Wednesday, 22 April 2020

Waziri Wa Kilimo Tanzania Aitaka Idara Ya Sera Na Mipango Kuanisha Kiasi Gani Cha Fedha Kilichowekezwa Kwenye Kilimo

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Idara ya sera na mipango ya Wizara ya Kilimo imetakiwa kubainisha kiasi gani cha fedha kimewekezwa Kwenye Kilimo kutoka serikalini, sekta binafsi na washirika wa maendeleo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 22 Aprili 2020 wakati akizungumza na watumishi wa idara hiyo katika ukumbi wa Wizara hiyo maarufu kama KILIMO IV Jijini Dodoma.

Amesema kuwa pamoja na majukumu muhimu yanayofanywa na Wizara ya Kilimo lakini idara hiyo inapaswa kuongeza juhudi na weledi katika utendaji kazi wake wa kila siku ili kuongeza Tija na uzalishaji wa mazao ya wakulima.

Waziri Hasunga ameitaka idara hiyo kubainisha Takwimu mbalimbali za uzalishaji wa mazao, bei za mazao, uchambuzi, ikiwa ni pamoja na takwimu za Mazao ya mboga, maua na matunda.

Alisema kuwa pamoja na mafanikio makubwa ambayo yameonekana katika sekta ya kilimo katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli lakini bado sekta ya kilimo inapaswa kuimarishwa zaidi ili kuwa na mafanikio makubwa zaidi katika kilimo.

“Nchi zilizoendelea Duniani zimefanya nini na kwa nini Tanzania tupo nyuma Kwenye kilimo, na Kuna viwanda vingapi vya kuchakata mazao ya Kilimo” Alihoji Mhe Hasunga wakati wa kikao kazi hicho

Katika hatua nyingine Waziri Hasunga ameitaka idara hiyo kubainisha kuhusu Uongezaji thamani upoje na sera inasema nini kuhusu uongezaji thamani wa mazao.

Kadhalika, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameitaka idara ya sera na mipango kubainisha kuwa Sera ya masoko ipoje na wataalamu wanasemaje kuhusu hali ya masoko. Pia ametaka kufahamu hali ikoje kupitia sera ya usalama wa chakula, Sera ya Ushirika, Sera ya matumizi Bora ya ardhi na Tunakwama wapi Kwenye kilimo

MWISHO


Share:

Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Latoa Elimu Ya Kujikinga Na Covid 19

SALVATORY NTANDU
Katika jitihada za kuhakikisha abiria wanakuwa salama na wanajinga na Ugonjwa hatari wa homa ya Mapafu unaosababishwa na Virusi vya Corona katika vyombo vya Usafiri Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani mkoa wa  Shinyanga limeanza kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya Moto sambamba na kukagua utekelezaji wa maelekezo serikali kuhusiana na  COVID 19.

Akizungumza na Mpekuzi Blog Aprili 22,2020 mwaka  huu Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani mkoani humo, Africanus Sulle alisema kuwa Elimu hiyo imeanza kutolewa tangu Aprili 16 na inatolewa katika vituo vyote vya mabasi  mkoani Shinyanga vinafanyiwa ukaguzi wa kina  kuhusiana namna ya kujikinga na Ugonjwa wa COVID 19.

Alisema kuwa kwa sasa wanahakikisha Mabasi ya abiria hayazidishi abiria sambamba na kuviondoa viti ambavyo wamiliki wa mabasi wameviweka ambavyo vinasababisha abiria kusongamana kinyume na maelekezo ya serikali.

“Tumejipanga kikamilifu Askari wetu wapo katika vituo vyote vya Mabasi mkoani humu, kuhakikisha wanakagua magari yote yanayoingia na kutoka ili kuhakikisha kama wanandoo za maji pamoja na vitakasa mikono (sanitizer)ili kuhakikisha kabla ya kuanza safari ni lazima wanae na wapofika pia ni muhimu kunawa mikono ili kujiweka salama”,alisema Sulle.

Pia Sulle alifafanua kuwa serikali imeagiza kuviondoa viti vilivyowekwa kwenya mabasi madogo aina ya Hice ili kupunguza msongamano kwa jambo ambalo limekuwa likisababisha abiria  kusogeleana na kila mmiliki wa gari anapaswa kuhakikisha anatekeleza agizo hilo.

“Tangu tumeanza ukaguzi Aprili 17 mwaka huu mwitikio umekuwa mzuri na tunaimani elimu tuliyowapatia abiria na wamiliki wa magari imeleta matokeo chanya kwani kila mmoja ameanza kutimiza wajibu wake pindi anapokwa anataka kusafiri kwa kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa COVID 19.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo cha Mabasi cha CDT ,Kahama Sylivesta Joseph alisema  baada ya serikali kutoa maelekezo hayo utekelezaji ulianza mara mmoja ambapo kwa sasa katika kituo hicho abiria haruhusiwi kuingia bila kuna mikono.

“Abiria wanaokaidi kunawa mikono wanakamatwa na migambo ambao tumewaweka na wanapelekewa kituo kidogo cha polisi CDT na hutozwa faini ambapo mpaka sasa zaidi ya abiria 6 walishakamtwa na kutozwa faini na idara ya afya ya Halmashauri ya Mji kwa kutotii maagizo ya serikali”,alisema Joseph.

Nae Masanja Duttu mmoja wa abiria aliyezungumza na Mpekuzi alisema serikali inapaswa kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote wanaokaidi kunawa mikono kwa maji na sabuni wanaoingia katika kituo hicho.

“Haiwezekani suala hili liendelee kufanyiwa mchezo chukueni hatua kali kwa watu wote bila upendeleo kwani asili ya watu wa kanda hii ya ziwa hawapendi kunawanawa kila mara jambo ambalo kwao linawawia ugumu kwani hawajazoea,”alisema Duttu.

Mwisho.


Share:

Waziri Wa Afya Ummy Mwalimu Ametoa Mchanganuo (Ki Mkoa ) wa Wagonjwa Wapya wa Corona Walioongezeka Tanzania

Leo Asubuhi Jumatano April 22, 2020 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema, hadi jana Aprili 21, 2020 jumla ya Wagonjwa 284 wamethibitika kuwa na Virusi vya Corona. Wagonjwa 256 wanaendelea vizuri, 7 wako kwenye uangalizi maalum, 11 wamepona na 10 wamefariki.

Kutokana na taarifa hiyo wa Waziri Mkuu, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kupitia ukurasa wake wa Twitter ametoa mchanganuo wa Ongezeko hilo la Wagonjwa kimkoa.

Ameandika;Jumla ya watu waliopata maambukizi ya  #COVID19 nchini sasa ni 284 kutoka 254 tuliowatolea Taarifa tar 20 April 2020. Mchanganuo wa wagonjwa wapya 30 ni kama ifuatavyo: Dar es salaam (10), Zanzibar (9), Mwanza (4), Pwani (2), Kagera (1), Dodoma (2), Manyara (1) na Morogoro (1) 


Share:

Afrika Kusini Yatangaza mpango wa matumizi ya mabilioni ya fedha Ili Kuuokoa Uchumi Wake Uliovurugwa na Janga la Corona

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametangaza mpango wa hatua za kiuchumi wa dola bilioni 26 ili  kuupiga jeki uchumi  wa nchi hiyo na kusaidia jamii masikini zilizoathirika na janga la virusi vya corona. 

Akilihutubia taifa usiku wa kuamkia leo Ramaphosa amesema athari za ugonjwa wa COVID-19 zinahitaji bajeti maalum na mpango huo wa kihistoria utasaidia uchumi wa taifa hilo la watu milioni 58. 

Ramaphosa amesema Afrika Kusini sasa inaingia kwenye awamu ya pili ya kushughulikia kadhia ya corona kwa kuufufua uchumi ambao kuanguka kwake kumevuruga uzalishaji na nafasi za ajira. 

Rais huyo amesema kiasi dola bilioni 2.3 zitaelekezwa kutoa msaada wa fedha kwa jamii masikini huku vifurushi 250,000 vya chakula vitasambazwa kwa raia walio na mahitaji katika kipindi cha wiki mbili zinazokuja. 

Nchini Afrika Kusini kunaripotiwa visa 3,465 vya maambukizi ya virusi vya Corona yaliyothibitishwa, na watu 58 wamefariki  kwa ugonjwa huo.

Credit:DW


Share:

Waliofariki kwa Corona Marekani Wafika 45,343.....Maambukizi Yafika 819,175

Marekani imeendelea kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na corona Duniani ambapo hadi mchana huu idadi ya waliofariki  imefika 45,343.

Marekani pia inaongoza kwa visa, vimefikia 819,175  na wamepona 82,973

Jana Jumanne Marekani ilirekodi vifo 2,750 kwa siku licha ya takwimu mpya kuonesha maambukizi ya kila siku yanapungua nchini humo. 

Majimbo ya New Jersey, Pennsylvania na Michigan kila moja liliripoti vifo vya zaidi ya watu 800 kwa siku, huku jimbo la New York lililo kitovu cha mlipuko wa virusi vya corona nchini Marekani lilirekodi vifo vya watu 481.


Share:

Waziri Mkuu Majaliwa Amesema Wagonjwa wa Corona Tanzania Wamefika 284..

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema, hadi Aprili 21, 2020 jumla ya Wagonjwa 284 wamethibitika kuwa na Virusi vya Corona. Wagonjwa 256 wanaendelea vizuri, 7 wako kwenye uangalizi maalum, 11 wamepona na 10 wamefariki

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jumatano April 22, 2020  akiwa kwenye Maombezi ya kuombea Taifa dhidi ya ugonjwa huu yanayofanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar

Aidha, Waziri Mkuu amesema jumla ya watu 2,815 waliokuwa karibu na Wagonjwa wamefuatiliwa afya zao ambapo kati yao, watu 1733 hawana maambukizi na watu 12 walikutwa na virusi hivyo (wapo kwenye orodha ya watu 284)

Mara ya mwisho (Jumatatu April 20, 2020) Waziri wa Afya  Ummy Mwalimu alitoa taarifa kuwa jumla ya visa vya wagonjwa wa Corona  ilikuwa 254 baada ya Wagonjwa 84 kuongezeka

==>>Msikilize hapo chini


Share:

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATANGAZA WAGONJWA WA CORONA TANZANIA WAMEFIKIA 284

Share:

Waziri Mkuu Awaagiza Wakuu wa Mikoa Nchini Kuwachukulia Hatua Wafanyabiashara Wanaopandisha Bei ya Sukari

Wakuu wa Mikoa kote nchini wameagizwa kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuuza sukari kwa shilingi 4500.

Waziri Mkuu Mhe.Kasim Majaliwa amesema hakuna sababu ya sukari kupanda bei kwani sukari ipo yakutosha, ilikuwa imepungua imeagizwa na imekwishaletwa.

Majaliwa ameyasema hayo leo Jumatano April 22, 2020 akiwa kwenye Maombezi ya kuombea Taifa dhidi ya ugonjwa huu yanayofanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar 

“Wiki hii waumini wa kiislamu wanaanza mfungo wa Ramadhan hivyo natoa wito kwa wafanyabiashara kuhakikisha vyakula muhimu vinauzwa kwa bei ya kawaida, Wakuu wa Mikoa na Wilaya wafanye ukaguzi mara kwa mara kwenye masoko ili kuhakikisha bei ni ile ile.

"Hakuna sababu ya bei ya Sukari kupanda, Sukari ipo tena ya kutosha, ilikuwa imepungua imeagizwa na imekwishaletwa, nawaagiza Wakuu wa Mikoa yeyote atakayeuza Sukari kwa Shilingi 4500, chukueni hatua kali dhidi yake" Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.


Share:

Wanandoa Kortini Kwa Kutoa Matamshi Chonganishi Kuhusu Corona

Mfanyabiashara Boniface Mwita (49), mkazi wa Tabata Kimanga na mkewe Rosemary Jenera (41), wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutoa maneno hatarishi kwamba hakuna corona, Serikali inadanganya.

Washtakiwa hao walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Vicky Mwaikambo na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga akisaidiana na Wankyo Simon. 

Akisoma mashtaka, Wankyo alidai kuwa washtakiwa wanashtakiwa kwa kosa la kutoa lugha hatarishi ama yenye kushawishi jamii.

Wanadaiwa Machi 20, 2020 ndani ya Dar es Salaam, wakiwa kwenye usafiri wa umma – daladala la kutoka Tabata kuelekea Muhimbili lenye namba ya usajili T 119 DKS aina ya Toyota Coaster, walitoa matamshi hatarishi.

Inadaiwa walisema: ‘Ugonjwa wa corona Serikali inadanganya, hakuna ugonjwa wowote na imefunga mashule kwa kuwa haina pesa na ada za kusomesha watoto bure’.

Jamhuri imeiambia mahakama kuwa matamshi hayo yangeweza kuleta hofu au hisia mbaya dhidi ya nchi yao ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wameachiwa kwa dhamana.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na itakuja tena Mei 6 mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.


Share:

LIVE: Maombi ya Kitaifa Dhidi ya Janga la Corona

Waziri  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, leo Aprili 22, 2020, anaongoza Taifa zima katika maombi maalum ya kuliombea taifa dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu (COVID-19) inayosababishwa na virusi vya corona.

Maombi hayo yameandaliwa na wizara ya afya kwa kushirikiana na viongozi wa madhehebu ya dini nchini, na yanafanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam 




Credit: Global Tv

Share:

Utoaji Wa Huduma Katika Wizara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi Wakati Huu Wa Kukabiliana Na Maambukizi Ya Virusi Vya (Covid-19)




Share:

Rais Magufuli Afanya Uteuzi Mpya Wizara Ya Afya




Share:

TAKUKURU SHINYANGA YAOKOA MILIONI 118.8 KUTOKA VYAMA VYA USHIRIKA NA SACCOS...YATAHADHARISHA WANAOJIITA MAAFISA WA TAKUKURU


Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Hussein Mussa akizungumza na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Jumatano Aprili 22,2020 ambapo amesema TAKUKURU mkoa wa Shinyanga imeokoa Tsh. Milioni 118,851,957/= kutoka Vyama vya Ushirika na Saccos.

Aidha ametahadharisha wananchi kuchukua tahadhari juu ya matapeli wanaojifanya kuwa ni maafisa wa TAKUKURU hivyo wananchi watoe taarifa katika ofisi ya TAKUKURU iliyo karibu pale wanapomtilia mashaka mtu anayejitambulisha kwao kuwa ni Afisa wa TAKUKURU.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Hussein Mussa akizungumza na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Jumatano Aprili 22,2020












Share:

Bunge Lapitisha Makadirio ya Jumla ya Shilingi 62,781,586,000 Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Katika  kutekeleza majukumu ya Wizara ya Madini kwa  Mwaka 2020/2021,  Bunge limeridhia  na kupitisha makadirio ya Jumla ya shilingi 62,781,586,000 kwa ajili ya Matumizi ya Wizara na Taasisi zake.

Akiwasilisha Bungeni jijini Dodoma April 21 ,2020   hotuba ya Makadirio Ya Mapato na Matumizi Ya Fedha Kwa Mwaka 2020/2021 Waziri wa Madini Mhe.Doto Mashaka Biteko alisema  Mchanganuo wa Bajeti hiyo ni kama ifuatavyo:-

 (i)Bajeti ya Maendeleo ni shilingi 8,500,000,000. ambazo zote ni fedha za ndani; na (ii)Bajeti ya Matumizi ya Kawaida ni shilingi 54,281,586,000. ambapo shilingi 21,045,927,000. ni kwa ajili ya Mishahara na shilingi  33,235,659,000 ni Matumizi Mengineyo (OC).

Aidha Waziri Biteko alisema katika Mwaka 2020/2021, Wizara inapanga kukusanya jumla ya shilingi 547,735,863,597 ikilinganishwa na shilingi 476,380,613,492 kwa mwaka 2019/2020 sawa na ongezeko la asilimia 14.98.

Kati ya fedha zitakazokusanywa, shilingi 526,722,547,000 sawa na asilimia 96.16 zitawasilishwa Hazina na shilingi 21,013,316,597 sawa na asilimia 84 85 3.84 zitatumika na Taasisi zilizo chini ya Wizara.

Katika kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa madini  Waziri Biteko alisema Wizara  itaendelea kutenga maeneo yanayofaa kwa Wachimbaji Wadogo; kuwapa elimu kuhusu uwepo na faida za kuuza madini yao katika masoko yaliyoanzishwa; kutoa huduma nafuu za kitaalam kwa Wachimbaji Wadogo ikiwa ni pamoja na kuwafahamisha kuhusu uwepo wa mashapo katika maeneo yaliyobainishwa na kutengwa kwa ajili yao; na kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo kuhusu utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji, biashara ya madini yenye tija na namna ya kupata mikopo kutoka kwenye Taasisi za fedha.

Waziri Biteko aliendelea kufafanua kuwa Kwa kipindi kinachoanzia mwezi Julai, 2019 hadi Februari, 2020 jumla ya kilo 25,435.12 za dhahabu zenye thamani ya shilingi 2,772,331,030,317.99 zilizalishwa na kusafirishwa nje ya nchi kutoka katika Migodi Mikubwa na ya Kati.

Migodi hiyo ni pamoja na Geita Gold Mine, North Mara Gold Mine, Pangea Minerals (Buzwagi Mine), Bulyanhulu Gold Mine, Shanta Mine (New Luika), STAMIGOLD Company (Biharamulo Mine) na Busolwa Gold Mine (Tanzania).
 
 Aidha, katika  kipindi hicho kilo 10,102.43 za dhahabu zenye thamani ya Shilingi 975,430,320,903.97 zilizalishwa na wachimbaji wadogo wa madini.

Kuhusu ujenzi wa ukuta  wa Mererani  Waziri Biteko alisema umesababisha kuongezeka kwa makusanyo ya Serikali kwa takribani mara 13 ya kiwango kilichokuwa kikikusanywa awali ambapo katika mwaka 2019 makusanyo yaliongezeka na kufikia shilingi 2,150,000,000 ikilinganishwa na shilingi 166,094,043 zilizokusanywa mwaka 2017 kabla ya ujenzi  wa ukuta huo.

Akiwasilisha  Taarifa Ya Kamati Ya Kudumu Ya Bunge Ya Nishati Na Madini Kuhusu Utekelezaji Wa Majukumu Ya Wizara Ya Madini (Fungu 100) Kwa Mwaka Wa Fedha 2019/2020 Pamoja Na Maoni Ya Kamati Kuhusu Makadirio Ya Mapato na Matumizi Kwa Mwaka Wa Fedha 2020/2021  Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.Dunstan Luka Kitandula   alisema  kwakuwa Wizara bado haijapata Fedha za maendeleo zilizoidhinishwa na Bunge Shilingi 7,039,810,200.00 kutoka hazina hivyo Kamati inasisitiza kuwa Serikali ihakikishe kabla ya kwisha kwa mwaka wa Fedha 2019/2020, maombi ya Fedha ambayo yamepokelewa Hazina yawasilishwe kwa Wizara ili Wizara  iweze kutekeleza kikamilifu majukumu yake.

Akiwasilisha maoni ya kambi Rasmi ya Upinzani Naibu Msemaji Mkuu kambi  Rasmi yaUpinzani  katika Wizara ya Madini  Mhe.Joseph Haule  amesema kuna umuhimu wa kupitia upya muundo wa Wizara ya Madini na kufanya marekebisho katika idara ama taasisi zenye Majukumu yanayofanana ili kuondoa gharama zisizohitajika .
 
Pia Kambi hiyo ya Upinzani imeishauri Serikali kuwaambia Watanzania hatima ya majadiliano ya ACACIA  na fedha ambazo ilitakiwa kulipwa kama zilishalipwa  kwa sababu ni jambo la umma watanzania walishirikishwa tangu Mwanzo.


Share:

Corona yakwamisha mwili wa Askofu Getrude Rwakatare kupelekwa bungeni Kuagwa

Uongozi wa Bunge umesema aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Askofu Getrude Rwakatare (70), hataagwa kwenye viwanja vya Bunge kama ilivyo kawaida kutokana na mlipuko wa virusi vya corona vinavyosababisha homa ya mapafu.

Umesema unawasiliana na familia ili kujua utaratibu wa mazishi na ndipo Bunge litajulishwa namna wabunge watakavyoshiriki kumuaga mwenzao.

Spika wa Bunge, Job Ndugai, aliyasema hayo jana, alipotoa taarifa hiyo bungeni jijini hapa na kuwataka wabunge kuwa na subira wakati huu.

“Tunaendelea na mawasiliano na familia, kwa kawaida mbunge akifariki (dunia), wakati vikao vya Bunge vikiendelea, tunaacha kikao kimoja, tunamleta hapa (bungeni) tunamuaga kwa pamoja, lakini kwa mazingira ya sasa ya corona, hatutaweza kumleta hapa,”alisema.

“Maelezo mengine yatapatikana kesho (leo) baada ya kumaliza mazungumzo kati ya familia na Bunge,” Spika Ndugai alisema.

Dk. Rwakatare ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, alifariki Aprili 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Alikuwa Askofu wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God, maarufu Mlima wa Moto.


Share:

Ubalozi wa Ufaransa kusaidiana na serikali kupambana na Corona

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania ameelekeza sehemu ya mamilioni yaliyotolewa na nchi hiyo kwa serikali kwa ajili ya kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona nchini Tanzania.

Balozi Frédéric Clavier amesema kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, Ufaransa imeipa Tanzania kiasi cha Euro milioni 310 (shilingi bilioni 777.9) kwa ajili ya afya, maji na usafi wa mazingira.

Hivi sasa ubalozi huo unaangazia kuelekeza Euro 500,000, (shilingi bilioni 1.3) katika mapambano dhidi ya homa ya mapafu (COVID-19), kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya na vifaa vya matibabu.

Kwa kushirikiana na makampuni binafsi nchini kama SAT na TOAM Ubalozi wa Ufaransa utaelekeza Euro 500,000 (shilingi bilioni 1.3) katika chakula, msaada wa kiuchumi na kinga za Corona kwa wananchi wa vijijini kwani wapo kwenye hatari kubwa zaidi endapo watapata maradhi hayo.

Clavier, amesema atahakikisha Tanzania inafaidika na misaada kutoka nchi zenye mahusiano na Ufaransa kulingana na idadi yake ya watu.

Aidha, balozi huyo ameyataka makampuni yote ya kifaransa nchini kuhakikisha yanasaidia kutoa vifaa tiba na vifaa vya usafi kwa serikali ili kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

Mnamo Aprili 18, Rais Emmanual Macron wa Ufaransa alitangaza kuelekezwa kwa Euro bilioni 1.2 (shilingi trilioni 3.01) katika kupambana na COVID-19 barani Afrika.


Share:

Kamati Mbili Za Kudumu Za Bunge Zawaalika Wadau Kutoa Maoni Kwa Njia Ya Barua Pepe Kuhusu Miswada Mitatu Ya Sheria Kabla Ya Mei 4,2020

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kamati mbili [2]  za kudumu za Bunge zinawaalika wadau kutoa maoni yao kwa njia ya barua pepe kuhusu miswada mitatu [3] ya sheria  iliyosomwa bungeni kwa mara ya kwanza Februari,7,2020 wakati wa mkutano wa kumi na nane wa bunge.


Katika taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano  na uhusiano wa kimataifa  Ofisi ya Bunge April 21,2020 ilitaja miswada hiyo kuwa ni pamoja na Muswaada wa sheria ya marekebisho ya  sheria mbalimbali  wa mwaka 2020 [The Written Laws[Miscellaneous Amendments ]Bill 2020  ulio chini ya Kamati ya kudumu ya katiba na sheria.

Wa pili ni  Muswada wa Sheria ya Afya ya mimea wa mwaka 2020 [The Plant  Health Bill ,2020]  chini ya kamati ya kudumu ya Bunge ya kilimo ,Mifugo na Maji.

Na Muswada wa tatu ni muswada wa sheria ya kusimamia na kuendeleza uvuvi wa mwaka ,2020 [The Deep Sea Fisheries  Management   and Development Bill ,2020] chini ya Kamati ya kudumu ya Bunge  ya kilimo, mifugo na Maji .

Kitengo hicho cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa ,Ofisi ya Bunge katika taarifa yake ilifafanua kuwa Maoni kuhusu Miswada hiyo mitatu yatawasilishwa kwa katibu wa Bunge kwa njia ya barua pepe kamati@bunge.go.tz kabla ya tarehe 4 ,Mei,2020  na Miswada husika inaweza kupakuliwa  kupitia tovuti  WWW.Parliament.go.tz.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger