Wednesday, 13 February 2019

NDEGE YAANGUKA NA KUUA WATU WATANO KENYA

 Watano wamefariki dunia leo Jumatano Februari 13, 2019 baada ya ndege ndogo waliyokuwa wanasafiria kuanguka katika kaunti ya Kericho nchini Kenya.

Ndege hiyo ilianguka kwenye msitu wa Londiani ikiwa na abiria watano, mkuu wa kikosi cha anga, Kamanda Rodgers Mbithi amesema abiria wote waliokuwa kwenye ndege hiyo wamefariki dunia.

Amesema waliopoteza maisha katika ndege hiyo Cesna 206-5-Y BSE ni wanaume watatu na wanawake wawili ambao hawajatambulika ni raia wa nchi gani.

Kwa mujibu wa kamanda wa kaunti ya Londiiani, Justus Munyao, ndege hiyo inamilikiwa na kampuni ya Safari ambayo huchukua abiria kutoka Ol Kiombo kuelekea Kaunti ya Turkana.

Amesena tukio hilo lilitokea saa 5 asubuhi kwenye msitu wa Masaita.

Kamanda wa Kikosi cha Rift Valley, Edward Mwamburi amesema polisi wameshafika eneo la tukio.
Via Mwananchi
Share:

UJUMBE WA GODZILLA KABLA YA KUFA ' HATA NIKIFA LEO JINA LANGU LITABAKIA'

Share:

FAMILIA YAPINGA RIPOTI YA POLISI KIFO CHA MWANAHARAKATI CAROLINE....YASISITIZA KAUAWA NA WASIOJULIKANA


Mwanaharakati Caroline Mwatha enzi za uhai wake
Baba na marafiki wa marehemu mwanaharakati Caroline Mwatha wamepinga ripoti ya polisi inayodai marehemu aliaga dunia akijaribu kutoa mimba yake

Wanasema mwenzao aliuawa kutokana na kazi yake ya kutetea haki za binadamu na kwamba jinsi mwili huo ulivyoletwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ni suala linalotatanisha.

Caroline Mwatha mwanaharakati aliyekuwa ametoweka alipatikana akiwa maiti katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Citry mnamo Jumanne, Februari 12,2019 huku polisi wakisema kifo chake kilisababishwa na jaribio la kutoa mimba.

Mama huyo wa watoto wawili alitoweka na kisa hicho kuripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Buruburu mnamo Jumatano, Februari 6, baada ya kumpeleka mwanawe shuleni.

 Kulingana na marafiki wa Mwatha, polisi wanafahamu ni nini kilimtokea marehemu kwa kuwa alichukuliwa na watu wasiojulikana kutoka nyumbani kwake.

 Akizungumza na wanahabari nje ya chumba cha maiti cha City, baba ya marehemu, Stanlus Mbai, alidai bintiye aliuawa kwa sababu ya kazi yake ya kutetea haki na ufichuzi kuhusu ufisadi eneo la Dandora, Kaunti ya Nairobi.

 "Hakika mbele zake Mungu, Caroline aliuawa kwa sababu ya kuamini katika ukweli, kifo chake hakijasababishwa na ugonjwa wala ajali, aliuawa kwa sababu ya kazi yake," baba yake Mwatha alisema.

 Bw Mbai alisema kwamba, mwanawe alihofia maisha yake na hivyo hakutaka wazazi wake kumfahamisha yeyote kuhusu kazi yake.

 Baba yake marehemu alihoji jinsi mwili wa marehemu ulivyowasilishwa katika chumba cha maiti cha City na ni mwanamume yupi huyo anayedaiwa kumpeleka Hospitali Kuu ya Kenyatta.

"Badala ya kuandika Caroline Mwatha, jina lake liliandikwa Caroline Mbeki, aliletwa City na mwanamke, twafahamu mwanzo alipelekwa Hospitali Kuu ya Kenyatta na mtu anayedai ni mume wake, mume wa Caro alikuwa Dubai wakati huo," baba alisema.

 Wakati huohuo, baba ya marehemu alidai kupokea simu kutoka kwa mtu asiyejulikana akimuuliza wapi alipofikia na shughuli ya kumsaka mwanawe, baadaye mwili ulipatikana City.

 Kilio cha baba kiliwahuzunisha hata na marafiki zake marehemu waliounga mkono kauli zake na kudai polisi wanafahamu kilichomtokea mwenzao.

 Inadaiwa kwamba, marehemu alichukuliwa nyumbani kwake kwa sababu ya kazi yake.

 "Caro ameaga kwa sababu ya kupigania haki za vijana, na polisi wanafahamu alivyokufa. Tunawataka watetezi wa haki za binadamu wote kutohofu kwa sababu kilichomtokea Caroline Mwatha kinaweza mtokea yeyote kati yetu" mmoja wa marafiki alisema.

Aidha kuna madai kutoka kwa marafiki zake marehemu kuwa, sajili waliyoikuta awali sio waliyoikuta wakati wa kuusaka mwili wa marehemu. 

Mama huyo wa watoto wawili alitoweka na kisa hicho kuripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Buruburu mnamo Jumatano, Februari 6, baada ya kumpeleka mwanawe shuleni. 

Share:

AKUTANA NA CHUI AKIVUTA BANGI

Share:

POLISI WASEMA MWANAHARAKATI CAROLINE AMEFARIKI AKITOA MIMBA YA MCHEPUKO

Share:

KESI KUPINGA WAKURUGENZI KUSIMAMIA UCHAGUZI YAKWAMA KORTINI


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali pingamizi la serikali kwenye shauri la kupinga utaratibu wa kuteuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri kuwa wasimamaizi wa uchaguzi.

Kesi hiyo iliyofunguliwa na Mwanaharakati Bob Chacha Wangwe ambapo leo tarehe 13 Februari 2019, mahakama imeelezea kuwa, waombaji wanahaki ya kisheria kufungua shauri hilo.

Awali serikali ilitaka kesi hiyo itupiliwe mbali kwa sababu, waombaji hawakustahili kufika mahakamani na badala yake kwenda kulalamika kwenye utawala wa tume.

Tarehe ya kuendelea kusikilizwa kesi hiyo itatajwa saa nane mchana baada ya mahakama kurejea tena.

Bob Chacha Wange kupitia wakiliwa wake Fatma Karume amemshtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) na mkurugenzi wake.

Bob Chacha Wangwe amefungua kesi hiyo kikatiba baada ya kuamini kuwepo kwa udhaifu wa tume hiyo. Amedai kuwa, tume hiyo inaongozwa na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao hawaendishi uchaguzi wa haki.

Bob Chacha Wange ni mtoto wa marehemu Chacha Wangwe aliyewahi kuwa Mbunghe wa Tarime mjini (Chadema).

Chanzo - Mwanahalisi online 
Share:

COCA-COLA YAZINDUA KINYWAJI KIPYA CHA SCHWEPPES +C


Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa fedha wa Coca Cola Kwanza Bw. Erastus Mtui akifatiwa na Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Coca Cola Kwanza Bi. Josephine Msalilwa, Mkurugenzi wa Logistics Bw. Pankaj Singh pamoja na Mkurugenzi wa mawasiliano na Matukio ya kijamii Bw. Haji Ally wakiwa kwenye Uzinduzi wa Kinywaji Kipya cha Schweppes +C.
Maneja Masoko na mauzo wa kampuni ya Coca Cola Kwanza Bi. Josephine Msalilwa akielezea kuhusu ladha tamu ya Kinywaji Kipya cha Schweppes +C
Kampuni ya Coca-Cola Tanzania, imezindua kinywaji kipya chenye ladha ya limao kinayojulikana kama Schweppes +C, ikiwa ni sehemu ya kuongeza machuguo ya bidhaa kwa wateja wakeKinywaji cha Schweppes +C kinawalenga zaidi wateja wenye umri mkubwa.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa kinywaji hicho jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola Basil Gadzios, alisema kampuni yake imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye ugunduzi na kuongeza idadi ya bidhaa tofauti tofauti ikiwa na lenga la kukidhi mahitaji ya wateja tofauti tofauti katika soko la Tanzania.

Tunayofuraha kuongeza bidhaa nyingine mpya sokoni ikiwa ni shehemu ya jitihada za kukidhi mahitaji ya wateja wetu. Schweppes +C yenye ladha ya limao inawaletea wateja wetu ladha ya kipekee ya limao ikiwa na Vitamini C ambayo tunaamini wataifurahia. Kinywaji kimetengenezwa mahsusi kumpa mtumiaji wake ladha nzuri ya juisi ya limao. Tukiwa kama kampuni ya vinywaji baridi, tumejidhatiti kuwaletea wateja wetu kilicho bora na bado tuna vingi kwa ajili yao, alisema mkurugenzi huyo.

Gadzios aliongeza kuwa, Coca-Cola inatarajia kuingiza sokoni bidhaa nyingine nyingi ambazo siyo tu zitakidhi mahitaji ya jamii ya leo bali pia zitaendana na wateja ambao mahitaji yao hubadilika katika soko la kileo huku akiongeza kuwa kinywaji hicho kipya kimetengenezwa kwa kuzingaatia viwaango vyaa kimataifa kikiwa na ladha ya kipekee ya limao.

“Kuwashirikisha wateja wetu, ni moja kati ya vipao mbele vya kampuni ya Coca-Cola. Hii inatusaidia kuyafahamu mahitaji yao ambayo hubadilikakulingana na muda na hivyo kutuwezesha kuwatengenezea bidhaa zinazoendana na mahitaji na matakwa yao kuwashirikisha.

Kuongezwa kwa Vitamin C kwenye kinywaji kipya cha Schweppes +C, kunakifanya kinywaji hiki kitofautiane na vinywaji vyetu vingine vilivyopo sokoni huku kikiwapa wateja ladha murua ya limao, alieleza.
Share:

WANACCM KAGERA WACHANGIA UJENZI WA DARASA LA SEKONDARI


Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kagera, Ramadan Kambuga (aliyevaa shati ya rangi ya njano) akiwaongoza makada wenzake wa chama hicho katika ujenzi wa chumba cha darasa katika Sekondari ya Kalema Kata Buendangabo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM.
Bw. Ramadan Kambuga akipanda mti katika eneo la shule hiyo.

Bw. Ramadan Kambuga, akiwa na makada wenzake wakati wa ujenzi wa darasa hilo. 

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa Kushirikiana na viongozi wa chama hicho ngazi ya Wilaya Bukoba mjini mkoani Kagera wameshiriki zoezi la usombaji mawe kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha darasa katika Shule ya Sekondari ya Kalema Kata Buendangabo na kupanda miti ikiwa ni kuazimisha miaka 42 ya
kuzaliwa kwa chama hicho. 

Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa chama hicho Mkoa wa Kagera, Ramadan Kambuga ambaye pia ameshiriki zoezi hilo,amesema kuwa ujenzi wa chumba hicho cha darasa ni utekelezaji wa ilani ya CCM. 

Kutokana na msongamano wa manafunzi darasani katika shule hiyo Bwana Kambuga ametoa kiasi cha shilingi laki moja ili isaidie kuongeza nguvu na kuweza kuondoa adha hiyo ambayo inawakabili wanafunzi wa shule hiyo. 

Bwana Kambuga pia amesema wao kama wadau wa maendeleo na wasimamizi wa serikali kupitia Chama cha Mapinduzi wataendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali  ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Share:

Breaking : MWIGULU NCHEMBA APATA AJALI,KAKIMBIZWA DODOMA

Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba (CCM) amepata ajali ya gari akiwa njiani barabara ya Iringa kuelekea Dodoma na amekimbizwa hospitali ya Dodoma. 


Taarifa zaidi zitakujia hivi punde.

Share:

BREAKING NEWS:ALIYEKUWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA APATA AJALI

Taarifa za hivi punde zinaeleza kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, kwa sasa Mbunge wa Iramba Magharibi, Dkt. Mwigulu Nchemba amepata ajali ya gari.  Kiongozi huyo amepta ajali akiwa njiani barabara ya Iringa kuelekea Dodoma na amekimbizwa hospitali ya Dodoma.

Source

Share:

MSANII WA MUZIKI GODZILLA AFARIKI DUNIA

Tasnia ya Muziki nchini imepata pigo kwa kumpoteza Golden Mbunda maarufu kama Godzilla, aliyefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam. Ingawa bado haijatolewa taarifa rasmi ya chanzo cha kifo cha rapa huyo mahiri, watu wa karibu wa msanii huyo wameleeza kuwa chanzo cha kifo chake ni shinikizo la damu pamoja na tatizo la tumbo. Mtu wa karibu wa Msanii huyo aliyejitambulisha kwa jina la Isabella ambaye alikuwa naye mara ya mwisho jana, saa chache kabla ya kufariki dunia, amesema msanii huyo alizidiwa ghafla akiwa…

Source

Share:

Tanzia : MSANII WA HIPHOP GODZILLA AFARIKI DUNIA

Msanii maarufu wa muziki Hip Hop Golden Mbunda maarufu Godzilla amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo Jumatano, February 13, 2019 akiwa nyumbani kwao, maeneo ya Salasala, DSM. Mwili wake umehifadhiwa ktk Hospitali ya Jeshi ya Lugalo.
Mtu wake wa karibu ameeleza kuwa presha ilishuka na sukari ilipanda pamoja na kuumwa na tumbo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, Godzilla amefariki dunia ghafla nyumbani kwao Salasala jijiji Dar es Salaam. Mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo.
Share:

Tuesday, 12 February 2019

Breaking : SHABIKI WA SIMBA SC SHINYANGA AFARIKI AKISHANGILIA USHINDI DHIDI YA AL AHLY


Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Janturu maarufu Mtaturu (40 -45) mkazi wa Katunda Mjini Shinyanga amefariki dunia muda mfupi baada ya Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba SC na Al Ahly kwenye mchezo wa Kundi D jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. 

Jamaa huyo anayedaiwa kuwa shabiki damu wa Simba SC amefariki dunia ikielezwa kuwa alikuwa akishangilia ushindi wa Simba SC ambayo imewafunga Al Ahly bao 1-0. 

Mashuhuda wa tukio wameiambia Malunde1 blog kuwa shabiki huyo wa Simba SC alikuwa na furaha kupita kiasi baada ya timu yake kupata bao hilo. 

“Huyu jamaa ni Muuza Nyama duka lake limeandikwa Mtaturu Butcher,lipo kona ya Buhangija.. Ni Mpenzi sana wa Simba SC, alikuwa kwenye kibanda cha kuangalizia mpira karibu na Stand ya Mabasi Ibinzamata,baada ya Simba SC kupata bao la kwanza,alichukua nguo nyekundu ya Simba na kulazimisha kumvalisha mtani wake shabiki wa Yanga,lakini shabiki huyo wa Yanga aliichana hiyo nguo, 

…mpira ulipomalizika ukatokea mzozo flani hivi akidai nguo yake iliyochanwa ,hata hivyo hawakupigana, baada ya hapo jamaa aliondoka kibandani, hatua kadhaa akaanguka na kuanza kutoa mapovu,amefariki akipelekwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga”,wanaeleza mashuhuda wa tukio hilo. 

Inaelezwa kuwa jamaa huyo ni shabiki damu wa Simba SC,na timu yake hiyo ilipofungwa bao 5-0 na Al Ahly hakuwa na raha takribani siku tatu. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule ameiambia Malunde1 blog kuwa bado hajapata taarifa kuhusu tukio na kuahidi kutoa taarifa baadaye. 

Malunde1 blog bado inafuatilia kwa ukaribu zaidi kuhusu tukio hili,Tutawaletea taarifa kamili hivi punde

Share:

JKT TANZANIA YAICHARAZA USALAMA FC YA MANYARA 4 -0


Na Beatrice Mbise - Manyara

Timu ya mpira wa miguu ya JKT Tanzania inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara imeicharaza goli nne kwa sifuri timu ya Usalama FC ya mkoa wa Manyara ambayo inashiriki ligi daraja la pili.

Katika mchezo huo wa kirafiki ambao umechezwa leo katika uwanja wa shule ya Singe Sekondari ya mjini Babati mkoani Manyara Afisa Habari wa JKT Tanzania Jamillah Mutabazi ameeleza umuhimu wa wao kucheza mchezo wa kirafiki kabla ya kukutana na timu ya Singida United ya mkoani Singida.

"Katika mchezo huu sisi JKT Tanzania tumeibuka mshindi kwa kufunga goli nne kwa bila, lengo la kufanya mchezo huu kwanza kabisa ni kuweka ule ukaribu, urafiki na ujirani baina yetu sisi na wenzetu wa timu ya Usalama FC, ni mchezo wa kirafiki ambao kwetu sisi ni wa faida kwa sababu kwanza wachezaji wanakuwa wanapata nafasi ya kufahamiana na kujuana.

"Mchezo huu umetuweka sehemu nzuri kwa sababu licha ya kwamba tunaweka miili fiti kwa ajili ya mchezo unaofuata ambao ni wa 'FA' tunaoenda kucheza mjini Singida lakini jinsi ambavyo mchezo ulikuwa ni wa taff mchezo mzuri wa kasi kwa wachezaji umekuwa wa faida kwao kwa sababu siku zote mazoezi ukifanya mwenyewe unashindwa kujitathmini kwamba uko kwenye position gani, lakini ukipata mtu ambaye unaweza uka compit nae ni kitu ambacho kitakujenga zaidi", amesema Mutabazi.

Kwa upande wake Afisa Habari wa timu ya Usalama FC ya mkoani Manyara Elia Kimani amesema kuwa huo ni mchezo wa kirafiki ni mchezo ambao umekuja ghafla na walikuwa hawajajiandaa kama wangekuwa na mechi ambapo mechi ilikuwa ipigwe jana ghafla lakini haikuchezwa kwa hiyo sio mchezo ambao utasema unakatisha watu tamaa kwa kuwa sio wa ligi.

"Kwenye ligi tuna mwenendo sio mzuri sana na wala sio mbaya sana kwa sababu sisi sio moja ya timu ambazo zinaenda kushuka daraja, sisi tunaendelea kubaki ligi daraja la pili kwa mwenendo lakini tayari tunaweka mipango kwa ajili kujipanga kwa msimu ujao.

"Timu imecheza vizuri wachezaji wamejitahidi kadri ya uwezo lakini mzoefu ni mzoefu tu, wametuzidi kwenye uzoefu tu sioni kama wametuzi sana kwenye kiwango kwa sababu tulikuwa tumeshawakata baadhi ya sehemu kwa hiyo hakuna suala la kukata tamaa hapo",amesema.

Huu ni mwendelezo wa maandalizi ya mechi ambazo timu ya Usalama FC wanataraji kuzimalizia mechi za ligi daraja la pili katika ngwe ya mwisho ambayo wanaelekea kumaliza na mechi hizo mbili zitachezwa hapa mjini Babati. 

Kikosi cha JKT Tanzania kimetokea mkoani Tanga ambapo katika mchezo uliopita walimenyana na kikosi cha Yanga SC ambapo walipoteza mchezo huo kwa kukubali kichapo cha goli moja.
Share:

TULIA TRUST YAKABIDHI VIFAA VYA UJENZI SHULE YA SEKONDARI KINYALA

Mbeya Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson,imekabidhi vifaa vya ujenzi kwa shule ya sekondari ya Kinyala wilayani Rungwe nkoani Mbeya. Akikabidhi vifaa hivyo meneja Tulia Trust Bi.Jacqueline Boaz amesema vifaa vya ujenzi vilivyokabidhiwa ni pamoja na mabati bando 13 yenye thamani ya shilingi milioni tano kwa shule ya sekondari Kinyala ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyo itoa Naibu Spika Dr.Tulia Ackson wakati wa harambee iliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa mwaka jana. BibJacqueline ameongeza kuwa katika harambee ile naibu…

Source

Share:

JAMAA AMNYONGA SIMBA HADI KUFA

Kama kuliwahi kuwapo duniani mtu aliyekuwa na uwezo wa kupambana na simba kwa mikono yake hadi kumuua mtu huyo ni lazima awe ni Samsoni kwani maandiko ya Bibilia yanasema alikuwa mtu mwenye nguvu za ajabu.

 Lakini juzi kulitokea mtu mwingine anayeweza kulinganishwa na Samson katika eneo la kaskazini mwa Colorado, Marekani

Mwanamume huyo alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia na hakuwa na silaha yoyote na hivyo ilimbidi kujitetea kwa jiwe kisha mikono yake na akafaulu kumuua simba huyo.

 Kwa mujibu wa ripoti ni kwamba, maafisa wa sekta ya uhifadhi wa wanyama pori walisema mwanamume kutoka eneo la kaskazini mwa Colorado, Marekani alimuua simba kwa kumnyonga, baada ya mnyama huyo kumvamia ghafla. 

Inaelezwa kuwa mwanamume huyo alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia karibu na makavazi ya Fort Collins wakati alipovamiwa na simba huyo kutoka nyuma. 

Msemaji wa mbuga ya Colorado Rebecca Ferrell alisema kuwa mwanamume huyo alifahamisha maafisa wa uchunguzi kuwa alimnyonga simba huyo hadi kufa, jambo ambalo lilithibitishwa na ripoti ya upasuaji iliyofanyiwa mzoga wa simba huyo. 

Ferrell alisema kuwa mwanamume huyo alifanya vyema kwa kupigana na mnyama huyo kujitetea kadri ya uwezo wake. 

Kwa kuwa alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia, hakuwa na silaha yoyote na hivyo ilimbidi kujitetea kwa jiwe kisha mikono.

 Ripoti ya Fox News ya Jumamosi, Februari 9 ilisema, baada ya vita vikali na kumuua mnyama huyo hatari, bwana huyo alijipeleka hospitalini kwa kuwa alikuwa amejeruhiwa usoni, mikononi, miguuni na mgongoni. 

 Uvamizi wa simba dhidi ya binadamu katika milima huwa haushuhudiwi kirahisi, kwani tangu 1990 ni watu 16 pekee waliovamiwa na wanyama hao na watatu kati yao waliuawa. 
Share:

KIJANA AMBAKA NA KUMUUA BIBI WA MIAKA 77 DODOMA


Picha ya mfano wa bibi

 Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la William Saimon, mkazi wa Bihawana, Jijini Dodoma anatuhumiwa kuhusika na tukio la kumkaba na kumbaka bibi kizee mwenye umri wa mika 77.

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma amesema Februari 11, 2019, saa 5: 55 usiku, bibi kizee aliyejulikana kwa jina la Jema Macheho (77) amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitali ya rufaa mkoa wa Dodoma baada ya kukabwa shingo kisha kubakwa na kijana huyo pamoja na wenzake vijana wengine wawili.

Kwa mujibu wa Kamanda Muroto, mtuhumiwa mmoja tayari ameshakamatwa na wenzake wawili bado wanaendelea kusakwa kwa ajili ya kuwafikisha katika vyombo vya dola. 

Aidha katika tukio lingine Kamanda Muroto amesema watu wengine wakiwamo raia wa China wamekamatwa wakiwa na mashine 68 za kuchezeshea kamari maeneo mbalimbali ya mkoa huo zilizohifadhiwa katika baa, maduka, grocery na vituo vya usafiri.

Kamanda Muroto amewatahadharisha wananchi wa mkoa wa Dodoma kuepukana na uhalifu kwani hakuna mtu ambaye atabaki salama kwakuwa uhalifu haulipi.
Chanzo - EATV
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger