Sunday, 12 January 2025
KIRUSWA AWATAKA MALAIGWANANI KUKEMEA TABIA YA JAMII HIYO KATIKA CHAGUZI
SIMBACHAWENE ATANGAZA UTARATIBU MPYA USAILI WA KADA ZA UALIMU KUANZIA JANUARI 14 HADI FEBRUARI 24
Saturday, 11 January 2025
WAZIRI JAFO ATINGA ENGARUKA KUTANGAZA NEEMA KUTOKA KWA RAIS SAMIA

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo Januari 10,2025 katika Kata ya Engaruka wilayani Monduli.
Na.Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo,amesema Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 14.48 kwa ajili ya ulipaji wa fidia katika mradi wa magadi soda wa Engaruka ambapo shilingi billion 6.2 zitatumika katika ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha mradi huo.
Waziri Jafo,ameyasema hayo leo Januari 10,2025 wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Engaruka wilayani Monduli.
Amesema kuwa wananchi 595 kutoka vijiji vinne vya Engaruka Chini, Mbaash, Idonyonado na Irerendeni watanufaika na fidia hiyo ya shilingi bilioni 6.2 huku fedha zingine zilizobaki zikienda katika shughuli mbalimbali za miradi mbalimbali ya huduma za kijamii.
Katika mkutano huo, Dkt. Jafo amewapa habari njema wananchi wa Kata hiyo ya Engaruka kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ameshatoa pesa za kuwalipa fidia wananchi hao watakaopisha mradi.
"Mradi huo tayari umetangazwa kwa lengo la kutafuta wawekezaji ambapo hadi sasa Makampuni kadhaa tayari wameonyesha nia ya kuwekeza kwenye mradi huu".amesema Dkt.Jafo
Aidha Dkt. Jafo amesema fedha hizo zimetolewa na Serikali ikiwa ni mkakati wa kuendeleza miradi ya kimkakati yenye tija kwa Taifa.
Dkt. Jafo mradi huo ni muhimu sana kwa uchumi wa Taifa kwani Viwanda vingi nchini vinatumia magadi soda kama malighafi muhimu vikiwemo viwanda vya kutengeneza vioo, sabuni, nguo, nk.
Aidha, Dkt. Jafo amesema kwamba mradi huo utasaidia sana kuokoa matumizi ya fedha za kigeni ambazo kwasasa zinatumia kuagiza Magadi soda kutoka nje ya nchi.
Katika kuweka msisitozo, Jafo amewashauri wananchi hao kuanza kufikiria kujenga hotel na nyumba za kulala Wageni na kubuni biashara mbalimbali za huduma kwani eneo hilo litafikiwa na wageni wengi wanaokuja kufanya kazi katika viwanda vitakavyojengwa eneo hilo.
Naye Naibu Waziri wa Madini, Mhe.Dkt.Stephen Kiruswa amesema mradi huo uwe ni chimbuko la mafanikio kwa wananchi wa wilaya ya Monduli na Longido kwani mradi huu ni mkubwa na unatija Kwa wananchi.
SERIKALI YASISITIZA UMUHIMU WA MAFUNZO YA UFUATILIAJI NA TATHIMINI KWA MAENDELEO YA MIRADI YA SERIKALI
Friday, 10 January 2025
WAZIRI BASHUNGWA AZINDUA MIKAKATI SITA YA MAWASILIANO KUONGEZA TIJA KWENYE UTENDAJI KAZI
Na Dotto Kwilasa, Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Innocent Bashungwa amewaelekeza wasemaji wa vyombo vya usalama na wakuu wa vitengo vya habari na mahusiano kufanya tathmini ya pamoja ya utendaji kazi wa vitengo vya habari katika Wizara na vitengo vyake vya usalama kwa kuzingatia mpango kazi unaosomana.
Bashungwa ameeleza hayo Januari 9,2025 Jijini Dodoma wakati akizindua mikakati Sita itakayotekelezwa ili kuweze kutimiza lengo na kuimarisha nguvu za kiutendaji na kueleza kuwa kuzinduliwa kwa mikakati hiyo kunapaswa kuwa chachu ya kuitekeleza kwa ufanisi ili ilete tija kwa Wizara kwani itasaida kuimarisha suala la Mawasiliano kwa umma.
"Hakikishe kuwa vitengo vyetu vya habari vinatengewa bajeti ili viweze kutelekeza mikakati hii ya mawasiliano kwani inaleta tija na mabadiliko chanya kwenye kuwahudumia watanzania,"amesema.
Amesema miongoni mwa malengo ya kuangaliwa kwenye mikakati hiyo ya mawasiliano ni kuongeza uelewa na ushiriki wa jamii kwenye kuimarisha usalama wa raia na mali zao sambamba na utunzaji wa amani na utulivu wa nchi.
Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo amewahasa washirki kikao kazi cha mwaka cha wasemaji wa vyombo vya usalama na maafisa habari, Mawasiliano na uhusiano wa Wizara hiyo kutumia jukaa hilo kijtathmini walipotoka, walipo na wanakoeleea ili kwa pamoja waweze kupata uzoefu ambao utasaidia kuimarisha sekta ya habari kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ally Gugu amesena mikakati hiyo inasaidia kuboresha upatikanaji wa habari ambayo ndiyo lengo la Serikali ya awamu ya sita ili kuiwezesha jamii kupata taarifa kwa wakati ambapo ni mapendekezo ya tume ya haki jinai.
"Katika kutekeleza maelekezo ya Serikali Wizara yetu imeanza na uandaaji wa mikakati hii ya mawasiliano ambayo imezinduliwa leo na baada ya hapo tutaenda kuitekeleza kwa vitendo na kwakuwa zipo shughuli mbalimbali ambazo zimepangwa kutekelezwa kwa miaka miwili na baada ya hapo tumepanga kufanya mapitio ili kuona hatua mbalimbali za utekelezaji wa mikakati hiyo, "amesema.
Awali akitoa taarifa kuhusu mikakati hiyo Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Christina Mwangosi amesema mikakati hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia miongozo ya Wizara, vyombo ya usalama pamoja na mkataba wahuduma kwa wateja.
"Mikakato hii ni ya miaka mwili na baada ya hapo tutafanya tathmini ya matokeo yatakayokuwa yamepatikana na ndipo tutaanza tena mikakati mingine kulingana na matokeo yatakayokuwa yamepatikana,"amesema.
Hata hivyo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imezindua Mikakati Sita ya mawasiliano yenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa urahisi kwenda kwa wananchi.
USIKU WA WADAU SHUPAVU SHINYANGA KUKUTANISHA VIONGOZI NA WADAU MASHUHURI

HolySmile Chini ya Mkurugenzi wake Arnold Bweichum inawaletea hafla ya kipekee inayokusanya wadau mashuhuri kutoka sekta mbalimbali – viongozi wa serikali, wawekezaji, wajasiriamali, wasanii, na wanaharakati wa maendeleo Usiku wa Wadau Shinyanga! Hii ni fursa adhimu ya kusherehekea juhudi na mafanikio ya wale walio mstari wa mbele kuboresha maisha ya wakazi wa Shinyanga.
📅 Tarehe: 1 Februari 2025
📍 Mahali: Ukumbi wa Makindo, Shinyanga
⏰ Saa: 12:00 jioni – 6:00 usiku
Hafla hii itakuwa na hadhi ya kipekee na kuwakutanisha watu mashuhuri wa kada na idara zote – sekta ya afya, elimu, kilimo, biashara, teknolojia, utalii, na sanaa.
Kutakuwa na;
1. Tuzo za Heshima na Pongezi: Kuwatambua na kuwapongeza wadau shupavu kwa mchango wao mkubwa.
2. Mahusiano ya Kibiashara (Networking): Kukutana na kushirikiana na watu wa maana kwa maendeleo binafsi na ya jamii.
3. Chakula cha jioni na burudani za kiwango cha juu: Furahia usiku wa heshima na burudani za kipekee kutoka kwa wasanii maarufu.
4. Nafasi ya kutangaza chapa yako: Weka chapa yako mbele ya viongozi na mashujaa wa maendeleo.
KIINGILIO
1. VIP Single: TZS 50,000
2. VVIP Single: TZS 100,000
3. Meza ya VVIP (Watu 5): TZS 500,000
4. Meza ya VVIP (Watu 12): TZS 1,000,000
NJIA ZA MALIPO:
✅ Voda Lipa Namba: 57845152
✅ Akaunti ya NMB: 30610057561
(Jina: HOLYSMILE)
MAWASILIANO
📞 Simu: 0756254146
Hii ni nafasi yako kushiriki tukio kubwa la kihistoria, lenye heshima na hadhi ya dhahabu. HolySmile, chini ya uratibu wangu kama Mkurugenzi, inahakikisha tukio hili linakuwa alama ya kumbukumbu kwa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla.
Tukutane Usiku wa Wadau Shinyanga – mahali ambapo heshima, mshikamano, na maendeleo vinakutana!













































