Monday, 21 October 2019
Sunday, 20 October 2019
TAMASHA LA TIGO FIESTA 2019 SAIZI YAKO ILIVYOKONGA MASHABIKI JIJINI DODOMA
Mwanadada Marianne Mdee ‘Mimi Mars’ akifanya vitu vyake kwenye tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako, lililofanyika juzi Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Msanii wa Bongofleva Abdul Chande ‘Dogo Janja’ akifanya vitu vyake kwenye tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako lililofanyika juzi Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
MKALI wa bongo fleva Nurdin Billal 'Shetta' akilishambulia jukwaa kwenye tamasha hilo jana.
MKALI wa nyimbo za injili Godluck Gozbert akilishambulia jukwaa la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako katika tamasha lililofanyika juzi Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
NYOTA wa muziki wa bongo fleva Heri Samir 'Mr Blue' akiimba katika tamasha la Tigo Fiesta 2019
Na MWANDISHI WETU, Dodoma
ZAIDI ya wasanii 16 juzi walitingisha baada ya kutoa burudani ya aina yake katika tamasha la Tigo Fiesta Saizi Yako, lililofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Juzi ilikuwa zamu ya Jiji la Dodoma na maeneo jirani kupata burudani hiyo ya aina yake baada ya kufanyika mikoa mingine mitatu tangu tamasha hilo lililopozinduliwa msimu huu.
Katika tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako mjini Dodoma, walihudhuria viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mawaziri na wabunge pamoja na mashabiki kutoka katika kila kona ya mkoa huo.
Kabla ya kuanza tamasha la Tigo Fiesta 2019, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Paul Kunambi, aliwatambulisha baadhi ya wabunge na mawaziri ambao walihudhuria kwenye tamasha hilo.
Kunambi alisema kuwa tamasha hilo kwa mwaka huu limetoa fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukuza biashara za wajasiriamali kutokana na kuongeza mitaji.
Alisema kuwa kumekuwa na ajira za muda mfupi ambazo zinachangiwa na tamasha hilo ikiwa ni sehemu ya kukuza kipato kwa vijana.
Alisema anaishukuru Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo kutokana na kuonyesha ubunifu wa hali ya juu na kuendeleza vipaji vya vijana kupitia tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako.
“Tunaishukuru Tigo kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na ubunifu wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuendeleza vijana kupitia muziki wa bongo fleva,” alisema.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tigo Kanda ya Kaskazini, Idan Komba, alisema wanaendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli kwa kuhakikisha wanakamilisha usajili kwa alama za vidole kwa wateja wote wa Tigo nchini.
“Tutaendelea kumuunga mkono Rais Magufuli ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usajili wa alama za vidole unafanyika na kuwafikia wateja wote wa simu za Tigo nchini,” alisema.
Tamasha hilo lilianza kwa wasanii chipukizi kupanda jukwaani na baadaye alipanda mkali wa bongo fleva anayefanya vizuri kwa sasa, Badest na kuimba kibao chake cha Nikagongee kilichowainua mashabiki na kuanza kumshangilia kwa kupiga kelele.
Baadaye alipanda jukwaani Heri Samir ‘Mr Blue’, na kuonyesha makali yake ikiwa ni pamoja na kuporomosha vibao vya zamani na vile vinavyotamba kwa sasa katika vituo mbalimbali vya redio nchini.
Mr Blue alianza na wimbo wa Tabasamu ambao aliimba live pamoja na bendi, baadaye akapiga wimbo wa Mbwa Koko, na kumalizia na Mboga Saba iliyowafanya mashabiki kuimba naye mwanzo hadi mwisho wa wimbo huo.
Hata hivyo Mr Blue alionyesha ukomavu wa hali ya juu kwenye onyesho la Tigo Fiesta Saizi Yako baada ya kumpandisha Nurdin Bilal ‘Shetta’, na kushirikiana naye kuimba wimbo wa Hatufanani.
Baadaye Shetta alibaki mwenyewe jukwaani na kutoa burudani kabambe ikiwa ni pamoja na kuimba nyimbo kama Shikorobo ilioonekana kuwavutia sana mashabiki waliohudhuria kwenye tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako.
Msanii wa bongo fleva, Abdul Chande ‘Dogo Janja’alipanda jukwaani na kutoa burudani murua ambapo aliimba nyimbo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ngarenaro, Kilele na Yente.
Nyota wa muziki wa injili, Godluck Gozbert alipewa nafasi kubwa na mashabiki kwenye tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako baada ya kupanda jukwaani na kuimba nyimbo mbalimbali zinazofanya vyema kwa sasa.
Staili aliyoingia nayo msanii huyo ilikuwa ya kipekee na kuwafanya mashabiki kumshangilia kwa kiasi kikubwa baada ya kuimba nyimbo za Shukrani, Nibadilishe na Hauwezi Kushindana.
Mwanadada Marianne Mdee ‘Mimi Mars’ alipanda jukwaani na kuonyesha manjonjo akiwa na wanenguaji wake.
Msanii huyo anayefanya vizuri kwenye muziki wa bongo fleva, alitawala vilivyo jukwaa kutokana na kuimba nyimbo zilizoteka hisia za mashabiki wake.
Msanii huyo aliimba wimbo wa Kodo, Polepole pamoja na Muwa na kuwafanya mashabiki kumshangilia vilivyo.
Wasanii wengine waliopanda jukwani kwenye tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako, ni pamoja na Barnaba Elias, Marioo, Juma Jux na Weusi.
PICHA: Rais Magufuli Awaapisha Viongozi Mbalimbali Ikulu Jijini Dar Es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mathias Bazi Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Gerald Godfrey Mweli kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshugulikia Elimu katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ali Sakila Bujiku kuwa Balozi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Viongozi mbalimbali walioapishwa kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mathias Bazi Kabunduguru, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Godfrey Mweli pamoja na Balozi Ali Sakila Bujiku wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Viongozi mbalimbali walioapishwa kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mathias Bazi Kabunduguru, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Godfrey Mweli pamoja na Balozi Ali Sakila Bujiku wakisaini Hati ya kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Augustine Mahiga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mathias Bazi Kabunduguru wapili kutoka (kushoto), Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Godfrey Mweli wa kwanza (kushoto), pamoja na Balozi Ali Sakila Bujiku wakwanza (kulia) mara baada ya uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa sambusa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
Waziri Mkuu Amwakilisha Rais Magufuli Urusi
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo (Jumapili, Oktoba 20, 2019) kwenda Urusi kuhudhuria mkutano baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na Urusi (Russia-Africa Summit), utakaofanyika jijini Sochi, Urusi, Oktoba 23 – 24, 2019.
Waziri Mkuu anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli.
Mkutano huo utakaoendeshwa chini ya uenyekiti wa pamoja (Co-chaired) wa Rais wa Shirikisho la Urusi, Vladimir Putin, na Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), unalenga kurejesha na kuimarisha uhusiano baina ya mataifa ya Afrika na Urusi ambao uliyumba baada ya kusambaratika kwa “Union of Soviet Socialist Republic” (USSR) mwaka 1991.
Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali utafanyika katika sehemu mbili, ambazo ni Kongamano la Biashara (Russia Business Forum) linalotarajiwa kufanyika Oktoba 23, na Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi za Urusi na Afrika uliopangwa kufanyika Oktoba 24, 2019.
Waziri Mkuu atashiriki kwenye mikutano yote miwili.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

RAIS MAGUFULI : KAZI ZA UONGOZI ZINAHITAJI UVUMILIVU...UTASEMWA,UTACHAFULIWA
.jpeg?itok=adUCRM9t×tamp=1571579736)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amewataka viongozi aliowaapisha leo Jumapili Oktoba 20,2019 Ikulu kuwa wavumilivu na wasihofie kuchafuliwa na watu, bali wajikite zaidi kwenye kutekeleza wajibu wao kama watumishi wa Umma.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es salaam wakati akiwaapisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI na Balozi, ambapo kazi ya uongozi inahitaji uvumilivu.
"Kazi za uongozi zinahitaji uvumilivu, zinahitaji kumtanguliza Mungu mbele, utasemwa, utachafuliwa lakini ndiyo kazi ya uongozi, naombeni katimizeni wajibu wenu kaangalieni haki, kaangalieni sheria kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote", amesema Rais Magufuli
"Kazi hizi ni lazima tuwatumikie wananchi wanyonge, juzi nilikuwa Mtwara kaimu wa TAKUKURU anafahamu tulikuta malalamiko kuhusu kulipwa korosho,baada ya kumuagiza amekuta vyama ushirika 32 vilivyokuwa vinawadhulumu , wananchi wameibiwa Bil. 1. 2", amesema Rais Magufuli.
RAIS MAGUFULI AMTUMBUA MKUU WA WILAYA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwe Rukia Muwango, pamoja na Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Bakari Mohamed Bakari, ambaye nafasi yake imechukuliwa na Hassan Abbas Rungwa.
Taarifa hiyo imetolewa Oktoba 19, 2019, na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, ambapo nafasi ya Mkuu wa Wilaya imechukuliwa na Hashim Abdallah Komba.
Uteuzi mwingine ambao umefanywa na Rais Magufuli leo ni wa Godfrey Mweli, ambaye amekuwa Naibu katibu mkuu TAMISEMI, akichukua nafasi ya Mathias Kabunduguru ambaye amekuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amemteua Mathias Kabunduguru, kuwa mtendaji mkuu wa Mahakama ya Tanzania, akichukua nafasi ya Hussein Katanga ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Naibu Waziri Wa Maliasili Na Utalii, Mhe.kanyasu Awataka Wazazi Watimize Wajibu Wao
Naibu Waziri Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewakumbusha Wazazi wenye watoto waliowapeleka kusoma katika shule binafsi wahakikishe wanawatimizia mahitaji yao ya muhimu katika kipindi chao chote cha masomo ili waweze kufaulu mitihani yao ya mwisho.
Badala ya kuja na zawadi nyingi siku ya mahafali ajili ya kuwapongeza wanapohitimu ilhali wanafunzi hao walikuwa wakirudishwa nyumbani kila wakati wakachukue ada ya shule.
Ametoa kauli hiyo jana wakati wa mahafali ya kidato cha nne kwa wanafunzi 60 yaliyofanyika katika shule ya Sekondari ya Rocks Hill iliyopo katika wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.
Amesema wazazi lazima wawekeze kwa watoto wao ili waweze kusoma katika mazingira ya kutokuwa na hofu ya kurudishwa nyumbani kwa sababu wazazi wao hawajawalipia ada ya shule.
"Ukiamua kumsomesha mtoto lazima ukubali kwamba elimu haijawahi kuwa bure, hivyo ni jukumu la kila mzazi kukidhi mahitaji ya mwanae likiwemo suala la kumlipia ada kwa wakati." alisisitiza Kanyasu
Amesema ni vyema wazazi hao kutambua dhamana waliyonayo katika kuwandaa watoto wao kielimu badala ya kusubili hadi watoto warudishwe nyumbani.
Mhe.Kanyasu amesema kitendo hicho cha wanafunzi kurudishwa nyumbani kwa ajili ya ada kimekuwa kikiwarudisha nyuma kimasomo kwa vile wamekuwa wakikosa baadhi ya vipindi.
Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewataka wazazi kuendelea kuwalea watoto wao katika maadili mema ili wasiweze kuharibikiwaa mara baada ya kuhitimu masomo yao.
Kwa upande wake Meneja wa Shule hiyo, Meshak Mpalanga amesema katika kipindi chao chote cha masomo wamelelewa kimaadili hali itakayowasaidia kupambana zaidi katika kuyamudu maisha
Akizungumzia jinsi walivyoandaliwa kwa ajili ya mtihani wao wa mwisho, Amesema anatarajia idadi kubwa ya wanafunzi watafaulu na kujiunga na kidato cha tano.
NayevMwanafunzi bora katika masomo yote aliyetajwa katika mahafali hayo, Diana Titus amesema wamejianda vyema na wapo tayari kwa ajili ya mtihani wao wa mwisho.
" Tunawashuru walimu wote kwa kutulea na kutufundisha, tunaamini sote tutafanya vizuri mitihani yetu.alisisitiza Mwanafunzi huyo

Tanesco Yakusanya Bilioni 46 Kwa Wiki
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa sasa linakusanya shilingi bilioni 46 kwa wiki hali inayofanya Shirika hilo kuendelea kujitegemea baada ya kuacha kupokea ruzuku kutoka serikalini ili kujiendesha.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani tarehe 18 Oktoba, 2019 wakati wa kikao chake na wafanyakazi wa TANESCO wa Kanda ya kaskazini kilichofanyika jijini Tanga na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Nishati, Raphael Nombo na viongozi kutoka TANESCO Makao Makuu.
” Niwapongeze TANESCO kwa kuendelea kujiendesha kwani hampokei tena ruzuku kutoka Serikalini na sasa mnakusanya shilingi Bilioni 46 kwa wiki tofauti na miaka miaka miwili iliyopita mlipokuwa mkikusanya bilioni Sita hadi Tisa kwa wiki, mnao uwezo, endeleeni.”alisema Dkt Kalemani
Kuhusu mkakati wa kuongeza mapato ya Shirika alisema kuwa, kunzia mwaka huu wa fedha, Kila Ofisi ya Mkoa ya TANESCO itapewa malengo ya makusanyo na atakayefikia malengo hayo atapewa motisha, ila atakayeshindwa atachukuliwa hatua.
Kuhusu ongezeko la wateja waliounganishwa na umeme, Dkt Kalemani ameliagiza Shirika hilo kufanya kazi kama makampuni ya simu kwa kufuata wateja kule waliko ili idadi ya wateja hao iongezeke na hivyo mapato ya Shirika kuongezeka.
Katika hatua nyingine, Dkt Kalemani alisema kuwa, kuanzia sasa miradi yote ya TANESCO inayotekelezwa kwa fedha za ndani itasimamiwa na wataalam wa ndani ya nchi ukiwemo mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (MW 2115).
” Niwapongeze TANESCO kwa kusimamia mradi huu mkubwa wa Julius Nyerere, zamani tulikuwa tukisimamiwa lakini sasa tunawasimamia wakandarasi na hii inaokoa fedha za Serikali ambazo zingetumika kutafuta wasimamizi wa miradi kutoka nje ya nchi kuja kusimamia miradi yetu.” alisema Waziri wa Nishati
Kuhusu suala la umeme vijijini, Dkt. Kalemani alisema kuwa bei ya umeme vijijini ni shilingi 27,000 bila kujali umbali aliopo mteja hivyo kila mtumishi ahakikishe hilo linatekelezeka.
Aidha, aliagiza wataalam wa TANESCO kuacha mara moja lugha lugha ya “hakuna vifaa” ambayo mara kadhaa imekuwa ikitumika wakati wateja wanapotaka kuunganishiwa umeme na kueleza kuwa vifaa vya umeme kama vile nguzo, mita, transfoma na nyaya vinazalishwa ndani ya nchi na kupatikana kwa urahisi hivyo lugha za visingizio zisiwepo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Raphael Nombo alizungumza na wafanyakazi hao kuhusu masuala ya muundo wa TANESCO, mikataba ya wafanyakazi na suala la mishahara.
TANESCO, Kanda ya Kaskazini inajumuisha mikoa minne ambayo ni Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara.

Makamu Wa Rais Kufungua Mkutano Wa mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO)
Eric Msuya – MAELEZO
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan anatalajia kumuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa 58 wa mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) utako anza Jumatatu tarehe 21 hadi 25 Oktoba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga, amesema Mkutano huo utaudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka Nchi 48 za Wanachama wa Shirika hilo pamoja na Masharika mbalimbali ya Kitaifa.
“Mkutano huu utakaoanza Jumatatu unatarajiwa kuhudhuriwa na Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa Serikali toka Nchi Wanachama, Wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa, Mabalozi wanaowakilisha Nchi zao hapa Nchini na Viongozi Waandamizi wa Serikali kutoka Nchi Wanachama” Amesema Mhe. Mahiga
Mkutano huo utaofanyika kwa siku tano, utajadili masuala mbalimbali ya kisheria za Kimataifa ikiwa pamoja na Changamoto za kisheria zinazoyakabili Mataifa Wanachama na Kuangalia namna bora ya kushughulikia changamoto hizo ili kuwa na Dunia yenye Amani, Usalama na Utulivu kwa ajili ya Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii.
Sambamba na hilo maswala mengi yatako jadiliwa katika mkutano huo ni, Sheria ya Kimataifa ya Bahari, Mitandao na Biashara na Uwekezaji, Kuvunjwa kwa Sheria ya Kimataifa Nchini Palestina, Utatuzi wa Migogoro kwa njia ya Amani, Matumizi ya Sheria za Nchi nje ya Nchi na Tume ya Sheria ya Kimataifa.
Tanzania ilijiunga na The Asian – African Legal Consultative Organisation (AALCO) mwaka 1973 chini ya Uongozi wa Rais Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, huku Tanzania ikiwa ni mara yake ya tatu kuwa wenyeji wa kushiriki katika mkutano huu wa Shirika la Mashauriano ya kisheria kwa nchi za Asia na Afrika
“Kwa mara nyingine tena, Tanzania tunakuwa wenyeji kwa mara ya tatu katika mkutano huu … Nchi yetu ina miaka 46 toka tujiunge na chama hichi, mafaniko ni mengi na maslahi ni makubwa na mapana tunayoendelea kuyapata katika chama hiki” Amesema Mhe. Mahiga
Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika ( The Asian-African Legal Consultative Organisation – AALCO kilianzishwa mwaka 1956 ikiwa ni matokeo ya Mkutano wa Kihistoria wa Bangung, Indonesia tarehe 18-24 April 1995 (Bandung Conference).
Waziri Mkuu Ataka Mikoa Iliyobakia Itekeleze Agizo Lake Kuhusu Uwekezaji
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka mikoa ambayo bado haijatekeleza agizo lake la kuandaa makongamano ya uwekezaji ihakikishe inafanya hivyo mara moja.
Ametoa agizo hilo jana mchana (Jumamosi, Oktoba 19, 2019) wakati akifungua Kongamano la Uwekezaji kwa mkoa wa Pwani katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
“Nitumie fursa hii kuwapongeza viongozi wa mkoa wa Pwani kwa kutekeleza agizo nililolitoa Juni 18, 2018 wakati wa kongamano la tatu la uwezeshaji wananchi kiuchumi la kuhakikisha mikoa yote inaandaa kongamano la uwekezaji na inakuwa na mwongozo wa uwekezaji wa mkoa. Mikoa ambayo haijatekeleza agizo hilo, ifanye hivyo mara moja,” amesema.
Waziri Mkuu amesema mkoa huo umeweza kubaini fursa zilizopo katika mkoa wa Pwani na kuzitangaza kupitia mwongozo wa uwekezaji ambao pia ameuzindua leo.
Amesema kaulimbiu ya kongamano hilo isemayo: ‘‘Ijenge Tanzania, wekeza Pwani mahali sahihi kwa uwekezaji (Build Tanzania, Invest in Pwani, the Best Place for Investment)” ina maana kuwa, licha ya mkoa wa Pwani kubainisha na kutangaza fursa za uwekezaji na biashara zilizopo, unajipambanua vizuri na kuonyesha kuwa ni kwa namna gani umejiandaa na umetengeneza mazingira bora yanayovutia wawekezaji wa ndani na nje.
“Ili kudhihirisha dhamira ya dhati ya kukuza uchumi kupitia viwanda, nimeelezwa kuwa mkoa umetenga hekta 53,016 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda ambavyo vitatumia rasilmali zilizopo ndani ya mkoa na maeneo mengine ya nchi kwa lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wanachi,” amesema.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri wahakikishe wanasimamia miundombinu inayoelekea kwenye viwanda vilivyopo kwenye maeneo yao.
"Kila mmoja ahakikishe maji, umeme na barabara vinafika kila eneo ambalo mwekezaji anataka kujenga kiwanda. Nitumie fursa hii kuwaomba mlete mabadiliko chanya yanayotokana na maboresho yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano."
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Bibi Angella Kairuki alisema kwamba Serikali imeanza kutekeleza mapendekezo ya mpango wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini (Blueprint for Improving Business Environment Regulatory Licensing in Tanzania) kwa kuondoa tozo 163 zilizokuwa zikilalamikiwa na wawekezaji.
“Pia tumetenganisha majukumu ya TBS ya TFDA ambayo sasa ni TMDA. TBS itashughulika na vyakula na TMDA itashughulika na dawa na vifaatiba. Vilevile, tumeondoa ada za usajili sehemu za kazi ambazo zamani ilikuwa ni sh. 28,000 na sasa hivi zinatolewa bure,” alisema.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikillo aliwataka watu wote wanaotaka kuwekeza nchini waufikirie kwanza mkoa wa Pwani kwa sasabu uko kimkakati na una fursa nyingi ikiwemo hali nzuri ya usalama na kwa maana hiyo mitaji yao italindwa.
“Mkoa wetu uko kwenye eneo la kimkakati la kuwezesha biashara kwa kuwa uko karibu na bandari ya Dar es Salaam na uwanja wa ndege; uko karibu na soko kubwa ambalo ni Dar es Salaam; unapitiwa na reli zote kwenda mikoani na nchi jirani; unapitiwa na barabara kuu itokayo Dar es Salaam na pia una bandari kavu ya Kwala.”
Mbali ya hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa alisema faida nyingine ambayo mkoa huo unayo ni uwepo wa miundombinu ya maji, umeme na nishati ya gesi asilia ambayo imeanza kutumiwa na baadhi ya viwanda kama Goodwill na Lodhia Steel.
Naye Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchumi ya Kijamii (ESRF) ambayo ilisimamia uandaaji wa mwongozo wa uwekezaji kwa mkoa wa Pwani, alisema taasisi yao inasaidia kuandaa na kuchambua fursa zilizopo kwenye mikoa mbalimbali. “Hadi sasa tumekwishaisadia mikoa 17 kuandaa miongozo ya uwekezaji na kwa sasa mikoa 12 imeshakamilisha na mikoa mitano iko kwenye hatua mbalimbali,” alisema.
Akitoa taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela ambao ni wadhamini wakuu, Afisa Mkuu wa Biashara, Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts alisema benki hiyo imeendelea kugusa sekta zote za uchumi na hivyo kuongeza tija kwenye mnyororo mzima wa uzalishaji.
Alisema huduma zao zimelenga kuongeza tija na ufanisi katika sekta ya viwanda nchini ikiwemo utoaji wa mikopo ya biashara kwa ajili ya kuongeza mikopo ya uendeshaji (working capita loans) na mikopo ya uwekezaji (investment loans).
“Benki yetu inatoa mikopo ya biashara na uwekezaji katika maeneo mbalimbali ambapo mikopo ya kilimo ni shilingi bilioni 357, uzalishaji wa viwanda (shilingi bilioni 214), biashara (shilingi bilioni 347), mahoteli (shilingi bilioni 87) na sekta ya madini (shilingi bilioni 91),” alisema.