Sunday, 3 November 2019

Hiki Ndo Kikosi cha Yanga Kitakachowavaa Waarabu Misri Leo

Kikosi cha Yanga  kitakachoanza leo dhidi ya Pyramids FC ya Misri kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaopigwa majira ya saa 3:00 Usiku.


Share:

Scholarships for Tanzanian Students| Ufadhili wa Kusoma Nje ya Nchi (Unalipiwa Kila Kitu) | Deadline ni Mwakani

πŸ“š FURSA ZA UFADHILI  WA KUSOMA NJE YA NCHI

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

    πŸŽ“ Tanzanian Scholarships

Kama wewe ni Mtanzania mwenye Ndoto ya Kusoma nje ya Nchi lakini hukuwa na uwezo, basi hii ni Nafasi yako. Kuna Nafasi Nyingi sana za Ufadhili zimetangazwa (Scholarships)


 Zote Hizo ni Full Funded( Unalipiwa kila Kitu) Japo kuna zingine utachangia kidogo 

_______________________ 

Bado hujachelewa, Deadline ni kuanzia Mwezi huu wa  kumi na moja  hadi Mwakani-2020
._______________________ 


1.Global Scholars Program- Clark University USA 

2.Hong Kong PhD Fellowship Scheme for International Students

3.Clarendon Fund Scholarships, University of Oxford, UK

4.Holland Scholarship for Non EEA International Students

5.Justus & Louise van Effen Excellence Scholarships in Netherlands

6.Oxford Pershing Square Graduate Scholarships in UK

7.Emile-Boutmy Scholarship in France for Non EU Students

8.Karen McKellin International Leader of Tomorrow Award, University of British Columbia

9.Weidenfeld-Hoffman Scholarships and Leadership Program

10.Radboud Scholarship Programme | Netherlands

Bofya hapo chini kujua zaidi
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡


http://ajirazote.com/scholarship/


Share:

Ufadhili wa Kusoma Nje ya Nchi | Scholarships for Tanzanian Students

πŸ“š FURSA ZA UFADHILI  WA KUSOMA NJE YA NCHI

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

    πŸŽ“ Tanzanian Scholarships

Kama wewe ni Mtanzania mwenye Ndoto ya Kusoma nje ya Nchi lakini hukuwa na uwezo, basi hii ni Nafasi yako. Kuna Nafasi Nyingi sana za Ufadhili zimetangazwa (Scholarships)

*πŸ“Œ PHD
*πŸ“Œ MASTERS
*πŸ“Œ UNDERGRADUATE

 

ZIKO WAPI😳😳
✈(1)Zipo za Hong Kong
πŸ›©(2) Marekani
✈(3)Uingereza
πŸ›«(4)Canada

 Zote Hizo ni Full Funded( Unalipiwa kila Kitu) Japo kuna zingine utachangia kidogo
. _______________________
Bado hujachelewa, Deadline ni kuanzia Mwezi huu wa kumi mwishoni hadi Mwakani-2020
._______________________ 

Bofya hapo chini kujua zaidi
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡


http://ajirazote.com/scholarship/


Share:

Apps 20 Hatari Unazoshauriwa Kuziondoa Kwenye Simu Yako Haraka

Watumiaji wa Android wamepewa orodha ya apps za kuziondoa kwenye simu zao kwa sababu za kiusalama wa data na kuondoa matangazo yanayotokea sehemu zisizohusika kwenye simu zao.

Ushauri huo umetolewa na watafiti kutoka ESET ambao wamegundua app 42 kwenye soko la Google Play Store ambazo zimekuwa zinakuja na mfumo wa kimatangazo usio rasmi – adware. Mfumo huo una sababisha betri ya simu kuisha haraka, utumiaji wa data – intaneti na ata kuchukua taarifa zako binafsi kwenye simu.

Baada ya utafiti wa ESET kuweka wazi Google waliondoa apps hizo kwenye soko lao la Apps, ila inakuitaji wewe kuziondoa mwenyewe. Pia kuzifahamu ni muhimu kwa watu ambao wanatumia masoko mengine ya apps nje ya soko la Google Play Store. Apps hizo zimepakuliwa zaidi ya mara milioni 8.

Apps hizo zinauwezo wa kuonesha matangazo ata kama simu imefungwa (locked) kitu ambacho huwa kinapigwa na Google, kwani kufanya hivyo kuna sababisha utumiaji mkubwa wa betri na nje ya makubaliano yao na watengenezaji wa apps.

Apps hizo ni: Smart Gallery, SaveInsta, Mini lite for Facebook, Free Radio FM Online, Free Video Downloader, Free social video downloader, File Downloader, Water Drink Reminder, Smart Notes for You, DU Recorder, Tank classic, Heroes Jump, Solucionario, Ringtone Maker, Video downloader, Ringtone Maker Pro, Basketball Perfect Shot, HikeTop+, MP4 video downloader, Flat Music Player, Free Top Video Downloader.

Pitia orodha vizuri  hapo chini na kama kuna app bado unaitumia unashauriwa kuiondoa.

==>>Apps za kuziondoa  <<Hapa>>


Share:

Yanga Kuvaana Tena Leo na Pyramids FC

Wawakilishi wa Tanzania, Yanga SC, Leo Jumapili wapo dimba la Ugenini nchini Misri kukipiga na Pyramids FC katika mechi ya marudiano kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho Barani Africa.

Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba, jijini Mwanza klabu ya Pyramids FC iliibuka na ushindi wa bao 2-1.

Mechi hiyo inatarajia kuanza saa tatu kamili ( 3:00) usiku.


Share:

Ratiba ya Michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo




Share:

Haji Manara: Simba ni Klabu Bingwa ya taifa hili

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amefunguka mambo kadhaa kuhusiana na kikosi cha timu hiyo kuelekea mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City leo;

 
Nyie ni Klabu Bingwa ya taifa hili,nyie ni timu bora kupita zote Afrika Mashariki na ya kati kwa sasa! Nyie ni Wachezaji mnaoishi comfortable kuliko wachezaji wengine wowote ktk ukanda huu wa Afrika!!

Na nyie ndio Timu maarufu kupita zote ktk Zone hii, na mmetajwa na CAF ni klabu ya kumi na Sita bora Afrika nzima!!


Nadhan mtakuwa mmeelewa Wanasimba wanahitaji nn jioni ya leo hapa Uhuru Stadium,hususan baada ya kupoteza Kwenye last game!!


No Excuse today zaidi ya ushindi, hamtaeleweka na mm mtaninifanya niiasi insta kwa muda bila sababu!!! Nipo huku Cairo nikiamini Mtatenda kitakachotendwa hapa ilipoishi Mitume mingi. 



Share:

Jafo Atoa ONYO Kwa Wanasiasa Uchaguzi Serikali Za Mitaa

Waziri wa Tamisemi Suleiman Jafo amewataka wanasiasa kuacha kutoa kauli za  upotoshaji ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu.

“Niwaombe wana siasa kuacha kutoa kauli tata lengo ni moja kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu. Pia nivisihi vyama visicheze rafu huko maana kuna malalamiko mengine yanakuja upinzani kwa upinzani wanahujumiana,”-Jafo

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Novemba 3, 2019, Jafo amesema uchukuaji wa fomu umekwenda vizuri katika maeneo mengi na zilipotokea dosari aliagiza hatua zichukuliwe kwa haraka.

Kuhusu uwezekano wa kuongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu Jafo amesema hakuna mpango huo hivyo wagombea wote wakamilishe zoezi hilo ndani ya muda.


Share:

Wanawake wa jamii ya kibarbeig Babati kunufaika na utalii

Wanawake jamii ya Kibarbeig wilayani Babati, mkoa wa Manyara wanatarajiwa kuanza kunufaika zaidi na Utalii baada ya kuanzishwa vituo vya kuvutia watalii katika maeneo yao.

Afisa Maendeleo ya jamii ya Taasisi ya Chemchem association, Walter Palangyo amesema,Taasisi hiyo iliyowekeza shughuli za Utalii,katika hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Burunge, kupitia hoteli za Kitalii za Chemchem imejipanga kuboresha maisha ya jamii hiyo ili inufaike zaidi na Utalii.

Ofisa Utamaduni wa wilaya ya Babati, Beatrice Maliseli  akizungumza katika uzinduzi wa kituo hicho Leo Jumapili Novemba 3, 2019, aliwataka wanawake wa jamii hiyo kukitumia  vizuri kujiongezea kipato.

Amesema sasa watalii wataweza kuwatembelea na kununua vifaa vyao , kuona ngoma na tamaduni zao na hivyo kujiongezea fedha kwa ajili ya maisha yao.

Maliseli aliwataka wanawake na vijana wa jamii hiyo,kuongeza ubunifu wa vifaa vyao na kuanza kujifunza lugha za kigeni ili waweze kuwasiliana vizuri na watalii.


Share:

Mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka 2019 Kuanza Kesho

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles  Msonde amesema jumla watahiniwa 485,866 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka 2019 kati yao wa shule ni 433, 052 na 52, 814 wa kujitegemea.

Dk Msonde ameeleza hayo leo Jumapili Novemba 3, 2019 wakati akizungumza kuhusu kuanza kwa mitihani hiyo kesho  katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema kati ya watahiniwa 433,052 waliosajiliwa wanaume ni 206,420 sawa na asilimia 47.67 na wanawake 226,632 sawa na asilimia 52.33 huku wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwa 842.

Dk Msonde amesema maandalizi kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa mitihani, vijitabu vya kujibia na nyaraka zote za muhimu zinazohusu mchakato huo katika mikoa ya yote ya Tanzania Bara na Visiwani.


Share:

Nafasi 200 za Kazi Zilizotangazwa , Tazama Hapa | Deadline Mwezi Huu

Hapa nimekuwekea mkusanyiko wa Nafasi mbalimbali za Kazi Zilizotangazwa Wiki Iliyopita na Wiki Hii. Usisahau kushare na rafiki yako anayetafuta kazi
  1.  Job Opportunity​ at CRDB Bank | Senior Specialist; Financial Literacy
  2. Job Vacancy at CRDB Bank | Manager; Strategic Partnership
  3. New Government Job | Senior Corporate Communications Officer II at UCSAF
  4. Job Vacancy at Precision Air | Reservation & Ticketing Sales Agent
  5. Job Vacancy at Precision Air | Sales Manager Northern & Lake Zone
  6.  Job Vacancy at Standard Chartered Bank | Credit Analyst, Global Subsidiaries
  7. New Job Opportunity | Sales Capability Manager – Serengeti Breweries Limited
  8. New Job Opportunity | Marketing Manager, Spirits – Serengeti Breweries Limited 
  9. Nafasi 61 za Kazi Shirika la Hifadhi ya Taifa TANAPA | Elimu ni Kuanzia Cheti/Diploma/Degree | Mwisho Tarehe 30 Mwezi Huu 
  10. Jobs at UNICEF | Individual Consultant -Evaluation of the Zanzibar Social Protection Policy  
  11. Project Finance Assistant Job at Sightsavers Singida, Tanzania
  12. Project Assistant Job at Sightsavers Singida, Tanzania 
  13. Compliance Manager at IntraHealth International Mwanza, TZ 
  14. Research and Innovation Hub Coordinator Job at International Rescue CommitteeDar es Salaam, TZ 
  15. Electrical Manager Job at Radar Recruitment Tanzania 
  16. Job Opportunity at VodacomTanzania, Network Director 
  17. Monitoring, Evaluation, and Learning (MEL) Team Lead – Tanzania PS3+ 
  18. Job Opportunity at Abt Associates, Communications Team Lead 
  19. Jobs in Tanzania 2019 : New Job Opportunities at Mom Easy Company Limited | Sales Officers (15 Post) 
  20. Job Opportunity at Bariadi District Council | Mtendaji wa Kijiji Daraja la III 
  21. Jobs in Tanzania 2019: New Job Vacancies at Oxfam Tanzania| Donor Contracts Coordinator (INT5881) 
  22. Jobs in Tanzania 2019: New Job Vacancies at Oxfam Tanzania| Warehouse Officer (INT5995) 
  23. Technical Manager Job at Mbeya Water Supply and sanitation Authority 
  24. Job Opportunity at PCI Tanzania ,Documentation Specialist 
  25. Job Opportunity at Pact Tanzania,Gender and Youth Officer 
  26. Job Opportunity at Pact Tanzania, Technical Services Coordinator-Case Management 
  27. Job Opportunity at Pact Tanzania, Technical Services Coordinator-Bi-Directional Referrals and Linkages 
  28. Job Opportunity at Pact Tanzania, Logistic Assistant/Driver 
  29. Field Assistant Grade Ii Job at Tropical Pesticides Research Institute TPRI 
  30. Job Opportunity at UONGOZI Institute, Research And Policy Department (Intern) 
  31. Job Opportunity at UONGOZI Institute, Finance And Administration Department (Intern)

==Kwa nafasi zingine za Kazi zaidi ya 5000, <<INGIA HAPA>.


Share:

Waziri Kigwangalla Kuogoza Kampeni Ya Kutangaza Vivutio Vya Utalii.

Na.Aron Msigwa – WMU
Waziri wa Malisili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema  ataongoza kampeni ya kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika ukanda wa kusini na ukanda wa Kaskazini magharibi kwenye hifadhi mpya za Taifa zilizotangazwa hivi karibuni.

Amesema kampeni hiyo itawahusisha wasanii na watu maarufu wenye ushawishi katika jamii na inalenga kuhamasisha utalii wa ndani na kutangaza vivutio vya utalii vilivyo katika hifadhi za Taifa za Ruaha,Mikumi, Nyerere na Burigi – Chato.

Dkt.Kigwangalla ameyasema hayo alipokuwa akizugumza na Menejimenti ya Shirika la hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) na wakuu wa Kanda wa shirika hilo jijini Arusha.

Amesema hatua hiyo ya kuwatumia wasanii na watu maarufu wenye ushawishi katika jamii inalenga kuogeza hamasa kwa watanzania wavijue na kuvitembelea vivutio vya utalii vilivyopo katika hifadhi hizo hivyo kuogeza idadi ya watalii wa ndani.

Dkt.Kigwangalla amesema wasanii hao na watu maarufu wana wafuasi wengi wanaofuatilia kazi zao na matukio wanayofanya katika jamii kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii hivyo ni vyema wakatumika kutangaza utalii katika maeneo hayo.

Amesema hatua kazi hii ya kuhamasisha utalii wa ndani ni vyema wadau na watumishi walio kweye sekta husika wakawa wa kwanza kuvijua vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo mbalimbali ili iwe rahisi kuvielezea na kuvitagaza.

“Tukitaka kutagaza soko la utalii wa ndani lazima sisi wenyewe tuanze kwanza kuyajua maeneo ya vivutio tuliyonayo ili iwe rahisi kuwafikia watu wengine, tuna marafiki zetu ndani na nje ya Tanzania inakua rahisi kwetu kuwaalika na kuwakaribisha kwenye vivutio hivyo kwa kuwa sisi wenyewe tunavijua” Amesisitiza Dkt.Kigwangalla.

Amesema mkakati wa sasa ni wa kusambaza uelewa kuhusu vivutio vilivyopo ndani ya nchi ili kuwahamasisha watanzania wengi zaidi kutembelea vivutio hivyo akibainisha kwamba mkakati huo utakuwa na matokeo ya haraka na gharama nafuu ya kuhamasisha utalii wa ndani katika maeneo mengine ya nchi tofauti na ilivyo sasa ambapo watu wengi wanayafahamu maeneo machache na hasa yaliyo mikoa ya Kaskazini.

“Nilipoamua kuutangaza mlima Kilimanjaro na mimi mwenyewe kushiriki kupanda mlima kila mtu alishuhudia nini kilichotokea, kila mtu alikua akiuzungumzia mlima na hii inaongeza umaarufu wa mlima ndani ya nchi huu ni mkakati tunaotakiwa kuutumia katika maeneo mengine” Amesema.

Dkt. Kigwangalla ameiagiza TANAPA iendelee kukusanya takwimu za makundi mbalimbali ya watalii wa ndani wanafanya utalii katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo watazania wanaoshiriki mbio za marathon.

Katika hatua nyingine Waziri wa Maliasili na Utalii ameiagiza TANAPA kuifanyia kazi na kuikamilisha miradi ya ujenzi wa magati na ununuzi wa vivuko na Boti zitakazokuwa zikitumika kusafirisha watalii katika ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi kwenye eneo la Hifadhi ya Taifa ya Saadani.

Amesema gati hizo zitajengwa Dar es salaam, Saadani, Pangani, Pangani na Tanga ili kuwezesha boti hizo kusimama katika maeneo hayo yenye vivutio vya utalii na kushusha watalii wanaotaka kutembelea maeneo hayo.

“Hili ni eneo muhimu sana kwetu na rahisi kuuza huduma zetu za utalii wa ndani ya maji kutokana na uwepo wa visiwa na idadi ya watu wanaokwenda kuvitembelea, Ni lazima tujipange kuzitumia fursa hizi kwa kuwa na boti nzuri zitakazowawezesha watu kufanya utalii, mikutano, harusi na sherehe mbalimbali ndai ya maji na hii itakua ni Biashara kubwa kwetu na njia moja nzuri ya kulitumia vizuri eneo la bahari tulilo nalo” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Amesema ili kuitangaza hifadhi ya Taifa ya Saadani ni lazima kuiunganisha na utalii wa fukwe ili kuwavutia watalii wengi zaidi na kuongeza kuwa hifadhi hiyo kutokana na maeneo mazuri yaliyopo,sehemu za kulala na ukaribu wake na Bagamoyo na Dar es salaam.

Dkt. Kigwangalla amefafanua kuwa uanzishaji safari za boti za siku kutokea Dar es Salaam kwenda Bagamoyo na kurudi Dar es salaam utawawezesha watalii kwenda kati katika maeneo hayo kwa haraka na ni rahisi kuuza huduma hiyo kwa wageni watakaokuwa wanakwenda kufanya utalii mwisho wa wiki na kuiwezesha Serikali kupata faida ya kiuchumi kutokana na uwepo wa huduma hizo.


Share:

PROFESA ASSAD OUT!! RAIS MAGUFULI ATEUA CAG MWINGINE


Na Muyonga Jumanne, Mwananchi 

 Rais Magufuli leo Novemba 3, 2019 amemteua Charles Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Uteuzi huo unaanza kesho, Kichere anachukua nafasi ya Profesa Mussa Assad ambaye kipindi chake cha uongozi cha miaka mitano kinaishia kesho.

Mteule huyo ambaye alikuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), alitenguliwa uteuzi wake na Rais Magufuli ambaye alimteua tena kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Juni 8, mwaka huu.

Akisoma taarifa ya uteuzi huo leo Jumapili Novemba 3, 2019, Balozi John Kijazi amesema nafasi ya Kichere itajazwa na Katarina Revocati ambaye alikuwa Msajili Mkuu wa Mahakama.

Pia, Rais Magufuli amewateua Aisha Amour kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Kanali Francis Mbindi kuwa kamishna wa kazi ofisi ya Waziri Mkuu na majaji 12 wa Mahakama Kuu.
Share:

MWONGOZO WA UWEKEZAJI WA MKOA WA MWATARA WAZINDULIWA

Share:

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia Ashauri Muda wa Kuchukua Fomu Serikali za Mitaa Uongezwe

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amemtaka Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo kuongeza muda kuchukua fomu za uchaguzi wa Serikali za mitaa kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza.

Wagombea wa vyama mbalimbali vya siasa walianza kuchukua na kurejesha fomu kuwania uwenyekiti wa kijiji, mtaa, kitongoji na ujumbe wa kamati ya mtaa kuanzia Oktoba 29, 2019. Shughuli hiyo inayofanyika kwa siku saba itakamilika Novemba 4, 2019.

Akizungumza mjini Dodoma jana Jumamosi Novemba 2, 2019 Mbatia alisema baadhi ya maeneo ofisi zilifunguliwa siku mbili tu, baada ya hapo zilifungwa jambo lililowakosesha  nafasi wagombea wengine kuchukua fomu.

Amesema Serikali imetoa muda wa siku saba kwa ajili ya wagombea kuchukua na kurudisha fomu lakini baadhi ya vituo vinafungwa kabla ya muda.

Amesema malalamiko ni mengi kila kona, na kumtaka Jafo kuongeza muda ili wenye nia ya kugombea kujitokeza kwa wingi.


Share:

Viongozi wa vyama vya Ushirika watakiwa kutotumia fedha za wanachama bila idhini ya Mkutano mkuu wa Chama.

SALVATORY NTANDU
Viongozi wa Chama cha  Ushirika wa  akiba na mikopo SHIRIKISHO SACCOS LIMITED wilayani  Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kutotumia fedha za wanachama kinyume na makisio yalioridhiwa  na mkutano mkuu na badala yake ili kuondoa migogoro isiyokuwa na tija.

Hayo yamebainishwa na Daniel Kimatha na Prisca Agustino kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa SHIRIKISHO SACOSS LIMITED uliofanyika Mjini kahama ambao ulikuwa na lengo la kutathimini hoja mbalimbali zinazokikabili chama hicho kwa mwaka 2019 na kuangalia namana bora ya kuzipatia ufumbuzi.

Wamesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongzo katika shirikisho hilo kutumia fedha kinyume na makisio yaliyoridhiwa na mkutano mkuu wa mwaka na kusababisha kuibuka kwa malalamiko kutoka kwa wanachama wao na badala yake wanapaswa kuwashirikisha kabla ya kufanya matumizi.

“katika mwaka huu wa 2019 viongozi wetu wametumia shilingi laki mmoja kinyume na makisio yalioridhiwa na mkutano mkuu suala hili halikubaliki walipaswa kutushirikisha,alisema Kimatha.

Akijibu hoja hizo Mwenyekiti wa {SHIRIKISHO SACCOS LIMITED} Tito  Greyson Okuku amekiri kujitokeza kwa suala hilo na kusema kuwa walitumia fedha za faida walizopata kutokana na rida walizokusanya  na kuomba radhi wanachama hao na kuahidi kuwa suala hilo halitajitokeza tena.

Kwa upande Dronick Kamugisha ni afisa Ushirika wa Halamshauri ya Mji wa Kahama amesema kutokana na kasoro mbalilimbali zilizojitokwza katika chama hicho wao kama Halamshauri wamejipanga kutoa elimu ili wananchama waelewe dhima ya Ushirika na namna bora ya Uendeshaji.

Naye Mkaguzi wa vyamba vya Ushirika mkoa wa Shinyanga Rodrick Kilemile  amesema ofisi yake imebaini vyama vingi vya ushirika hawana wataalamu wa mahesabu hali ambayo imekuwa ikiwapa shida katika uandaaji wa taarifa za mwaka na kusababisha kuwepo kwa migororo.


Share:

Milioni 600 Kujenga Upya Kituo Cha Afya Lukole Kilichoachwa na Wakimbizi Mkoani Kagera.

Na Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera.
Zaidi  ya  sh milioni 600 Za kitanzania  zimetengwa na Halmashauli  ya  wilaya ya Ngara  ili kujenga upya kituo cha afya Lukole kilichokuwa kimejengwa kwa tope na kilichokuwa  kikiwahudumia wakimbizi waliokuwa wakiishi katika kambi hiyo.
 
Hatua hiyo imefikiwa baada ya  wakimbizi  kutoka nchi jirani za Burundi na Rwanda  waliokuwa wakiishi  kambini hapo kuondoka na kituo cha afya  kuendelea kuwahudumia wananchi wanaoishi jirani na kambi hiyo.
 
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauli ya Ngara  Aidan Bahama   amesema kwa bahati mbaya kituo  hicho kilijengwa  kwa tope na kupelekea  baadhi ya majengo  Kuwa na hali mbaya na kuwa katika  hatari ya kuanguka.
 
Kadhalika Aidan ambaye ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo na amemshukuru  mh rais John Pombe Magufuli kwa kutoa pesa ambapo baada ya ujenzi huo kituo hicho kitakuwa ni moja ya vituo bora wilayani Ngara.
 
Nao baadhi ya wananchi na wafanyakazi katika kituo hicho cha Afya Ambao ni Bw Joseph Hezzron,bw James Charles,Bi Noral Charles Mihayo  wameipongeza hatua hiyo ya serikali nakusema kuwa nijitihada za kujali huduma za wananchi.
 
Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa Jumla ya majengo sita yatajengwa katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na jengo la wagonjwa wa nje,jengo la upasuaji,maabara,jengo la kuhifadia maiti na nyumba moja ya mtumishi.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger