu wa Mkoa alisema Serikali haikusudi kuwapanga bei elekezi ya saruji lakini wafanyabiashara wanalojukumu la kuuza bidhaa hiyo kwa bei ambayo haitawafanya wananchi wanyonge washindwe kujenga na kuishi katika nyumba bora.

Dkt. Sengati alisema kimsingi hakuna sababu ambazo zinazoweza kuhalalisha wafanyabiashara hao kupandisha saruji ambapo wapo wanauza shilingi 23,000/- hadi 30,000/= kwa mfuko mmoja wakati wao wananua kiwandani kwa wastani unaoanzia 11,000 hadi shilingi 13,000/=.

Alisema gharama za usafirishaji na posho za vibarua na madereva haiwezi kufanya bei ipande kwa kiasi hicho ambacho inawaumiza wananchi.

Dkt. Sengati alisema pamoja na kuwa sio jukumu la Serikali kupanga bei lakini ina wajibu wa kuhakikisha bei za bidhaa zilizoko sokoni haziwaumizi wananchi wanyonge na kuwafanya wachukie Serikali yao

Alisema wafanyabiashara ni wadau muhimu katika kushirikiana na Serikali kwenye shughuli za maendeleo ni vema wakahakikisha saruji inauzwa kwa bei nafuu ambayo haiwaumizi wananchi na kuwafanya wajisichie Serikali yao.

“Tumebaini wafanyabiashara wa rejareja wanauza saruji kwa shilingi 23,000/= hadi 30,000/= wakati bidhaa hizo amechukulia hapa hapa Tabora na hana gharama kubwa za kusafirisha mizigo…kitendo hicho ni kutaka kutengeneza fedha nyingi kwa kuwaumiza wanyonge… hakikubaliki, serikali haiwezi kuvulimia ,tutawachukulia hatua” alisema.

Dkt. Sengati alisema wafanyabiashara wanatakiwa kuwa wazalendo kwa kuungana na maono na mtazamo wa Serikali ya Awamu ya Tano ambao unataka ubora na unafuu wa maisha kwa wananchi.

Mmiliki wa Kampuni ya Vimajo and Sons ambaye ni miongoni  wa wanyabishara wakubwa wa Saruji Mkoani Victor Chami alisema hivi sasa saruji inapatikana kwa shida na wakati mwingine wanalazimika kununua kwa wafanyabiashara wenzao ambao wanaakiba  na ndio maana ameongeza kiashi hicho kidogo.

Mfanyabiashara huyo aliongeza kuwa hivi sasa wameamua kununua saruji aina ya Camel baada ya waliyokuwa wakinunua kwa wingi Mkoani Tabora ya Dangote kutopatikana.

Alisema wananunua saruji hiyo kwa gharama ya shilingi 13, 340/= kiwandani Dar salaam na  gharama za usafiri ni shilingi 5,000/= na vibarua wa kushusha wanawalipa shilingi 100/= na zinazobaki ndio faida yao.

Chami alisema kutoka na uhitaji mkubwa wa saruji hapa nchini kwa sababu ya miradi mikubwa inayojengwa na Serikali na mahitaji ya wananchi ni vema Seikali ikawabana Wazalishaji wa Saruji ili waongeza uzalishaji na waachane na kupeleka nje ya nchi.

Alisema pindi Serikali itakapokamilisha miradi yake ndio wazalishaji waruhusiwe kupeleka nje ya Tanzania.

Chami alisema yeye atauza saruji kwa bei ya awali ya shilingi 18,500/= kama ilivyokuwa kabla ya kuadimika kwa saruji mkoani humo.

Naye Beatus Massawe alisema ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa saruji mkoani ni vema kumuomba Dangote kuanzisha Ghala kubwa Tabora kwa ajili ya Mikoa ya Kanda ya Magharibi.

Alisema kuwepo kwa ghala hilo litawasaidia kupata bidhaa hiyo kwa muda mfupi na gharama ambayo itawafanya wauze kwa bei ya chini kwa wananchi.

Massawe alisema sanjari na hilo alimuomba Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora ili awasiliane na Shirika la Reli Tanzania liweze kuongeza Mabehewa ya kuleta saruji kwa wingi mkoani Tabora.

Baada ya mkutano huo Wafanyabiashara hao kwa pamoja walikubaliana kuwa bei ya Saruji aina ya Simba kwa rejareja iuzwe kwa shilingi 18,500/- kwa mfuko, Dangote iuzwe kwa kiwango cha shilingi 19,000/=, Camel iuzwe kwa shilingi 19,500/= na Nyati iuzwe kwa shilingi 20,000/-.
Walifikia uamuzi huo baada ya kujumulisha gharama kutoka uzalishaji kiwandani , za usafiri, posho ya vibarua na faida ya Mawakala.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora alisema baada ya makubaliano hayo Serikali haitasita kuwachukulia hatua wafanyabiashara ambao watakutwa wanauza zaidia ya hapo.




Share:

UONGOZI SAO HILL WATOA MIEZI MIWILI KWA WAKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI WA MABWENI

Kutoka kushoto Msimamizi wa mradi anayefuata ni Afisa Ugavi wa shamba John Keraryo na wa mwisho Mhifadhi Mkuu wa Shamba Juma Mwita Mseti akipata maelezo kutoka kwa wasimamizi haoMhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Sao Hill Juma Mwita  akipa maelezo wakati wa kukagua miradi ya ujenzi wa mabweni

Na fredy Mgunda,Mufindi.

TFS kupitia Shamba la Miti Sao Hill linatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jamii inayozunguka shamba ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mabweni katika shule za sekondari.


Wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Sao Hill Juma Mwita amesema lengo za ukaguzi wa miradi ni kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati kama ilivyokusudiwa.


Hata hivyo Mwita aliwataka wajenzi na wasimamizi wa miradi ya ujenzi wa mabweni kuhakikisha miradi hii inakamilika ndani ya miezi miwili ili wanafunzi wanapofungua shule mwezi Januari mabweni hayo yaweze kutumika.


"Lengo la mabweni haya ni kusaidia watoto wetu wa kike ili wakae mahali salama wakiwa shuleni na hii itasaidia sana wanafunzi hao kusoma katika mazingira mazuri."Alisema Mhifadhi Mkuu wa Shamba


Mwita aliongeza kuwa TFS inasaidia jamii katika miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuonyesha shukrani na kuwakumbusha wananchi kuendelea kulinda misitu iliyopo kwa faida mbalimbali zinazoonekana.


Naye Mwalimu Paul Msukwa kutoka Shule Sekondari Ihanu alisema kuwa mabweni haya yatawasaidia sana wanafunzi wa kike kuondokana na changamoto zinazowakabili na itasaidia ufaulu kupanda.


"Mabweni haya mawili yaliyokaguliwa ambayo yapo katika Shule ya Sekondari Luganga na Ihanu yatakuwa na uwezo wa kuchuka wanafunzi 160 kwa wakati mmoja" alisema

KAWAIDA:
Share:

IBRAHIM NGWADA AMECHAGULIWA KUWA MEYA WA MANISPAA YA IRINGA

 

Ibrahim Ngwada akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kushinda kuwa meya wa Manispaa ya Iringa

Na fredy Mgunda,Iringa.

Ibrahim Ngwada amechaguliwa Kuwa meya wa manispaa ya Iringa  kwa kupata kura 19 huku akifuatiwa na Jackson Chaula kwa kupata kura tano katika uchaguzi uliofanyika  ukumbi wa  chama cha mapinduzi (CCM) Manispaa ya Iringa.

Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo wa kumtafuta meya na naibu meya wa Manispaa ya Iringa Toviki Kivike alisema kuwa uchaguzi wa meya umefanyika kwa amani,uwazi na haki na wagombea wote wameridhika mara baada ya matokeo hayo kutangazwa.


Aidha msimamizi huyo alisema kuwa uchaguzi wa naibu meya ulifanyika mara mbili kutokana na ushindani ulikuwepo hivyo kuamriwa kurudia ndio alipopatikana mashindi.


Baada ya kutangazwa kuwa meya wa Manispaa ya Iringa  Ibrahim Ngwada  alisema kuwa anazitambua changamoto za wananchi wa manispaa za Iringa hivyo atahakikisha anazitatua vilivyo ili wananchi wapate maendeleo.

Ngwada aliongeza kwa kusema kuwa miaka mitano iliyopita Manispaa hiyo ilikuwa chini ya CHADEMA na walifanya maendeleo hivyoatakikisha wanafanya kazi kubwa kuleta maendeleo zaidi ya yaliyofanywa na watangulizi wake kuwa sasa manispaa hiyo ipo chini ya CCM.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 25,2020

 


Share:

Business Development Manager at RSK Consulting Limited

Business Development Manager Company Name RSK Tanzania Company Location Dar es Salaam, Tanzania We are looking for a talented and aggresive individual to fill an opening in our Business Development Support unit. The ideal candidate will lead initiatives to generate and engage with business partners to build new business for the company. This candidate will be focused […]

The post Business Development Manager at RSK Consulting Limited appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Supervisor Officers at Job Junction Tanzania

position: SUPERVISOR OFFICERS Details Employer name : JOB JUNCTION TANZANIA Work Type : Full Time Years of Experience 1 year Location: Dar es Salaam District Dar Es Salaam Minimum Qualification: Diploma Main Job Task and Responsibilities: • Helping the team understand performance targets and goals • Training or ensuring that workers are properly trained for their specific roles • […]

The post Supervisor Officers at Job Junction Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

11 New International Job Vacancies at African Development Bank Group (AfDB) – Various Posts

-The first thing you will notice about the AfDB is the passion of its employees to help reduce poverty on the continent, improve living conditions for Africans and mobilize resources for the continent’s economic and social development. That is what drives us to seek motivated individuals who share this commitment to poverty reduction. Our network […]

The post 11 New International Job Vacancies at African Development Bank Group (AfDB) – Various Posts appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Names Called for Interview at GEITA Town Council on 26th – 27th November, 2020

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, President’s Office, Regional Administration and Local Government MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MJI GEITA Names Called for Interview at GEITA Town Council on 26th – 27th November, 2020 Overview Geita District is located in the Geita Region of Tanzania. According to the 2012 census, the population of the district […]

The post Names Called for Interview at GEITA Town Council on 26th – 27th November, 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Digital Transformation at CVPeople Tanzania, Human Resource Manager

Human Resource Manager – Digital Transformation   Dar es Salaam , Tanzania | Posted on 11/23/2020 Job Description Job Purpose This role reports to the Managing Director and is key in the design and implementation of the Country’s HR digital transformation initiatives. You will lead the delivery of the Country’s people agenda, ensuring the required HR strategies […]

The post Digital Transformation at CVPeople Tanzania, Human Resource Manager appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

WATENDAJI Executive Officers at MUFINDI District Council IRINGA

Iringa is a city in Tanzania with a population of 1,211,900 (as of 2020). It is situated at a latitude of 7.77°S and longitude of 35.69°E. The name is derived from the Hehe word lilinga, meaning fort. Iringa is the administrative capital of Iringa Region. Iringa Municipal Council is the administrative designation of the Municipality […]

The post WATENDAJI Executive Officers at MUFINDI District Council IRINGA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Warehouse Manager at Médecins Sans Frontières (MSF)

JOB VACANCY – WAREHOUSE MANAGER    Médecins Sans Frontières (MSF) is an international, independent, medical humanitarian organisation that delivers emergency aid to people affected by armed conflict, epidemics, natural disasters and exclusion from healthcare. MSF offers assistance to people based on need, irrespective of race, religion, gender or political affiliation. MSF is therefore guided by […]

The post Warehouse Manager at Médecins Sans Frontières (MSF) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Strategic Information Officer at Health Links Initiative (HLI)

Health Links Initiative (HLI) is a non-profit organization dedicated to contribute in strengthening health systems in Tanzania. It was registered in September 2011 under the Non-Governmental Organizations Act, 2002. HLI vision is “Better quality assurance practices in public health laboratory and medicine in Tanzania”.  HLI brings together a team of experts with vast experience in […]

The post Strategic Information Officer at Health Links Initiative (HLI) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger