Mawaziri wa Jumuiya ya Madola wameipongeza Tanzania kwa juhudi zake za kuendeleza mazungumzo kama njia ya kujenga maridhiano, kuimarisha demokrasia na kudumisha amani. Aidha, Jumuiya imeendelea kuhimiza wadau kuzingatia mazungumzo ya maridhiano kama nyenzo muhimu ya kutatua tofauti na kuimarisha mshikamano wa kitaifa.
Kutokana na umuhimu wa ujumbe huo, inapendekezwa kufanyika mkutano na waandishi wa habari ili kuufafanua na kuuhabarisha umma kuhusu utayari wa Jumuiya ya Madola kushirikiana na Serikali na wadau kuhakikisha mazungumzo tofauti na propaganda ambazo zinaenezwa na wanaharakati ambayo inaonesha kana kwamba serikali imeshinikizwa
Kwa hiyo pendekezo ni kwamba kwenye press conference msisitizo utakuwa ni namna gani Jumuiya ya Madola inasukuma roho ya mazungumzo na maridhiano na jinsi gani Jumuiya inatambua juhudi mfano za Tume ya Uchunguzi ya Jaji CHANDE...kuhusu uchunguzi wa masuala ya jinai na hivyo kuondoa propaganda kwamba hakuna juhudi zozote zile

0 comments:
Post a Comment