Saturday, 26 April 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRILI 26,2025



Magazeti ya leo




Share:

Friday, 25 April 2025

ZANZIBAR STRENGTHENS TIES WITH UN TOURISM AT REGIONAL FORUM, SHOWCASING COMMITMENT TO SUSTAINABLE TOURISM

Executive Secretary of the Zanzibar Commission for Tourism, Mr. Arif Manji, presented a handcrafted Zanzibari door to Sandra Carvão, Chief of Tourism Market Intelligence and Competitiveness at the UN Tourism, during the two-day 2nd Regional Forum on Gastronomy Tourism for Africa, held from April 23–24 at Gran Meliá in Arusha.

The discussions highlighted the UN Roadmap for Sustainable Waste Management (2019–2030) and its alignment with Zanzibar’s Greener Zanzibar Initiative, underscoring the vital link between sustainable tourism and environmental responsibility.

Ms. Carvão expressed her admiration for Zanzibar’s proactive approach to waste management, especially the upcoming mandatory waste management program for the tourism sector, set to launch on July 1st, 2025. She noted that the initiative reflects Zanzibar’s growing leadership in environmental stewardship and affirmed UN Tourism’s interest in continued collaboration.

Share:

TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA TIBA YA WANYAMA DUNIANI

Ng'ombe aliyeletwa kwa ajili ya kufanyiwa matibabu na madaktari wa mifugo katika Mkoa wa Manyara wakati wa ufunguzi wa siku ya Wanyama Duniani
Madaktari wakiendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wanyama walioletwa kupata tiba na kukaguliwa kutambua changamoto zinazowakabili
Baadhi ya madaktari wa wanyama wakiendelea kutoa huduma kwa wanyama walioletwa kwa ajili ya matibabu Mkoani Manyara
Tiba ikiendelea kutolewa kwa wanyama Mkoani Manyara wakati wa Ufunguzi wa siku ya Wanyama Duniani

*
 
Na Regina Ndumbaro Manyara.

Tanzania inaadhimisha Siku ya Tiba ya Wanyama Duniani mwaka huu kwa mafanikio makubwa, ambapo maadhimisho hayo yamefanyika katika mkoa wa Manyara kuanzia tarehe 24 hadi 26 Aprili 2025. 

Hii ni siku muhimu inayolenga kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa afya ya wanyama na mchango wa madaktari wa mifugo katika ustawi wa jamii na uchumi. 

Tukio hili limepambwa na shughuli mbalimbali katika wilaya za Babati, Mbulu na Hanang, likiwa na kauli mbiu inayobeba uzito wa afya bora ya mifugo kama msingi wa maendeleo endelevu.

Uzinduzi rasmi wa maadhimisho haya umefanyika katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Babati, ambapo wananchi wengi walifurika kushuhudia hafla hiyo. 

Mandhari ya kijani kibichi ya uwanja huo na maandalizi mazuri yamevutia watu kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo. 

Hafla hiyo imekuwa ya kipekee kwa kuwa iliambatana na burudani, maonyesho ya huduma za mifugo, na utoaji wa elimu kuhusu tiba na utunzaji bora wa wanyama.

Madaktari wa mifugo kutoka kila kona ya nchi wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika kutoa huduma mbalimbali kwa jamii. 

Huduma zilizotolewa ni pamoja na chanjo, tiba za magonjwa, upasuaji wa kufunga uzazi, pamoja na ushauri kuhusu mbinu bora za ufugaji. 

Ushirikiano kati ya wataalamu kutoka sekta ya umma na binafsi, pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali, umeonyesha mshikamano mkubwa unaolenga kuimarisha afya ya mifugo nchini.

Wafugaji wa mkoa wa Manyara wamejitokeza kwa wingi kuleta mifugo yao, ambapo zaidi ya wanyama 3,000 wamepewa huduma katika siku ya kwanza pekee. 

Mwitikio huu mkubwa ni ishara ya hamasa na uelewa unaoongezeka miongoni mwa jamii kuhusu umuhimu wa huduma za kitaalamu kwa mifugo. 

Wafugaji wameonyesha furaha na mshangao kwa namna huduma zilivyotolewa kwa umahiri na kwa hali ya juu.

Maadhimisho haya yamewezekana kutokana na ushirikiano thabiti kati6 ya Chama cha Madaktari wa Mifugo Tanzania (TVA) na serikali kupitia mamlaka za mikoa na wilaya. 

Ushirikiano huu umewezesha utekelezaji mzuri wa shughuli zote na kutoa matumaini ya kuendeleza juhudi hizi hata baada ya maadhimisho. 

Tukio hili limeacha alama muhimu katika sekta ya mifugo na limeweka msingi wa kuboresha afya ya wanyama kwa maendeleo ya taifa.


Share:

SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI BADO NI TISHIO LICHA YA JUHUDI ZA SERIKALI



Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Licha ya jitihada zinazoendelea kufanywa na serikali kupitia Wizara ya Afya na wadau mbalimbali, saratani ya mlango wa kizazi bado imeendelea kuwa tishio kubwa kwa afya ya wanawake nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 24, 2025 jijini Dodoma katika wiki ya chanjo kitaifa, Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa Chanjo, Lodalis Gadao, amesema saratani hiyo huanzia kwenye mlango wa kizazi – sehemu inayounganisha mfuko wa uzazi na uke – kutokana na seli kukua kwa kasi isiyo ya kawaida.

Takwimu kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonyesha kuwa takriban asilimia 36 ya vifo vinavyotokana na saratani nchini husababishwa na aina hii. Kila mwaka, zaidi ya wanawake 100,000 huambukizwa, huku zaidi ya 6,000 wakipoteza maisha.

Gadao ameeleza kuwa changamoto kubwa ni uelewa mdogo na mwitikio hafifu wa wanawake kujitokeza kwa uchunguzi na kupata chanjo ya HPV. Zaidi ya asilimia 70 ya wagonjwa hufika hospitalini wakiwa katika hatua za mwisho, hali inayopunguza mafanikio ya matibabu.

Ametaja wanawake wanaoishi na VVU na watoto wa kike wanaoanza ngono katika umri mdogo kuwa katika hatari kubwa zaidi ya kupata ugonjwa huo. Uchunguzi umebainisha kuwa kati ya wasichana wanne wanaojihusisha na mapenzi mapema, watatu huambukizwa.

Mikakati ya kudhibiti ugonjwa huo inahusisha utoaji wa chanjo kwa watoto wa kike kuanzia miaka 9 na kuelimisha jamii kuhusu madhara ya kuwa na wapenzi wengi.

Dk. Tumaini Haonga, Afisa wa Programu ya Elimu kwa Umma, alisema baadhi ya walengwa wanashindwa kupata chanjo kutokana na changamoto kama kuhama hama kwa wakulima na wafugaji, au wazazi wa mijini kukosa muda wa kuwapeleka watoto wao.

Wizara imehimiza jamii kushiriki kikamilifu katika kutoa elimu ya afya ya uzazi, na kuwasisitiza wanawake kufanyiwa uchunguzi mara kwa mara ili kugundua ugonjwa huo mapema na kupata tiba stahiki.








Share:

MAWAKILI WA SERIKALI TOENI USHAURI UNAOZINGATIA MASLAHI YA TAIFA


Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akizungumza kwa njia ya mtandao na waajiriwa wapya wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa mafunzo elekezi yaliyofanyika mkoa wa Pwani.

************

Mawakili wa Serikali wametakiwa kutoa ushauri wa kisheria unaozingatia maslahi mapana ya Serikali na Taifa ili kuiwezesha Serikali kuokoa fedha zitakazosaidia kukuza uchumi kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.

Wito huo umetolewa na Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi tarehe 24 Aprili 2025 wakati akizungumza na Mawakili wapya wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OWMS) kwenye mafunzo elekezi yaliyotolewa kwa watumishi hao yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani. ​

Akizungumza na Mawakili hao kwa njia ya mtandao, Dkt. Possi amesisitiza kuwa Mawakili wa Serikali wana jukumu la kutunza siri wakati wote wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku katika uendeshaji wa mashauri ya Serikali ili kulinda maslahi ya Serikali na kuleta heshima ya taaluma ya sheria nchini katika kuhakikisha kuwa Serikali inapata haki yake katika kila shauri linalofunguliwa dhidi yake au linalofunguliwa na Serikali dhidi ya watu wasio na nia njema na Serikali.

Dkt. Possi alieleza kuwa OWMS ina jukumu kubwa la kuendesha mashauri yote ya madai na usuluhishi kwa niaba ya Serikali. Hivyo ni muhimu kwa Mawakili wa Serikali kufahamu vyema utamaduni wa Ofisi hiyo, muundo wake na namna inavyotekeleza majukumu yake. Pia, amewasihi wajenge mahusiano mazuri na taasisi nyingine zinazoshirikiana na OWMS mathalani Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Mahakama.

Vile vile, amewataka wawe na utamaduni wa kufanya utafiti wa kina wa kisheria kabla ya kuendesha shauri lolote la madai au usuluhishi ili kuhakikisha haki inatendeka kwa kuwa utafiti unamuwezesha Wakili wa Serikali kujenga hoja imara, kuelewa mazingira ya kisheria na kujiandaa vizuri wakati wa usikilizwaji wa shauri.

Pia, amewasihi Mawakili hao kujenga tabia ya ​kujiendeleza kitaaluma ili waweze kuendesha mashauri ya madai na usuluhishi kwa weledi katika maeneo maalum ya sheria mathalani sheria za kimataifa zinazohusu mafuta na gesi na zinazovutia wawekezaji kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza nchini kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha, amewasisitiza wajiendeleze hasa katika mazingira ya sasa ambapo sheria zinabadilika kwa kasi kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia ili waweze kuwa na maarifa ya kisasa na ujuzi wa hali ya juu katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa kuzingatia maslahi ya umma.

Aidha, Dkt. Possi amewahimiza Mawakili wa Serikali kuwa na nidhamu ya kazi kwa kuwahi kazini; kujenga mahusiano mazuri na watumishi wenzao; na kuepuka kuwa kikwazo kwa wengine katika utekelezaji wa majukumu kwa kuwa ​kuwahi kazini na kuwa na nidhamu ni misingi muhimu kwa watumishi wa umma katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, kuboresha utendaji kazi kwa kujenga heshima, uaminifu na ushirikiano mzuri mahala pa kazi.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri na Udhibiti Ubora wa Ofisi hiyo, ndugu Camilius Ruhinda amesema kuwa Mawakili wa Serikali wapya wanapaswa kutambua kuwa wana jukumu kubwa la kuendesha na kusimamia mashauri ya madai na usuluhishi kwa mujibu wa sheria, weledi na kwa kuzingatia utii kwa mamlaka, pamoja na kuheshimu viongozi wao muda wote na mamlaka ya mahakama.

Ameongeza kuwa ni muhimu kwa Wakili wa Serikali kuwa na muonekano nadhifu wa mavazi na mwenendo unaoakisi taaluma ya sheria na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa ujumla.

Mafunzo hayo elekezi yamelenga kuwajengea uwezo Mawakili wa Serikali kuhusu namna Serikali inavyofanyakazi ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.
Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri na Udhibiti Ubora wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ndugu Camilius Ruhinda akizungumza na waajiriwa wapya wa Ofisi hiyo wakati wa mafunzo elekezi yaliyofanyika mkoani Pwani.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Masijala ya Sheria wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ndugu Dennice Leonard akizungumza na waajiriwa wapya wa Ofisi hiyo wakati wa mafunzo elekezi yaliyofanyika mkoani Pwani.
Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ndugu Ditrick Luambano akichangia mada wakati wa mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya wa Ofisi hiyo wakati wa mafunzo elekezi yaliyofanyika mkoani Pwani.
Watumishi Wapya wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza kwa njia ya mtandao Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi wakati wa mafunzo elekezi yaliyofanyika mkoani Pwani.
Baadhi ya watumishi wapya wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri na Udhibiti Ubora wa Ofisi hiyo, ndugu Camilius Ruhinda wakati wa mafunzo elekezi yaliyofanyika mkoani Pwani.
Share:

Thursday, 24 April 2025

DKT. JAFO: ZALISHENI MAFUTA YA KULA KWA WINGI KUKIDHI MAHITAJI



Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb), ametoa rai Wazalishaji wa ndani kuongeza uzalishaji wa mafuta ya kula ili kupunguza uagizwaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi, kwa lengo la kulinda viwanda vya ndani na ajira za Watanzania.

Vilevile Dkt. Jafo amebainisha kuwa Serikali iko tayari kuwasaidia wadau wanaotaka kuwekeza katika viwanda hususani viwanda vya uchakataji mafuta ya kula

Akizungumza wakati wa ziara yake katika Kiwanda cha Mafuta cha Sunshine kilichopo Zuzu Jijini Dodoma Aprili 23,2025, Dkt. Jafo amesema kuwa hakuna sababu kwa Watanzania kuendelea kutegemea mafuta kutoka nje ya nchi wakati uwezo wa kuzalisha upo.

"Watanzania sasa kuna kila sababu ya kujivunia vya kwetu. Tutumie bidhaa zetu. Tukizalisha kwa wingi tutakidhi mahitaji ya ndani na kupunguza matumizi ya fedha za kigeni ambazo zimekuwa zikitetemesha uchumi wa nchi," amesema Dkt. Jafo.

Vilevile Dkt. Jafo amebainisha kuwa Serikali imefanya uwekezaji kwenye kilimo cha mazao ya kuzalisha mafuta na kuwa ni imani yake kuwa muda mfupi ujao Tanzania haitakuwa na haja ya kuagiza mafuta ya kula kutoka nje.

Kwa upande wake, Afisa Biashara kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Amri Kibwana, aliwataka wakazi wa Mkoa huo kuendelea kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Naye Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Sunshine, Bw. Athumani Omary, aliiomba Serikali kuwalinda Wazalishaji wa ndani kwa kudhibiti uingizwaji wa mafuta kutoka nje, akisema hali hiyo inaathiri ukuaji wa viwanda vya ndani.

"Tunaomba Serikali ituangalie kama wazalishaji wa ndani. Uingizwaji wa mafuta kutoka nje unaua viwanda vya ndani na kupunguza ajira," amesema Omary.
Share:

Wednesday, 23 April 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI APRILI 24, 2025

Share:

Tuesday, 22 April 2025

MBINU YA KUSHINDA VITA VIKALI VYA KIBIASHARA!



Naitwa Juma Ally kutokea Same, katika maisha yangu nimekuja kuamini kuwa hakuna sehemu ambayo ina vita kali iliyojificha kama kwenye biashara maana watu wengi huwa wapendi kuona wenzao wanafanikiwa kimaisha. 

Kutokana na hilo watu hufanya kila njama kuhakikisha wanawashusha wenzao kibiashara, sasa baada ya kufanya tathimini na kujiridhisha kuwa sehemu nilipopanga naweza kufanya biashara, niliongea na mwenye nyumba na alinikubalia kufungua.

Iliniambia itabidi nilipie kodi pia, sikuwa na tatizo na hilo, nililipa na kuanza biashara, baada ya kufungua na kuona biashara inaanza kusimama, mtoto wa mwenye nyumba akaanza visa. 

Aliniambia pale nilipojenge kibanda changu cha kazi siku yoyote ataniambia nibomoe wajenge nyumba, nikamwambia sawa haina shida nitafanya hivyo siku ikiwadia, 

Miezi ilipita na biashara ikasimama, ikabidi niongeze kibanda cha pili, baada ya kuona vile, mtoto wa mwenye nyumba aliniambia nisijenge au kuongeza kitu kingine chochote. 

Natamani kuboresha na kufanya marekebisho mengi, ila nikifirilia naona nitazidisha wivu tu na baada itakuwa ugomvi. 

Maana kuna kipindi niliongeza friji na hiyo ikawa shida tena, kwa hiyo nikawa naafanya biashara hivyo hivyo, tatizo lilikuwa kwa wale watoto niliijua siku yoyote wakiamka vibaya, naweza kubomolewa kibanda changu cha biashara ingawa Baba yao hana shida kabisa.

Kuna mfanyabiashara mwenzangu aliniambia naweza kushinda vita hiyo kupitia kwa Kiwanga Doctors kutokea Migori nchini Kenya ambaye amekuwa akiwasaidia wafanyabiashara wengi Afrika Mashariki na Kati. 

Basi akanipatiwa mawasiliano yake ambayo ni +254 116469840, niliongea na akanihakikishia ndani ya siku tatu mambo yatakuwa mazuri baada ya kutupa uchawi wake na kunipa pete ya miujiza (magic ring) ambayo imenisaidia. 

Hazikupita siku watoto wa yule Baba wakaniruhusu nijenge kabisa, halafu nitakuwa nawalipa kidogo kidogo fedha ya ardhi yao hadi pale itakapokamlika. 

Ikiwa nawe anahitaji huduma kama hiyo, basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kupitia namba +254 116469840 au tembelea tovuti yao kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi. 

Share:

NIMEACHANA NA HUYU MWANAUME MAANA ANAOMBA SANA FEDHA!

Jina langu ni Naomi kutokea Lindi, nina umri wa mshangazi, yaani miaka 37, kuna kipindi nilikuwa natafuta mwanaume wa kuwa kama baba kwa ajili ya mtoto wangu maana nilikuwa nina mtoto mmoja. 

Huyu mtoto baba yake alifariki nikiwa mjamzito kwa hiyo hamjui hata baba yake. Kwa sasa ana umri wa miaka 6 na tayari ameana shule na ninashukuru anaendelea vizuri. 

Kuna muda nilimpata mwanaume ambaye nilihisi ananipenda kumbe alikuwa anataka pesa yangu, maana kila mara alikuwa  ananiomba hela sababu nilikuwa nafanya biashara ambayo kusema kweli kuna kitu nilikuwa napata. 

Yeye alikuwa ana kazi lakini hakuwa na hata senti ya kunipa, mwisho wa siku nikaona ananinyonya  na alikuwa akiniomba pesa nikimwambia sina basi atanunua hadi nimpe kitu ambacho kinanikera sana

Katika kuperuzi katika mitandao ya kijamii ndipo nikakutana na huduma ya Kiwanga Doctors kutokea Migori nchini Kenya, huyu alinifanyia dawa ya kuwa na mvuto wa mapenzi hasa upande wa ndoa (marriage spell) maana ndio hasa nilikuwa nahiitaji.

Mwisho wa siku nilipata mwanaume mtu mzima kidogo na akakubali kuishi na mimi bila wasiwasi wowote na sasa tunaendelea vizuri na tayari tumejaliwa kupata mtoto mmoja. 

Ikiwa unapitia kitu kama hicho, ninakushauri kuwa fika au wasiliana na Kiwanga Doctors. Tiba zao zinafanya kazi haraka na wanaweza kukusaidia katika changamoto mbalimbali za kimaisha, kuanzia masuala ya uhusiano hadi matatizo ya kiafya. 

Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kupitia namba +254 116469840 au tembelea tovuti yao kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi. 



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger