Friday, 18 October 2019

MUUGUZI MATATANI KWA KUBAKA HOSPITALINI IGUNGA.... ...'ALIMDUNGA SINDANO YA USINGIZI MREMBO



Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini Tanzania, limeisimamisha kwa muda wa miezi mitatu leseni ya muuguzi, aliyemchoma sindano ya usingizi na kisha kumbaka, msichana mwenye umri wa miaka 16, aliyekuwa akimuuguza mama yake, katika hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

Inaelezwa kuwa muuguzi huyo Damiani Samson Mgaya, mnamo mwaka 2017, akiwa katika kituo cha Afya cha Igurubi , wilayani humo alishawahi kufanya tukio kama hilo, ambapo alipelekwa polisi na kisha mahakamani na hatimae aliachiwa huru na kurejeshwa kazini mwaka 2018.

Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 18, 2019, na Msajili wa Baraza hilo Agnes Mtawa na kusema kuwa baada ya mtumishi huyo kurejeshwa kazini, alihamishwa kutoka kituo cha Afya cha Igurubi na kupelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Igunga.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa baada ya kufanya ufuatiliaji, ilibainika kuwa mtumishi huyo alitoroka kituoni hapo na kuviomba vyombo vya ulinzi na usalama, vimsake popote alipo ili akamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria.
Share:

Nafasi Mpya za Kazi SIMIYU (Halmashauri Ya Wilaya Bariadi.) | Mtendaji wa Kijiji Daraja la Tatu

Nafasi Mpya za Kazi SIMIYU (Halmashauri Ya Wilaya Bariadi.) | Mtendaji wa Kijiji Daraja la Tatu
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
👉 Wanahitajita Watendaji Daraja la Tatu
👉  Elimu ni Kuanzia Kidato cha nne, sita na Cheti 
👉  Mwisho wa Kutuma Maombi : 30th October, 2019.
👉 Mshahara ni TGS B/1

 ==>>Pia zipo nafasi mbalimbali za kazi UBER TANZANIA, VODACOM, AIRTEL, JUMIA, NOKIA TANZANIA,UMOJA WA MATAIFA

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Bonyeza hapo chini kujua zaidi

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://ajirazote.com/jobs


Share:

MWANAMKE AJIUA KWA KANGA KISA AMEAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI

Picha ya Kanga,haihusiani na habari hapa chini

Na Walter Mguluchuma - Malunde 1 blog Nkasi
Mwanamke aliyefahamikakwa jina la Shija Lutonja (23) mkazi wa kijiji cha Kakoma wilayani Nkasi mkoani Rukwa amejinyonga kwa kutumia kanga yake huku akiacha ujumbe kuwa amepata maambuzi ya Virusi vya UKIMWI na mmewe yupo kafungwa jela.

Akizungumza na Malunde1 blog, Aafisa mtendaji wa kijiji cha Kakoma Richard Kandege amesema tukio hilo limetokea juzi majira ya kati ya saa tatu hadi nne asubuhi ambapo mwanamke huyo alikutwa amejinyonga nje ya mji wake kwenye mti kwa kutumia kanga.

"Aligundulika amejinyonga baada ya watu waliokuwa wakipita katika maeneo hayo kuona mwili ukining’inia juu ya mti na kutoa taarifa haraka kwenye ofisi ya serikali ya kijiji kisha tulitoa taarifa polisi",ameeleza.

"Polisi walifika eneo la tukio na katika uchunguzi wao hawakuona majeraha yoyote katika mwili wa marehemu zaidi ya yale ya kujinyonga. Walikuta ujumbe mfupi wa maneno kwenye mwili wa marehemu aliouandika kuwa ameamua kujiua mwenyewe kwa sababu ya kuwa amepimwa na amekutwa na Virusi vya Ukimwi lakini pia mumewe amefungwa jela hivi karibuni hivyo haoni sababu ya yeye kuendelea kuishi hapa duniani",amesema Kandege.

Mwenyekiti huyo wa kijiji amesema tukio hilo limeacha simanzi kubwa katika kijiji hicho kwa kuwa ni mara ya kwanza kwa Mwanamke katika kijiji hicho kuchukua maamuzi kama hayo ya kujinyonga hadi kufa.

Mkuu wa wilaya Nkasi Said Mtanda amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuitaka jamii kuacha kujichukulia sheria mikononi wakati jambo lake lilikuwa ni la kawaida kabisa kwani si yeye mtu pekee katika wilaya hiyo mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi bali alipaswa kuwashirikisha watu anao waanini ili wamempe ushauri na asingefikia hatua hiyo.
Share:

Waziri Mkuu Aeleza Jinsi Ya Kufikia Nchi Ya Kipato Cha Kati

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ili Tanzania ifikie lengo la kuwa nchi ya kipato cha kati inayoongozwa na uchumi wa viwanda, haina budi kuhakikisha kuwa inatimiza vigezo kadhaa, kikiwamo cha ukuaji wa uchumi kwa kiwango cha asilimia 12 kwa mwaka.

Amesema vigezo vingine ni mchango wa viwanda katika Pato la Taifa usiopungua asilimia 15; utoaji ajira rasmi na za moja kwa moja uongezeke na kufikia asilimia 40 ya ajira zote; na sekta ya viwanda iweze kuiingizia nchi mapato ya fedha za kigeni zaidi ya asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni.

Alitoa kauli hiyo jana usiku (Alhamisi Oktoba 17, 2019) wakati akizungumza na wageni na washiriki waliohudhuria hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa mwaka 2018 iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli alisema: “Ili kufikia vigezo hivyo na kuongeza kasi ya ukuaji wa sekta ya viwanda, ni lazima tujizatiti na kuimarisha ushirikiano wa karibu baina ya sekta ya umma na sekta binafsi,” huku akiwasihi washiriki katika hafla hiyo waitumie fursa hiyo kutafakari mbinu mpya za kufikia vigezo hivyo muhimu vya kuijenga Tanzania mpya ya viwanda.

“Kila mmoja wetu anatambua umuhimu wa sekta ya viwanda katika kukuza uchumi wa nchi yoyote duniani. Viwanda ndivyo vimekuwa chimbuko la maendeleo ya haraka ya nchi mbalimbali duniani na mhimili mkuu wa kutegemewa katika kuondoa umasikini kwa kutoa ajira nyingi na za uhakika kwa wananchi. Maendeleo ya sayasi na teknolojia yanategemea sana sekta ya viwanda.”

“Takwimu pia, zinaonesha kwamba katika mwaka 2018, sekta ya viwanda imetoa ajira rasmi 306,180 ikilinganishwa na ajira 280,899 za mwaka 2017; sawa na ongezeko la asilimia tisa. Tutaendelea kuchukua hatua zinazostahiki ili kuwezesha sekta hii ikue kwa haraka na kutoa mchango mkubwa zaidi katika Pato la Taifa na hivyo kuchangia katika kukuza uchumi na kuondoa umaskini wa wananchi wetu,” alisema Waziri Mkuu.

Aliema kutokana na jitihada kubwa zinazoendelea kufanywa na Serikali za kujenga uchumi wa viwanda, jumla ya viwanda vipya zaidi ya 4,000 vimejengwa katika mikoa mbalimbali. “Viwanda vilivyojengwa vinazalisha bidhaa za ujenzi (saruji, nondo, vigae, mabomba, marumaru, n.k); pamoja na viwanda vya kusindika mazao ya kilimo ikiwemo nafaka, matunda, mafuta ya kupikia na bidhaa za ngozi,” alisema.

Alisema viwanda vingi vimeanzishwa nchini na ni faraja kuona wawekezaji wa ndani nao wanaendelea kufungua viwanda vipya pamoja kuongeza uwekezaji wao. “Moja ya viwanda vinavyohamasishwa ni vile vinavyochochea uzalishaji wa ajira kwa wingi. Ujenzi wa viwanda vipya nchini, katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano, umechangia kupatikana kwa ajira mpya 482,601 nchi nzima,” alisema.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wenye viwanda na washiriki wa hafla hiyo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Bw. Innocent Bashungwa alisema wizara yake kwa kushirikiana na sekta binafsi itaendelea kuondoa kero zinazokwamisha ufanisi na ukuaji wa sekta ya viwanda zikiwemo kero kubwa zinazolalamikiwa na sekta hiyo.

Alizitaja baadhi ya kero hizo kuwa ni ucheleweshaji wa malipo ya madai ya kodi za ongezeko la thamani (VAT) na asilimia 15 ya ziada inayolipwa na waagizaji wa sukari ya viwandani; ushindani usio na uwiano na bidhaa za bei nafuu kutoka nje ya nchi kama vile nondo, mabomba ya plastiki, nguo na mavazi, bidhaa za ngozi na marumaru.

“Pia tutaangalia upya uwepo wa utitiri wa tozo na ada za juu zinazotozwa na taasisi mbalimbali za Serikali, ongezeko la kodi ya kuagiza mali ghafi kutoka nje ya nchini, na kucheleweshwa upatikanaji wa vibali vya kufanya kazi kwa wataalam wa kigeni wasiopatikana hapa nchini (expetriates employees),” alisema.

Kuhusu usajili wa makampuni, Waziri Bashungwa alisema Wizara hiyo kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imekamilisha kuweka mifumo ya kusajili majina ya biashara kwa njia ya mtandao. “Mifumo hiyo inawawezesha wafanyabiashara kusajili jina la biashara, uandikishwaji wa makampuni, usajili wa alama za biashara na usajili wa viwanda mahali popote walipo kupitia tovuti ya wakala (www.brela.go.tz).”

Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Bw. Subhash Patel, alisema CTI inaunga mkono azma ya Rais Magufuli ya kuleta viwanda nchini. “Hakuna nchi itakuwa imefanikiwa duniani bila kuwekeza kwenye viwanda,” alisema.

Akielezea uwepo wa fursa za biashara kwa wawekezaji wa Kitanzania, Bw. Patel alisema Tanzania ina majirani ambao hawana bandari na hiyo ni fursa tosha ya kuwekeza na kuendeleza biashara kwenye nchi jirani.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

SHIRIKA LA INADES FORMATION TANZANIA LATAKA JAMII KUTAMBUA HAKI NA SHERIA ZA MNYAMA PUNDA

Mnyama aina ya Punda ambaye anapiganiwa kupata haki na sheria zake na Shirika la Inades Formation Tanzania (IFTz)

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Shirika la Inades Formation Tanzania (IFTz) limeitaka jamii kutambua haki na sheria za mnyama punda pamoja na kutambua mchango wa punda katika maisha ya jamii.

Akizungumza na vyombo vya habari  mratibu wa kuboresha maisha kupitia ustawi wa mnyama kazi punda Fadhili  Nyingi  ambapo amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuboresha maisha ya watu waishio vijijini kupitia mnyama punda pamoja na  kurasimisha sekta ya punda katika halmashauri ya wilaya ya iringa.

Lengo la kwa la mradi ni kuongeza uelewa wa watu juu ya haki za wanyama na ufugaji bora wa Punda,mwisho wa siku watu wanatakiwa kujua punda anatakiwa kula nini,analala wapi na anahaki gani za msingi kutoka kwa binadamu” alisema Nyingi

Nyingi alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa wanaongeza uelewa kwa wananchi juu ya mnyama punda na kuwa sekta rasmi kama zilivyo sekta nyingine.

Aidha ameeleza mafanikio waliyopata kutokana na mradi huo ikiwa ni pamoja na kubadili mitizamo ya wananchi na kupunguzwa ukatili dhidi ya mnyama punda.

“Mafanikio yapo toka tumeanza mradi huu,maana wananchi wengi waliopo vijijini wameanza kubadilika kimtadhamo juu ya mnyama punda ndio maana sasa wameanza kuacha kuuza punda” alisema Nyingi

Kwa upande wake afisa mfawidhi nyanda za juu kusini bwana Nong’ona Solomoni amebainisha baadhi ya magonjwa yanayokumkumba mnyama punda ni pamoja na pepo punda,homa ya farasi na vidonda.

Hata hivyo kupitia mradi huo wa Inades Formation Tanzania wamefanikiwa kuunda vikundi 6 vya kukopeshana pamoja kutoa elimu juu ya haki za wanyama.
Share:

RAIS MUSEVENI : MBUNGE BOBI WINE NI ADUI WA UGANDA

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemtaja mkosoaji wake mwanamuziki aliyegeuka kuwa mwanasiasa Bobi Wine, kama "adui wa mafanikio ya nchi".

Rais Museveni ameyasema hayo katika mahojiano na BBC.

Bwana Museveni anataka kugombea muhula wa sita kama rais mnamo mwaka 2021 baada ya kuwa rais wa nchi hiyo kwa miaka 33.

Bobi Wine, ambaye ni kiongozi wa vuguvugu la 'The People Power', anamshutumu rais huyo kwa kuongoza kwa mfumo wa ukandamizaji.

Bwana Museveni amekataa kumueleza mwandishi wa BBC , Alan Kasujja ikiwa serikali yake ni ya ukandamizaji , lakini akasema anamshughulikia Bobi Wine kama adui.Rais wa Uganda amesema ataendelea kuwa madarakani zaidi ili kushughulikia matatizo ya Uganda na Afrika

Rais huyo wa Uganda amemlaumu Bobi akisema kuwa alikwenda Marekani na kusema kwamba watu wasije kuwekeza Uganda: ''Unapoenda na kuwaambia wageni kwamba hawapaswi kuja na kuwekeza katika nchi yetu, inamaanisha umeanzisha vita dhidi ya mafanikio yetu. Kwa hiyo kwa nini sasa unataka kurejea na kunufaika na mafanikio hayo?".

Hii huenda ndio moja ya sababu za kufutwa kwa matamasha ya muziki ya Bobi Wine, bado sijaongea na polisi kupata taarifa zaidi, alisema.

Juhudi za Bobi Wine kuhamasisha umma dhidi ya rais Yoweri Museveni zimekuwa zikizimwa na maafisa wa usalama

Rais huyo wa Uganda anasema bado ataendelea kuwepo madarakani kwa miaka mingine zaidi kukamilisha kile ambacho yeye binafsi na wapiganaji wenzake walikipanga kukifanikisha katika nchi yao na Afrika.

''Nyumba yangu inanisubiri, lakini tuna masuala kama Uganda ya kushughulikia. Ni masuala hayo ambayo yanatufanya tufanye kile tunachotaka kukifanya kisiasa pamoja na wenzetu. Kama chama tawala (NRM) kitafikiria kuwa hakihitaji mchango wa wazee basi tutaondoka madarakani kwa furaha na kufanya mambo mengine ." Museveni alimueleza mwandishi wa BBC Allan Kasujja mjini Kampala.

''Hatupo hapa kwa ajili ya maonyesho, hatuendi kwenye ukumbi wa michezo ya maigizo , sisi ni watu ambao tupo hapa kushughulikia masuala makubwa ya Uganda na Afrika ." Alisistiza kiongozi huyo wa Uganda.

Kiongozi wa upinzani Dkt Kizza Besigye alikabiliwa na nguvu ya maafisa wa usalama kila alipojaribu kuonyesha upinzani dhidi ya serikali ya Museveni

Rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani Uganda sasa kwa zaidi ya miongo mitatu.

Bwana Museveni amekuwa akikabiliwa na miito ya kumtaka ajiuzulu hasa kutoka kwa vijana na wapinzani wake .

Mpinzani wake wa muda mrefu Dkt Kizza Besigye amepitia misukosuko mingi katika harakati zake za kisiasa pamoja na Mbunge Bobi Wine ambaye juhudi zake za kutumia usanii wake wa kimuziki kuhimiza ajiuzulu zimekuwa zikizimwa na maafisa wa usalama.

Chanzo - BBC
Share:

RC CHALAMILA SASA KUWACHAPA VIBOKO WALE HAWAJAOA AU KUOLEWA


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, amesema kwa sasa atakuja na mpango wa kuwachalaza bakora wanawake na wanaume mkoani kwake, ambao hawajaoa au kuolewa na kueleza akishamaliza kuwachapa, atawaagiza waende wakatafute wapenzi wao wa kufunga nao ndoa.

Chalamila ametoa kauli hiyo mkoani Mbeya, ambapo amesema njia ya kutumia bakora ni miongoni mwa njia ambazo zinasaidia sana kwenye kuhamasisha jambo.

"Siku hizi tunatumia bakora katika kila jambo, tukikukuta umekaa nyumbani na huolewi ni bakora tu nenda katafute mume na ukiwa umekaa nyumbani huoi ni bakora tu nenda katafute mke, kuna umri ambao unatosha lazima uchangamshwe'' amesema Chalamila.

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa huo, alitawala kwenye vyombo mbalimbali vya habari baada ya kuonekana anawachapa bakora baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kiwanja, iliyopo Chunya mkoani Mbeya, baada ya kuteketeza kwa moto mabweni yao.
Share:

Urusi yafanya majaribio ya makombora ya kisasa ya nyuklia karibu na Marekani

Rais Vladimir Putin wa Russia ameshuhudia majarbio ya makombora matano ya kisasa ya nyuklia katika eneo la Bahari ya Arctic nchini humo ambalo linapakana na Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa, makombora hayo ya nyuklia yamefanyiwa majaribio katika mazoezi makubwa ya kijeshi ambayo yamefanyika katika eneo zima la Arctic kaskazini mwa nchi hiyo.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema makombora ya kuvuka mabara yaliyofanyiwa majaribio ni pamoja na RS-24, RSM-50 na Sineva.

Mazoezi ya kijeshi ya Russia yanayofanyika katika eneo la Arctic yanajumuisha wanajeshi 12,000, nyambizi tano za nyuklia, ndege 105 za kivita na magari 213 ya kurusha makombora.

Mazoezi hayo yaliyopewa jina ya Grom-19 au Radi 19 yalikamilika Alhamisi kwa mafanikio. 

Wakati akitazama mazoezi hayo kwa njia ya video akiwa mjini Moscow, Rais Putin, akiwa ameandamana na Waziri  wa Ulinzi Sergei Shoigu amesema majeshi ya Russia yalikuwa yanafanya mazoezi kuhusu vita vya nyuklia na vita vya kawaida. 

Mazoezi hayo yamekuja baada ya ya Rais Trump wa Marekani kutangaza kuwa meli za kivita za nchi yake zitaimarisha harakati katika Bahari ya Arctic.

Credit:Parstoday


Share:

Kijana Aliyeishi kwa kupumulia mashine afariki dunia

Hamad Awadh, aliyeishi kwa kutegemea mashine ya kumsaidia kupumua amefariki dunia jana jioni Oktoba 17, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Mke wa Awadh aitwaye Catherine Kulekana amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema, hali ya mumewe ilianza kubadilika usiku wa kuamkia jana akawa chini ya uangalizi wa madaktari hospitalini hapo. Ilipofika asubuhi hali yake haikurejea kawaida na saa 10 jioni alifariki.

Juni 10, 2019 Mloganzila ilimpa msaada wa mashine hiyo ya kumsaidia kupumua yenye thamani ya Sh4 milioni kutokana na matatizo yake ya afya ambayo yalimlazimu kutumia mashine ya Oksjeni muda wote ili aweze kupumua. Awadh alifikishwa Mloganzila Julai 9, 2018 na kuruhusiwa Juni 9, 2019 baada ya afya yake kuimarika.

Licha ya kutakiwa kurejea hospitali kila baada ya muda alishindwa kutokana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutokuwa na usafiri wa kutoka nyumbani kwake Kipawa hadi katika hospitali hiyo umbali wa zaidi ya kilomita 10.

Wadau na taasisi mbalimbali walijitokeza kumsaidia ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) lililomfungia umeme katika nyumba aliyokuwa akiishi na kumpatia Sh10 milioni za matibabu. Awadh aliomba msaada Tanesco kutokana na mashine ya kumsaidia kupumua kutumia umeme mwingi.
 
Pia, Hospitali ya Mloganzila ilitoa gari la wagonjwa kwa ajili ya kumpeleka Awadh katika hospitali hiyo kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake, mara ya mwisho hali yake ilibadilika na kulazwa hadi umauti ulipomkuta.


Share:

Naibu Waziri Mabula Aagiza Wakala Huduma Za Misitu Kupima Shamba La Miti La Rubya Ukerewe

Na Munir Shemweta, WANMM UKEREWE
Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuhakikisha inalipima na kupatiwa hati shamba lake la Miti la Rubya lenye ukubwa wa hekta 1,926.3 lililopo kijiji cha Bugula tarafa ya Ilangala kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo jana wakati alipokwenda kukagua ujenzi wa nyumba za watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakati akiwa katika ziara yake ya siku moja katika kisiwa cha Ukerewe kufuatilia utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika hamashauri za mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Alisema, kinachohitajika sasa kwa Wakala wa Huduma za Misitu ni kuhakikisha shamba hilo la Miti la Rubya linapimwa na kupatiwa hati itakayoonesha mipaka halisi ya shamba hilo ili kuepuka migogoro ya ardhi.

‘’Miji inakuwa kuwa na wananchi bado wanahitaji maeneo bila kuwa na hati inaoonesha mipaka ya shamba kunaweza kuleta migogoro na tuelewe hati inalinda mipaka ya shamba lisivamiwe   na wananchi’’ alisema Dokt Mabula

Pamoja na kuagiza kupimwa hilo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliagiza pia eneo la shamba kuwa Mpango Kina utakaonesha kila matumizi ya sehemu ya ardhi ya shamba hilo kwa kuwa katika eneo hilo mbali na shamba la misitu lakini kuna makazi ya watu.

Kwa upande wake Meneja wa Shamba la Miti la Rubya wilayani Ukerewe Festo Chaula alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba an Maendeleo ya Makazi kuwa, Shamba la Miti la Rubya ni miongoni mwa mashamba 23 yanayomilikwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania lililoanzishwa mwaka 1951 kwa Tangazo la Serikali Namba 230.

Alisema, pamoja na shamba hilo la Rubya pia Wakala inalo eneo lingine lilipandwa miti kwa ubia na halmashauri ya wilaya ya Ukerewe lenye ukubwa wa hekta 1,152 ambapo miti iliyopandwa eneo hilo ni ya Misindano.

Kwa mujibu wa Chaula, katika kuboresha makazi ya watumishi wa wakala wa Huduma za Misitu TFS katika mwaka huu wa fedha 2019/2020 TFS imetenga zaidi ya milioni 383.8 kwa ajii ya ujenzi wa nyumba tatu, tenki la kuhifadhia maji, ukarabati wa nyumba mbili na ujenzi wa uzio wa bustani ya miti ambapo ujenzi wa nyumba tatu ulianza Agosti mwaka huu.

Katika Hatua Nyingine Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameitaka halmashauri ya wilaya ya Ukerewe kufanya zoezi la upimaji maeneo katika halmashauri hiyo kama operesheni maalum ili kuondoa migogoro ya ardhi sambamba na kuondoa ujenzi holela.

Akizungumza na Madiwani pamoja na Watumishi wa Sekta ya Ardhi katika halmashauri hiyo, Dkt Mabula alisema tayari halmashauri hiyo inavyo vifaa vya upimaji inachotakiwa kwa sasa katika kuharakisha zoezi hilo ni kuwasiliana na Ofisi ya Ardhi Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kupatiwa Wapimaji.

Hata hivyo, Dkt Mabula alishangazwa na halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kutokuwa na kijiji chenye mpango wa matumizi bora ya ardhi wakati asilimia kumi ya kisiwa hicho ni ardhi ya nchi kavu. Halmashauri kerewe ina jumla ya vijiji 73 ambapo Naibu Waziri aliwataka Madiwani wa Halmashauri ya Ukerewe kuhakikisha inapanga mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa vijiji vyake ili kuainisha matumizi mbalimbali ya vijiji hivyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe George Nyamaha alieleza kuwa halmashauri yake imekuwa na chanagmoto kubwa ya upungufu wa wataalamu wa sekta ya rdhi jambo alilolieleza kuwa linasababisha idara hiyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.


Share:

Watanzania Waishio Na Vvu Waaswa Kuendelea Kutumia Dawa Za Kufubaza Virusi

NA.MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Uwekezaji, Dorothy Mwaluko amewaasa Watanzania wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kuendelea kutumia dawa za kufubaza virusi hivyo ili waweze kuishi maisha yenye afya na amani wakati wote.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanachama wa Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI katika Konga ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Mkoani alipowatembelea kukagua utekelezaji wa majukumu ikiwa ni pamoja na namna konga hiyo inavyoendesha shughuli za uzalishaji Wilayani hapo Oktoba 17, 2017 Mkoani Morogoro.

“Kipekee ninawapongeza kwa ujasiri wenu wa kujitokeza na kuonesha ulimwengu kuwa janga hili lipo na ni letu sote, kwani naamini hakuna mtu ambaye halijamgusa kwa namna moja au nyingine hivyo niwaombe mjitahidi kuendelea kutumia dawa hizi za kufubaza makali ya virusi ili kuendelea kuimarika zaidi,”alisema Mwaluko.

Aliwasisitiza kuendelea kuwa mabalozi wazuri kwa wengine ambao hawajatambua hali zao na wale waliotambua hali zao kuendelea kufubaza virusi na kutoacha kutumia  dawa hizo kwa kuzingatia umuhimu wake.

“Napenda kuwahamasisha msiache wala kuchoka kutumia dawa hizi kwa kuzingatia umuhimu wake katika kuhakikisha zinawapa nafuu na kuondoa magonjwa nyemelezi kuendelea kuwa na afya njema na kushiriki katika shughuli za kimaendeleo na kufanya dunia mahali salama pa kuishi,”alisisitiza Mwaluko.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utafiti na Tathimini kutoka Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela aklieleza kuwa, hali ya kiwango cha maambukizi Mapya ni asilimia 4.7 Kitaifa na maambukizi hayo ni mengi kwa wanawake kuliko wanaume hivyo Serikali itaendeelea kuhudumia kundi hili kwa kuhakikisha lilapewa dawa hizo kwa kadri itakiwavyo.

“Serikali imejipanga kuhakikisha kundi la WAVIU wote wanahudumiwa na kupatiwa mahitaji yao muhimu ikiwemo upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi (ARV) hivyo na kuhakikisha kundi kubwa la wanawake ambao ndiyo wanaoathiriwa zaidi linafikiwa kadiri iwezekanavyo na hii itaendeelea kusaidia kundi hilo kupunguza hatari ya kuingia katika maambukizi mapya,”alieleza Dkt.Kamwela.

Aliongezea kuwa takwimu zinaonesha hali ya maambukizi mapya kwa kila mwaka ni watu 72000 ambapo kundi la vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 linaongoza kwa asilimia 40 na kueleza kundi la wanawake wanachangia asilimia 80 ya maambukizi hayo.

“Serikali imetoa kipaumbele kuwa mwitikio wa masuala ya UKIMWI umelenga kundi la vijana ili kupunguza maambukizi mapya yanayolikumba kundi hilo,”alifafanua Dkt.Kamwela.

Aliongezea kuwa wananchi wasipotambua hali zao mapema wanasababisha kuanza tiba kwa kuchelewa na hivyo kulazimika kuanza dawa wakati wa hatari na kuwalazimu kuwa na juhudi za ziada katika kutumia dawa ili kutokomeza maambukizi mapya na kufubaza virusi vya UKIMWI.

Aidha Mwenyekiti wa Baraza la Watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi wa Konga hiyo Halida Ally alieleza kuwa hali ya utoro wa dawa imechangia kuongezeka kwa maambukizi mapya ambapo walifanikiwa kuhamasisha watu 30,712 kupima hali zao ambapo jumla ya watu 2,038 walikutwa na maambukizi kati yao wanawake ni 1,327  na wanaume ni 711.

Alisema hali ya utoro wa dawa ni changamoto katika kuhudumia kundi hilo inayochangiwa na uwepo wa sababu mbalimbali ambapo katika kundi la WAVIU 2,038 wanaotumia dawa za kufubaza virusi ni 1,707 kati yao wanawake ni 1,034 na wanaume ni 673 katika kundi hilo watoro wa dawa ni 996 kati yao wanaume ni 335 na wanawake ni 673 hali ambayo inachangia kuongezeka kwa maambukizi mapya na kuongeza ukubwa wa janga hilo katika Halmashauri yao.

Naye mmoja ya wanachama wa konga hiyo Betina Januari aliipongeza Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika mapambano dhidi ya Ukimwi na kuahidi uendelea kutoa ushirikiano katika jitihada za kuwawekea mazingira wezeshi na kufikia malengo ya sufuri tatu ifikapo 2030.

KONGA Kilombero ni Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (VVU) ngazi ya Wilaya. KONGA ya Kilombero imeundwa mwaka 2013 ikiwa na vikundi 14 vyenye jumla ya wanachama 354 ambapo wanawake ni 237 na wanaume 117.


Share:

TIGO FIESTA 2019 SAIZI YAKO KURINDIMA LEO DODOMA


Wafanyabiashara mbalimbali katika Mkoa wa Dodoma wameeleza namna ambavyo wamejiandaa kutumia fursa za kibiashara zinazotokana na msimu wa tamasha la Tigo Fiesta ikiwamo kukuza na kuboresha huduma zao ili kukidhi mahitaji ya wateja.
Mkuu wa Wilaya, Patrobas Katambi amesema ni msimu wa mavuno kwa wajasiriamali huku akiwataka kutumia vema fursa za kibiashara.

Tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako litarindima Jumamosi hii tarehe 19 katika uwanja wa Jamhuri likiwa na dhumuni la kuchochea shughuli za kiuchumi pamoja na kutoa burudani kwa wateja wa Tigo na wakazi wa mkoa huo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti jana, wafanyabiashara hao wamesema msimu wa Tigo Fiesta huleta fursa nyingi za kiuchumi kutokana na namna ambavyo linawakusanya watu kutoka maeneo mbalimbali ambao hugeuka kuwa wateja wa bidhaa na huduma kama chakula, malazi pamoja na usafiri.

Samuel Kakolanya ambaye ni dereva wa bajaji wa eneo la Chako ni Chako, alisema ni fursa ya kipekee kwa madereva na wasafirishaji kwani hali ya biashara huwa nzuri kutokana na mahiataji kuongezeka hasa nyakati za usiku.

“Kwanza nawapongeza sana waandaaji wa tamasha hili kwasababu ukiangalia mwaka jana biashara ilikuwa nzuri sana, tunapata wateja wengi tofauti na siku za kawaida kwahiyo msimu huu pia tunategemea mambo mazuri zaidi,” alisema Kakolanya.

Naye, Juma Yusuph ambaye ni dereva wa pikipiki maarufu ‘bodaboda’ eneo la Jamhuri alisema msimu huo hugeuka kuwa neema kwao kutokana na biashara kuwa ya kasi.

“Sisi shughuli zetu zinategemea zaidi wingi wa watu na ukiangalia kama Fiesta ya mwaka jana niliona ongezeko kubwa la biashara tofauti na siku zote na hii inaonesha kukiwa na Fiesta hali inakuwa nzuri kutokana na Population ‘watu’ kuwa kubwa,” alisema.

Mbali na wasafirishaji, wafanyabiashara wa huduma za vyakula maarufu kama mama tilie walieleza kuwa kutokana na manufaa ya tamasha hilo wamejiandaa kuboresha huduma zao ili kukidhi mahitaji ya wateja.

“Tunachokifanya ni kujiongeza kiuchumi na kikubwa ni kuhakikisha naweka huduma za aina mbalimbali kama supu, chips pamoja kuboresha hili banda langu ili kuwavutia zaidi wateja siku hiyo,” alisema Mariam Meshack.

Aidha, watoa huduma za malazi (hoteli) walieleza namna ambayo wameanza kuboresha huduma ili kukidhi mahitaji ya wateja siku ya tamasha la Fiesta.

Meneja wa hoteli ya Los Angelos iliyopo mtaa wa Mji mpya, Benedicta Simon alisema

“Tunapokea wageni kutoka mikoa jirani kama Singida na pia wasanii mbalimbali wanafikia hapa, tumeanza kwa kubadilisha muenekano wa hoteli na ndani ya wiki hii tutaweka huduma ya intaneti ili kuwapa mazingira rafiki wateja wetu,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi aliwataka wakazi wa Dodoma kuchangamkia fursa akisema kuwa msimu wa Tigo Fiesta hugeuka kuwa msimu wa mavuno kwa wafanyabiashara.

“Ujio wa Fiesta hapa Dodoma itakuwa ni fursa ya ajira kwa vijana kwakuwa italeta fursa nyingi, wawe bodaboda, madereva teksi na mama lishe hivyo watu wategemee kuneemeka zaidi na fursa hii na Tigo imekuwaa rafiki wa vijana na kwa hapa Dodoma imeajiri vijana zaidi ya 600,” alisema.

Aliwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo zaidi kwa kusajili namba za simu kwa mfumo wa alama za vidole kwakuwa Tigo wanashirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) kutoa namba na vitambulisho kwaajili ya zoezi hilo.

Share:

RC SHIGELLA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAMILIKI WAPYA WA KIWANDA CHA KUZALISHA SARUJI CHA RHINO JIJINI TANGA

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na wamiliki wapya wa  kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Rhino kilichopo Jijini Tanga ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayej
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na wamiliki wapya wa  kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Rhino kilichopo Jijini Tanga ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha kushoto  ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
VIONGOZI mbalimbali wakifuatilia mazungumzo hayo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na aliyevaa miwani kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji na Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) faidha Salim
Share:

BASI LA FREYS COACH LAUNGUA MOTO


Na Josephine Charles - Malunde 1 blog
Basi la Freys Coach lenye namba za usajili T119BDY Gari la Freys  Coachla linalofanya safari zake kutoka Shinyanga kwenda  Tanga limeungua moto katika  eneo la Mhizi Usanda Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga barabara ya Tabora - Shinyanga.


Tukio hilo limetokea leo Ijumaa Oktoba 18,2019 majira ya saa 12 na nusu baada ya kutoka Shinyanga Mjini kuelekea Tanga.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio wanasema basi hilo limeungua matairi mawili ya nyuma upande wa kulia na kwamba hakuna madhara yaliyojitokeza kwa abiria walishuka na kuanza zoezi la kuzima moto huo kwa maji na mchanga na muda mfupi Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifika eneo la tukio na kufanikisha kuzima moto huo.

"Tumezima kwa maji na mchanga,zimamoto nao wamefika,gari limezima,hakuna uharibifu wala majeruhi,gari halijateketea,abiria tumefanya juhudi za kuzima,tunasubiri magari mengine kutoka Mwanza ili tuendelee na safari",wamesema abiria wakizungumza na Malunde 1 blog .

Muonekano wa basi la Freys Coach baada ya kuungua leo. Picha zote na Josephine Charles - Malunde 1 blog
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 18,2019



Share:

Thursday, 17 October 2019

DHAMIRA YA SERIKALI NI KUHAKIKISHA MTAMBO WA KUZALISHA UMEME HALE UNAREJEA KWENYE HALI YAKE YA KAWAIDA-WAZIRI DKT KALEMANI

Share:

WAZIRI MKUU AAGIZA WAKURUGENZI WAWILI WA HALMASHAURI WAFIKE OFISINI KWAKE KESHO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtama na Mkurugenzi wa Umwagiliaji wa Kanda ya Kusini, wafike ofisini kwake Dar es Salaam kesho asubuhi na taarifa kuhusu skimu wa umwagiliaji wa Narunyu.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Oktoba 17, 2019) wakati alipoenda kukagua skimu hiyo ambayo imekuwa ikilalamikiwa tangu 2017. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtama ni Bw. Warioba Gunze na Mkurugenzi wa Umwagiliaji wa Kanda ya Kusini, ni Mhandisi Mndeme.

Amechukua uamuzi huo baada ya kufika eneo la mradi na kupokea malalamiko ya wanajumuiya ya umwagiliaji kutoka kwa Mwenyekiti wao, Bw. Bakari Awadhi juu ya kusuasua kwa mradi huo lakini alipotaka apate maelezo ya wataalamu hakuna hata mmoja ambaye alikuwepo.

"Nilitaraji niwakute hapa Mkurugenzi wa Halmashauri, Afisa Umwagiliaji wa Wilaya na Mkurugenzi wa Umwagiliaji wa Kanda. Nimeagiza wanikute uwanja wa ndege Lindi au Dar es Salaam na kesho asubuhi waje ofisini kwangu wanipe taarifa kamili ya mradi huu. Nataka nijue fedha zilizobakia zaidi ya sh. milioni 240 ziko wapi."

"Walipaswa niwakute hapa wananisubiri kwa sababu nilitoa taarifa tangu jana kwamba nitapita hapa. Nimepata taarifa kwamba wamesafiri kutoka Mtwara na leo asubuhi walikuwepo Lindi mjini. Waje ofisini kesho, wakishindwa, nitachukua maamuzi mengine," amesema.

Akielezea umuhimu wa mradi huo wakati akizungumza na baadhi ya wanaushirika waliokuwepo, Waziri Mkuu amesema ni wa muhimu kwa sababu unatiririsha maji wakati wote. "Huu ni mradi wa kuringia. Mradi huu unatiririsha maji wakati huu wa kiangazi, tena mengi tu."

Amesema kutokana na umuhimu wa mradi huo, hivi sasa wangekuwa wanazalisha mazao ya kila aina. "Hapa ni mahali pa kuzalisha mazao mengi, leo unalima mahindi, ukivuna unapanda matikiti, ukitoa unapanda nyanya. Sasa nitapasimamia mwenyewe," amesisitiza.

Amewataka wanaushirika wanaounda jumuiya ya umwagiliaji wahakikishe kila mmoja anatambua eneo lake na mara kazi ikianza wawe tayari kuanza kilimo. "Huu mradi una manufaa kwa watu wa Ruo, Mahumbika hadi Mnazi Mmoja. Lazima tuung'ang'anie kwa sababu kuna idadi kubwa ya wakulima wanaoutegemea. Huu mradi lazima tuuvalie njuga."

Waziri Mkuu alipofika uwanja wa ndege wa Lindi, maafisa hao walikuwa hawajafika kwa sababu simu zao hazikupatikana, na akaagiza waje Dar es Salaam kesho asubuhi.

Mapema, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Bw. Shaibu Ndemanga alimweleza Waziri Mkuu kwamba katika mafaili aliyoyapitia ofisini kwake alibaini kwamba mradi huo ulitengewa sh. milioni 788 ambapo mkandarasi wa kwanza Chest Investments Company alilipwa sh. milioni 121 lakini akashindwa kazi.

"Mkandarasi wa pili ambaye ni D & L naye alilipwa zaidi ya shilingi milioni 400 naye pia akashindwa kazi ya kuondoka tope. Kwenye ripoti, inaonesha zilibakia sh. milioni 249," alisema.

Naye Mwenyekiti wa wanajumuiya ya umwagiliaji ya Narunyu, Bw. Bakari Awadhi alisema skimu hiyo yenye ukubwa hekta 1,200 imekuwa ikijaa maji na kufunika mitaro na hatimaye kujaa mchanga.

Alimwomba Waziri Mkuu awasaidie kuifufua skimu hiyo kwa sababu inawanufaisha wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger