Wednesday, 30 January 2019

WANACHAMA WA THRDC KANDA YA ZIWA WALAANI MAUAJI YA WATOTO NJOMBE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI   KULAANI MAUAJI YA WATOTO WASIOKUWA NA HATIA MKOANI NJOMBE 


 1.0 Utangulizi 

Sisi waanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu  (THRDC) Kanda  ya  Ziwa tumesikitishwa sana na  mauaji  ya  watoto kumi (10) yaliyotokea  Mkoani  Njombe (Nyanda  za juu  Kusini) na  kuacha  simanzi kubwa  kwa Taifa, familia, ndugu jamaa na marafiki.  Hivyo  basi  tunaungana  na wapenda  amani wote nchini  kwenye kuomboleza  msiba   huu  wa kitaifa. 

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi na waandishi mbali mbali ambao wamekuwa wakifwatilia suala la mauaji ya watoto hao, chanzo kikubwa cha mauaji hayo ni imani za kishirikina. Watu (waganga) ambao wamekuwa wakihusishwa na imani za kishirikina wamekuwa ni chanzo cha mauaji yaliyotokea mjini Njombe. Waganga hao wamekuwa wakiua wakiteka watoto na kuwaua huku wakichukua sehemu mbali mbali za miili yao. Aidha, jeshi la polisi linaendelea na upelelezi kuhakikisha wauaji hao wanatiwa nguvuni na kujibu mashtaka yatakayowakabili.

Ndugu  Waandishi wa habari  ifahamike  kuwa haki  ya  kuishi ni haki ya msingi  na ya Kikatiba kwa  kila  binadamu. Nchini Tanzania  haki  hiyo inalindwa  na Katiba  yetu  ya  Jamhuri  ya  Muungano wa Tanzania) kupitia  Ibara  ya 14. HIvyo basi kuvunja haki hii ni kukiuka Katiba pamoja na mikataba mbali mbali ya Kimataifa ambayo Tanzania ni nchi mwanachama.

Ndugu  waandishi,  mauaji  yaliyotokea  Mkoani Njombe  siyo  ya  kufumbiwa  macho   kwani kitendo  hicho  ni uhalifu   mkubwa   unaokiuka msingi  wa  haki ya  kuishi  na  utu wa  binadamu. Katika taifa  letu  hakuna  mwenye  mamlaka  ya  kuiondoa  roho  ya  binadamu  mwingine isipokuwa kwa mujibu wa sheria za nchi. Hata hivyo, historia yetu kama taifa la Tanzania japo bado tuna sheria inayomruhusu Rais kusaini adhabu ya kifo, ni mara chache sana tumeshuhudia marais wetu wastaafu na rais aliyepo madarakani wakisaini adhabu hii ya kifo. Ni dhahiri kwamba, suala la kutoa uhai wa mtu ni jambo baya kutokea katika taifa letu.

 2.0 Ulinzi wa Mtoto Kisheria 

Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 kifungu cha 9 inasema; mtoto ana haki ya KUISHI kujaliwa utu wake, kuheshimiwa, kupumzika (kucheza), kuwa huru, kuwa na afya bora, kupata elimu pamoja na makazi kutoka kwa wazazi wake.

 Hata hivyo, jukumu hili la ulinzi wa maisha ya mtoto lipo pia Kikatiba na katika Ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kila mtu ana wajibu wa kulinda na kuteteta Katiba na sheria za nchi. 

Ipo pia mikataba ya Kimataifa ambayo Tanzania ni mwanachama ambayo imeweka haki mbali mbali za mtoto ikiwemo haki ya kuishi. Baadhi ya Mikataba hiyo ni pamoja na Mkataba wa Kimataifa kuhusu watoto wa mwaka 1989, Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kisiasa na Haki za Kiraia wa mwaka 1966, Nyongeza ya Mkataba wa Maputo wa Mwaka 2003. 

Mikataba yote hii na mingine inaelekeza juu ya haki za watoto na ulinzi wa utu wao.

Ndugu waandishi  mauaji ya  watoto  kumi  ni  ukatili  mkubwa, kwani uhai  wa watoto hawa  umekatisha  ghafla maisha na ndoto zao  na kuleta  simanzi kubwa  kwa  ndugu  jamaa , marafiki  na taifa  kwa  ujumla. Taifa limepoteza kizazi ambacho kingeweza kulitumikia kwa maslahi mapana ya nchi.

Ndugu waandishi wa habari, Ikumbukwe kuwa watoto ni kundi ambalo kwa namna moja ama nyingine hawawezi kupata haki zao bila ya msaada wa watu wengine. Hivyo basi, inapotokea kundi hili la watoto linaathirika na matendo ya kinyama kama haya ya mauaji, ni jukumu letu sote kukemea vikali na kupaza sauti zetu ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wauaji wa watoto hawa.

 Hivyo basi, nyinyi kama waandishi wa habari na sisi watetezi wa haki za binadamu naomba tushikamane katika kipindi hiki kuwasemea watoto na kuhakikisha haki na utu wao unalindwa wakati wote.

3.0 Wito Wetu
Jeshi la polisi lifanye uchunguzi wa kina na kuwabaini wote waliohusika na mauaji tajwa na kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya wote waliohusika na mauaji hayo.

Vyombo  vya  ulinzi  na usalama  viwe macho  na  waganga  wanaohusisha   utajiri/mafanikio  na  vitendo  vya  kishirikina na kuwachukulia hatua stahiki pindi wanapokiuka sheria na Katiba ya nchi.

Waandishi wa habari watumie  kalamu  zao  kwenye  kutoa  elimu kwa  jamii  juu  ya  athari  za ushirikina ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa kero kwa jamii na kusababisha hasara na simanzi kwa ndugu, jamaa, marafiki na taifa kwa ujumla.

Jamii  ishiriki  kikamilifu  kwenye  kuripoti  viashiria  vya ushirikina na uvunjifu wa haki za binadamu katika jamii.
Tamko   hili limetolewa na wanachama wa Mtandao wa  Watetezi wa Haki za Binadamu  kanda  ya  Ziwa.

 Mashirika  Wanachama 
OJADACT
ADLG
WOTE SAWA
SAUTI YA WANAWAKE  UKEREWE
UVUUMA 

Na Edwin Soko
Share:

VIGOGO NIDA WASOMEWA HATI MPYA YA MASHTAKA 100

Vigogo sita wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) akiwamo Mkurugenzi Mkuu wa zamani, Dickson Maimu, wamefikishwa mahakamani na kusomewa hati mpya ya mashtaka 100 yakiwamo 22 ya kughushi, nyaraka za kumdanganya mwajiri 43, kujipatia fedha mawili, matumizi mabaya moja na kutakatisha fedha na kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh. bilioni 1.175.

Mbali na Maimu, washtakiwa wengine ni Aveline Mombuli, Astery Ndege, George Ntaliwa, Xavery Silverius maarufu kama Sliverius Kayombo na Sabina Nyoni.

Walisomewa mashtaka yao jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salum Ally.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Mawakili wa Serikali, Simon Wankyo na Leonard Swai. Wankyo alidai kuwa kesi hiyo namba 07/2019 ina mashtaka 100 dhidi ya washtakiwa hao.

Alidai mshtakiwa wa kwanza, wa tatu, wanne na watano wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kula njama la kwanza na la 85.

Alidai kuwa Maimu, Ndege na Ntalima wanakabiliwa na mashtaka 22 ya kughushi nyaraka malipo kutoka Nida.

Upande huo wa Jamhuri ulidai Maimu, Ndege na Ntalima wanakabiliwa na mashtaka 43 ya kuandaa nyaraka za uongo za malipo ya kumdanganya mwajiri wao.

Swai naye alidai Maimu, Ndege, Ntalima na Kayombo, wanakabiliwa na mashtaka 25 ya kutakatisha fedha haramu.

Aliendelea kudai katika mashtaka matano mshtakiwa Maimu, Ndege, Ntalima, Kayombo, Mombuli na Nyoni kwa nyakati tofauti waliisababishia Nida hasara ya Sh. 1,175,785,600 walishindwa kutimiza majukumu yao na kupitia nyadhifa walizokuwa nazo waliisababishia hasara hiyo.

Katika shtaka la 95, ilidaiwa kuwa kati ya Novemba 7, 2011, makao makuu ya Nida ofisi zilizopo Kinondoni, Maimu akiwa mtumishi wa umma kama Mkurugenzi Mkuu na Nyoni akiwa kama Mkurugenzi wa Sheria walitumia madaraka yao vibaya na kusababisha Shule ya Sheria na Kampuni ya M-S Law Partner kujipatia faida ya Sh. 899,935,494.

Ilidaiwa Juni 5, 2013 katika Benki ya CRDB tawi la Lumumba, Ilala jijini Dar es Salaam Kayombo kuwa alijipatia kwa njia ya udanganyifu Sh. 45,515,961, huku akijua ni mazalia ya kughushi na utakatishaji fedha haramu.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Swai alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na aliomba mahakama kupanga tarehe ya kuwasomewa washtakiwa maelezo ya mashahidi.

Pia, alidai wameshawasilisha taarifa Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa kuhusu kusikiliza kesi hiyo.

Hakimu alisema washtakiwa watasomewa maelezo ya mashahidi Februari 12, mwaka huu na wapelekwe mahabusu.

Alisema mshtakiwa wa pili, Mombuli na Nyoni, wanakabiliwa na mashtaka ya kuwasilisha nyaraka za kumdanganya mwajiri na matumizi mabaya ya madaraka wawasilishe upya maombi ya dhamana Mahakama Kuu.
Share:

AHUKUMIWA JELA SIKU 30 KWA KUMUITA MPENZI WAKE MAMA MZEE

Mwanaume mwenye umri wa makamo kutoka Maralal kaunti ya Samburu amefungwa jela kwa siku 30 baada ya mahakama kumpata na hatia ya kutumia lugha chafu kwa aliyekuwa mpenzi wake.

 Mshukiwa Joseph Naroto anasemekana kumtusi mpenzi wake wa zamani Winnie Letito kuwa yeye ni kahaba na mwanamke mzee. 

Naroto anasemekana  kukopa pesa kutoka kwa Winnie wakati wakichumbiana ila alipotaka arejeshe pesa hizo mwezi Septemba mwaka wa 2017, mshukiwa alianza kuwa mkali na kumrushia cheche za matusi kila mara.

  Kesi dhidi ya Naroto ilisikizwa Jumanne, Januari 29 ambapo alikana mashtaka hayo na mahakama iliamru mshukiwa azuiliwe kwa siku 30 baada ya kushindwa kulipa dhamana ya KSh 3,000.

Chanzo:Tuko
Share:

AFISA POLISI ASHIKILIWA KWA MADAI YA KUMNAJISI MTOTO KITUONI

Afisa mmoja wa polisi Kaunti ya Kisumu ametiwa mbaroni kwa madai ya kumnajisi mshukiwa aliyekuwa akizuiliwa,  Tobias Nakuwa Lobolia alikamatwa Jumanne, Januari 29, kwa madai ya kumnyanyasa kimapenzi msichana wa miaka 15 aliyekuwa akizuiliwa mahabusu.

Afisa huyo wa polisi alishutumiwa kwa kumnajisi mtoto huyo ndani ya kituo cha polisi mnamo Disemba 2018, hakimu wa Kisumu aliamrisha uchunguzi kufanywa baada ya mtoto huyo kulalamika akiwa kortini na alimtambua afisa huyo baada ya maafisa hao kuletwa mbele yake.


 Mshukiwa alilalamika Jumatatu, Disemab 17, 2018, alipofikishwa kortini na Hakimu akaamrisha uchunguzi kufanywa mara moja.

 "Kwamba mnamo terehe 15 ya Disemba 2018 at mchana, afisa aliyetajwa aliingia katika seli ya wanawake na kumnyanyasa kimapenzi kwa kushika titi zake,"  


 Hata hivyo kutuo cha polisi alipokuwa akizuiliwa msichana huyo hakikutajwa, na hii ni kwa sababu za kiusalama.

 Tobias sasa huenda akafunguliwa mashtaka kwa kutumia cheo chake vibaya chini ya kifungu cha sheria nambari 24 cha Sheria Kuhusu Uhalifu wa Kingono ya 2006. 

Chanzo:Tuko
Share:

MAUAJI YA WATOTO YATUA BUNGENI..LUGOLA ASEMA NI USHIRIKINA

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amesema imebainika kuwa mauaji ya watoto mkoani Njombe ni ya imani za kishirikina.

Lugola ametoa kauli hiyo leo Jumatano Januari 30, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na mbunge wa Mufindi Kusini (CCM), Mendrad Kigola.

Mbunge huyo amehoji ni mkakati gani umewekwa na Serikali katika kukomesha mauaji ya watoto katika mkoa wa Njombe ili kurudisha amani mkoani humo.

Akijibu swali hilo, Waziri Lugola amesema tangu juzi Januari 28, 2019 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni yupo mkoani Njombe ambako anafanya vikao vya ndani na kamati za ulinzi ili kutafuta chanzo.

"Tumeshapata orodha ya majina ya wahusika na tumebaini sababu kubwa ni imani za kishirikina, lakini nawaonya wote wanaohusika kuwa wasitingishe kibiriti katika serikali ya Rais John Magufuli, watashughulikiwa," amesema Lugola.

Waziri amesema Serikali iko macho na itaendelea kuwa macho katika kuwalinda watu wake na vyombo vya ulinzi havitalala.

Na Habel Chidawali,Mwananchi 
Share:

SERIKALI YAAPA KUWANASA WAUAJI WA WATOTO MKOANI NJOMBE

Waziri Kangi Lugola amesema tayari serikali imepata majina ya wote waliohusika katika mauaji ya watoto Njombe.

Serikali imeahidi kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kuhusika katika mauaji ya watoto mkoani Njombe.

Watoto sita, wakiwemo watatu wa familia moja wenye umri chini ya miaka 10 wamepatikana wakiwa wamefariki katika mazingira ya kutatanisha mkoani humo.

Akizungumza Bungeni leo, Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amesema tayari wameshabaini baadhi ya wale waliohusika na mauaji hayo na hatua kali zitachukuliwa.

"Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mauaji hayo yametokana na imani za kishirikina...n tayari tumeshawabaini baadhi ya wale ambao wameshiriki. Nawataka watu waache kuichezea serikali, tutaanza na mkoa wa Njombe," ameonya Lugola.

Lugola hata hivyo hakusema ni watu wangapi mpaka sasa wametiwa mbaroni kutokana na mauaji hayo.

Chanzo:Bbc
Share:

HAUSIGELI KENYA WAONGEZWA MSHAHARA


Na Theopista Nsanzugwanko - Habarileo

Serikali ya Kenya imetangaza kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wa ndani katika miji mikubwa kufi kia Shilingi za Kenya 13,500, ambayo ni sawa na zaidi ya 300,000 za Tanzania.

Lakini, kwa upande wake, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limesema katika kuhakikisha mishahara inapanda katika sekta za umma na binafsi baada ya kukaa kwa zaidi ya miaka mine, wameunda tume maalum kwa ajili ya kuchambua sababu za kutaka mishahara kupanda.

 Tume hiyo itaangalia namna ya kupanda mishahara kwa wafanyakazi wote, wakiwemo wa ndani, kwa kuongeza kima cha chini cha sasa cha Sh. 100,000. 

Kwa Kenya, wizara inayoshughulikia masuala ya ajira imetaka waajiri katika miji mikubwa, kuwalipa wafanyakazi wa kazi za ndani kiwango hicho cha mshahara, hasa kwa wanaoishi miji mikubwa ya Nairobi, Mombasa na Kisumu.


Aidha, wale wanaoishi katika Manispaa na Halmashauri za miji watawalipa wafanyakazi wao mishahara ya Shilingi za Kenya 12,522, sawa na Shilingi za Tanzania 284,586 au Shilingi za Kenya 600 sawa na 13,600 kwa siku . 

Hatua hiyo imetokana na wafanyakazi wa ndani kuandamana katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi katika Viwanja vya Uhuru Park. Wafanyakazi watakaonufaika na malipo hayo mapya ni wafanya usafi, wasimamizi wa bustani, waangalizi wa watoto, wasaidizi wa kazi za ndani, walinzi na wahudumu.

Marekebisho hayo yamesainiwa na Waziri wa Kazi, Ukur Yattani Desemba 19. Alisema agizo hilo jipya la mishahara, litaongezwa katika posho ya nyumba kwa wafanyakazi. Pia waajiri wanatakiwa kutoa michango katika mifuko ya hifadhi ya jamii kwa mwezi. 

Share:

MUSWADA WA VYAMA VYA SIASA WAPITA WABUNGE WA CCM, UPINZANI WAKIVUTANA


Na Sharon Sauwa, Mwananchi 
 Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018 jana ulipitishwa bungeni, Dodoma.

Kabla ya kupitishwa kwa muswada huo uliowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama aliyeuita kuwa ni kiboko, kuliibuka mvutano mkali kati ya wabunge wa upinzani na CCM.

Baada ya kupitishwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema, “Kilichobaki tutaupeleka kwa Mheshimiwa Rais ili akiridhia ausaini uwe sheria.”

Awali, Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ilipendekeza kurekebishwa au kufutwa kwa maeneo saba makubwa huku Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ukiwataka wabunge kuukwamisha.

Muswada huo umepita huku Taasisi sita za kiraia zikiongozwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), zikiwa zimetoa onyo kuwa hakuna mtu aliye salama endapo utapitishwa.

Taasisi hizo zinajumuisha Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Twaweza, Baraza la Habari Tanzania (MCT), Center for Strategic Litigation na Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (Wahamaza).

Waziri Mhagama alisema pamoja na mambo mengine, muswada unalenga kumpa uwezo Msajili wa kuhakiki chama cha siasa wakati wowote. “Lengo ni kuhakikisha chama cha siasa kinakuwa na sifa za usajili muda wote wa uhai wake na kueleza bayana mamlaka ya msajili wa vyama vya siasa kuhakiki muda wowote utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa ili kuhakikisha chama cha siasa kinazingatia na kutekeleza masharti ya usajili,” alisema.

Hata hivyo, Ester Bulaya akisoma maoni ya kambi ya upinzani alisema kifungu kinachompa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kuingilia mfumo wa uchaguzi ndani ya chama kitapunguza uhuru wa vyama kufanya chaguzi bila mashinikizo.

Alisema kifungu kingine ni kinachotoa masharti ya namna ya utoaji wa elimu ya uraia hakikutilia maanani kuwa vyama vya siasa vina uhusiano wa kiitikadi na vyama rafiki kutoka nje ya nchi.

Bulaya ambaye ni mbunge wa Bunda Mjini (Chadema) alisema Katiba inatoa masharti ya mtu anayetaka kugombea urais na umakamu wa Rais wa Tanzania kwamba anatakiwa kuwa raia kwa kuzaliwa lakini masharti hayo hayakuwekwa kwa wazazi wake.

“Kambi ya upinzani inahoji kwa nini mtu anayegombea nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa Taifa hili wazazi wake hawawekewi masharti ya uraia na Katiba iweje mtu anayetaka kusajili chama cha siasa awekewe masharti hayo?” alihoji.

Mvutano ulivyokuwa

Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee, akichangia muswada huo alisema katika ibara ya 8 c ya muswada huo kuna uvunjwaji wa Katiba.

Alisema muswada huo unataka kufutwa kwa chama ambacho kitashindwa kuwa na kumbukumbu ya wanachama wake wakati Katiba imeeleza mazingira ambayo yanaweza kukifanya chama kufutwa.

Mdee aliungwa mkono Mbunge wa Tanga Mjini (CUF) Mussa Mbarouk aliyewataka wenzake wa CCM kutambua kuwa ipo siku nao watakuwa chama cha upinzani na kwamba sheria hiyo itawahusu.

Hata hivyo, Mbunge wa Mbinga Mjini (CCM), Sixtus Mapunda alisema muswada huo ndio mwarobaini wa kuondoa uhasama unaotokana na vyama vya siasa, “Ilifika hatua vijana wetu badala ya kutulinda wanageuka kuwa wana migambo au Al Qaeda, tunakwenda katika uchaguzi vijana wanamwagiana tindikali, wanakatana masikio, migongo. Hii sheria inakwenda kuondoa hawa Mungiki,” alisema.

Mbunge wa Madaba (CCM) Joseph Mhagama aliwataka wabunge wa upinzani kuacha upotoshaji juu ya muswada huo akisema unalenga kuweka uwazi na uwajibikaji katika uendeshaji wa vyama vya siasa.

Via Mwananchi
Share:

Picha : WAKENYA WATUA TANZANIA KUJIFUNZA KUHUSU MIRADI MAJI TAKA


Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI) Tim Ndezi akiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA). 

Ujumbe huo ulilenga kutembelea na kujionea miradi ya majitaka maeneo ya Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi maalum ya Maji Taka inayotekelezwa katika maeneo yasiyopimwa na yenye msongamano. Wageni hao ni maofisa wa Serikali ya Kenya kutoka Kampuni ya majisafi na majitaka Nairobi (NCWSC) na Huduma za jamii, Mashirika binafsi na viongozi wa vikundi vya jamii wapo nchini kwa siku 5 wakitembelea Dar es Salaam na Mwanza. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mji Mpya, Kata ya Vingunguti Rahimu Seif Gassi (kulia) kiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka. Wageni hao ni maofisa wa Serikali ya Kenya kutokea upande wa Maji na Huduma za jamii, Mashirika binafsi na viongozi wa vikundu vya jami wapo nchini kwa siku 5 wakitembelea Dar es Salaam na Mwanza.
Mhandisi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI), Festo Dominick Makoba ambaye ndiye msimamizi wa eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Moja ya Choo cha kisasa vinavyojenga na Shirika la CCI kwa kusaidiana na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) ili kuwawezesha wananchi wanaoishi katika maeneo yasiyo rasmi.
Moja ya chemba za vyoo vya kisasa.
Muonekano wa Choo cha zamani ambacho wakazi wa Vingunguti walivyokuwa wakitumia.
Mhandisi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI), Festo Dominick Makoba ambaye ndiye msimamizi wa eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam akionyesha namna mabomba ya vyoo yalivyopita.
Wageni wakiendelea na ziara.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mji Mpya, Kata ya Vingunguti jijini Dar es Salaam, Rahimu Seif Gassi (kulia) kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI) Tim Ndezi akiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Wananchi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam akiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Wananchi wakimsikiliza mwenyekiti.
Bi Kellen Muchira kutoka Shirika la Caritas Switzerland lililopo nchini Kenya akizungumza machache juu ya jinsi walivyoweza kufika Tanzania kujifunza namna ya Shirika la CCI na DAWASA wanavyoweza kushirikiana kuwasaidia wakazi wanaoishi katika makazi yasiyo rasmi kukusanya Maji Taka.
Afisa Miradi wa Akiba Mahirani Trust ya nchini Kenya, Patriki Njoroge akieleza machache mbele ya wakazi wa Vinguti jijini Dar es Salaam wakati walipofika Tanzania kujifunza namna ya Shirika la CCI na DAWASA wanavyoweza kushirikiana kuwasaidia wakazi wanaoishi katika makazi yasiyo rasmi kukusanya Maji Taka.
Makazi wa Vingunguti akisoma risara mbele ya wageni.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Mhandisi Charles Makoye akiwaelezea juu ya mradi wa kuchakata maji Taka uliopo Toangoma wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) (mwenye shati jeupe) akiwaonyesha chemba ya mradi wa kuchataka Maji Taka iliopo Toangoma jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Mhandisi Charles Makoye (Kulia) akiendelea kutoa maelezo.
Wageni wakiwa katika picha ya pamoja.

Share:

WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO MAZITO KWA MAAFISA USTAWI WA JAMII

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa watekeleze majukumu yao kwa bidii, weledi, uadilifu na wasijihusishe na vitendo vya rushwa.


Amesema maafisa hao wanatakiwa watumie mbinu shirikishi ambazo zinahusisha jamii yenyewe na wataalamu ambao ni watoa huduma ngazi ya jamii (Community Case Worker) ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao.


Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo jana (Jumanne, Januari 29, 2019) kwenye Mkutano wa Mwaka wa Kiutendaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, jijini Dodoma.


Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka maafisa hao wahakikishe kwamba haki za msingi za makundi hayo zinapatikana kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo katika kutoa huduma ya taaluma yao.


Amesema taaluma ya Ustawi wa Jamii imepewa dhamana ya kuwa mlinzi wa mtoto, kumhudumia na kusimamia haki zake, hivyo amewatakawazuie na watokomeze aina zote za ukatili kwa watoto, wazee na wenye ulemavu.


Waziri Mkuu amesema jukumu hilo pia linahusisha watoto waliopo kwenye mazingira hatarishi na wanaoishi na kufanya kazi mitaani, wazee, wanawake wasio na uwezo na watu wenye ulemavu.


Amesema pamoja na mafanikio makubwa ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imeyapata ni muhimu wakaendelea kuongeza nguvu na weledi ili kutorudi nyuma katika kujenga msingi wa kuimarisha ustawi wa makundi maalumu.


Pia, Waziri Mkuu amewaagiza maafisa hao wakasimamie utekelezaji wa mkakati wa Mkono kwa Mkono, Familia kwa Familia, Kaya kwa Kaya kupitia huduma ya kuzuia ukatili ngazi ya familia wenye lengo la kuzuia ukatili ndani ya familia ili ulete matokeo tarajiwa.


“Tambueni umuhimu wenu na kwamba jamii inawategemea kutekeleza majukumu yenu kikamilifu ili kupunguza matatizo ya kijamii kwa wale wenye uhitaji wakiwemo watoto, watu wenye ulemavu, wazee, familia zenye migogoro na akina mama wanaonyanyaswa na makundi mengine.”


Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewashukuru wadau wa maendeleo kwa namna wanavyoshirikiana na Serikali katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo likiwemo suala la uimarishaji wa huduma za ustawi wa jamii nchini.


Amesema anatambua mchango mkubwa kutoka kwa shirika la UNICEF, USAID, UN WOMEN, UNFPA, John Snow Inc, Pact, HelpAge International, World Vision, Save the Children, Plan International na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine wameendelea kushirikiana na Serikali kuinua kiwango cha utoaji huduma za ustawi wa jamii nchini.


“Ninapenda kuwahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Magufuli, ipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi ili tuweze kufikia malengo ya maendeleo endelevu ifikapo 2030.”


Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Uadilifu, Weledi na Uwajibikaji katika Utoaji wa Huduma za Ustawi wa Jamii Ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ni Nguzo katika kuelekea Uchumi wa Kati wa Viwanda.”


Waziri Mkuu amepongeza kwa kuanzisha utamaduni huo wa kukutana Watendaji wa Sekta ya Ustawi wa Jamii kwa kuwa hiko ni kiashiria kwamba kuna mabadiliko katika utendaji kwa kuzingatia kuwa mkutano huu haujawahi kufanyika toka mwaka 2006.


Mkutano huo wa siku tatu unajumuisha Maafisa Ustawi wa Jamii 164 kutoka mikoa yote Tanzania Bara, wadau wa maendeleo, wawakilishi wa wazee, watoto waishio katika mazingira hatarishi waliohitimu mafunzo ya VETA pamoja na watoto waliokuwa wakiishi mitaani ambao kwa sasa wameunda kikundi cha burudani.
Share:

Tuesday, 29 January 2019

RAIS MAGUFULI AFUNGUKA KUHUSU WAKUU WA WILAYA NA MIKOA KUWEKA NDANI WATU

Rais John Magufuli amewaasa wakuu wa wilaya kutotumia vibaya sheria na mamlaka walizopewa ikiwamo za kuweka watu ndani na kuwatoa wakidai wamejifunza bila kupelekwa mahakamani.


Magufuli ameyasema hayo leo wakati wa kuwaapisha majaji 15 wa Mahakama Kuu na sita wa Mahakama ya Rufani.

Amesema siyo haki na viongozi wengi wamezungumza kuhusu suala hilo na yeye anarudia kwa sababu kama mkuu wa wilaya ana mamlaka hayo na mkuu wa mkoa akiamua kuweka watu ndani itakuwa ni vurugu, huku akibainisha kuwa mambo mengine yanahitaji kutolewa maelekezo tu.

“Kuelekeza kunaweza kuwa na matokeo chanya wakati mwingine kuliko hata kuweka watu ndani,” amesema.

Magufuli Magufuli amesema ameamua kumtoa katika uongozi aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Mwanga, Aaron Mbogho na kumhamishia katika kitengo cha wadudu kwa sababu yeye ni mtaalamu wa eneo hilo.

Amesema yaliyokuwa yakitokea wilaya ya Mwanga ya kuwaweka watendaji wa Serikali ndani akiwamo katibu tawala, mkurugenzi kila mmoja alikuwa akiyaona huku vurugu zote zilikuwa zikianzia kwa kiongozi huyo.

“Hata katika mazungumzo yake amekuwa akisema yeye ni mtaalamu pekee wa wadudu Tanzania hakuna kama yeye hivyo nikaamua kumpeleka huko huenda atafanya vizuri...” amesema Magufuli.


Na Aurea Simtowe, Mwananchi
Share:

KOMPANY KUTEMWA RASMI MAN CITY

Nahodha wa klabu ya Manchester City Vincent Kompany hatopewa kandarasi mpya kulingana na mkufunzi Pep Guardiola.

Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 anayeichezea Ubelgiji inakamilika mwisho wa msimu huu .

Ameichezea klabu hiyo mara 14 msimu huu na sasa anauguza jeraha la misuli.


Ripoti wikendi zinasema kuwa City ilitaka kumpatia Kompany mkataba wa miezi kumi na mbili lakini hali yake ya maungo ndio ilizua wasiwasi.

Amecheza mechi tatu pekee tangu mwanzo wa mwezi Novemba huku mechi yake ya mwisho ikiwa ushindi dhidi ya Liverpool mnamo tarehe tatu Januari.

Kompany aliwasili katika klabu ya City mwaka 2008 kutoka klabu ya Hamburg na kutia saini kandarasi ya miaka sita hadi mwaka 2012.


''Sitaki klabu iseme , ni sawa unaweza kuondoka, wakati huohuo ni muhimu kujua kwamba kuna wakati ambapo ni mwisho kwa kila mtu, Ndio maana nikasema kuwa sio uamuzi wangu'', alisema Guardiola.

Chanzo:Bbc

Share:

WANAOHUSIKA NA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE HAWATAACHWA SALAMA:NAIBU WAZIRI MASAUNI

SERIKALI imelaani mauaji ya kinyama ya watoto watatu wa familia moja yaliyotokea mkoani Njombe na kusema kuwa tukio hilo halitapita bure na inataka iwe fundisho kwa watu wenye roho za kinyama wanaotekeleza mauaji ya watoto wadogo hapa nchini. Akizungumza katika mazishi ya watoto watatu Godliver, Giliad na Gasper Nziku wote wa familia moja ambao wamefariki dunia kwa kuchinjwa na kutupwa maeneo tofauti, yaliyofanyika Kijiji cha Ikando, Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe yaliyofanyika jana Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, HAMADI MASAUNI ameyasema hayo wakati akitoa salamu…

Source

Share:

VENEZUELA YAWEKEWA VIKWAZO VINGINE VYA KIUCHUMI

Marekani imeliwekea vikwazo shirika la mafuta la serikali ya Venezuela PDVSA na kulitaka jeshi la nchi hiyo kuyaunga mkono mabadiliko ya amani ya uongozi.

Mshauri wa masuala ya ulinzi wa rais Donald Trump John Bolton amedai kuwa rais wa Venezuela Nicolás Maduro na washirika wake hawataweza tena kuiba rasilimali za raia wa Venezuela.

Harakati za upinzani nchini humo kuung'oa madarakani utawala wa Maduro zimeshika kasi katika kipindi cha siku za hivi karibuni.

Marekani na nchi zaidi ya 20 zinamtambua kiongozi wa upinzani Juan Guaidó kama rais wa mpito wa nchi hiyo.

Waziri wa Fedha wa Marekani Steven Mnuchin amesema mapato yatakayotokana na uuzwaji wa mafuta kutoka nchi hiyo yatazuiwa kwenda kwenye mifuko ya serikali ya Maduro.

Kampuni hiyo inaweza kuondokana na vikwazo pale itakapomtambua Guaidó kama rais halali.

Chanzo:Bbc
Share:

BUNDI AZUA GUMZO BAADA YA KUTINGA MAPEMA BUNGENI DODOMA

Katika hali isiyo ya kawaida Ndege aina ya bundi ameonekana Bungeni akiwa juu kabisa. 

Spika wa bunge, Job Ndugai, amemshuhudia Bunge huyo laivu na kusema alipomuona alichanganyikiwa kidogo na kisha akawatoa hofu Wabunge kuwa kwa Dodoma kumuona ndege huyo mchana si tatizo isipokuwa ukimuona usiku ndio unaweza kuogopa.

Watumishi wa Bunge waliingia ndani ya jengo hilo kwa ajili ya ukaguzi na kumuona ndege huyo juu ya paa la ukumbi wa Bunge.

Ndege huyu hakutoka licha ya maofisa hao kutaka kumtoa, aliruka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Hata hivyo, haikujulikana muda aliotoka na mahali alikoelekea lakini Spika Job Ndugai akasema ni mambo ya kawaida kwa Dodoma.

"Waheshimiwa wabunge, asubuhi tumeanza kumwona Bundi ndani ya jengo hili, lakini kwa Dodoma Bundi wa mchana hana madhara kwa hiyo ni mambo ya kawaida kabisa," amesema Ndugai.

==>>Msikilize spika hapo chini

Share:

ONYO LA RAIS MAGUFULI KWA ALIOWATEUA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewataka Wakuu wa Wilaya nchini kutotumia mamlaka yao vibaya kwa kuwaweka ndani baadhi ya watendaji wenzao ikiwa ni kinyume na sheria.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya mbili, Mwanga pamoja na Tarime ambapo alibainisha sababu za kuwatengua waliokuwa kwenye nafasi hizo kuwa ni kutokana na kutumia vibaya mamlaka yao.

 "Mnasheria na mamlaka mlizopewa msizitumie vibaya sheria mnazo lakini msizitumie vibaya mtu anawekwa ndani halafu hamumpeleki mahakamani", alisema 
Rais Magufuli.

"Viongozi wengi wamelizungumzia hili namimi nalirudia, kuna masuala mengine hayahitaji mtu kuweka ndani yanahitaji kutoa maelekezo tu", aliongeza Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amehoji juu ya hatua mtu anayetuhumiwa kubaka watoto 11 kushindwa kukutwa na hatia na mahakama baada ya ushahidi kutojitosheleza.

Chanzo:Eatv
Share:

CLIFORD NDIMBO KAULA CAF







Cliford Mario Ndimbo.

Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF), limemteua Afisa Habari wa TFF kuwa Afisa Habari wa mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika kati ya Mamelodi Sundowns na ASEC Mimosas.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirikisho la soka nchini (TFF), Ndimbo atasimamia taarifa zote za mchezo huo utakaopigwa Ijumaa Februari 1, 2019 nchini Afrika Kusini kwenye uwanja wa Loftus Versfeld.

Mamelodi Sundowns na ASEC Mimosas zipo kundi A na mchezo huo utakuwa ni wa tatu kwa kila timu katika hatua hiyo ya makundi.

Timu hizo zote zina alama 3 baada ya kushinda mchezo mmoja na kufungwa moja. Mamelodi wapo nafasi ya tatu kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa huku ASEC wakiwa katika nafasi ya 3.

Vinara wa kundi hilo ni timu ya Wydad Casablanca ambayo nayo ina alama 3 huku Lobi Stars ya Nigeria ikiwa na alama 3 katika nafasi ya 4 ya kundi hilo.

Chanzo:Eatv
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger