Saturday, 5 April 2025

Picha : MKUTANO MKUU WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA 'SPC' 2025

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club -SPC) imefanya Mkutano Mkuu wake leo Jumamosi Aprili 5, 2025 ukihudhuriwa na wanachama viongozi wa vyombo vya habari na wageni waalikwa.

Katika mkutano huo, masuala ya uendeshaji wa klabu, tathmini ya mwaka uliopita na mipango ya maendeleo ya mwaka huu yanajadiliwa kwa kina lengo likiwa ni kuimarisha mshikamano na malengo ya kulinda maslahi ya wanahabari mkoani Shinyanga. 

Picha zote na Kadama Malunde

Share:

TUME YA MADINI KUENDELEA KUWASAIDIA WASAMBAZAJI NA WAUZAJI BARUTI




Tume ya Madini imesema itaendelea kutoa ushirikiano na kuwasaidia wasambazaji na wauzaji wa baruti nchini ili wafanye shughuli zao kwa mujibu wa Sheria na kanuni za baruti zilizopo.

Mkaguzi Mkuu wa Migodi Mhandisi Hamisi Kamando amesema hayo ,Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi kilichowakutanisha wadau wa baruti, pamoja na Wakaguzi wa Migodi na Baruti Nchini.

Mhandisi Kamando amesema kutokana na ongezeko la shughuli za uchimbaji wa madini kumepelekea kupanuka kwa biashara ya baruti hapa nchini.

“Ongezeko la uhitaji wa matumizi ya baruti hapa nchini imepelekea uwepo wa changamoto kadhaa katika usimamizi wake,hivyo watumishi wa Idara ya Ukaguzi wa Migodi na Mazingira kutoka Tume ya madini wataendelea na udhibiti katika maeneo yao ili kuepusha madhara,amesema.

Ametoa wito kwa wadau wa baruti nchini kujiunga katika Chama Cha Wauza Baruti Tanzania (TEDA), ili Serikali iweze kuwasaidia kwa pamoja.

Mdau wa Baruti kutoka Mkoa wa Geita Mhandisi Ramadhani Kamaka ameeleza kunufaishwa na kikao hicho na kuiomba Serikali kutoa elimu zaidi kwa mamlaka ambazo zinahusika katika usimamizi wa baruti nchini.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger