Tuesday 26 February 2019

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI

Na Amiri kilagalila Takribani ya vijiji 20 vilivyopo kata 6 wilayani ludewa mkoani Njombe vinatarajia kunufaika na mradi wa umeme wa megawati 1.6 uliopo katika kijiji cha Lugalawa wilayani humo. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mara baada ya kutembelewa na barozi wa nchi ya Ujerumani nchini Tanzania DETLEF WACHTER,Mkuu wa mkoa wa Njombe CHRISTOPHER OLESENDEKA amesema kuwa mradi huo wa kufua umeme kwa kutumia maji unatarajia kukamilika mwezi aprili mwaka huu. “ni kwamba tuna mradi wa kufua umeme kwa kutumia maji katika kijiji cha Lugalawa wilaya ya Ludewa…

Source

Share:

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUMALIZA TATIZO LA VYUMBA VYA MADARASA

Na Allawi Kaboyo. kufatia kuwepo kwa uhaba wa vyumba vya madarasa na kupelekea uwepo wa mrundikano wa wanafunzi katika shule za sekondari Tunamkumbuka na Butulage zilizopo halmashauri ya wilaya Bukoba mkoani Kagera, wananchi katika maeneo hayo waliamua kuanzisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwa kila shule ambapo serikali imewaunga mkono kwa kuwapelekea kila shule shilingi milioni 25 ili kumalizia ujenzi huo. Akiwaelezea wananchi upatikanaji wa fedha hizo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi ulipofikia Februari 25 mwaka huu mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye pia ni diwani wa kata…

Source

Share:

BILIONI 1.2 ZA BENK YA NMB KUTUMIKA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU KANDA YA ZIWA VICTORIA

Na mwandishi wetu Benki ya NMB kanda ya ziwa Victoria inatarajia kutumia zaidi ya Sh1.2 bilioni kuboresha mazingira ya utoaji huduma katika sekta ya elimu na afya kwenye mikoa iliyoko ndani ya kanda hiyo Kaimu meneja wa NMB wa kanda ya ziwa Abrahim Agustino alisema fedha hizo zinatumika kuweka samani katika shule za msingi na sekondari na kuboresha miundombinu katika vituo vya afya na Hospitali pale wananchi na viongozi wanapopeleka ombi la kusaidiwa nguvu zao Agustino alisema hayo jana wakati akikabidhi meza 62 na viti 62 vyenye thamani ya Sh…

Source

Share:

SERIKALI YAUNGANA NA WANANCHI UJENZI WA MADARASA

Share:

MCHUNGAJI AZUA GUMZO BAADA KUDAI KUMFUFUA MTU...WAUZA MAJENEZA WAIBUKA



Mchungaji Alph Lukau kutoka Afrika Kusini amezua gumzo baada ya kudai kumfufua mtu wakati wa ibada yake ya Jumapili ya Februari 24,2019.

Imeelezwa kuwa mtu huyo aliyedaiwa kufariki tangu Ijumaa alikuwa akipumua ndani ya jeneza.

Wananchi wameitaka serikali iwazuie wachungaji hao wanaowahadaa wananchi kwa miujiza.

Baada ya kusambaa kwa habari za Mchungaji wa Afrika Kusini Alph Lukau kumfufua mtu  kampuni inayouza masanduku ya mazishi (jeneza) imejitokeza na kusema kuwa sanduku hilo halikutoka kwao, na pia wanafikiria kumshtaki mchungaji huyo.
Akizungumza na Television ya SABC nchini Afrika Kusini, mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya mazishi ya Kings and Queens, Mis. Vivian Mponda, amesema kwamba wao walifuatwa na mmoja wa wanafamilia wakiomba kutumia usafiri, lakini sanduku lililotumika halikuwa la kwao na wala mwili huo haukuhifadhiwa hapo kama wanavyodai, kwani huwa hawahifadhi mwili bila taarifa rasmi.

“Hatukuwauzia sanduku hivyo sio la kutoka Kings & Queens na hatuna sanduku la vile kwenye mochwari yetu, ila gari walikodi kwetu wakisema wanataka kulitumia kwenye mazishi ya ndugu yao”, amesema Ms. Vivian.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji (SABC) habari zinasema kwamba waandishi walimfuatilia mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Eliot na mpenzi wake ambaye alikuwepo siku ya tukio (kufufuliwa), na kugundua kuwa waliondoka nyumbani kwao tangu Jumatano, na hawajarudi mpaka sasa.

Wakiendelea kuchunguza hilo imebainika kuwa hata mtu aliyesema amempangisha nyumba yake ambaye ndiye alimfia mikononi sio kweli, kwani mwenye yeye ni mwanamke na aliyekuwepo siku ya tukio hilo alikuwa ni mwanaume.

Jumapili ya Februari 24 mchumgaji Alph Lukau wa kanisa la Aleluia Ministry la Afrika Kusini amezua mtafaruku mkubwa mitandaoni baada kudai amemfufua mtu, aliyeletwa na mwenye nyumba wake akidai kuwa alifariki baada ya kumkimbiza hospitali alipoumwa, na ndipo akaamua kumpeleka kanisani kumuombea.
Share:

SHIRECU YAENDELEA KUFANYA UKARABATI MKUBWA WA MAGARI YAKE KUJIANDAA NA MSIMU MPYA WA PAMBA


TAARIFA KWA UMMA
Katika kuelekea msimu mpya wa pamba wa mwaka 2019/2020 Chama Kikuu cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Region Co-Operative Union (1984) Ltd - SHIRECU) kimeweza kufanya marekebisho magari yake ili kujiandaa na msimu wa pamba wa mwaka 2019/2020.

Ukarabati huo unajumuisha magari makubwa na madogo,ambapo kati ya magari makubwa 30 yenye uwezo wa kubeba tani 10 hadi 15,magari makubwa matatu yamekarabatiwa na mengine yanaendelea na ukarabati,aidha magari madogo matatu(3) kati ya 13 aina ya land cruiser hardtop 1 hz yamekarabatiwa na kuendelea kufanya shughuli za kila siku za union.

Ukarabati huo umelenga kuandaa magari kwa ajili ya kuwasaidia wakulima kupitia vyama vya msingi kupata huduma ya uchukuzi katika msimu wa pamba unaotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.

Aidha pia magari hayo makubwa yatatumika kwa kukodishwa na watu binafsi ili kuweza kuongeza mapato kwa chama kikuu cha ushirika mkoa wa Shinyanga.

Imetolewa na: 

Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano 
Shinyanga Regional Cooperative Union (SHIRECU(1984)LTD). 
26.02.2019.
Magari yaliyokarabatiwa na SHIRECU
Share:

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA DAKTARI BINGWA WA UPASUAJI WA UBONGO NA MISHIPA YA FAHAMU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing nchini China mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu. Picha na Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Mazungumzo na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing nchini China aliyeambatana na ujumbe wake pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Maseru na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Respicious Boniface Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing nchini China wanne kutoka kulia, Balozi wa China hapa nchini Wang Ke watatu kutoka kulia pamoja Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Respicious Boniface. Wengine katika picha ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Balozi Zuhura Bundala pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Maseru.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing China wanne kutoka kulia mara baada ya kumaliza kupiga picha ya kumbukumbu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Share:

MKURUGENZI ITIGI NA WENZAKE 6 KUENDELEA KUSOTA RUMANDE KESI YA MAUAJI KANISANI


Mkurugenzi Mtendaji (DED) halmashauri ya mji wa Itigi, wilayani Manyoni mkoani Singida, Pius Luhende na wenzake sita wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya mkulima Isaac Petro (28) wataendelea kukaa rumande hadi Machi 11, mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Askari Wanyamapori wa halmashauri Rodney Elias (42), Askari wa Wanyamapori Hifadhi ya Doloto wilayani Manyoni, Makoye Steven, Mwanasheria wa halmashauri hiyo, Eric Paul (31) na Ofisa Tarafa Itigi, Eliutha Augustino (43).

Wengine ni Ofisa Kilimo na Mifugo, Silvanus Lungwisha (50) na Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Kazikazi, Yusuph John (25).

Wakili anayemtetea mshitakiwa Luhende, Victoria Revocati ameuomba upande wa mashitaka kuharakisha upelelezi ili mteja wake aweze kupata haki yake mapema kutokana na ukweli kuwa kesi hiyo haina dhamana.

Hata hivyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Consolata Singano alimweleza mshitakiwa huyo kupitia kwa Wakili wake kuwa kwa sasa bado ni mapema mno kulalamikia ukamilikaji wa upelelezi kutokana na uzito wa kesi, ambayo ni kesi ya mauaji.

Washitakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuwa mnamo Februari 2, mwaka huu huko kwenye Genge namba 48 kijiji cha Kazikazi, kata ya Kitaraka tarafa ya Itigi wilayani Manyoni, walishirikiana kumuua kwa risasi mkulima wa kijiji hicho, Isaack Petro (28) kinyume na Kifungu cha 116 na 197 vya Sheria ya Kanuni za Adhabu.

Walipofikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 11 mwaka huu, Washitakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa Mahakama hiyo haina Mamlaka kisheria kusikiliza shauri hilo.

Washitakiwa wote saba wamerejeshwa rumande hadi Machi 11, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Share:

WALEVI WA NGONO SASA KUKIONA CHA MOTO

Watu wanaopenda kufanya ngono na wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari nchini sasa kukamatwa.

Kazi ya kuanza kukabiliana na watu wenye tabia hiyo inaanzia mkoani Kilimanjaro ambapo Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu ameagiza waliowapa mimba wanafunzi mkoani humo wakamatwe.

Ni baada ya taarifa ya mkoa huo kuonesha kwamba, kuanzia Januari hadi Desemba mwaka 2018, jumla ya wanafunzi wa kike 57 walipachikwa mimba na hatimaye kukatisha masomo yao.

Taarifa hiyo ilimshtua Waziri Majaliwa na hasa baada ya kuelezwa kuwa, katika kesi hizo 57 za wanafunzi kupachikwa mimba, ni kesi sita tu ndio zilizofikishwa mahakamani.

Agizo hilo la kukamatwa malevi hao wa ngono wote limetolewa na Waziri Majaliwa mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano uliofanyika katika Uwanja wa Isanja, Sanya Juu katika Wilaya ya Siha, Kilimanjaro.

Chanzo- Mwanahalisionline
Share:

ABIRIA WANUSURIKA KUFA BAADA YA TRENI KUGONGA BASI ASUBUHI HII


Treni ya kusafirishia abiria imeligonga basi katika mtaa wa Pipeline jijini Nairobi nchini Kenya ikitoka Embakasi.

 Ajali hiyo imetokea asubuhi ya Jumanne, Februari 26 na imelihusisha basi la kampuni ya City Hoppa na hakuna aliyejeruhiwa.

Kufikia muda wa kuchapisha ripoti hii, shughuli zilikuwa zimekwama eneo hilo huku Shirika la Reli Nchini likijitahidi kutoa huduma za kuondoa basi hilo.

Hii sio mara ya kwanza kwa ajali za aina hii kutokea na katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kumeshihudiwa kadhaa. Mwaka wa 2018, treni iligonga lori la kusafirishia mafuta eneo la Pipeline na ajali hiyo ilisababisha msongamano mkubwa wa magari kwenye Barabara ya Outering. 

Share:

MTOTO ALIWA NA MAMBA AKIOGA ZIWANI

Mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Nyambeba katika halmashauri ya Buchosa mkoani Mwanza, Stivine Wiliam (10) amekufa kwa kuliwa na mamba alipokuwa akioga ndani ya Ziwa Victoria.

Kufariki kwa mtoto huyo kumefikisha idadi ya watu waliopoteza maisha kwa kuliwa na mamba kufikia 14 tangu mwaka 2016 hadi sasa.

Kutokana na ukubwa wa tatizo hilo, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole aliiambia Mwananchi jana Jumatatu, Februari 25 kuwa Serikali inaangalia uwezekano wa kutunga sheria ndogo kukataza watu kuoga ndani ya Ziwa Victoria kama moja ya hatua za kukabiliana na matukio hayo.

Akizungumzia tukio la mtoto huyo kukamatwa na kuliwa na mamba, Afisa Mtendaji Kijiji cha Nyambeba, Edward Pastory alisema tukio hilo lilitokea saa 10:00 jioni ya Februari 22, 2019.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, jumla ya watu watano wamepoteza maisha wilayani Sengerema kwa kuliwa na mamba.

Kaimu Afisa Ardhi na Maliasili Halmasahuri ya Buchosa, Ariko Ndile alitaja maeneo yanayokumbwa na matukio hayo kuwa ni vijiji vya Nyambeba, Kanyala, kisaba, Izindabo na Kisiwa cha Kome katika kata ya Buhama.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Buchosa, Crispin Luanda alisema ofisi yake imeanza kuchukua hatua kwa kuchimba visima 14 katika maeneo mbalimbali kuwezesha wananchi kupata huduma ya maji badala ya kutegemea huduma hiyo ziwani.
Na  Daniel Makaka, Mwananchi 
Share:

BALOZI AMPIGA MAKOFI ASKARI WA USALAMA BARABARANI

Wanaharakati na spika wa bunge la Uganda wameshutumu vikali kitendo cha balozi wa Uganda nchini Burundi, Meja Jenerali Matia Kyaligonza kumpiga kofi askari mwanamke wa usalama barabarani mwishoni mwa wiki.

Picha za kufanyiwa fujo askari huyo zilionekana kwenye mitandao ya kijamii ambazo zimeibua hasira miongoni mwa wananchi, huku taasisi za jeshi na polisi zikimkosoa Jenerali huyo.

Mvutano kati ya walinzi wa balozi huyo na askari aliyetambulika kwa jina la Esther Namaganda aliyewazuia kukiuka sheria za barabarani ulishuhudiwa na wananchi mtaa wa Seeta.

Esther alionekana kwenye video iliyochukuliwa mtu aliyeshuhudia tukio hilo akifanyiwa fujo na balozi huyo.

Katika video hiyo iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii, mmoja wa askari anaonekana akiuvuta mkono wa Sajenti Esther ambaye anajaribu kukabiliana naye.

Balozi Kyaligonza, ambaye alionekana akiwa amevalia shati jeupe, alikuwa akizunguka eneo la tukio hilo akiwa ameshikilia bakora.

Msemaji wa Jeshi la Uganda, Brigadia Jenerali, Richard Karemeire ameomba radhi kwa shambulio dhidi ya Sajenti Esther.

''Tunaomba msamaha kwa askari polisi… hata hivyo habari njema ni kwamba sisi kama jeshi la Uganda tumechukua hatua za haraka kwa hao askari wawili wamekamatwa na upelelezi unaendelea kwa pamoja na polisi na baada ya hapo hatua kali zitachuliwa dhidi yao,'' amesema.

Spika na wanaharakati

Spika wa bunge la Uganda, Rebecca Kadaga amelaani vikali kitendo hicho wakati alipokutana na wanaharakati wa haki za wanawake waliowasilisha malalamiko kwake.

''Tabia hii ya kumshambulia mtu ambaye anafanya kazi aliyopewa na serikali haikubaliki miongoni mwa viongozi na mtu mwingine yeyote haikubaliki, nafurahi kwamba wahusika wamekamatwa na ningemtaka mkuu wa jeshi la polisi kumpandisha cheo mwanamke huyo,''

Angela Asiimwe msemaji wa kundi la wanaharakati wa haki za wanawake nchini Uganda alisema ''Ulikua ni ukiukaji mkubwa wa haki zetu wanawake na Waganda kwa ujumla, nafurahi kwamba baadhi ya waliompiga Sajenti Namaganda wamekamatwa.''

Chanzo - Mwananchi
Share:

Monday 25 February 2019

MAHAKAMA YASOGEZA MBELE KESI YA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE

Na Amiri kilagalila Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe leo imewapandisha kizimbani kwa mara ya pili watuhumiwa watatu wa mauaji ya watoto watatu wa familia moja wa kijiji cha Ikando kata ya kichiwa wilayani Njombe. Watuhumiwa hao ni JOEL JOSEPH NZIKU,NASSON ALFREDO KADUMA na ALPHONCE EDWARD DANDA ambao Wanakabiliwa na mashtaka ya kuwaua watoto hao kijijini humo. Watoto hao ni Godliver Nziku, Gasper Nziku na Giriad Nziku ambao ni watoto wa familia moja huku ikielezwa kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa la kuwaua januari 20 mwaka huu. hakimu mkazi mkoa…

Source

Share:

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE

Na Amiri kilagalila Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Njombe limewataka Mafundi wanaojihusisha na shughuli za nishati ya umeme mkoani humo kupata leseni kutoka mamlaka ya uthibiti wa nishati na maji EWURA ili kupambana na mafundi wasiokuwa na weledi na kazi zao wala kutambulika kisheria huku wakisababisha matatizo kwa wateja. Wito huo umetolewa na mhandisi wa mpango na kaimu meneja wa Tanesco mkoa wa njombe, YUSUPH SALIM wakati akizungumza na mafundi umeme pamoja na wahandisi katika mkutano wa pamoja ulioandaliwa na umoja wa makandarasi (UMAU) katika ukumbi wa Miriam…

Source

Share:

BABA MZAZI AFURAHIA MTOTO WAKE KUFUNGWA JELA MIAKA 30 MTWARA


Mzee Musa Katambo, baba mzazi wa Ally Katambo (30), ambaye amehukumiwa kwenda jela miaka 30 baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kumkuta na hatia ya kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 11, amefurahia kifungo cha mwanawe. 

Ally alitiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo kutokana na kumfanyia binti yake huyo mwanafunzi wa darasa la nne kitendo cha kinyama.

Mzee huyo alishangilia na kuipongeza mahakama kwa kutoa hukumu hiyo ya kifungo cha miaka 30 jela dhidi ya mwanae, akisema kosa alilolifanya la ubakaji ni kinyume cha sheria za nchi.

Katambo ambaye anaishi kijijini kwake Ndanda wilayani Masasi Mkoani Mtwara, alisema kwamba hajutii maamuzi ya mahakama dhidi ya mtoto wake huyo kufungwa miaka 30 jela, na kwamba serikali imetenda haki katika kusimamia sheria hasa juu ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

Mzee Katambo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza na gazeti hili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Masasi, baada ya mtoto wake huyo kuuhukumiwa kwenda jela miaka 30.

Alisema amefurahishwa na hukumu hiyo kwa sababu itatoa fundisho kwa vijana wengine wenye tabia kama ya mtoto wake kwa kuwa watakaposikia wataacha kufanya vitendo hivyo, ambavyo vinaonekana kuchochewa na imani za kishirikina, badala yake vijana wafanye kazi kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao.

Alisema serikali ya sasa inasimamia haki kuhusiana na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto hasa pale wanapofanyiwa vitendo hivyo na wazazi wao.

Alisema kitendo alichofanya mtoto wake dhidi ya mjukuu wake ni cha kikatili na kimeiletea aibu familia yake.

“Kwa kweli enzi zetu sisi yaani ile miaka ya zamani hakukuwa na mambo kama haya ya ajabu, mzazi kumbaka mwanawe wa kumzaa kisa kaambiwa na mganga ili apate utajiri,” alisema na kuongeza:

“Mambo kama haya sisi ndio kwanza tunayaona siku hizi zamani hayakuwapo kabisa kwa hili mimi naipongeza serikali imetenda haki kabisa.” 

Mzee Katembo alisema siku ya kwanza alipopata taarifa ya kuwa mjukuu wake amebakwa na baba yake mzazi na binti huyo kulazwa katika hospitali ya Mision ya Ndanda mjini Masasi, alipoteza fahamu kwa vile katika maisha yake hakuwahi kusikia jambo kama hilo la baba kumbaka mtoto wake wa kumzaa.

Aliongeza kuwa hata alipokuwa akifunga safari ya kwenda hospitalini Ndanda kwa ajili ya kumuona mjukuu wake anaendeleaje baada ya kulazwa pia alipokuwa akiingia ndani ya hospitali hiyo, alikuwa akianguka na kupoteza fahamu kwa mara mbili mpaka tatu ndipo anapata fahamu.

Na Hamisi Nasiri - Nipashe
Share:

WATUMISHI WA SERIKALI WALIOFARIKI KWA AJALI YA GARI MTONI WAAGWA




Miili ya wataalam tisa wa idara ya ardhi na idara nyingine za Serikali waliofariki kwa ajali ya gari baada ya kutumbukia Mto Kikwawila , inaagwa leo Februari 25, katika viwanja vya Can, Tangani mjini Ifakara.

Kwenye tukio hilo Viongozi mbali mbali wa serikali wamehudhuria, akiwemo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe, pamoja na wafanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero na Ifakara.

Ajali hiyo ilitokea Jumamosi ya Februari 23 saa 11 jioni katika Mto Kikwawila baada ya gari aina ya Toyota Land Cruiser Hard Top linalomilikiwa na wilaya ya Kilombero, kutumbukia kwenye mto huo na kusababisha vifo vya watumishi hao wa kitengo cha upimaji ardhi, huku wanne wakijeruhiwa.
Share:

SHIRECU YAFANIKIWA KUWAHUDUMIA WAKULIMA WA PAMBA KWA MSIMU WA 2018/19

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger