Friday, 15 February 2019

MANISPAA YA ILALA YATOA MKOPO WA TSH.153,000,000 MILIONI KWA VIKUNDI

Na Heri Shaban MANISPAA ya Ilala Dar es salaam imekabidhi mkopo wa tsh. 153,000,000mil kwa Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu. Zoezi la utoaji wa mikopo hiyo liliongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri ambapo kila kikundi kilipewa Hundi ya shilingi millioni 3 na Kikundi cha Vijana kilichopo Kitunda kilipewa milioni kumi. Akizungumza katika zoezi hilo Shauri aliagiza kila Kata Manisipaa Ilala waanzishe Viwanda vidogo vidogo ili waweze kukuza uchumi katika wilaya ya Ilala. “Serikali yetu tukufu inayoongozwa na Rais wa awamu ya tano John Magufuli Leo imetekeleza utoaji…

Source

Share:

Thursday, 14 February 2019

Video Mpya : FATUMA SHAH - CANDLELIGHT


Msanii wa Bongo Fleva Fatuma Shah ameachia video mpya leo siku ya Wapendanao 'Valentine day' inaitwa Candlelight 


Ngoma hii ni zawadi kwako katika msimu huu wa wapendanao.
Tazama video hii hapa
Share:

ASHUSHIWA KICHAPO BAADA YA KUGOMA KUFANYA MAPENZI NA MMEWE KINYUME NA MAUMBILE

Mwanamke mmoja mkazi wa Kijichi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, anadai kupigwa na kujeruhiwa usoni ambako ameshonwa nyuzi sita na mumewe baada ya kumkatalia kufanya mapenzi kinyume na maumbile.


Akizungumza leo Alhamisi Februari 14, 2019 mwanamke huyo anadai mume wake amekuwa akimtaka wafanye mapenzi kinyume na maumbile muda mrefu lakini amekuwa akikataa kwa sababu ni haramu kwa mujibu wa mafundisho ya dini.

Akieleza zaidi alidai kwa muda mrefu ndoa yake imeingia kwenye mgogoro na mumewe amekuwa akimwambia kuwa hajui mapenzi.

“Alianza kunitaka kinyume na maumbile miezi mitatu tangu anioe nikamkatalia, mpaka nikapata mimba ikiwa na miezi sababu bado akawa anataka nikamkatalia,” anasema.

Amedai kuwa baada ya kufuatlia historia ya mumuwe, majirani wanaomfahamu walimweleza kuwa tabia hiyo ndiyo imesababisha kuachana na wake zake zaidi ya wawili.

Hata hivyo, mwanaume huyo amekanusha tuhuma hizo na kueleza kuwa mgogoro wa ndoa yake umesababishwa na wakwe zake wanaomdai mahari mpaka imefikia hatua ya kumweleza kuwa ni maskini.

Na Muhammed Khamis, Mwananchi 
Share:

MWANASIASA MKONGWE TANZANIA HAMIS MGEJA ATANGAZA KUPUMZIKA SIASA

Mwanasiasa mkongwe nchini na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Shinyanga, Hamisi Mgeja (kulia pichani) ametangaza kupumzika siasa kwa muda na kujikita kwenye shughuli nyingine.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake mjini Kahama, Mgeja amesema kwa sasa akili yake ameielekeza zaidi katika shughuli za kilimo pamoja na michezo hasa soka la watoto wadogo ili kuwajengea hamasa na kuvutia wadau mbali mbali waweze kuwekeza katika kizazi kijacho.

“Mwalimu (Julius Nyerere) alitufundisha siasa ni kilimo, nimeamua kujikita shambani kumuenzi kwa vitendo na kuhamashisha vijana kujihusisha na kilimo kitakachowaongezea tija na kipato katika maisha yao,” alisema Mgeja aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga.

“Hapa kwetu kilimo ni uti wa mgongo na ni kazi kama nyingine. Kwa kuwa Mwalimu alisema kazi ni kipimo cha utu, nawahamasisha vijana waje shambani tuungane pamoja kujiletea maendeleo" amesema.

Hivi karibuni, Mgeja ameonekana kwenye majukwaa ya michezo hasa soka la vijana wadogo.

Kuhusu hilo Mgeja amesema, “Soka letu ili lisonge mbele upo wajibu kwa wadau kuwekeza katika soka la watoto na ndio maana tumeanzisha Kahama United Sports Academy ili kukuza vipaji vya watoto wadogo.

“Kwa kutambua mchango wangu wadau wamenipatia heshima ya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini nikishirikiana na wadau wa michezo wilayani Kahama chini ya Mwenyekiti wetu, Charles Lubala na Katibu wake, Mwalimu Daniel Mbilinyi. Ipo siku soka letu litafika pale tunapopatarajia kama wadau watainuka na kuungana pamoja nasi huku chini kwenye kuvumbua na kukuza vipaji,” amesema.

Mgeja alikuwa mmoja kati ya majina ya wanasiasa wakongwe waliosikika zaidi kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, baada ya kuihama CCM na kujiunga na Chadema kumuunga mkono swahiba wake aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliyeshindwa.
CHANZO - HABARILEO

Hamis Mgeja (kulia) akimpatia jezi mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi kweny moja ya shughuli za kimichezo za Hamis hivi karibuni mjini Kahama (Picha kutoka Maktaba ya Malunde1 blog)


Share:

MWENYE NYUMBA ATUPWA JELA KWA UHARIBIFU KWENYE CHUMBA CHA MPANGAJI

Mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam Zamazam Mohamed amehukumiwa na Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, Dar es Salaam kwenda jela miezi sita au kulipa na faini ya Sh 600,000, baada ya kufanya uharibifu kwenye chumba cha mpangaji wake na kusababisha upotevu wa mali yenye thamani ya Sh 390,000.


Akisomewa hukumu hiyo na Hakimu wa mahakama hiyo, Mark Mochiwa, amesema mahakama hiyo imejiridhisha pasipo na shaka, kwamba Februari 28, mwaka jana, eneo la Mkwajuni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshitakiwa alivunja mlango wa chumba cha mlalamikaji Ovano Vitus.

Amesema katika uvunjaji wa mlango wa chumba hicho, ulisababisha upotevu wa simu pamoja na video, vyote vikiwa na thamani ya fedha hizo.

Shahidi namba moja wa mlalamikaji Issa Mohamed, alidai alipopigiwa simu na mlalamikaji na kufika eneo la tukio alikuta mlango umevunjwa na kwa muda wa siku mbili haujajengwa.

Amedai kuwa, hata walipokwenda serikali ya mtaa na kumtaka mshitakiwa afike kujielezea alikataa, baadaye walifika ofisi za kata na alipoitwa tena aligoma ndipo wakaamua kwenda kuchukua RB katika kituo cha polisi cha Oysterbay ambapo alikamatwa.

Lakini pia shahidi ambaye pia aliitwa na mshitakiwa alithibitisha kwamba mlango wa mlalamikiwa ulikuwa umevunjwa na wakati huo ulikuwa ukijengwa, kwa madai alimtaka mpangaji huyo aondoke na kumwachia chumba chake.

Wakati huohuo, watu wawili wamepandishwa kizimbani akiwemo dereva Hamidu Mussa (25) katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni kwa tuhuma za kuvunja na kuiba vitu vyenye thamani ya Sh 860,000.

Mussa wakati akisomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Felister Massawe na Mwendesha Mashitaka konstebo wa polisi, Januari Kasekwa alidai kwamba mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 10, mwaka jana, eneo la Kinondoni Shamba Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Alidai kwamba mshitakiwa alivunja nyumba ya malalamikaji Joseph Simba, na kuiba radio Sabufa, compyuta, video, CPU, kioo pamoja na maganda ya simu, vyote vikiwa na thamani hiyo.

Mshitakiwa alikana mashitaka hayo, kesi hiyo imeghairishwa hadi Februari 20 itakapotajwa tena. Dhamana ipo wazi ambapo alihitajika kuwa na wadhamini wawili watakaotimiza masharti ya dhamana na kusaini ahadi ya milioni mbili.

Wakati huohuo, Jackline Elisha, mkazi wa Oysterbay alisomewa mashitaka ya kuiba mkoba wa Tuilumba Tala, wenye gharama ya Sh 60,000.

Mwendesha mashitaka Kasekwa alidai mbele ya Hakimu Massawe kwamba mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Februari 3, mwaka huu, eneo la KKKT Msasani wilaya ya Kinondoni.

Chanzo - Habarileo
Share:

MWAKYEMBE AIFAGILIA NEMBO MAALUM YA AFCON U17 ILIYOZINDULIWA LEO

Nembo maalum ya mashindano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON U17) imezinduliwa leo Alhamisi February 14 jijini Dar es Salaam.

Hafla ya uzinduzi wa nembo hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa jijini chini ya Usimamizi wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.

Mwakyembe ameipongeza Nembo hiyo na kusema kuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuitangaza Tanzania hasa vivutio vya utalii.


"Nembo hii imebeba vitu vikubwa vitatu katika nchi yetu na mashindano haya. Kwanza imebeba dhana ya utalii. Kivutio chetu kikubwa cha Tanzania Kimataifa ni mlima Kilimanjaro. Tunauona hapa.


Lakini pili imebeba dhana ya uhifadhi. Tumeambiwa kuna pembe ya tembo na ya kifaru. Ambao ni wanyama wetu tunaowahifadhi kwa nguvu zetu zote. Tatu, yote haya yanahusu michezo na ndio maana kuna mpira," alisema Dk Mwakyembe.


Mkurugenzi wa masoko wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Aaron Nyanda alisema kuwa nembo hiyo imechorwa kwa lengo la kuitangaza Tanzania.


"Tulianzisha mchakato kwa watu kubuni nembo ambayo tumeipata hii inayoonyesha vivutio vilivyopo hapa nchini. Na mshindi aliyeshinda atapata fursa ya kwenda nchini Peru ambako kutafanyika Fainali za Dunia kwa vijana wa umri huo iwapo tutafanikiwa kufuzu," alisema Nyanda.
Share:

YANGA YAPIGWA FAINI


Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, katika kikao chake Februari 12, 2019 ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi pamoja na malalamiko yaliyowasilishwa mbele yake na kufanya maamuzi ikiwemo kuipiga faini Yanga.

Kamati imepitia ripoti ya mechi namba 239 iliyowakutanisha wenyeji Coastal Union dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya 1-1.

Klabu ya Yanga imetozwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) baada ya wachezaji wake kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi. Kitendo hicho ni kinyume cha Kanuni ya 14(14) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, na adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo.

Mbali na Yanga, Coastal Union pia imetozwa faini ya sh. 500,000 kutokana na timu yake kuoneshwa kadi zaidi ya tano katika mchezo huo uliofanyika Februari 3, 2019. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 43(10) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti kwa klabu.

Kamishna wa mechi hiyo Charles Mchau, na Mwamuzi Nassoro Mwinchui wamefungiwa miezi mitatu kila mmoja kutokana na taarifa zao kuwa na upungufu, na kushindwa kuumudu mchezo huo. Adhabu dhidi yao ni kwa mujibu wa Kanuni ya 40(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makamishna, na Kanuni ya 39(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.
Share:

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amefanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Taifa kwa watu wenye ulemavu na Mwenyekiti wa wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Walioteuliwa kushika nyadhifa hizo ni Dkt. Lucas Luhende Kija ambaye atakuwa mwenyekiti wa baraza la ushauri la taifa kwa watu wenye ulemavu akitokea chuo kikuu kishirikishi cha elimu (DUCE) ambapo alikuwa Mhadhiri.

Mwenyekiti mpya wa bodi ya REA ni Dkt. Michael Pius Nyagoga ambaye awali alikuwa kamishna msaidizi wa Sera, Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha na Mipango.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imesema kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 13, Februari 2019.
Share:

Pata Habari 24 Hours : Pakua Upya App ya Malunde 1 blog ...Imeboreshwa Kukupa Raha zaidi

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
Share:

WAJAWAZITO WANAPATA TABU WAKATI WA KUJIFUNGUA KWA KUKOSA VIFAA MUHIMU-MAVUNDE

Naibu waziri sera,Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu ,Ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh  Antoy Peter Mavunde amesema kuwa asilimia kubwa ya wakina mama wanapata tabu wakati wa kujifungua kwa kukosa vifaa muhimu . Mavunde ameyasema hayo katika kituo cha afya cha makole kilichopo Jijini Dodoma, wakati akikabidhi Msaada katika kituo hicho ikiwa ni kuonesha upendo kwa wakina mama wajawazito wanao kwenda kujifungua na ikiwa ni siku ya wapenda nao, hivyo ameamua kutenga siku hiyo kwaajili ya kuwasaidia kutokana na changamoto kubwa ambazo zimekuwa zikiwakabili…

Source

Share:

Video Mpya : ABDUKIBA - MUBASHARA

Video Mpya ya Abdukiba - Mubashara

Share:

Wimbo Mpya: NANDY Ft SKALES - BABY ME

Wimbo Mpya: Nandy x Skales - Baby Me


Share:

ALIYEJENGA NYUMBA MOJA KWENYE NCHI MBILI AFUNGUKA...VYUMBA VIPO TANZANIA,VINGINE KENYA


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Damas Ndumbaro na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji wakiwa kwenye Nyumba iliyojengwa mpakani mwa Tanzania na Kenya. Horohoro. Mhe. Ndumbaro akiwa upande wa Kenya na Mhe. Kijaji akiwa upande wa Tanzania.
**
 Juma Ally, aliyejenga nyumba katikati ya mpaka Tanzania na Kenya katika kijiji cha Jasini wilayani Mkinga Mkoa wa Tanga amesema haoni tatizo nyumba yake kuwa eneo hilo.

Amesema nyumba hiyo ipo katikati ya mpaka huo, na baadhi ya vyumba vyake vipo upande wa Tanzania na vingine upande wa Kenya.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Februari 14, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Damas Ndumbaro na naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji kutembelea kijiji hicho.

Katika ziara yao hiyo mawaziri hao walikumbana na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na suala la mipaka.

Katika maelezo yake, Juma amesema kuwa wao ni wakazi wa muda mrefu katika eneo hilo na hata huduma za kijamii wanazipata kutoka Kenya.

Amesema licha ya kupata huduma hizo Kenya, wao ni Watanzania.

“Nilivyojenga nilijua nimejenga Tanzania kwa kuwa ni nchi yangu ila baada ya mawaziri kufika hapa ndiyo nikasikia kuwa nyumba yangu iko upande wa Kenya na Tanzania,” amesema Juma.

Na  Raisa Said, Mwananchi 
Share:

UWANJA WA TAIFA KUFUNGWA


Uwanja wa taifa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema uwanja mkuu wa taifa utafungwa kwa muda ili kupisha maandalizi ya fainali za michuano ya AFCON kwa vijana chini ya miaka 17.

Akiongea leo Februari 14,2019 kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika makao makuu ya shirikisho la soka nchini (TFF), Mwakyembe amesema ili eneo la kuchezea na miundombinu mingine ya uwanja huo iwe kwenye ubora ni lazima ipunguziwe majukumu.

''Tutaufunga uwanja wetu wa taifa kwa muda wa mwezi mmoja kabla ya mashindano kuanza ili kuweka sawa ubora wa miundombinu yake kwaajili ya michuano hiyo mikubwa Afrika'', amesema.

Michuano hiyo inaanza 14–28 April 2019 hivyo uwanja wa taifa utafungwa kuanzia Machi 14.

Kwasasa uwanja huo unatumika kwa mechi za ligi kuu soka Tanzania bara zinazohusisha vilabu vya Yanga, Simba pamoja na Azam FC inapocheza na timu hizo. Pia Simba inautumia katika michuano ya klabu bingwa Afrika.
Share:

KILICHOENDELEA LEO MAHAKAMANI KATIKA KESI YA MBOWE NA VIGOGO WENGINE CHADEMA

Kesi namba 112/2018 inayowakabili baadhi ya viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiwemo Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe na wabunge wengine saba wa chama hico, imeendelea leo, Alhamisi, Februari 14, kwa kutajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.


Kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambaye aliteuliwa kuwa Jaji, ilitajwa leo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kevin Mhina, ambapo shauri la kesi hiyo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na bado linasubiri rufaa ya kupinga dhamana iliyokatwa na upande wa mashtaka dhidi ya Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, ambayo itaanza kusikilizwa Februari 18, 2019 katika Mahakama ya Rufaa.


Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 28, 2019 kwa ajili ya kutajwa huku akieleza kuwa itapangiwa hakimu mara baada ya rufaa kusikilizwa.

Novemba 23, 2018 Jaji Mashauri alipokuwa hakimu mkazi mkuu wa mahakama ya Kisutu alifuta dhamana kwa Mbowe na Matiko kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.

Baada ya uamuzi huo, washitakiwa hao wanaowakilishwa na wakili Peter Kibatala walikata rufaa mahakama kuu kupinga kufutiwa dhamana.

Hata hivyo, baada ya mahakama kuu chini ya Jaji Sam Rumanyika kusikiliza mapingamizi ya pande zote iliamua kuanza usikilizaji wa rufaa hiyo.

Upande wa Serikali ukiongozwa na mwanasheria, Paul Kadushi ulikata rufaa katika mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na kuiomba mahakama kuacha kuendelea kusikiliza rufaa hiyo kwa sababu haina mamlaka.
Share:

MWENYEKITI WA CHADEMA APOTEA KUSIKOJULIKANA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Deusdedit Nsimeki ameeleza kuwa anafuatilia taarifa juu ya madai ya kupotea Mwenyekiti wa Kijiji cha Gijedubung anayetokana na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye anafahamika kwa jina la Faustine Kwaslema.

Kwa mujibu wa Kamanda Nsimeki, kwa sasa hana taarifa ya awali juu ya tukio hilo bali ameanza kulifuatilia ili kujua nini kilichotokea kwa mwenyekiti huyo ambaye inasemekana amepotea kusikojulikana mpaka sasa.

"Ngoja nifuatilie maana sijaipata bado kama mtu ametoweka vyombo vipo, wenye ndugu zao walitakiwa wapeleke taarifa polisi, ila na wao wanafanya makosa makubwa msemaji ni mimi nashangaa kwanini wao wanazungumza", amesema Kamanda Nsimeki.

Mapema leo kupitia mitandao ya kijamii kulianza kusambaa taarifa ya juu ya hali ya hofu na wasiwasi kufuatia kutoonekana kwa Mwenyekiti huyo wa Kijiji.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa ilimnukuu Mtendaji wa Kijiji, John Isdory ambaye amedai Faustine alitoka nyumbani kwake asubuhi ya Februari 9 akiwa na usafiri wa Pikipiki na hakurejea tena mpaka sasa.
Chanzo - EATV
Share:

SIMBA YAPATA KOCHA MSAIDIZI

Hivi karibuni mwekezaji na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya klabu ya Simba Mohammed Dewji aliweka wazi kuwa tayari wameshatoa maelekezo kwa CEO wa Simba Crescentius Magori kuhakikisha timu inapata kocha msaidizi jambo ambalo limekamilika.

Nafasi hiyo iliyoachwa wazi mwanzo mwa msimu huu na aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma, imezibwa na kocha mtanzania Denis Kitambi.

Kitambi amewahi kuzifundisha vilabu vya Ndanda FC akiwa kama kocha mkuu, Azam FC akiwa kocha msaidizi chini ya Stewart Hall ambaye pia alikwenda kufanya naye kazi kama kocha wake msaidizi katika klabu ya AFC Leopards ya Kenya.

Imeelezwa kuwa tayari amekwishajiunga na kambi ya timu hiyo jijini Dar es Salaam ambapo mchezo wake wa kwanza kukaa kwenye benchi la ufundi utakuwa ni dhidi ya Yanga Jumamosi hii.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger