Tuesday, 5 February 2019

Picha : RAIS MAGUFULI AKINUNUA NA KUNYWA MADAFU MTAANI DAR



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa na Katibu Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole kunywa Dafu alilonunua kwa mjasiriamali Paschal Sabas mara baada a kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la CCM (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.Picha na Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akinywa Dafu alilonunua kwa mjasiriamali Paschal Sabas mara baada a kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza Wajasiriamali wadogo Paschal Sabas Mjasiliamali wa Madafu pamoja Dunia Seleman Simba Mjasiliamali wa Miwa mara baada ya kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la CCM  (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlipa pesa Paschal Sabas Mjasiliamali wa Madafu mara baada kununua Madafu yake, alipotembelea ili kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la CCM  (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlipa pesa Paschal Sabas Mjasiliamali wa Madafu mara baada kununua Madafu yake, alipotembelea ili kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la CCM  (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlipa pesa Paschal Sabas Mjasiliamali wa Madafu mara baada kununua Madafu yake, alipotembelea ili kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufguli na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole wakimsikiliza Msimamizi wa Ujenzi wa ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega wa Kitega Uchumi la CCM  (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufguli na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Ujenzi wa ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
Picha na Ikulu
Share:

DAWA ZA MITI ZA KUTIBU UKIMWI ZAMTOKEA PUANI MCHUNGAJI WA KANISA

Mahakama nchini Zimbabwe imemlima faini ya dola 700 mchungaji mmoja mashuhuri nchini Zimbabwe baada ya kumkuta na hatia ya kudanganya kuwa ana dawa ya miti shamba inayotibu Ukimwi.

Walter Magaya awali alikiri mashtaka ya kuvunja sheria Udhibiti wa Dawa ya nchi hiyo kwa kuuza dawa ambazo hajithibitishwa.

Polisi walimkamata mwezi Novemba 2018, na kuzuia dawa hizo ambazo alisema zinawatibu watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

Zimbabwe ni nchi ya sita ya kiafrika kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kuwa na maambukizi ya kasi ya virusi vya Ukimwi.

Takribani watu 1.3 walikuwa wanaishi na Ukimwi nchini humo mwa 2016 kulingana na taarifa zilizokusanywa na Umoja wa Mataifa.

Mchungaji huyo ambaye hujiita Mtume ana miaka 35 na miongoni mwa viongozi vijana wenye haiba ya kuvutia mabao wameibuka nchini humo toka mdororo wa uchumi uliposhika kasi.

Mwandishi wa BBC jijini Harare Shingai Nyoka anaripoti kuwa wachungaji hao wamekuwa wakiahidi kuwatibu wagonjwa kimiujiza na pia kutajirisha watu kwa kutumia muujiza.

Mwezi Oktoba mwaka jana, aliwaambia wafuasi wa kanisa lake kuwa dawa hiyo, iitwayo aguma, ina nguvu za kimiujiza zinazoweza kuangamiza virusi vya ukimwi kwa siku 14.

"Dawa hii ni asilimia 100 ya asili. Nasema hivyo kwa kuwa tumegundua haina madhara kwa afya kabisa," alinukuliwa akisema hivyo na vyombo vya habari vya Zimbabwe.

Serikali ya Zimbabwe ilisema kuwa kauli hiyo ni uhalifu na polisi wakavamia ofisi zake.

Karatasi ya mashtaka dhidi yake ilidai kuwa Magaya "aliteketeza baadhi ya vidhibiti kwa kuvimwaga chooni na kuyachoma moto makontena ofisini kwake muda mfupi kabla ya kukamatwa. Hata hivyo, baadhi ya vidhibiti vilinaswa."

Wakili wa mchungaji huyo,Everson Chatambudza, ameiambia mahakama kuwa mteja wake aliamini kuwa dawa hiyo ilikuwa ya asili na nzuri lakini amekiri kuvunja sheria kwa kuisambaza bila kupata kibali cha wizara ya Afya.

"Kulikuwa na jitihada kwa upande wa mshatakiwa kufuata sheria. Siku tatu kabla ya kuizindua aliiandikia barua wizara kuhusu ugunduzi wake... lakini kwa bahati mbaya hakupata majibu yoyote," amenukuliwa mwanasheria huyo na gazeti la serikali la Herald.

Magaya mwaka jana pia alizindua rangi ya midomo (lipstiki) ambayo alidai inatibu shinikizo la damu.

Chanzo- BBC
Share:

IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI

Mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) Simon Sirro amefanya mabadiliko ya makamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza na Kinondoni.

RPC mkoa wa Kinondoni, ACP Muliro Jumanne Muliro amekwenda kuwa RPC Mwanza huku ACP Jonathan Shana amehamishiwa makao makuu ya polisi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 5,2019 kwa vyombo vya habari na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Ahmed Msangi ilieleza kuwa nafasi ya Kamanda wa kinondoni imechukuliwa na Mussa Taibu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida katika utendaji kazi kwa jeshi la polisi.

Share:

BUNGE LAREJEA BAADA YA VING'ORA KUZUA TAHARUKI

Share:

RPC ASIMULIA TUKIO LA MAUAJI KANISANI "DED ALIFUNGA MLANGO WA KANISA,ASKARI WAKAFYATUA RISASI"


Na  Sylivester Richard - Singida 

Jeshi la polisi mkoani Singida linawashikilia watu 7 kutokana na tuhuma za mauaji ya  Isaka Petro , (28), mkazi wa kijiji cha Kaskazi, Tarafa ya Itigi  Wilaya ya Manyoni ambaye  alifariki dunia papo hapo baada ya kupigwa na kitu kunachodhaniwa kuwa ni risasi upande wa kisogoni wakati akiwa kwenye ibada na waumini wenzake katika kanisa la Sabato lililoko kijijini hapo.


Akiongea na waandishi wa habari leo Jumanne Februari 5,2019, Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida, ACP Sweetbert  Njewike amewataja watuhumiwa wanaoshikiliwa kuwa ni pamoja na Pius Shija, (54), Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Itigi, Silvanus  Lungwsha, (50), Afisa kilimo na mifugo - Itigi na Elik Paulo , (31) Afisa Sheria Itigi. 

Wengine ni Eliutha Augustino, (43), Afisa Tarafa - Itigi , Yusuph John , (25), Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaskazi, mkazi wa Itigi, Rodey Elias ,(42) Afisa wanyamapori mwajiriwa wa Halimashauri ya Itigi na Makoye Steveni Askari wa wanyamapori Hifadhi ya Doloto.

Kamanda Njewike ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea siku ya tarehe 02.02. 2019 majira ya saa 8:20 mchana huko katika kijiji cha Kaskazi, Tarafa ya Itigi  Wilaya ya Manyoni ambapo Isaka Petro , (28), mkazi wa kijiji hicho alifariki dunia papo hapo baada ya kupigwa na kitu kunachodhaniwa kuwa ni risasi upande wa kisogoni wakati akiwa kwenye ibaada na waumini wenzake katika kanisa la Sabato lililoko Kijijini hapo.

Njewike amesema Marehemu aliuawa baada ya Maafisa 7 wa Halimashauri ya Itigi wakiongozwa na Pius Shija -  Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri hiyo kuwatafuta watuhumiwa wa kosa la kuharibu mali lililotokea tarehe 01.02.2019 ambapo mlalamikaji Rose Andrew alidai kuharibiwa mali yake iliyopo ndani ya shamba la Tanganyika Parkers linalomilikiwa na Halimashauri hiyo.

Hata hivyo Kamanda ameleza kuwa Maafisa hao walipata taarifa kuwa baadhi ya watuhumiwa wa kosa la kuharibu mali wapo katika kanisa la Wasabato lililopo Kijijini hapo ndipo walipokwenda kwa lengo la kuwakamata. 

Ameongeza kuwa baada ya Mkurugenzi kuingia ndani ya Kanisa hilo kulitokea vurugu ndipo Mkurugenzi huyo alienda nje  na kufunga mlango kwa nje na askari wa wanyamapori waliokuwa na silaha walifyatua risasi kadhaa ambapo mmoja alimpiga Marehemu kisogoni na kufariki dunia papo hapo .

 Kamanda amefafanua kuwa watuhumiwa bado wanashikiliwa kwa uchunguzi na muda wowote watafikishwa Mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
Share:

RAIS MAGUFULI ATEMBELEA OFISI ZA AFRICAN MEDIA GROUP WAMILIKI WA CHANNEL 10 NA MAGIC FM,ASEMA NI MALI YA CCM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh. Dkt John Pombe Magufuli Magufuli leo ametembelea kituo cha televisheni cha channeli ten ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 42 ya chama cha Mapinduzi ambacho Rais ndio mwenyekiti wa chama hicho.

Amesema kutokana na Uhitaji wa vifaa vya kisasa kama Kamera za kisasa, Rais ameahidi kuwachangia milioni Mia Moja kwa ajili ya ununuzi wa kamera hizo, na atawatafutia milioni zingine 100 ili zitumike katika maboresho ya kituo hicho.

Aidha amewathibitishia kuwa hakuna mfanyakazi atakayefukuzwa kwa sababu ya itikadi zake na ameahidi kuwatafutia jengo la CCM lenye hadhi nzuri ili waweze kuhamishia ofisi za kituo hicho. 

"Nimefika hapa leo ili niwaambie African Media Group ni mali ya CCM.Hakuna atakayefukuzwa kazi no matter wewe ni muumini wa chama gani" 

"Ili kuboresha kazi yenu, tutanunua vifaa vipya ili muweze kuwafikia watu wengi sana.Sikujua Channel 10 na Magic FM zinatokea kwenye jengo la ajabu kiasi hiki.

"Tutasaidiana kufanya utafiti wa majengo ya CCM ili tuangalie wapi tunaweza kuweka ofisi za vituo hivi.Hata mkitaka jengo la Ofisi ya Mwenyekiti wa CCM, Mimi nitakubali.Hata jengo la kupanga tutatafuta, ofisi nyingi zimehamia Dodoma.

Kadhalika amesisitiza kwamba vyombo vya habari vipo huru katika utendaji wake lakini amewaasa kuzingatia Sheria, kanuni, taratibu na tamaduni za Nchi ili kusaidia Nchi katika kulinda amani na utulivu na kukuza uchumi ambao utawanufaisha Watanzania.


"Vyombo vya habari vinatakuwa kuwa free vizungumze, Tanazania freedom of expression ipo‬.‪Ndio maana kuna vyombo vya habari vilivyosajiliwa zaidi ya 170 na zaidi‬.Tuzingatie mipaka ya uandishi, maadili ya nchi yetu, tabia za jamii zetu na Katiba yetu‬.‪Kwamba hili linaweza kuzungumzwa hapa, hili linafaa huku au hili linafaa kwenye vikao‬"
Share:

MADURO AMUOMBA PAPA FRANCIS KUINGILIA MGOGORO VENEZUELA

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amemwandikia barua kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis akimwomba kuingilia kati kwenye mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini mwake.

"Nimemwandikia barua Papa Francis, akisema kwamba anamwomba kiongozi huyo kusaidia kufanikisha mchakato wa majadiliano", alisema rais Maduro wakati akizungumza na kituo cha habari cha Italia cha SkyTg24. 

"Ninamuomba Papa kutusaidia, kwenye mchakato wa majadiliano. Ninatumai tutapata majibu ya kutia moyo kutoka kwake", aliongeza Maduro.

 Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwa pamoja wamesema wana matumaini ya ufumbuzi wa amani kwenye mgogoro huo wa kisiasa, huku Merkel akisema taifa lake linamtambua kiongozi wa upinzani Juan Guaido aliyejitangazia mwenyewe kuwa rais wa mpito.

Merkel ambaye yuko ziara ya siku mbili nchini Japan, ameungana na mataifa mengine ya Ulaya, kumtambua Guaido kama rais wa mpito na kusema anapaswa kuandaa uchaguzi mpya haraka iwezekanavyo. 

Waziri mkuu Abe, hata hivyo hakutoa msimamo juu ya Guaido, lakini alisema Japan inataka suluhisho la amani na demokrasia kwenye mgogoro huo.

Chanzo:Dw
Share:

MSANII NGULI WA FILAMU AFARIKI DUNIA


Msanii nguli wa filamu wa Marekani, Kristoff St. John (52) amefariki dunia baada ya mwili wake kukutwa nyumbani kwake huko San Francisco, usiku wa Februari 2, 2019.

Kristoff ambaye alishawahi kuwekwa kwenye hospitali ya watu wenye matatizo ya akili baada ya kujaribu kujiua kwa bunduki, alipata umaarufu mkubwa kwa kuigiza kwenye filamu, ambazo alianza kujihusisha nazo akiwa na miaka nane tu.

Mpaka sasa chanzo cha kifo chake hakijajulikana, ila polisi wa Francisco wameshuku huenda ikawa ni kuzidisha madawa, yaliyosababisha kifo chake.

Star huyo ameshawahi kuigiza kwenye filamu mbali mbali zikiwemo That’s My Mama, Wonder Woman, Roots, The Next Generation, na nyinginezo nyingi.

Star huyo hivi karibuni alimchumbia mchumba wake Kseniya Olegovna Mikhaleva, na walitarajia kufunga ndoa ndani ya mwaka huu.
Share:

Breaking: KIKAO CHA BUNGE CHAAHIRISHWA GHAFLA BAADA YA ALARM KUASHIRIA HATARI KULIA


Habari za hivi punde kutoka Dodoma zinasema kikao cha Bunge kimesitishwa kwa muda baada ya alarm kulia ghafla Bungeni saa 5:02 asubuhi na wabunge wametoka nje akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. 

Taarifa tutakuletea hivi punde.
Share:

MKURUGENZI WA HALMASHAURI MBARONI KWA TUHUMA ZA MAUAJI KANISANI SINGIDA

Watu watano, akiwamo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Pius Luhende, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Singida, wakituhumiwa kusababisha kifo cha mfugaji Peter Chambalo, anayedaiwa kupigwa risasi akiwa kanisani.

Akizungumza na Nipashe jana, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Ahmed Msangi, alikiri kutokea kwa tukio hilo juzi na kueleza kuwa mpaka sasa, wanaoshikiliwa ni watu wa watano akiwamo mkurugenzi huyo.

Msangi alitaja watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa kuwa ni askari wanyamapori wawili, mmoja kutoka Mamlaka ya Wanyamapori (Tawa) na mwingine kutoka Halmashauri ya Ipigi, mwanasheria na mtendaji wa kata.

“Ni kweli tukio limetokea, lakini siyo kweli kuwa askari wa Jeshi la Polisi wamehusika na tukio hilo," Msangi alisema, "kwanza hawakuwapo kwenye tukio hili.

"Waliokuwapo ni askari wanyamapori, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, mwanasheria wake na mtendaji wa kata. Kilichotokea ni kwamba, walipofika katika kijiji cha Kazikazi, Kata ya Kitaraka, Tarafa ya Itigi, kulitokea kutoelewana, hivyo kusababisha vurugu," alisema.

Aliongeza kuwa, wakati wa vurugu hizo, inadaiwa askari walifyatua risasi na kumjeruhi mtu huyo ambaye alifariki dunia.

“Uchunguzi wa tukio hili unaendelea na hivi sasa Mkuu wa Mkoa huo, Kamanda wa Polisi wapo eneo la tukio kupata maelezo zaidi, hizi ndizo taarifa nilizonazo hadi sasa,” Msangi alisema.


Romana Mallya - Nipashe
Share:

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO FEBRUARI 5,2019.

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Februari 5, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:

Monday, 4 February 2019

MAHAKAMA YAAMURU WADHAMINI WA TUNDU LISSU WAFIKE MAHAKAMANI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru wadhamini wa Mbunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya Chama cha Chadema, Tundu Lissu kufika Mahakamani hapo Februari 25, 2019 kueleza maendeleo ya afya yake.

Amri hiyo, imetolewa leo Februari 4, 2019 baada ya Wakili wa serikali Mwandamizi Patrick Mwita kudai mahakamani hapo, Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa na kwamba hadi sasa hawajajua hali ya mshtakiwa wa nne, ambae ni Lisu inaendeleaje. 

"Mheshimiwa, Kesi hii leo imekuja kwaajili ya kuendelea kusikilizwa lakini hadi sasa hatuna taarifa ya hali ya mshtakiwa wa nne,tunaamini hata Mahakama hii haina rekodi ya Maendeleo yake" amedai Wakili Mwita

Hakimu Simba amesema, kwa kuwa mahakama hiyo haina rekodi ya taarifa ya hali ya Lisu hivyo Februari 25 wadhamini wafike Mahakamani ili kueleza maendeleo ya afya yake.

Kesi hiyo ambayo ipo katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa upande wa mashtaka, inamkabili Lissu na wenzake Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.

Kwa pamoja, wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Inadaiwa, Januari 12 hadi 14, 2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifaza uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar.’

Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.

Mshtakiwa Mehboob anadaiwa kuwa Januari 13 ,2016 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya Ilala, alichapisha gazeti la Mawio lililokuwa na taarifa za uchochezi.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa huyo pia alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.
Share:

WAGANGA WA TIBA ASILI BARIADI WAPEWA SIKU 16 WAWE NA KITAMBULISHO CHA WAJASIRIAMALI

Waganga wa tiba asili waliopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu wamepewa siku 16 kuhakikisha kila mmoja anakuwa na kitambulisho cha wajasiriamali kilichotolewa na Rais John Magufuli.

Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Wilaya hiyo Festo Kiswaga wakati akiongea na viongozi wa waganga hao mkoa, alipokutana nao kujadili namna bora ya kuboresha kazi zao.

Kiswaga amesema kuwa katika wilaya hiyo kuna waganga wa tiba asili 600, na kwamba mganga yeyote ambaye hatakuwa na kitambulisho hicho baada ya siku hizo kuisha atafutiwa leseni yake na kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Hadi kufikia Februari 20, mwaka huu kila mganga wa jadi awe na kitambulisho hicho, usipokuwa nacho tutakunyang’anya leseni yako kukuzuia kuendelea kufanya kazi zako, baada ya muda huo,” amesema.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waganga hao, Samson Maduhu amesema ndani ya muda huo waganga wote 600 wanafikiwa na kupatiwa vitambulisho hivyo.
Share:

NAPE NNAUYE AJIUZULU UENYEKITI KAMATI YA BUNGE


Nape Nnauye
Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai amethibitisha kupokea barua ya mbunge wa Mtama Mh. Nape Nnauye kujiuzulu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.

Kagaigai amesema leo Jumatatu Februari 04, 2019 Nape ameandika barua kwenda kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ya kujiuzulu nafasi hiyo na tayari spika amempatia nakala ya barua hiyo.

''Ni kweli nimeiona barua aliyomwamndikia Spika na mimi nimepata nakala yangu kwahiyo ni kweli amejiuzulu labda awe na mawazo mengine'', amesema.

Hata hivyo www.eatv.tv imemtafuta Nape Nnauye ambaye alipokea simu yake kisha kusema yupo kwenye kikao hawezi kuendelea na maongezi. ''Nipo kwenye mkutano siwezi kuongea'', alisema.

Machi mwaka 2017, Nape aling’olewa kwenye nafasi ya Uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo sasa ipo chini ya Waziri Harrison Mwakyembe.
Chanzo-EATV
Share:

MFANYABIASHARA ATEKWA AKINUNUA JENEZA ARUSHA

Mfanyabiashara wa madini ya tanzanite jijini Arusha, Jeremiah Simon(49) mkazi wa Sekei wilayani Arumeru, anadaiwa kutekwa wakati akiwa katika eneo la mochwari, Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa maandalizi ya kununua jeneza.


Simon ni Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wa madini (brokers) mkoani Arusha.

Imeelezwa kuwa mfanyabiashara huyo alitekwa kutoka katika eneo hilo Jumatatu, Januari 28, mwaka huu, majira ya jioni.

Kwa mujibu wa mke wake , Janet Jeremia, mumewe alichukuliwa na watu wasiofahamika akiwa na mtu mwingine aitwaye Loth Greyson ambaye ni jirani yake. Imeelezwa kuwa watekaji hao waliokuwa kwenye gari aina ya Land Cruiser nyeupe, baada ya siku moja walimwachia Loth kwa sharti la kutozungumza chochote juu ya tukio hilo.

Janet alisema tangu siku hiyo hadi sasa hajui mume wake alipo ila siku ya Jumanne, Januari 29 mwaka huu, alimpigia simu na kumweleza kuwa yupo salama na baada ya hapo hakuweza kumpata tena kupitia mawasiliano hayo.

Awali, shuhuda wa tukio hilo ambaye ni fundi wa kutengeneza majeneza eneo hilo, Salimu Mzirai alisema siku hiyo lilikuja gari aina ya Landcruiser rangi nyeupe na waliteremka watu wapatao watatu na kuwachukua watu wawili akiwemo mfanyabiashara huyo.

Kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani hapa, Longinus Tibushubwamu, alithibitisha tukio hilo na kueleza wapo katika hatua ya uchunguzi.

Kwa upande wake, kaka wa mfanyabiashara huyo aitwaye Joseph Simon, mkazi Simanjiro Manyara alisema alipata taarifa za kutoweka kwa mdogo wake siku ya Jumatatu jambo ambalo limewaumiza.

Hata hivyo, Loth alipopatikana hakuweza kuzungumzia tukio hilo japo alithibitisha kutekwa na watu wasiojulikana na hakutambua walipelekwa wapi kwa kuwa alikuwa amefungwa kitambaa usoni.

Chanzo - Habarileo
Share:

WATU 28 MBARONI MATUKIO YA UTEKAJI NA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE


Baadhi ya wafanyabiashara wa miji ya Njombe na Makambako mkoani Njombe ni miongoni mwa watu 28 wanaoshikiliwa na polisi wakituhusishwa  na mwendelezo wa matukio ya utekaji na mauaji ya watoto yanayoendelea wilayani Njombe.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, Renata Mzinga amesema leo Jumatatu Februari 04, 2019 ofisini kwake wakati akitoa taarifa ya msako wa kubaini mtandao wa watu wanaojihusisha na matukio hayo.

Amesema pia waganga sita wanaodaiwa kujihusisha na matukio hayo wametiwa mbaroni na wanaendelea na mahojiano dhidi yao.

"Tunaendelea na msako mkali kwa kushirikiana na kikosi maalumu kutoka makao na hadi leo hii tunawashikilia watu 28 wakiwamo waganga wa jadi sita, wafanyabiashara na watu wengine wa kawaida," amesema.

Amesema matukio yote yaliyojitokeza ya mauaji, wamekamatwa watu kuhusiana na uhusika wao na vyombo vya dola vinaendelea na upelelezi wa kuwabaini wahalifu.

Kamanda huyo amesema wana taarifa za watuhumiwa waliokimbia wakiwamo waganga wa jadi lakini wameshajua walikokimbilia na vyombo vya dola vitawasaka popote hadi watiwe nguvuni.

“Tunaendelea kuwasihi wananchi wa Njombe waendelee kutoa ushirikiano wa kuwabaini wahusika wa mauaji ya watoto wadogo wasio na hatia,” amesema.

Na Godfrey Kahango, Mwananchi
Share:

MO DEWJI "ROHO YANGU BADO INANIUMA,NAIPENDA SANA SIMBA


Mwekezaji mkuu wa klabu ya Simba Mfanyabiashara, Mohemmed Dewji amesema hajakata tamaa na matokeo ya Simba japo yanamuuma sana.

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu tangu Simba ilipofungwa na AS Vita na pia kufungwa na Al Ahly Jumamosi iliyopita Mo Dewji, amemua kuweka wazi maumivu yake.

''Roho yangu bado inaniuma. Naipenda sana Simba, na bado sijakata tamaa. Roma haikujengwa kwa siku moja'', ameandika Mo Dewji kwenye mtandao wa Twitter.

Simba ambayo imerejea nchini mchana wa leo ikitokea Misri ambako ilicheza mchezo wa tatu wa kundi D dhidi ya Al Ahly na kufungwa mabao 5-0, ipo kwenye nafasi ya tatu ya kundi D ikiwa na alama 3.

Simba bado ina mechi mbili za nyumbani dhidi ya AS Vita na Al Ahly na mechi moja ugenini dhidi ya JS Saoura ya Algeria.
Chanzo - EATV
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger