Tuesday, 8 April 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRILI 8,2025



Magazeti ya leo







Share:

Monday, 7 April 2025

MKOA WA LINDI WAKO TAYARI KUUPOKEA MWENGE WA UHURU 2025

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack akikagua Jengo la kituo cha Polisi Nandagala Mkoani Lindi

Na Regina Ndumbaro- Lindi

Mkoa wa Lindi uko tayari kuupokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2025, ambapo maandalizi mbalimbali yamekamilika ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa miradi itakayopitiwa na mbio hizo muhimu za kitaifa. 

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack, ametembelea na kukagua miradi inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge huo wilayani Ruangwa, ambapo ameonesha kuridhishwa na maendeleo na utekelezaji wake.

Katika ukaguzi huo, Mhe. Telack ametembelea mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwilahi katika Kijiji cha Likangara yenye urefu wa mita 650, mradi unaogharimu zaidi ya Shilingi Milioni 513. 

Aidha, amekagua mradi wa dampo salama unaotekelezwa na kikundi cha vijana wa usafi wa mazingira katika Kijiji cha Lipande wenye thamani ya Shilingi Milioni 15. 

Mradi mwingine ni ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja katika Shule ya Msingi Dodoma, Kata ya Nachingwea, wenye thamani ya Shilingi Milioni 48.

Miradi mingine mikubwa inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru ni pamoja na mradi wa maji katika Kijiji cha Mpara, Kata ya Likunja, unaojumuisha uchimbaji wa visima na ujenzi wa miundombinu ya maji kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Milioni 325. 

Vilevile, Mwenge utatembelea ujenzi wa Kituo cha Polisi Nandagala chenye thamani ya Shilingi Milioni 164 na Kituo cha Afya Namakuku, ambapo Mwenge utaweka jiwe la msingi kwenye jengo la OPD lenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 153.

Aidha, Mwenge wa Uhuru pia utaweka jiwe la msingi kwenye mradi mkubwa wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Namakuku, mradi unaogharimu zaidi ya Shilingi Milioni 591.

 Hii ni ishara ya dhamira ya Mkoa wa Lindi ya kuboresha huduma za kijamii kama elimu, afya, usalama na mazingira kwa manufaa ya wananchi wake.

Kwa mujibu wa ratiba rasmi, Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa Mei 28, 2025 katika Kijiji cha Namichiga, ambapo utapitia miradi yote iliyotajwa na hatimaye kukesha katika Kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa. 

Mkoa wa Lindi unaendelea kujiandaa kikamilifu kuhakikisha tukio hilo linafanyika kwa mafanikio makubwa.  


Jengo la Kituo cha Polisi Nandagala ambacho ni miongoni mwa miradi iliyokaguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack akiwa na baadhi ya viongozi Mkoani Lindi wakati wa Ukaguzi wa miradi mbalimbali na maandalizi ya kuupokea Mwenge tarehe 28 March Mwaka huu
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack akiwa anatembea kwaajili ya kukagua miradi kwa ukaribisho na maandalizi ya Mwenge wa uhuru Mkoani Lindi
Share:

HABARI NJEMA KWA WANAOSUMBULIWA NA UGONJWA WA KISUKARI


Unajua kutokana na mtindo wa maisha kwa dunia ya sasa ulioletwa na mageuzi ya viwanda, watu wengi wamekuwa wakikumbwa na magonjwa mbalimbali kama kisukari ingawa kuna wengine huwa wanarithi ugonjwa huo.

Jina langu ni Emmy, ni binti wa miaka 22, ninaishi na Bibi yangu Kakameganchini Kenya, mwanzoni mwa mwaka 2019 Bibi yangu alianza kuumwa, sikuweza kujua ni kitu gani hasa kinamsumbua Mzee huyo ambaye nilikuwa namtunza.

Nilimpeka hospitali ambayo ipo eneno la jirani, baada ya kufanyiwa vipimo na uchunguzi wa kina, Bibi akagundulika kuwa ana ugonjwa kisukari, binafsi mwenyewe sikuweza kutarajia ugonjwa huo!.

Pale hospitali tulipewa dawa na Bibi akaanza kuzitumia, nilikuwa na matumaini mengi kuwa siku sio nyingi ataanza kupata nafuhu, huku mimi nikiendelea na kazi zangu za kila siku za kuniingizia kipato ambacho kitaniwezesha kuendesha familia hii.

Hata hivyo, Bibi hakuweza kupata nafuhu au kupona kwa muda ambao nilidhani ambao ndio alikuwa anamalizia dawa zake, tuliamua kwenda Hospitali nyingine ya kisasa zaidi kupata huduma ya kukabiliana na maradhi hayo.

Huko nako alipewa aina tofauti ya dawa  ambazo mwanzo zilionekana kufanya kazi na kuwa na mategemeo kuwa siku za usoni atapona kabisa na kurejea katika hali yake ya kawaida ambayo tulimzoea nayo siku zote.

Siku zilienda Bibi akiendelea kuumwa, baadhi ya watu ambao niliwaeleza kuhusu kuumwa kwa Bibi yangu, walinishauri nijaribu kutafuta dawa za mitishamba ambazo zimekuwa zikiwasaidia watu wengi.

Huu ni ushauri ambao mpenzi wangu James alinipa, licha ya wasiwasi wangu kuhusu tiba asilia, aliendelea kunisisitiza kuchukua hatua hiyo, kutokana nilikuwa namwamini kwa jinsi ambavyo amekuwa akifanya mambo yake, nilikubali wazo lake.

"Unajua Emmy hili jambo ambalo nimekuambia nina uhakika nalo kwa asilimia 100, ebu soma tovuti ya Kiwanga Doctors(www.kiwangadoctors.com), utaona jinsi ambavyo watu wengi wamepona kupitia tiba zake," aliniambia James.

Basi nikasoma katika tovuti ile na kujiridhisha, huku pia nikachuka namba ya Kiwanga Doctors ndipo nikawasiliana naye na kumueleza shida hiyo ya Bibi yangu na yeye mara moja aliweza kunitumia dawa ambazo zimeleta tabasamu usoni kwake.

Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +254 116469840 au tembelea tovuti yao, www.kiwangadoctors.co.tz kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi.  

Share:

Sunday, 6 April 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 7, 2025


Magazeti













Share:

DAWA ZA URAIBU MBAYA

Jina langu ni Abel kutokea Mbozi, ni kwenye uhusiano kwa miaka sita na mpenzi wangu, Nadia, hadi sasa naona tupo pamoja naamini hakuna kitu ambacho kitakuja kutuachanisha kutokana tumepitia changamoto nyingi na kuzishinda.

Nakumbuka miongoni mwa changamoto hizo ni mpenzi wangu kuwa na urahibu wa dawa za kulevya, alijikuta katika janga hilo kwa bahati mbaya kutokana na aina ya marafiki aliokuwa nao.

Wakati wa Wekiendi walipokuwa wanatoka kwa ajili ya starehe, rafiki zake walikuwa wanatumia dawa hizo, hivyo walitumia ujanja wakawa wanamchanganyia kwenye kinywaji hadi akawa na urahibu wa dawa hizo hatari.

Kuna wakati aliharibikiwa sana hadi akawa anachukua vitu vyangu ndani anaenda kuuza ili apate fedha ya kwenda kununua dawa na kukata kiu yake kwa wakati huo.

Nilijaribu kumpelekea kituo cha kulea watu wenye urahibu wa dawa za kulevya lakini baada wiki moja alitoroka huko na kurejea nyumbani.

Tatizo mimi nilikuwa sishindi nyumbani kutokana na kazi yangu, ndugu zake wote wapo kijijini, hivyo mzigo wote ukabaki kuwa wangu, nilijaribu kupita huko na kule kuomba msaada ili aweze kuachana na dawa hizo bila mafanikio.

Ilifikia wakati nikakataa kabisa mazoea na yeye nikataka kuachana naye, lakini kila ambavyo nikifikiria jinsi mimi na yeye tumetoka mbali ndivyo ambavyo roho yangu ilikuwa inazidi kuuma na ukizingatia amejipata katika hali hiyo bila yeye mwenyewe kupenda.

Baada ya kuzunguka sana, niliweza kukutana na tovuti ya Kiwanga Doctors kutokea Migori, Kenya hapa alieleza kuwa anaweza kumsaidia mtu aliyeathirika na matumizi ya dawa za kulevya na kuweza kuachana nazo kabisa.

Nilichukua namba yake na kumpigia, katika mazungumzo yetu ya muda mfupi, Kiwanga Doctors alinihakikishia kuwa Nadia atapona kabisa kutoka kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

Niliendelea kugonjea hilo kutokea kwani ni kitu ambacho nilikitamani sana kukiona kutokana nilimpenda sana mpenzi wangu na sikuwa tayari kumpoteza kivyovyote vile na isitoshe tulikuwa na mipango mengi ya mbeleni.

Basi taratibu Nadia alianza kurejea kwenye hali yake ya kawaida na kuwa mwanamke mzuri kama hapo awali alivyokuwa had nikaamua kuwa naye na kumpa nafasi katika moyo wangu.

Hadi sasa mpenzi wangu amefanikiwa kuachana na matumizi ya dawa za kulevya hadi baadhi ya rafiki zake ambao walipitia kipindi kama chake wanashangaa amewezaje kwa muda mfupi hivyo.

Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +254 116469840 au tembelea tovuti yao, www.kiwangadoctors.co.tz kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi. 

Share:

VIONGOZI WA MIKOA NA WILAYA WAAGIZWA KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI MBIO ZA MWENGE


OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika Mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka 2025, ambazo zinalenga kuchochea utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuleta maendeleo nchini.

Ametoa agizo hilo akiwa katika Shule ya Msingi Ukombozi, Ikwiriri, kabla ya kumkaribisha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa, Ismail Ussi, kuzungumza na wananchi waliokusanyika kushuhudia uraghabishaji wa falsafa ya Mwenge wa Uhuru uliofanywa na wanafunzi wa shule hiyo.

Mhe. Mchengerwa amesisitiza kuwa atahakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu kwenye maeneo yote ambayo Mwenge wa Uhuru utapita kukagua miradi ya maendeleo na kuwaelekeza Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanahamasisha wananchi kwa nguvu zote kushiriki shughuli hizo muhimu.

“Mbio za Mwenge zinahamasisha maendeleo, na ndio maana zinaambatana na uzinduzi wa miradi ya kimkakati ya maendeleo. Ushiriki wa wananchi ni fursa muhimu ya kuwajengea uelewa katika usimamizi na utekelezaji wa miradi hiyo,” amesema Waziri Mchengerwa.

Aidha, Waziri Mchengerwa amemweleza Kiongozi wa Mbio za Mwenge Taifa, kuwa Wilaya ya Rufiji imepiga hatua kubwa katika miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule, barabara, masoko, vituo vya afya na zahanati, miradi ambayo baadhi yake itakaguliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu.

Kwa upande wake, Ismail Ussi amesema kila Mtanzania anapaswa kuienzi falsafa ya Baba wa Taifa, akisisitiza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendeleza falsafa hiyo kwa kumkabidhi jukumu la kuongoza Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, ambapo miradi ya maendeleo itakaguliwa na kuzinduliwa pale itakapobainika kutekelezwa kwa viwango stahiki.
Share:

Saturday, 5 April 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 5,2025


Magazeti






Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger