Monday, 22 August 2022
Sunday, 21 August 2022
MAFUNZO KWA WATAALAM TCRA YANA UMUHIMU KATIKA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA - DK.MOHAMED
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dk. Khalid Salum Mohamed akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakati Waziri huyo alipotembelea Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk.Emmanuel Manase akizungumza hali ya mawasiliano na Jiographia Zanzibar katika Mawasiliano walivyoweza kutoa wakati ziara ya Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dk.Khalid Salum Mohamed alipotembelea Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dk.Jabir Bakari akizungumza kuhusiana na mikakati ya TCRA katika kutoa huduma bora kwa pande zote kwa Tanzania Bara na Zanzibar kwenye sekta ya mawasiliano kwenye kikao kazi cha Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dk.Khalid Salum Mohamed wakati alipotembelea Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dk.Jabir Bakari akizungumza kuhusiana na mikakati ya TCRA katika kutoa huduma bora kwa pande zote kwa Tanzania Bara na Zanzibar kwenye sekta ya mawasiliano kwenye kikao kazi cha Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dk.Khalid Salum Mohamed wakati alipotembelea Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.****************************
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk Khalid Salum Mohamed amesema kuwa katika kwenda na mabadiliko ya Teknolojia ni kazi kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni kuwekeza kuwaongezea utaalamu wa viwango vya kimataifa wafanyakazi katika kudhibiti makosa ya usalama mtandaoni.
Akizungumza wakati alipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, Dk Mohamed amesema teknolojia imekuwa ikibadilika kwa kasi na kusababisha changamoto nyingi zinazoikabili sekta ya mawasiliano ikiwemo makosa ya usalama mtandaoni wa watumiaji wa mwisho.
Amesema ili kudhibiti makosa hayo, ni lazima TCRA kuwekeza kwenye kuwapatia mafunzo ya kitaalamu yanayokubalika kimataifa katika kudhibiti makosa hayo na kupunguza hasara katika nchi kwani teknolojia ina faida na hasara
"Ni muhimu jamii kuelimishwa zaidi kuhusu majanga ya kimtandao ambayo yamekuwa yakihatarisha usalama wa nchi na mifumo ya mawasiliano Tanzania Bara ikiharibika, maana yake mawasiliano ya Jamuhuri ya Muungano yameharibiwa na kujenga kwake ni gharama inayotokana na watalaam kupewa mafunzi yasiyotarajiwa" amesema Dk Mohamed.
Pia alieleza kuwa mamlaka hiyo inatarajia kuingia mkataba wa makubaliano na Shirika la Viwango Zanzibar (ZBS) kwa ajili ya ukaguzi wa vifaa vya mawasiliano vinavyoingia kutoka nje ya nchi katika kudhibiti bidhaa za mawasiliano.
Aliongeza kuwa TCRA kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) zimejenga minara 42 ya mawasiliano katika visiwa vyote 42 hivyo imesaidia kuondoa changamoto ya mawasiliano kwa wakazi wa maeneo hayo.
"Muendelee kushirikiana katika kuboresha ustawi wa sekta ya mawasiliano kwa sababu ni ya muungano hivyo rasilimali zilizopo zitumike kustawisha jamii kwa kujenga uchumi imara na kuleta maendeleo. Pia mnapaswa kuona namna ya kutekeleza sera ya uchumi wa buluu katika kuhakikisha wananchi wote wanapata mawasiliano bora," alisisitiza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TCRA, Dk Jabir Bakari alisema kuwa wataendelea kuhakikisha wanatoa ushauri wa kitaalamu kwa kampuni za simu ili kutoa huduma bora za mawasiliano.
Pia amesema kuwa yapo maeneo mawili ya muungano ambayo mamlaka hiyo huyashughulikia ikiwemo mawasiliano na posta ambayo yanatakiwa kutoa matokeo chanya katika uchumi wa buluu na uchumi wa kidigitali.
"Tutafanyia kazi maelekezo tuliyopewa ya kuhakikisha Zanzibar inakuwa na huduma bora za mawasiliano katika visiwa vyote vidogovidogo," alisema Dk Bakari.
RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA MREMA
.jpg)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametuma Salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mwanasiasa Mkongwe nchini Tanzania, Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) ambaye amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Aminieli Eligaisha amesema, Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16,2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo Jumapili Agosti 21,2022 saa 12: 15.
"Nitamkumbuka kwa mchango wake katika mageuzi ya siasa, uzalendo na upendo kwa Watanzania. Pole kwa familia na wana TLP. Mungu amweke mahali pema.Amina" Amesema Rais Samia
Tanzia : MWANASIASA MKONGWE AUGUSTINO LYATONGA MREMA AFARIKI DUNIA
Mwanasiasa Mkongwe nchini Tanzania, Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Aminieli Eligaisha amesema, Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16,2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo Jumapili Agosti 21,2022 saa 12: 15.
Mrema alizaliwa Desemba 31, 1944, Vunjo mkoani Kilimanjaro na amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, mgombea Urais kupitia NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na amewahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.
MREMBO AFARIKI KWA KUZAMA SWIMMING POOL AKIJIREKODI LIVE FACEBOOK

Mrembo Hellen Wendy aliyefia kwenye swimming pool nchini Canada
**
MREMBO raia wa Kenya aliyekuwa akifanya kazi ya uuguzi nchini Canada, Hellen Wendy amefariki dunia baada ya kuzama wakati akiwa anaogelea kwenye ‘swimming pool’.
Kabla hajafikwa na umauti, Hellen alikuwa akijirekodi ‘live video’ kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, ambapo anaonekana kwenye video hiyo, akiwa anazungumza na marafiki zake kwenye mtandao huo.
Akiwa anaendelea kufurahi na marafiki zake huku akiogelea, ghafla Hellen alionekana akianza kutapatapa kwenye maji na akasikika akipiga mayowe ya kuomba msaada, kisha akazama.
Video aliyokuwa ameianzisha Facebook, iliendelea kuwa kwa takribani saa 3, huku ikionesha kwamba alifariki dunia dakika 10 au dakika ya 11 tangu alipoanza kurekodi video hiyo.
Saturday, 20 August 2022
DC JOKATE AHAMASISHA WANANCHI TEMEKE KUJITOKEZA KUHESABIWA
Wananchi wa Wilaya ya Temeke waliojitokeza kwenye Bonanza la hitimisho la hamasa ya Sensa ya watu na Makazi lililofanyika katika viwanja vya Zakiem Mbagala Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwegelo akiongoza matembezi maalumu katika kuhamasisha sensa ya makazi na watu leo katika viwanja vya Zakiem Mbagala Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe Jokate Mwegelo katikati akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Ndg. Ndg. Elihuruma Mabelya ( Kulia ) na Mbunge wa Jimbo la Mbagala Mhe. Abdallah Chaurembo ( Kushoto ) wakiwa kwenye Bonanza maalum la kuhamasisha Sensa ya Watu na Makazi.
Wananchi wa Wilaya ya Temeke waliojitokeza kwenye Bonanza la hitimisho la hamasa ya Sensa ya watu na Makazi lililofanyika katika viwanja vya Zakiem Mbagala Jijini Dar es Salaam**********************
NA MWANDISHI WETU
Katika kuelekea siku ya Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23,2022, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwegelo amewahamasisha Wananchi wa Wilaya hiyo kujitokeza na kushiriki kwa wingi ili kuipatia fursa serikali kuweka mikakati muhimu katika Taifa.
“Hiyo ni siku ya mapumziko mahususi kutoa nafasi kwa Wananchi wote kuweza kushiriki bila kuwa na sabbabu zingine kwenye zoezi hili la sensa” amesema DC Jokate
“Nawaomba Wananchi wenzangu wa Temeke tume watulivu, tuonyeshe ushirikiano kwa Makarani watakaofika kwenye maeneo yetu” amesema DC Jokate
Amesema hayo leo kwenye Bonaza kutwa lililofanyika katika viwanja vya Zakhiem Mbagala vilivyopo katika wilaya hua Temeke na kuhudhuriwa na Viongozi Mbalimbali wakiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Naibu Meya na Madiwani wa wilaya hiyo na Baadhi ya Wasanii wa Bongo Fleva Juma Nature, Yamato Band na wengineo.
Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Ndg. Elihuruma Mabelya amezidi kuwasisitizia Wananchi wa wilaya hiyo kuwaitiske zoezi la Sensa ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
“Zoezi la Sensa ni muhimu, hamasa imefanyika na leo ni hitimisho la hamasa ambayo Mkuu wetu wa Wilaya ameifanya Usiku na mchana. Wilaya yetu ina mitaa 142 na kata 23 ambayo inahitaji maendeleo” amesema Mabelya.
Tukumbuke siku ya Tarehe 23 mwezi huu wa nane mwaka 2022 itakuwa sensa ya makati na watu itakayofanyika Nchi nzima na siku hiyo itakuwa ni siku ya mapumziko kitaifa.
AL SHABAB WAUA WATU 10

Mamlaka nchini Somalia zinasema kuwa takribani watu 10 wameuawa baada ya kundi la al-Shabab kuvamia hoteli moja iliyopo katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.
Polisi wamesema kuwa washambuliaji hao walitega mabomu mawili nje ya hoteli hiyo kabla ya kuingia ndani na kuanza kufyatua risasi.
Kikosi maalum cha polisi kimesema kuwa kilifanikiwa kuwaokoa makumi ya wageni na wafanyakazi waliokua kwenye hoteli hiyo ya Hayat.
Mmoja wa maafisa hao aitwae Mohamed Abdikadir amesema kuwa "Vikosi vya usalama vimeendelea kupambana na vikosi hivi vya kigaidi , tumefanikiwa kuokoa watu wengi ila tuna taarifa za raia wa8 kupoteza maisha mpaka sasa".
Tovuti moja inayohusiana na Al-Shabab ilithibitisha kundi hilo kufanya uhalifu huo
JAMBO ATUA DODOMA KUNUNUA ZABIBU

Kampuni ya Jambo Food Products ya Mjini Shinyanga jana imeanza kununua zabibu kutoka kwa wakulima katika maeneo mbalimbali mkoani Dodoma ikiwa ni siku chache baada ya tamko la Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Mohamed Bashe alililotoa wakati akijibu changamoto za wakulima wa zabibu walizowasilisha mbele ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan aliposimama kuwasilimia eneo la Mpunguzi,Jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Ndg. Emmanuel Ngusa amewahakikishia wakulima wa zabibu wa Mkoani Dodoma juu ya nia na dhamira ya Kampuni ya Jambo kuendelea kuwa soko la uhakika la zabibu baada kujiridhisha ubora.
Zoezi la ununuaji wa zabibu katika mashamba ya Mpunguzi,Handali na Hombolo limeshuhudiwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Anthony Peter Mavunde


DK. KALEMANI: TUJITOKEZE KUHESABIWA KWA AJILI YA MAENDELEO
MBUNGE wa Jimbo la Chato,Dk. Medard Kalemani amewataka wananchi kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi Agosti 23,2022.
Kauli hiyo ameitoa leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya zamani vya stendi ya zamani ya Chato wakati akiwahamasisha wananchi kuhesabiwa.
Aidha amedai kufahamika kwa idadi ya watu na makazi yao itasaidia serikali kupanga maendeleo toshelevu kwa jamii.
"Ninawahamasisha ndugu zangu tujitokeze kuhesabiwa kwa ajili ya maendeleo...tunataka kuonyesha kuwa Chato tuko wengi ", amesema Dk. Kalemani.
Kadhalika amewataka kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali kusogeza maendeleo kwa wananchi hali itakayosaidia wananchi kujiletea maendeleo kwa wakati.
"Jambo la kwanza niwaombe sana mjitokeza kuhesabiwa...pili kuunga mkono juhudi za serikali...tatu kushikamana na mwisho ni kuchapa kazi kwa bidii"amesema.
Hata hivyo amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Chato kuwa serikali inaendelea kutoa fedha nyingi za maendeleo ya wilaya hiyo ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanatimia.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chato, Mandia Kihiyo,amesema kuwa taratibu zote za maandalizi ya zoezi la sensa zimekamilika na kwamba wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano mkubwa kwa makalani wote wakataopita kwenye makazi Yao.
OJADACT YAWANOA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA KUANDIKA HABARI MWENDELEZO ZA SENSA
Mwenyekiti wa OJADACT bwana Edwin Soko akizungumza wakati mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za sensa kwa mwendelezo, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi.
Na Mwandishi wetu Mwanza
Chama cha waandishi wa habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania(OJADACT) kimeendesha mafunzo kwa kundi la waandishi wa habari ili kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari za sensa kwa mwendelezo.
Mgeni Rasmi kwenye mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi ameipongeza OJADACT kwa ubunifu huo wa kuandaa mafunzo ya kuwafanya waandishi wa habari kuwa na tabia ya kuendeleza habari za sensa hata kama sensa itapita.
"Huu ni ubunifu wenye faida kubwa kwa Taifa kwa kuwa kuendelea kuandika habari za sensa itaisadia jamii kujenga uelewa wa umuhimu wa kushiriki zoezi la sensa Nchini, hivyo niwapongeze waandishi wa habari kujifunza zaidi kwenye mafunzo haya ya leo", amesema Makilagi.
Pia amesema kuwa, sensa ina faida kubwa sana kwa Taifa katika nyanja zote za uchumi, jamii na kisiasa, kwani bila kuwa na idadi kamili ya watu wako ni ngumu kutekeleza maendeleo.
Mwenyekiti wa OJADACT bwana Edwin Soko amewahamasisha waandishi wa habari waendelee kuandika habari mwendelezo za sensa kwani hii itasaidia kujua umuhimu wa sensa kwa Taifa na wajibu wa serikali kwenye kuleta maendeleo.
Soko pia amewataka waandishi pia kufuata maadili ya uandishi wa habari pindi wanapoandika habari mwendelezo za sensa.
Soko amewashukuru Taasisi ya MYCN, Furaha Nyanza Co.LTD , Toto Gift Shop na Desk and Chair Foundation kwa kufanikisha mafunzo hayo ya kuandika habari za sensa yaliyoandaliwa na OJADACT.
Mratibu wa OJADACT Lucyphine Kilanga amewakumbusha waandishi wa habari kwenye kujua historia za sensa kuanzia sensa ya kwanza ya mwaka 1910 na hadi sensa ya tano ya mwaka 2002 na kubainisha wajibu wa kila mtanzania kushiriki kwenye sensa.
Kwa upande wake mshiriki Alphonce Tonny toka Mkoa wa Mwanza amesema kuwa mafunzo hayo yamempa mtazamo mpya kwa waandishi wa habari kwani mwanzoni walijua wajibu wao ni kuandika tu habari za sensa na ikipita basi kazi imeisha lakini kumbe bado kuna umuhimu mkubwa wa kufanya mwendelezo wa habari za sensa ili jamii ielewe umuhimu wa sensa .
Naye mshiriki Mwamvita Issa toka Mkoa wa Shinyanga amesema kuwa, mafunzo hayo yamemjengea uwezo mkubwa wa kujua namna bora ya kuendelea kuandika habari za sensa.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi akizungumza wakati mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za sensa kwa mwendelezo
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi akizungumza wakati mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za sensa kwa mwendelezo
Mwenyekiti wa OJADACT bwana Edwin Soko akizungumza wakati mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za sensa kwa mwendelezo
Mwenyekiti wa OJADACT bwana Edwin Soko akizungumza wakati mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za sensa kwa mwendelezo
Mratibu wa OJADACT Lucyphine Kilanga akizungumza wakati mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za sensa kwa mwendelezo
Mshiriki Alphonce Tonny toka Mkoa wa Mwanza akizungumza wakati mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za sensa kwa mwendelezo




































