Tuesday, 12 February 2019

Wizara ya elimu:: USA scholarship Opportunities Academic Year 2019

Study opportunity tenable in the united state of america for academic year 2019

1.0 Call for Application

The general Public is hereby informed that, the United States Embassy Public Affairs’ Section is now accepting application for 2020 Fulbright Foreign Student Programme to pursue Master`s and Doctorates Degrees offered in the US Universities for the academic year 2019.

U.S. Embassy encourages candidates with disabilities to apply as special accommodations are available.

2.0 Mode of Application

Applications must be submitted online using the Embark Visiting Scholar system, accessible at https://apply.iie.org/ffsp2020The submission deadline for applications is April 5, 2019. For more information, please email drs_exchanges@state.gov.

For more information please refer to the following link https://tz.usembassy.gov/education-culture/educational-exchange-programs/fulbright-program/fulbright-jsd/

Issued by

Permanent Secretary,

Ministry of Education, Science and Technology,

College of Business Studies and Law,

Universities of Dodoma (UDOM) Building No. 10,

P. O. Box 10,

40479 DODOMA.

The post Wizara ya elimu:: USA scholarship Opportunities Academic Year 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Monday, 11 February 2019

Wimbo Mpya : NYANDA BHETELI - NAKUTAMBULILE


Hii hapa ngoma mpya ya msanii Nyanda Bheteli kutoka Kahama mkoani Shinyanga inaitwa Nakutambulile,imetengenezwa Lwenge Studio Kahama 0757396248/ 0688032828. Isikilize hapa chini
Share:

Ngoma Mpya : MWANAKWELA - HURUMA

Msanii wa nyimbo za asili kutoka Kahama, Mwanakwela anatualika kusikiliza ngoma yake inaitwa Huruma..imetengenezwa Lwenge Studio Kahama 0757396248/ 0688032828
Share:

WATENDAJI SEGEREA WAKOSA UAMINIFU KWENYE FEDHA ZA SERIKALI

Na Heri Shaban MBUNGE wa Segerea Bonah Ladislaus(CCM) amewalalamikia Watendaji kwa kukosa uaminifu katika fedha za Serikali. Bonah aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara Kata ya Vingunguti Jimboni Segerea Dar es salaam uliofanyika katika kata hiyo hii leo. Aidha alisema Rais wa awamu ya tano John Magufuli ametoa shilingi bilioni 2 kwa ajili ya miundombinu ya afya hivyo ni vema watendaji kushirikiana kikamilifu katika kuzisimamia ili miradi ikatekelezeke sawa sawa na ilivyopangwa. “Serikali imeleta fedha za kutosha shilingi bilioni 2 Jimbo la Segerea changamoto kubwa iliyokuwepo tuna watendaji wasio waminifu…

Source

Share:

Wimbo Mpya : BHULEMELA THOMAS - BHALOMOLOMO

Huu hapa wimbo mpya wa Msanii wa Nyimbo za Asili Bhulemela Thomas kutoka Kahama Shinyanga inaitwa Bhalomolomo. Imetengenezwa Lwenge Studio 0757396248/0688032828 .Sikiliza hapa
Share:

SIMBA YAWAOMBA RADHI MASHABIKI WAKE, KUELEKEA KWENYE MCHEZO DHIDI YA AL AHLY

Na Shabani Rapwi. Klabu ya Simba SC imewaomba radhi mashabiki wake kuelekea kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaopigwa siku ya kesho Jumanne kwenye dimba la Taifa, Jijini Dar es Salaam, Saa 10:00 Jioni, kuwa tiketi za Platinum hazitakuwepo kwenye mchezo huo. Taarifa iliyotolewa hii leo Jumatatu na klabu hiyo kupitia mtandao wa Twitter kuwa tiketi za Platinum hazitakuwepo kwenye mchezo wa hapo kesho dhidi ya Al Ahly kama awali ilivyo tangazwa, huku walikuwa wameshanunua tiketi hizo watarudishiwa pesa zao na…

Source

Share:

MKUU WA MAJESHI NCHINI ATUA MKOANI NJOMBE

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo amefanya kikao na Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani humo kuhusu matukio ya mauaji ya watoto yaliyoanza Novemba mwaka jana. Jenerali Mabeyo ambaye ni Mwenyekiti wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama amesema kuwa yuko mkoani humo kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya zoezi la kukabiliana na matukio hayo kwakuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinashirikiana. “Vyombo vyote vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kwa kushirikiana ikiwa ni pamoja na jeshi. Na mimi kama Mwenyekiti wa vyombo vyote vya ulinzi…

Source

Share:

IRAN KUENDELEA NA MPANGO WA NYUKLIA

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema nchi yake imepania kutanua nguvu zake za kijeshi na mpango wake wa silaha za nyuklia licha ya shinikizo kutoka kwa nchi alizozitaja kuwa mahasimu zinazotaka kudhibiti uwezo wake wa kujihami.

 Akiwahutubia maelfu ya watu waliojitokeza katika ukumbi wa Azadi mjini Tehran kuadhimisha miaka 40 tangu Mapinduzi ya Kiislamu, Rouhani amesema hawajawaomba yeyote wala hawataomba ruhusa kutengeza aina mbali mbali za makombora na wataendelea na njia yao ya kujiongeza nguvu za kijeshi.

 Mamilioni ya watu wanahudhuria maadhimisho hayo ya miaka 40 tangu mapinduzi ya Kiislamu katika mji mkuu Tehran na miji mingine, siku inayokuchukuliwa kama ushindi wa mapinduzi yaliyoung'oa utawala wa Kifalme mnamo tarehe 11 Februari, 1979.

Chanzo:Dw
Share:

ATANGAZA KUUZA NYETI ZAKE KISA KAFIRISIKA BAADA YA KUKOSA UDIWANI


Mwanamume mmoja aliyebwagwa kwenye kinyang’anyiro cha udiwani katika kaunti ya migori anayedai kuwa amefirisika, ametangaza kutaka kuuza nyeti zake kwa Ksh 500,000 ambazo ni sawa na zaidi ya milioni 11 za Tanzania.

Mwanaume huyo anayejulikana kwa jina la Ian- Harriet Kowiti kutoka eneo la Uriri, Kaunti ya Migori nchini Kenya amesema kuwa amechoshwa na maisha ya ukata, na sasa ameamua kutafuta pesa kwa kuuza korodani moja.

Pia mwanaume huyo amesema kwamba yuko tayari kuuza figo moja kwa Sh1.5 milioni za Kenya ambazo ni sawa na zaidi ya milioni 34 za Tanzania, kwa mteja wa nchini humo, au mara tatu ya pesa hizo kwa mteja kutoka nje ya nchi.

“Ina haja gani kuwa na korodani mbili kati ya miguu yangu wakati hata nikiwa na moja bado naweza kufanya ‘kazi’ vyema? Nataka kuuza kwa kuwa nimekosa pesa na pia sihitaji korodani mbili ili kuishi. Najua kuna mtu mahali amekosa mtoto kwa ajili ya tatizo kama hili,” amesema Kohiti.

Katika uchaguzi uliopita, Kowiti ambaye ana miaka 27 alijaribu kuwania kama mgombea huru katika wadi moja, lakini akabwagwa, amesema kuwa anapanga kuuza sehemu hiyo ili kuboresha maisha yake.
Share:

MKUU WA MAJESHI ATINGA NJOMBE SAKATA LA MAUAJI YA WATOTO


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, akiwasili Mkoani Njombe.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo ametinga mkoani Njombe na kufanya mkutano wa ndani na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe pamoja na vikosi maalumu vilivyopo mkoani humo kwa ajili ya kuchunguza matukio ya mauaji ya watoto.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe Mabeyo amesema “vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kwa kushirikiana pamoja na jeshi, na mimi ndiye mwenyekiti wa vyombo vyote vya ulinzi hivyo ninaowajibu na si kwamba jeshi limeingia sasa, hapana hatujafikia hatua ya kuingiza jeshi,”

"Wananchi karibu nchi nzima wamesikia kinachoendelea Njombe, wengine yamewatia hofu lakini si Tanzania tu mpaka nje ya mipaka yetu taarifa zimesambaa,” amesema.

“Kwa hiyo pasiwepo na hofu suala hili ni la kitaifa zaidi, linahusu pengine familia moja moja sababu zinajionesha kabisa ni za kifamilia zaidi,” amesema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Renatha Mzinga amesema watuhumiwa 30 wanashikiliwa kutokana na kuhusika kwao na utekaji na mauaji ya watoto hao.
Share:

TUNDU LISSU ASIMULIA JINSI "MAZISHI YAKE YALIVYOANDALIWA"


Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antiphas Lissu amesema anahofia kutaja majina ya watu waliomtahadharisha kuhusu namna mazishi ya kifo chake namna yalivyopangwa kwa kuwa hataki watu hao wapitie matatizo ambayo yeye tayari amekwishapitia.

Akizungumza na watanzania waishio Marekani, Lissu amesema kwamba alipatiwa taarifa na watu ambao hana mashaka nao kwamba siku aliposhambuliwa ilipangwa kuwa akifa asipelekwe Dar es salaam wala bungeni bali apelekwe akazikwe kijijini kwao.

Lissu amesema kwamba ipo siku itafika na majina atayataja, na kwamba watu hao watakuwa salama kwa kuwa yeye tayari ameshanusurika risasi 16 na hataki watu wapitie yeye alipopitia.

"Someone ambaye sitilii shaka maneno yake aliniambia the order was akifa, hakuna shughuli Bungeni na msimlete Dar mkimbizeni kijijini mkamzike as soon as possible. Nahofia kutaja majina ila kuna siku nitayataja. Itakapokuwa salama kwao, si kwangu maana mimi ni survivor wa 16 bullets".

Pamoja na hayo Lissu ameeleza kwamba yeye anamarafiki wengi ndani ya Chama Cha Mapinduzi lakini kitendo cha viongozi ndani ya chama hicho kushindwa kwenda kumuona ni kutokana na kikao walichokalishwa na kuonywa (pasipo kumtaja jina) kwamba wasishabikie tukio lililompata.

Chanzo - EATV
Share:

MKURUGENZI WA ITIGI AFIKISHWA MAHAMANI TUHUMA MAUAJI YA MUUMINI KANISANI


 Mkurugenzi wa halmashauri ya Itigi, Pius Luhende (54) na washtakiwa wengine sita leo Jumatatu Februari 11, 2019 wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoani Singida wakikabiliwa na shtaka moja la mauaji ya Isaka Petro.

Washtakiwa wengine ni Rodney Elias, Makoye Stephen, Erick Paul ,Eliutha Augostino, Silivanus Lugwisha na Yusuf John (25).

Mwanasheria wa Serikali mkuu, Emil Kiria amedai mbele ya hakimu mkazi mfawidhi, Consolata Singano kuwa Februari 2, 2019 eneo la genge 48 kijiji cha Kazikazi kata ya Kitaraka tarafa ya Itigi, washitakiwa kwa pamoja walimuua Petro.

Kiria amesema washitakiwa hao walifanya kosa hilo kinyume na sheria kanuni ya adhabu kifungu cha 116 na 197.

Washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Kiria amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kuiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine ya kutaja kesi hiyo.

Hakimu Singano amesema kwa vile kosa hilo halidhaminiki, washitakiwa wataendelea kuwa chini ya ulinzi hadi Februari 25, 2019 itakapotajwa tena.
Na Gasper Andrew, Mwananchi 
Share:

WAMBURA ASOMEWA MASHTAKA 17 LIMO LA UTAKATISHAJI FEDHA MIL 75

Aliyekuwa Makamu wa Rais TFF, Michael Wambura amesomewa mashitaka 17 Mahakamani Kisutu ikiwemo utakatishaji fedha Mil.75

Kesi imeahirishwa hadi Feb. 14 kwa ajili ya Hakimu kuamua kama aifute kesi ama la, Wambura amepelekwa rumande kusubiri uamuzi wa Mahakama.
Share:

WAMBURA AACHANA NA SOKA

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura kupitia kwa Mwanasheria wake Emmanuel Muga imeelezwa kuwa ameridhia adhabu ya kufungiwa Maisha na TFF na FIFA.  Pamoja na hayo Wambura kupitia kwa mwanasheri wake Emmanuel Muga ametangaza kuwa kwa sasa kuanzia leo February 11 2019, anaachana rasmi na shughuli za mpira wa miguu, atabaki kama mtu wa kawaida tu. Hata hivyo Wambura pia ameamua kufuta kesi zote alizokuwa amezifungua kuhusiana na kupinga maamuzi ya kamati ya maadili ya TFF.

Source

Share:

KIKWETE AWASILI NIGERIA KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU

Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewasili Abuja, nchini Nigeria kuongoza Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola kwenye Uchaguzi Mkuu nchini humo. Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Februari 16 mwaka huu. 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Kikwete ameandika; "Nimewalisi Abuja, Nigeria kuongoza Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola kwenye Uchaguzi Mkuu wa Nigeria unaotarajiwa kufanyika tarehe 16 Februari 2019 kufuatia ombi la Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola. "

Share:

PAPA FRANCIS AMTEUA ASKOFU NKWANDE KUWA ASKOFU MKUU JIMBO KUU LA MWANZA


Baba Mtakatifu Francisko ametemua Askofu Renatus Leonard Nkwande wa Jimbo Katoliki la Bunda, kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza, Tanzania. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule alipadrishwa kunako mwaka 1995.

 Tarehe 27 Novemba 2010, akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Bunda na kuwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 20 Februari 2011 na Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, utume ambao ameutekeleza kwa muda wa miaka 7 kama Askofu na miaka 23 kama Padre.

 Jimbo kuu la Mwanza lilikuwa wazi, baada ya Baba Mtakatifu Francisko kumteua Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwa'ichi kuwa Askofu mkuu mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Dar es Salaam hapo tarehe 21 juni 2018.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Renatus Leonard Nkwande wa Jimbo kuu la Mwanza, alizaliwa kunako tarehe 12 Novemba, 1965, Parokia ya Sumve, Jimbo kuu la Mwanza. Alipata masomo yake ya sekondari, Seminari ya Makoko, Jimbo Katoliki la Musoma na baadaye Nyegezi, Jimbo kuu la Mwanza. 

Kunako Mwaka 1987 alijiunga na Seminari Kuu ya Kibosho, Jimbo Katoliki la Moshi, kwa ajili ya masomo ya Falsafa na baadaye mwaka 1989 aliendelea na masomo ya Taalimungu Seminari kuu ya Segerea, iliyoko Jimbo kuu la Dar es Salaam. 

Alipadrishwa kunako tarehe 2 Julai 1995 akiwa ni Padre wa Jimbo kuu la Mwanza.

Tangu alipopadrishwa amefanya shughuli mbali mbali za kichungaji kama Paroko msaidizi, Gombera wa Seminari ndogo ya Nyegezi, Jimbo kuu la Mwanza na baadaye kunako mwaka 2002 hadi 2005 alikwenda Roma kwa masomo ya Sheria za Kanisa, kwenye Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana. Tangu mwaka 2008 hadi 2009 alikuwa ni Makamu wa Askofu, Jimbo kuu la Mwanza. 

Na baadaye mwaka 2009 aliteuliwa kuwa msimamizi wa Kitume wa Jimbo kuu la Mwanza kufuatia kifo cha Askofu mkuu Athony Mayala.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Share:

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA 11.02 2019 SOLSKJAER KUBAKI OLD TRAFORD

Ole Gunnar Solskjaer anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha wa kudumu wa klabu ya Manchester United, lakini klabu hiyo inatazamiwa kusubiri mpaka mwisho wa msimu ili kutoa tangazo hilo. (Sun)

Kocha Rafael Benitez amempigia chapuo kiungo raia wa Paraguay Miguel Almiron, 25, tkuwa atafanya vyema klabuni hapo mara baada ya kuvunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo. (Guardian)

Peter Schmeichel amedai kuwa mtoto wake ambaye ni kipa wa Leicester City Kasper, 32, anapanga kuihama klabu hiyo kwa kuwa hana furaha ya Maisha chini ya kocha Claude Puel. (Sun)

Wolves ndiyo vinara katika mbio za kumsajili kinda raia wa Ureno Joao Felix, 19, na tayari kocha Nuno Espirito Santo kameeleza nia ya kumtaka kiungo huyo wa Benfica. (Mirror)

Solskjaer amemuhakikishia kiungo raia wa Brazil Fred, 25, kuwa yupo kwenye mipango yake, baada ya kumng'oa kumuondoa kwenye kikosi kilichoivaa Fulham mwishoni mwa wiki. (Manchester Evening News)

Chelsea watataka kupewa mchezaji raia wa Ivory Coast iFranck Kessie, 22, endapo AC Milan watataka kumsajili moja kwa moja kwa moja kiungo wake raia wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 24. (Daily Star)
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger