Friday, 1 February 2019

MCHUNGAJI KKKT ATUHUMIWA KUFANYA MAPENZI NA MTOTO WA MCHUNGAJI MWENZAKE

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela amelishauri Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Iringa kumuondoa na kutomfumbia macho aliyekuwa Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi hiyo mchungaji Yusto Kinyori kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mtoto wa mchungaji mwenzake kwenye gari. Kasesela amesema hayo kwenye Mkutano Mkuu wa kumchagua Msaidizi wa Askofu wa kanisa hilo uliofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT usharika wa Ipogolo ambapo amesema kuwa anayo video clip ikionesha mchungaji huyo akifanya mapenzi kwenye gari na mtoto wa mchungaji mwenzake. Kasesela…

Source

Share:

Ministry of Education, Science and Technology: China Scholarships 2019

Ministry of Education, Science and Technology:: Scholarship tenable in people’s republic of china for the academic year 2019/2020

  1.  Call for Application

The General Public is hereby informed that, the Chinese Government has opened new scholarships for Undergraduate, scholars and Post-graduates to Tanzanians for the academic year 2019/2020. The online application and the corresponding application documents should be submitted to application receiving agency. For more information, please visit the following link: http://www.csc.edu.cn/studyinchina or http://www.compuschina.org

Eligibility:

To be eligible, applicants must:

  • Be a citizen of the United Republic of Tanzania;
  • Be in good health;
  • Be a high school graduate under the age of 25 when applying for Bachelor degrees programs;
  • Be a Bachelor’s degree holder under the age of 35 when applying for Master’s programs;
  • Be a Master’s degree holder under the age of 40 when applying for Doctoral programs;

2.0 Application Documents

a) Completely filled application form for Chinese Government Scholarship (in Chinese or English);

b) Certified copies of Certificate for Secondary Education Examination (CSEE), Advanced Certificate for Secondary Education Examination, Diploma, Bachelor`s Degree and Master`s Degree. Documents in languages other than Chinese or English must be attached with certified Chinese or English translations;

c) Academic transcripts: Transcripts in languages other than Chinese or English must be attached with certified Chinese or English translations;

d) A Study Plan or Research Proposal in Chinese or English. (A minimum of 200 words for undergraduates, and 800 words for postgraduates);

e) Recommendation letters: Applicants for graduate programs or senior scholar programs must submit two letters of recommendation in Chinese or English from professors or associate professors;

f) Certified copies of birth certificates

g) Applicants for music studies are requested to submit their own works and those applying for fine arts programs must submit their own works which include two sketches, two colour paintings and two other works;

h) Applicants with good Bachelor’s degree in Mechanical and/or Electronics Engineering can apply for Masters’ programme which are offered at Tianjin University of Technology and Education;

j) Applicants under the age of 18 should submit the valid documents of their legal guardians in China; and

i) Applicants planning to stay in China for more than 6 months must submit a photocopy of the Foreigner Physical Examination Form completed in English (the original copy should be kept by the applicant). The form designed by the Chinese quarantine authority can be downloaded from http://my.china-embassy.org/eng/whjy/P020190109380893894433.pdf The physical examinations must cover all the items listed in the Foreigner Physical Examination Form. Incomplete records or those without the signature of the attending physician, the official stamp of the hospital or a scaled photograph of the applicants are invalid. Please select the appropriate time to take physical examination as the result is valid for only 6 months.

3.0 Please submit the following documents where applicable

k) Pre-admission Letter from Chinese Government Scholarship universities; and

l) Language qualification certificate. E.g., HSK certificates, IELTS or TOFEL report.

Instruction for online application of the Chinese government scholarship information system

Step 1: Visit http://www.csc.edu.cn/laihua or www.capuschina.org and click “Scholarship Application Online for International Students”;

Step 2: Read “Tips for online application” carefully before clicking “NEXT” to the registration page;

Step 3: Log in with your user name and password. For new user, please click “Create an account” for registration;

Step 4: Fill in the correct Program Category and Agency Number. An Agency Number represents a specific application receiving agency and a correct choice of Program Category is necessary before filling in the Agency Number. Please make sure you fill it in correctly, otherwise you will not be able to continue your online application or your application will not be accepted. Your ‘Program Category’ is: Type A and Agency Number is: 8341. Once the correct ‘Agency Number’ is entered, the name of the agency will automatically emerge;

Step 5: Fill in the Online Application Form and Upload Supporting Documents truly, correctly and completely following the steps listed on the left of the page. Applicants are required to select a discipline before choosing their majors. Please refer to the Disciplines Index, which could be downloaded from help, if you have any doubt about the disciplines and majors;

Step 6: Check each part of your Application carefully before submitting it. Click Submit to submit your Application. The submitted documents will be the only reference for the applied universities to confirm the admission;

Step 7: You can make changes to your application by clicking Withdraw and Edit the Application on the top of the page. But make sure to submit it again by 4 clicking Submit after finishing all the changes. Otherwise, the retrieved application will become invalid and your new application will not be received either;

Step 8: You can download and print the completed Application Form by clicking Print the Application Form; and

Step 9: Send the printed paper application form and other supporting documents to the address below.

Note: Please use Firefox or Internet Explorer 11.0. Menu selection functions may not work in other browsers.

Kindly submit your application to the undersigned not later than 11th March, 2019.

Issued by:

Permanent Secretary,

Ministry of Education, Science and Technology,

College of Business and Law,

University of Dodoma,

P. O. Box. 10,

40479 DODOMA.

The post Ministry of Education, Science and Technology: China Scholarships 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

BILIONI 50.4 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO BUKOBA KWA MWAKA 2019/2020

Na Allawi Kaboyo Bukoba. Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya Bukoba mkoani Kagera, limepitisha bajeti ya zaidi ya shilling bilioni 50.4 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2019-2020. Akisoma rasimu ya bajeti hiyo katika baraza la madiwani lililofanyika Januari 31 mwaka huu katika ukumbi wa halmashauri hiyo, afisa mipango wa halmashauri ya wilaya Bukoba JULIAN TARIMO ameeleza vipaumbele vilivyolengwa kuwa ni afya elimu maji na miundombinu pamoja na mambo mengine na kuwataka madiwani hao kuipitisha bajeti hiyo kwa kuwa inalenga maslahi…

Source

Share:

WATENDAJI WAPEWA ONYO KALI UGAWAJI VITAMBULISHO AWAMU YA PILI KAGERA

Na mwandishi wetu Kagera Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti amegawa vitambulisho 35,000 awamu ya pili kwa Wafanyabiashara Wadogo katika Mkoa wa Kagera na kuwaagiza Watendaji wa Serikali chini ya usimamizi wa Wakuu wa Wilaya kuendelea na zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivyo na kuhakikisha ifikapo Februari 28, 2019 vitambulisho vyote viwe vimegawiwa kwa Wafanyabiashara Wadogo. Katika zoezi fupi la kukabidhi vitambulisho hivyo 35,000 vya awamu ya pili kwa Wakuu wa Wilaya iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Februari 1, 2019 Mkuu wa…

Source

Share:

MWANANCHI YEYOTE ATAKAYEUWAWA NINAANZA KUSHUGHULIKA NA MWENYEKITI WA MTAA HUO-OLESENDEKA

Na Amiri kilagalila Mkuu wa mkoa wa Njombe CHRISTOPHER OLESENDEKA amewaagiza viongozi wa serikali za mitaa wakiwemo wenyeviti wa vijiji kuhakikisha wanashiriki katika zoezi la kutoa taarifa za wahusika wa mauaji mkoani Njombe huku akiapa kuanza kushughulika na viongozi hao wa vijiji endapo yatatokea mauaji yanayofanana na yaliyotokea mkoani humo. OLESENDEKA alitoa maagizo hayo hii leo katika viwanja vya polisi mjini makambako wakati akizungumza na mamia ya wananchi wa mji huo kwa lengo la kuwaomba wananchi kuonyesha ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama katika kushiriki kuwafichua wanaohusika katika mauaji…

Source

Share:

SERIKALI YAONGEZA USALAMA WA TAARIFA ZAKE

Naibu waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dokta Marry Mwanjelwa amezitaka taasisi za umma kuhakikisha suala la usalama wa taarifa za serikali linakuwa la lazima wakati wa kubuni,kusanifu,kujenga,kusimika na kuendesha mifumo ya TEHAMA. Dokta Mwanjelwa alitoa agizo hilo jiji Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha pili cha serikali mtandao. Amesema njia moja wapo ya kujihakikishia usalama ni kuhakikisha utengenezaji wa mifumo unazingatia programu ambazo wataalamu wao wanaweza kutambua kinachofanyika badala ya kuwa na mifumo ambayo hawajui kinachofanyika nyuma ya pazi. “kwa namna ya kipekee kabisa…

Source

Share:

MSAIDIZI WA ASKOFU KKKT AREKODIWA VIDEO AKIFANYA MAPENZI NA MTOTO WA MCHUNGAJI MWENZAKE KWENYE GARI


Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela amelishauri Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Iringa kumuondoa /kutomfumbia macho aliyekuwa Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi hiyo mchungaji Yusto Kinyori kwa tuhuma ya kufanya mapenzi na mtoto wa mchungaji mwenzake kwenye gari.

Kasesela amesema hayo kwenye Mkutano Mkuu wa kumchagua Msaidizi wa Askofu wa kanisa hilo uliofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT usharika wa Ipogolo ambapo amesema kuwa anayo video clip ikionesha mchungaji huyo akifanya mapenzi kwenye gari na mtoto wa mchungaji mwenzake.

Kasesela amesema kuwa kinachomuuma zaidi viongozi wa dini ndiyo wanaotumwa kwenda serikali kuwawakilisha baadhi ya viongozi au kutoa matamko mbalimbali kwa niaba ya kanisa lakini kiongozi huyo amekengeuka kwa sababu ya kitendo alichokifanya na kushauri kanisa limuondoe haraka kwa sababu analiaibisha kanisa.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Iringa Mchungaji Blastone Gavile amesema mkutano huo maalumu umefanyika kutokana na vikao vilivyofanyika mwishoni mwa mwakajana kujadili ofisi ya msaidizi wa askofu kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili.

Mara baada ya kufanya uchaguzi huo walimpata msaidizi wa askofu Askari Mgeyekwa ambaye alikuwa mkuu wa KKKT usharika wa Kihesa na ameibuka kidedea kwa kupata kura 480, kura za hapana 17 na zilizoharibika 10 na jumla ya wapiga kura walikuwa 457.
Chanzo - EATV
Share:

ALIYEMLA MWENZAKE AKAMATWA AKIJIFANYA DAKTARI


Raia mmoja nchini Urusi, Boris Kondrashin mwenye umri wa miaka 35, amekamatwa na polisi akijifanya daktari, baada ya kubainika kufanya tukio la mauji miaka 20 iliyopita, na kunywa damu ya mtu aliyemuua.

Boris alikamatwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa wakazi wa mji wa Chelyabinsk nchini humo, mara tu walipomkumbuka na kukumbuka yale aliyoyafanya miaka ya nyuma.

Boris ambaye ni mtoto kutoka familia yenye heshima nchini humo huku baba yake akiwa ni mtaalamu wa masuala ya saikolojia, alitumia pesa zake kupata vyeti feki na kujifanya daktari wa saikolojia na daktari wa matatizo ya uraibu (adiction), ambapo alifanikiwa kupata kazi katika hospitali mbali mbali katika mji wa Chelyabinsk.

Mwaka 1998 kijana huyo alipokuwa mwanafunzi, alimuua mwanafunzi mwenzake na kumkatakata, kisha kula sehemu za mwili wake ikiwemo ini, na kunywa damu yake.

Polisi walipomkamata alikiri kufanya kosa hilo akijifananisha na 'vampire', na kwamba alitumwa na shetani kukamilisha kazi hiyo.

Hata hivyo mahakama ilimkuta kijana huyo na matatizo ya akili, hivyo alipelekwa kwenye kituo cha magonjwa ya akili, na alipopata unafuu aliachiwa huru.

Wakazi wa maeneo hayo wamesema kwamba walimtambua baada ya mwanamke mmoja kwenda hospitali hapo kupata matibabu.

 Mwanaume huyo amesema alimkumbuka daktari huyo kuwa ndiye aliyemwambia kuwa yuko kwenye orodha ya wanafunzi wengine ambao alipanga kuwaua na kuwanywa damu zao.
Boris Kondrashin
Share:

AKAMATWA AKISAFIRISHA MAITI YA MTOTO


Mwanaume mmoja anashikiliwa na vyombo vya usalama nchini Malawi baada ya kukutwa akisafiri na maiti ya mtoto kwenye treni.

Akithibitisha kukamatwa kwa mtu huyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini humo, Joseph Sauka, amesema kwamba mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la James Majawa, 28, wa kijiji cha Chimphamba alikuwa akisafiri kutoka Limbe kwenda Nayuchi.

Kamanda Sauka ameeleza kwamba maiti ya Mtoto huyo ilibainika baada ya harufu ya kitu kilichoharibika kuenea kwenye Treni hiyo iliyokuwa na abiria wengine.

Amefafanua kwamba baada ya upekuzi ndipo maiti hiyo ikabainika huku ikiwa imetolewa sehemu za siri.

Hata hivyo Kamanda Sauka ameeleza kwamba bado wanaendelea na uchunguzi zaidi huku wakisisitiza kwamba maiti hiyo siyo ya mtoto mwenye ualbino.
Share:

MWANAMUZIKI BOBI WINE ATANGAZA KUGOMBEA URAIS UGANDA KUMNG'OA MUSEVENI

Mwanamuziki Bobi Wine ambaye ni mbunge amesema atawania urais nchini Uganda katika uchaguzi mkuu ujao akidhamiria kumwondosha madarakani, Rais Yoweri Museveni.

Bobi Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, amekiambia kituo cha televisheni cha Marekani cha CNN kuwa amejiandaa kumkabili Rais Museveni.

“Tuna Waganda wengi waliojiandikisha kama wapiga kura wapya, na hii ndiyo njia pekee ya kumwondosha Museveni,” amesema Bob Wine ambaye yuko ziarani nchini Marekani.

Alipoulizwa kama ana uwezo wa kukabiliana na Rais aliyekaa madarakani kwa muda mrefu, mwanasiasa huyo anayewavutia vijana wengi alijibu: “ Sawa, jambo hili limekuwa likijitokeza mara kwa mara na watu wengi wamekuja kwangu wakitaka niwanie nafasi hii.

“Tumekuwa tukijadiliana na timu yangu na lazima niseme tumeamua (yeye na timu yake) kwa dhati kabisa kukabiliana na Rais Museveni katika uchaguzi ujao wa Rais.

Museveni alishinda katika uchaguzi uliofanyika 2016 na kulingana na matakwa ya katiba hakuruhusiwa kuwania tena madaraka kutokana na umri wake lakini marekebisho yaliyofanyika baadaye yalimwondolea kizingiti hicho.

Pia, Bunge la nchi hiyo lilipitisha marekebisho ya sheria kwa kurefusha muhula wa Rais kuwa madarakani kutoka miaka mitano hadi kufikia saba. 







Share:

SERIKALI KUONGEZA NGUVU YA SEKTA BINAFSI KUWAINUA WAJASIRIAMALI ILALA

Na Heri Shaban Serikali imesema itashirikiana na Kampuni ya Guru Planet kuwainua Wajasiriamali wa Wilaya ya Ilala. Hayo yalisemwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto wakati wa ufunguzi wa tamasha la Wajasiriamali lililoandaliwa na Kampuni ya Guru Planet kwa kushirikiana na Manispaa ya Ilala Dar es Salam jana ambapo zaidi ya vikundi 300 vimeshiriki. Akizunguza katika tamasha hilo Naibu Meya Ilala Kumbilamoto alisema dhumuni la manispaa ya Ilala kufanya tamasha Kwa kushirikiana na Kampuni ya Guru Planet ulitokana na Guru Planet imekuwa ikiendesha shughuli zake za kuwajengea…

Source

Share:

Uchawi Bariadi : BINTI AKUTWA CHINI YA UVUNGU WA KITANDA CHA BIBI YAKE HAJITAMBUI


Tukio la Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ikinabushu (jina limehifadhiwa) kukutwa chini ya uvungu wa kitanda cha bibi yake, limetikisa viunga vya mji wa Bariadi, Simiyu. 

Taarifa zaidi zinaripoti kwamba, mwanafunzi huo alitoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu tarehe 25 Januari mwaka huu hapo kijijini kwao Ikinabushu na baada ya siku tano alikutwa chumbani kwa bibi yake akiwa hajitambui.

Binti huyo inaeleza kwamba, alikuwa akiishi kwenye nyumba aliyokuwa akiishi bibi yake (Kwandu Kiuluma) na ndugu zake wengine akiwemo mama yake wa kambo na ndugu zake.

Kaka wa binti huo Samson Lambo amesema kuwa, aliambiwa na baba yake mdogo anayeishi Kigoma kwamba, amepokea taarifa za kupotea kwa mdogo wake na kwamba, yeye hakua akijua kuhusu ndugu mkasa huo.

Samson anasema, alipoanza kufuatilia na kuuliza, baadhi ya watu walimweleza kwamba, walikutana na mdogo wake huyo kwenye ghala maeneo ya nyumbani kwao na walipomwita alikataa na kuingia kwenye ghala hilo.

“Nilipopata taarifa hizo niliongeza wasiwasi kuhusu kupotea kwake. Kama familia tulikaa na kuamua kumtafuta kwa njia mbadala ili kujua alipo,” amesema Samson na kuongeza;

“Kwenye kikao chetu cha familia baada ya kuamini kuna mambo ya nguvu za giza, tulikubaliana kumwita mganga. Baada ya mganga kufanya dawa zake, akatuambia kuwa mtoto yupo ndani.”

Samsoni anasema, walimuuliza mganga huyo kwamba humo ndani anapatikana wapi?, ndipo walipoambiwa wakamwangalie chini ya uvungu wa kitanda cha bibi yake na kumkuta akiwa amelala hapo.

“Tulichofanya ni kumtoa kwani alikuwa na madaftari yake ya shule na alituomba maji na chakula,” amesema.

Mwanafunzi huo alisema kuwa, hana kumbukumbu yoyote kama alitoweka lakini siku moja akiwa kitandani, aliwaona watu wengi wanaume kwa wanawake wamemzunguka akiwemo bibi yake huyo.

Binti huyo amesema kuwa, alikuwa akienda shule kama kawaida na anashangaa kuambiwa kwamba hakuwa akienda shule, “mimi nashangaa kuwa eti siendi shule, najiona nilikuwa naenda shule kila siku.”

Hata hivyo, bibi huo (Kwandu) licha ya kukiri binti huyo kukutwa chini ya uvubgu wa kitanda chake, alisema hahusiki na kuongeza;

“Labda kuna watu wamefanya hivyo kupitia mimi lakini sihusiki kwa kupotea kwa mjukuu wangu.”

Deusdedit Nsimeki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ameeleza kuwa, wanamshikilia bibi huo kwa mahojiano zaidi.

Chanzo - Mwanahalisionline
Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Share:

MASHETANI WEKUNDU WAMPATIA MKATABA MNONO ANTHONY MARTIAL

Mshambuliaji machachari wa Manchester United Anthony Martial amesaini kandarasi mpya na Manchester United itakayombakisha katika uga wa Old Trafford mpaka Juni 2024.

Anthony Martial amefunga magoli 46  katika mechi 162 alizoichezea Manchester United.

Martial mwenye miaka 23, alijiunga na United kutoka Monaco Septemba 2015 kwa pauni milioni 36, lakini hakuwa na furaha klabuni hapo mwaka 2018 na kocha aliyepita Jose Mourinho alikuwa radhi kumuuza.

Mkataba wake mpya utamfanya asalie na Mashetani Wekundu mpaka atakapotimu miaka 29, na kuna kipengele kinachoruhusu mkataba huo kuongezwa kwa mwaka mmoja.

 "Kwa umri wake, ana ubongo mzuri wa mpira, ambao, ukijumuishwa na kipaji chake cha kipekee kinamfanya awe mchezaji mwenye mustakabali mzuri kabisa,"
alisema kocha wa muda wa United Ole Gunnar Solskjaer.

Mwezi Juni, ajenti wa Martial alisema mteja wake alikuwa anataka kuhama, na Mourinho alikuwa radhi, lakini uongozi wa United ulizima jaribio hilo na wakafungua ukurasa mpya wa majadiliano.

Chanzo:Bbc
Share:

MAMA AVUA NGUO MAHAKAMANI ... ASHINDA KESI

Jepkosgei alikuwa akitarajia uamuzi wa kesi iliyojikokota kortini kwa muda wa miaka 10, Mama huyo aliamua kuvua nguo zote mahakamani baada ya jaji kuahirisha uamuzi wa kese hio tena kwa kudai alihitaji muda zaidi kupitia ushahidi.

Alikasirishwa na jaji na kuanza kupiga kelele kortini huku akivua nguo mbele ya umma.

Jepkosgei alishikwa na hamaki na kuvua nguo zote mbele ya Jaji Anthony Ndung’u kwa kuahirisha kesi hiyo, kwa mara nyingine.

Ndung’u alipotazamiwa kutoa uamuzi wake Alhamisi, Januari 17 kuhusu kesi hiyo iliyojikokota kortini tangu 2009, aliiahirisha kwa kudai alihitaji muda zaidi kupitia ushahidi uliowasilishwa kabla ya hatimaye kusoma uamuzi huo na hatua hiyo ikamkera sana Jepkosgei.

Jumatano, Januari 30 Katika Mahakama ya Nakuru, Jaji aliusoma uamuzi wake na kumfanya Jepkosgei kuridhika mno.

 “Kwa kufuata utaratibu naondoa amri inayomzuia Jepkemoi, msimamizi wa ardhi ya Chemerus kugawanya ardhi nambari Nakuru/Municipality Block 13/312. Msimamizi ana uhuru wa kuitumia ardhi atakavyo," Ndung'u aliamrisha.

Chanzo:Tuko
Share:

MKENYA CLIFTON MIHESO ATUA ULAYA


Aliyekuwa winga wa Afc Leopards Mkenya Clifton Miheso amejiunga na klabu ya Ureno Clube Olimpico de Montijo.

Klabu hiyo ya Ureno imethibitisha kwamba imesajili mchezaji huyo wa Harambee stars ambaye alikuwa akiipigia Buildcon ya Zambia.

Klabu hiyo inasema Miheso ataongeza nguvu kwenye kikosi chao.

Ikumbukwe kuwa hii itakuwa mara ya kwanza kwa Miheso mwenye umri wa miaka ishirini na tano kupigia klabu ya Ulaya.

Klabu hiyo ya Olympic imetakia Miheso kila la heri klabuni hapo ambayo inapatikana mjini Montijo.

Montijo inacheza katika ligi ya daraja la tatu huko Ureno.
Share:

AFARIKI TENA BAADA YA KUFUFUKA

Hirpha Negero aliamka katika jeneza lake mwezi Novemba muda mfupi kabla ya kuzikwa.

Mawanamume wa Ethiopia aliyefufuka wakati wa mazishi yake miezi mwili iliyopita amefariki dunia.

Hirpha Negero alithibitishwa kufa mwezi Novemba ambapo aliwekwa ndani ya jeneza kwa saa tano, lakini wakati wa mazishi yake wanavijiji walisikia akigonga jeneza.

''Nilisikia mtu akilia, nilijihisi kuishiwa na pumzi ndipo nikajaribu kujitoa katika hali hiyo, nilikua mnyonge , hata sikuweza kuzungumza," alisema Hirpha

Baadae alisema alifanikiwa kuwaita watu, hapakua na mtu yeyote karibu.

Mchimba kaburi Etana Kena anasema watu waligutushwa na tukio hilo na wote walikimbia na kuliacha jeneza, ilibidi ajifungulie mwenyewe.

Baada kisa hicho hafla ya mazishi iligeuka kuwa sherehe.

 "Nimezika zaidi ya miili 50 au 60. Sijawahi kushuhudia maajabu kama haya. Alionekana kama amefariki," Kena ambaye ni mjomba wa Hirpha alisema

Bw.Hirpha alisema kuwa aliona mahali pazuri sana wakati alipokua amepoteza fahamu, ambapo mwanamume aliyekua amevalia nguo nyeupe alimwambia rudi nyumbani.

Dkt Birra Leggese amesema huenda Hirpha alipoteza fahamu vibaya sana "deep coma".

Mchimba kaburi wa awali alimzika tena Hirpha kwa mara ya pili siku ya Alhamisi, siku moja baada ya kifo chake.

 ''mara hii nilikua na hakika amefariki kwasababu, alishuhudia jinsi alivyougua kwa muda mrefu." alisema
Share:

NANI HUDANGANYA ZAIDI KATI YA WANAUME NA WANAWAKE?

Ndiyo, wanaume huongopa zaidi ya wanawake, hayo ni matokeo ya utafiti mkubwa uliofanyika kuhusu udanganyifu.

Taarifa za tafiti  565 zikihusisha watu 44,000 zilichakatwa na taasisi ya Max Planck na Technion za Ujerumani na Israel.


Lakini,wanawake si wakweli kihivyo. 42% ya wanaume waligundulika ni waongo,ikilinganishwa na 38% ya wanawake.

Utafiti huo pia umebaini kuwa vijana ni waongo zaidi ya wazee.

 kila mwaka kiwango cha ukweli hupanda kwa 0.28%.

Habari ndio hio.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger