Mwanamuziki Oliver Mtukudzi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 66.
Wednesday, 23 January 2019
FIFA YAMFUNGIA MAISHA MICHAEL WAMBURA KUJIHUSISHA NA MPIRA WA MIGUU
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), limetangaza kumfungia Michael Wambura maisha.
Kifungo hicho kinamfanya Wambura kutojihusisha na soka maisha.
Hukumu hiyo ya kamati ya maadili ya Fifa inaelezwa kukazia ile hukumu ya kamati ya rufaa ya TFF ambayo Wambura licha ya kuwa Makamu Mwenyekiti wa TFF, hakutakiwa kujihusisha na soka.
MBAO FC WAAMUA KUMBEBA ZAHERA...WAITOA GOR MAHIA
Mbao FC
Mapema jana baada ya mchezo wa Yanga na Kariobangi Sharks kumalizika kwa Yanga kutolewa kwa kufungwa mabao 3-2, kocha Mwinyi Zahera alisema hajaumizwa na matokeo kwasababu bado kuna timu za Tanzania ambazo zinaweza kubeba taifa.
Mbao FC leo wameyabeba malengo ya Zahera kwa kushinda mechi yao ya robo fainali ya michuano ya SportPesa Cup kwa kuwatoa mabingwa watetezi Gor Mahia kwa kuwafunga kwa penalti 4-3 baada ya kutoka 1-1 katika dakika 90.
Zahera alisema ''Mimi siwezi kuumia kwasababu tumetolewa ila nawatakia Simba na Mbao FC watuwakilishe vizuri ili wazifunge AFC Leopards na Gor Mahia ili waende fainali wakachukue ubingwa ubaki Tanzania'', amesema Zahera.
Mbao FC sasa itakutana na Kariobangi Sharks iliyowatoa Yanga katika mchezo wa nusu fainali huku mshindi wa robo fainali kati ya Simba na AFC Leopards atakutana na Bandari FC ambayo nayo iliitoa Singida United.
RAIS MAGUFULI ASIKIA KILIO CHA SHEIKH MSIKITI WA UDOM
Rais John Magufuli amesikia kilio kilichofikishwa na Sheikh Mussa Kundecha, kuhusu kitendo kilichofanywa na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) cha kuvunja msikiti uliokuwa ukijengwa.
Amesema, kuwa suala hilo litashughulikiwa na kwamba, ni utaratibu wa kawaida kwa vyuo kuwepo kwa huduma ya nyumba za ibada kama ilivyo kwa Vyuo Vikuu vingine.
Sheikh Kundecha, Amiri Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislam asubuhi ya leo alimweleza Rais Magufuli kadhia iliyotokea UDOM na kumwomba kuliangalia suala hilo kutokana na umuhimu wake.
“Ni utaratibu wa kawaida, pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuna Msikiti, madhehebu yote yanafanya ibada pale. Kuna Kanisa ambapo madhehebu yote yanafanya ibada pale, wanapangiana muda tu. Niseme hili la Dodoma litafanyiwa kazi,” amesema Rais Magufuli na kuongeza;
“Spiriti ile ile iliyokuwepo UDSM ndio itakayokuwepo Dodoma. Sisi Tanzania tumelelewa na Mwalimu Nyerere namna ya kuvumiliana. Uvumilivu huu tukiendelea kuujenga, utalifikisha taifa hili mahali pema.”
Awali Sheikh Kundecha alisema,
“Wiki moja iliyopita tulijiwa na wenzetu Waislamu kutoka Dodoma, wakiongelea suala la msikiti. Tunashukuru serikali kwa kutenga eneo la ibada, ni jambo muhimu,” amesema Sheikh Kundecha.
Amesema kuwa, ni muhimu kuwa na maeneo ya ibada katika maeneo ya kijamii hasa kutokana na utaratibu wa Ibada ya Kiislam na kwamba, kwa kuzingatia hilo uongozi wa chuo awali ulitoa eneo na Waislam walianza kuchangishana kwa ajili ya ujenzi wa msikiti huo.
“Waislam wakawa wanachangishana ili kujenga nyumba hiyo ya ibada lakini ghafla taarifa ya chuo ikatolewa kusitisha ujenzi wa msikiti huo,” amesema Sheikh Kundecha na kuongeza;
“Tuliamini labda taarifa hiyo ya kusitisha ilitolewa ili kuweka baadhi ya mambo sawa lakni mara wakaleta magreda na kuanza kuubomoa na na mnajua pesa za kuchangisha zilivyo ngumu. Sasa leo anasikia greda imevunja, hii inaleta shida kwa wanaochangia. Nakuomba maeneo ya namna hiyo uyatazame ili isilete mizozo.”
RAIS MAGUFULI AKERWA WANAOVAA OVYO OVYO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka viongozi wa dini kukemea maovu katika jamii, ikiwemo mmomonyoko wa maadili.
Akizungumza na viongozi wa dini waliofika Ikulu jijini Dar es salaam, Rais Magufuli amesema kwamba inafahamika kuwa watu wasiovaa mavazi ya heshima hawaruhusiwi kuingia kanisani, lakini itakuwa vyema kama watu hao hawataruhusiwa kuingia sehemu yoyote.
Akizidi kufafanua hilo Rais Magufuli amesema anavutiwa na kanisa la Askofu Kakobe wanavyofunga viremba, kwani hayo ndio maadili ya Mtanzania.
“Najua Roman Catholic wanaweka matangazo kuwa wenye nguo zisizo na heshima hawaruhusiwi kuingia kanisani, sasa tuende mbali na hapo, tusizungumze tu wasiruhusiwe kuja kanisani, wasiruhusiwe mahali popote, ndio maana nafurahi kanisa la mzee Kakobe wanafunga na vitambaa wote, hawataki kuonekana nywele ingawa nywele za Kakobe huwa tunaziona”, amesema Rais Magufuli.
Hii leo Rais Magufuli amekutana na viongozi wa Dini Ikulu jijini Dar es salaam, kujadili changamoto mbali mbali zinazowakabili kwenye sekta yao.
RAIS MAGUFULI : HAKUNA ALIYEMZUIA MBOWE KUFANYA MKUTANO KWENYE JIMBO LAKE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, Freeman Mbowe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema hakuna kiongozi wa kisiasa ambaye amezuiliwa kufanya mikutano kwenye eneo lake ambalo amechaguliwa na kusema hali hiyo ndiyo demokrasia.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na viongozi wa madhebebu mbalimbali ya dini ili kujadili masuala mbalimbali yanayoendelea nchini.
Akijibu swali la mchungaji Lyimo ambaye aliohudhuria hafla hiyo, Rais wa Magufuli amesema hakuna mtu aliyezuiliwa kufanya mikutano kwenye maeneo yao bali lengo ni kuhakikisha waliochaguliwa na wanapewa nafasi.
"Kama ni Mbunge wa Ubungo hakuna aliyezuiliwa, yeye ni Mbunge wa Jimbo lile Mheshimiwa Kubenea, hakuna anayemzuia Mheshimiwa Mbowe kufanya mkutano kwenye jimbo lake la hai."
"Nataka vyama yetu viige mfano mzuri wa viongozi wa dini wanavyoheshimiana na kupendana, kwa sababu jukumu langu mlinipa ni kuilinda amani ya Tanzania. Hakuna mtu aliyezuiliwa kufanya mikutano mahali pake."
MWENYEKITI KILIMANI AMCOS AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA WIZI WA SHILINGI MILIONI TATU
Na Amiri Kilagalila Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Njombe imemfikisha katika mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Njombe Bw. Ernest Shauritana Manga mwenyekiti wa chama cha ushirika cha Kilimani AMCOS kilichopo katika halmashauri ya mji wa Makambako kwa kukabiliwa na kosa la wizi wa sh.milioni tatu (3) ambayo ni mali ya chama hicho. Akizungumza na waandishi wa habari habari mapema hii leo ofisini kwake,kaimu kamanda mkuu wa Takukuru mkoa wa Njombe Charles Mulebya amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu 270 cha…
Picha : RAFIKI SDO YAKABIDHI VITENDEA KAZI VYA MILIONI 19.4 KWA WAWEZESHAJI WA VIKUNDI SHINYANGA
Shirika la RAFIKI SDO ‘Rafiki Social Development Organization’ limekabidhi vitendea kazi ikiwemo baiskeli 76 na mabegi 76 vyenye thamani ya shilingi milioni 19.4 kwa wasichana na wanawake ‘Wawezeshaji wa vikundi’ kwenye wilaya ya Shinyanga ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao vizuri katika mitaa na vijiji wanavyohudumia.
Hafla fupi ya makabidhiano ya vitendea kazi hivyo imefanyika leo Jumatano,Januari 23,2019 katika ofisi ya RAFIKI SDO mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
Awali akizungumza, Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a alisema vitendea kazi hivyo vitatumika kwenye kata ambako shirika lao linatekeleza shughuli za miradi ya maendeleo na kuongeza kuwa baiskeli hizo zinakamilisha idadi ya baiskeli 148 kwani tayair walishatoa zingine 72.
“Wawezeshaji hawa 76 tuliwapa elimu,sasa wanakwenda kuunda vikundi vya wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 kwa ajili ya kuwafundisha masuala ya ujasiriamali,malezi,mabadiliko ya tabia na masuala mtambuka,watatumia vitendea kazi hivi kuwafikia wananchi kwenye maeneo yao kwenye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga”,alisema Ng’ong’a.
“Shirika letu limeajiri wawezeshaji wa vikundi 131 kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2016 hadi 2019,kati ya 72 ni wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na 59 halmashauri ya Shinyanga,tunawapatia mishahara kila mwezi,wanalipiwa NSSF na wameunganishwa na mfuko wa huduma za afya”,aliongeza Ng’ong’a.
Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko alilipongeza shirika la RAFIKI SDO kwa kushirikiana na serikali katika shughuli za maendeleo huku akibainisha kuwa shirika hilo linatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kuwezesha wananchi kiuchumi.
Mboneko aliwataka Wawezeshaji hao kutumia vyema vitendea kazi walivyopatiwa ,kuomba mikopo kwenye halmashauri na kuhakikisha wanatumia mikopo hiyo kwa shughuli za maendeleo.
Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo pia kuwahimiza wanawake kutoa taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto huku akiwashauri kutumia mikusanyiko ya watu kutangaza na kuuza bidhaa wanazotengeneza.
Aidha aliwaagiza maendeleo ya jamii kutembelea vikundi vilivyoanzishwa na kuvishauri huku akizitaka halmashauri kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyo mstari wa mbele kwenye masuala ya maendeleo.
Nao wawezeshaji hao walilishukuru shirika hilo kuwa karibu nao na kueleza kuwa hivi sasa wameweza kuanzisha biashara ndogo ndogo kwa ajili ya kujiinua kiuchumi lakini pia tabia hatarishi zimepungua na wanaendelea kupaza sauti juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Muonekano wa baiskeli zilizotolewa na Shirika la RAFIKI SDO kwa Wawezeshaji wa vikundi katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi begi na baiskeli Anna Kulwa kutoka kijiji cha Kizungu kata ya Lyamidati halmashauri ya wilaya ya Shinyanga . Wa kwanza kushoto ni Afisa Maendeleo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Mhoja na Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, Jackson Njau, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a wakishuhudia zoezi la makabidhiano ya vitendea kazi.
Anna Kulwa akishikana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a.
Muonekano wa mabegi yakiwa kwenye baiskeli.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikabidhi vitendea kazi kwa Rahim Ibrahim kutoka kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Baiskeli na mabegi yaliyotolewa na RAFIKI SDO kwa wawezeshaji wa vikundi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vitendea kazi vilivyotolewa na shirika la RAFIKI SDO kwa Wawezeshaji wa vikundi katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga, Charles Maugira.
Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a akizungumza wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi kwa wawezeshaji wa vikundi.
Kulia ni Msaidizi wa Meneja shirika la RAFIKI SDO, Neema Lweeka akielezea kuhusu shirika hilo na shughuli za maendeleo wanazotekeleza hususani miradi ya afya,elimu,uwezeshaji kiuchumi,ulinzi wa mtoto,haki na utawala na utoaji elimu ya stadi za maisha.
Wawezeshaji wa vikundi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akifurahia jambo na Wawezeshaji wa vikundi waliopatiwa vitendea kazi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiagana na wawezeshaji wa vikundi.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
WATU WASIOJULIKANA WAENDELEA KUTIKISA KAGERA KWA MAUAJI
Na Mwandishi wetu-Kagera, Watu watatu mkoani Kagera wameuawa katika matukio tofauti ikiwemo kuchomwa moto na mmoja kuondolewa sehemu zake za siri huku AK.47 ikitumika katika mauaji hayo. Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Revocatus Malimi,amethibitisha kutokea kwa matukio hayo wakati akiongea na waandishi wa habari jana ofisini kwake. Kamanda Malimi,alisema tukio la kwanza lilitokea January 19 mwaka huu huko maeneo ya Kitongoji cha Nyakanyasi Tarafa ya Kaisho Wilayani Kyerwa mkoani humo. Alimtaja marehemu aliyeuawa kwa jina la Peter Ezekiel ( 27 ) mkazi wa Kitongoji hicho mkulima alikutwa ameuawa katika…
VIONGOZI WA DINI WAKEMEA MICHEZO YA KUBAHATISHA, ONGEZEKO LA BAA, MBELE YA RAIS MAGUFULI
Na Bakari Chijumba. Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohora Tanzania, Zainuddin Adamjee ameshangazwa na tabia ya vyombo vya habari hapa nchini na viongozi hapa nchini kuunga mkono michezo ya kubahatisha licha ya kuwa ni haramu katika dini zote. Adamjee akizungumza leo 23 January 2019, katika kikao kati ya Rais John Magufuli na viongozi wa madhehebu ya dini Ikulu jijini Dar es Salaam, amesema hivi sasa vijana wengi nchini ambao ni nguvu kazi ya Taifa wanacheza kamari kila dakika kwa sababu kila ukifungua televisheni ni matangazo ya michezo hiyo. “Mambo mengi…
VIUNGO SITA VYA BINADAMU VISIVYO NA TIJA
Mabadiliko yamejiri baada ya kipindi cha muda mrefu lakini pia ni mchakato wa polepole.
Tabia nyingine zinazidi kusalia katika vizazi vingi hata baada ya kukosa madhumuni.
Vipengele hivi vya uvumbuzi, au sifa za kimwili, hupatikana katika wanadamu pia.
"Mwili wako kimsingi ni makumbusho ya historia ya asili," anasema mwanahistoria wa binadamu Dorsa Amir katika chapisho lake la mtandao wa Twitter.
Kwa nini sifa hizi zinaendelea kusalia hata ingawa zinaonekana kupoteza umuhimu wao? Kwa sababu mabadiliko ni mchakato wa taratibu.
WATU WANNE WANASWA WAKIPANGA SHAMBULIZI DHIDI YA WAISLAMU
Brian Colaneri na Andrew Crysel (kushoto kwenda kulia) pamoja na mvulana wa miaka 16 wanashitakiwa kwa kupanga shambulizi la mabomu dhidi ya Waislamu.
Watu wanne wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa tuhuma za kupanga shambulio dhidi ya jumuiya ndogo ya waislamu katika jimbo la New York.
Watu hao wanatuhumiwa kukutwa na mabomu ya kungeneza nyumbani na silaha za moto, na kupanga kushambulia jumuiya ya Islamberg iliyoanzishwa na kiongozi wa dini kutoka Pakistani kwenye miaka ya 80.
Njama hizo zilibainika baada ya polisi kupashwa habari na mwanafunzi.
Watuhumiwa watatu Andrew Crysel, 18, Vincent Vetromile, 19 na Brian Colaneri, 20, wanatarajiwa kupandishwa mahakamani leo Jumatano.
Kwa mujibu wa polisi, watatu kati ya watuhumiwa hao walikuwa pamoja katika mafunzo ya uskauti.
Wapelelezi wanasema watuhumiwa hao ambao walikuwa wakiishi katika jiji la Greece, kaskazini-magharibi mwa jimbo la New York walikuwa wametengeneza mabomu matatu na walikuwa na silaha 23 walizozificha katika sehemu tofauti.
Chanzo:Bbc
DAWASA YAMTUA NDOO YA MAJI MAMA MARIA NYERERE
Mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Makongoro Nyerere akitoa shukrani zake mbele ya wageni waliohudhuria hafla ya kukabidhi tenki la maji nyumbani kwa Hayati Mwalimu Nyerere lililokarabatiwa na DAWASA hivi karibuni.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DAWASA Neli Msuya akitoa ufafanuzi wa mradi huo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Cyprian Luhemeja akitoa maelezo juu ya mradi huo mbele ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (wa pili toka kushoto) na Mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Makongoro Nyerere pamoja wageni waliohudhuria hafla ya kukabidhi tenki la maji nyumbani kwa Hayati Mwalimu Nyerere lililokarabatiwa na DAWASA hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (Katikati), akizungumza mbele ya wanahabari juu ya mradi wa ukarabati wa tenki la maji alilokabidhiwa Mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Makongoro Nyerere (kushoto). Pembeni ni Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Cyprian Luhemeja (kwanza kulia).
Wafanyakazi wa DAWASA, Wanahabari na wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini.
Mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Makongoro Nyerere (kulia) akiwakaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Cyprian Luhemeja (kwanza kulia) pamoja na wageni wengine waliokuwa wameambatana nao kukabidhi mradi wa tenki la maji lililokarabatiwa na DAWASA. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Kaimu Mkurugenzi wa miradi DAWASA Lydia Ndibalema akitoa maelezo machache kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (wa pili toka kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Cyprian Luhemeja (kwanza kushoto) na Mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Makongoro Nyerere pamoja wageni waliohudhuria hafla ya kukabidhi tenki la maji nyumbani kwa Hayati Mwalimu Nyerere lililokarabatiwa na DAWASA hivi karibuni.
Kaimu Mkurugenzi wa miradi DAWASA Lydia Ndibalema akitoa maelezo machache kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (wa pili toka kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Cyprian Luhemeja (kwanza kushoto) na Mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Makongoro Nyerere pamoja wageni waliohudhuria hafla ya kukabidhi tenki la maji nyumbani kwa Hayati Mwalimu Nyerere lililokarabatiwa na DAWASA hivi karibuni.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Cyprian Luhemeja akitoa maelezo machache kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange na wageni waalikwa
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) mapema leo amekabidhi tenki la maji lenye ujazo wa lita 170,000 kwa mke wa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mama Maria Nyerere.
Tenki ambalo lilikuwa halitumiki na sasa litatumika na litawawezesha kupata maji nyumbani kwa Hayati Mwalimu Nyerere, Msasani jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumaliza kukabidhi tenki hilo Msasani, jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange amesema wameamua kukarabati tenki hilo lilokuwa halitumiki kwa muda mrefu kutokana na miundombinu ya tenki kuwa chakavu nakupelekea kuwa na ukosefu wa maji ya kutosha nyumbani kwa Mama Nyerere.
Amesema maji ni kila kitu katika maisha ya binadamu hivyo hatuna budi kuyalinda na kuyatunza ili yaweze kututunza pia.
Nae Mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Makongoro Nyerere ameishukuru DAWASA kuweza kulikarabati tenki hilo lililokuwa limekufa na halitumiki kwa muda mrefu.
"Kiukweli sina cha kusema zaidi ya kutoa shukrani zangu za pekee kwenu kwa niaba ya mama yangu, hili tenki lilikuwa halitumiki kwa muda mrefu ila nyie mmelifufua na sasa tunapata maji ya kutosha," amesema Makongoro Nyerere.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema wao walijitoa kukarabati tenki hilo kwa kuondoa laini ndogo ya inchi moja ilikuwa inasababisha kutumia mota kuvuta maji ilikuwezesha kupata maji yakutosha hivyo kupelekea bili ya maji kuwa kubwa pamoja gharama za umeme.
RAIS MAGUFULI AAMBIWA ANATISHA, SIYO RAHISI MTU KUROPOKA MBELE YAKE
Mwenyekiti wa Wanawake wa Wakiislam Mkoa wa Dar es Salaam, Pili Abdallah amewaomba mawaziri kuwa na mazoea ya kukutana na viongozi wa dini ili kuwa na uhuru wa kuwaeleza masuala mengi ya kitaifa.
Wito huo ameutoa leo Jumatano Januari 23, 2019 kwenye mkutano maalumu na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kati yao na Rais Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Pili amesema kuna masuala ambayo hayafai kuzungumza moja kwa moja na Rais, hivyo itakuwa rahisi kuyazungumza wakikutana na mawaziri.
”Rais naomba mawaziri nao waonane na viongozi wa dini kwa wakati wao kama ulivyokutana hivi, mawaziri wakiita vikao kama hivi tutaweza kusema mengi kwa sababu baba (Rais Magufuli) unatisha, siyo rahisi mtu kuropokaropoka, tunaweza tukawa na mengi lakini tukayafichaficha,” amesema mama huyo na kuongeza:
“Hata mimi nina mengi lakini kama ningempata waziri husika, tuko naye tungeweza kuongea mengi na ungefikishiwa mengi ya kutupeleka mbele.”
Na Emmanuel Mtengwa, Mwananchi
MGAMBO WADAKWA WAKIOMBA RUSHWA YA MAGUNIA YA MKAA
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Katavi, inawashikilia askari mgambo wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani hapa, kwa tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa ya magunia matatu ya mkaa pamoja na Sh 20,000.
Wawili hao wanadaiwa kupokea rushwa hiyo kutoka kwa wananachi ili waweze kusafirisha mkaa bila kuwa na leseni wala kibali cha mamlaka husika.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi, Christopher Nakuwa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Lazaro Kambaulaya na Charles Kisauko.
Nakuwa alikuwa akitoa taarifa ya utekelezaji ya majukumu ya Takukuru mbele ya waandishi wa habari jana mjini hapa kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2018.
Katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba mwaka jana Takukuru iliendelea kutekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rukwa namba 11 ya mwaka 2007.
Kipindi hicho taasisis hiyo imepokea malalamiko 18 ya vitendo vya rushwa na kufungua majalada matano ikiwemo ya migogoro ya viwanja.
Peti Siyame - Habarileo Mpanda
TPDC YAFUNGUA MILANGO YA USHIRIKIANO NA ZPDC
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba (kushoto) akipokea zawadi ya mlango kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Zanzibar (ZPDC) ikiwa ni ishara ya kufungua milango ya ushirikiano baina ya TPDC na ZPDC.
Viongozi mbalimbali wa TPDC na ZPDC wakifuatilia kwa makini maelezo yanayotolewa na Juvent Ndege (pipeline shift supervisor) katika kituo cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam.
**
Hivi karibuni Shirika la Maendeleo ya Petroli Zanzibar (ZPDC) lilifanya ziara yake ya kwanza kutembelea Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kufanya mazungumzo yenye lengo la kufungua milango ya ushirikiano baina ya mashirika haya ya mafuta na gesi hapa nchini. Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ZPDC Bi. Mwanamkaa Abdulrahman Mohamed.
Katika historia fupi ya ZPDC iliyosomwa na Bi Mwanamkaa Mohamed, alisema na kusisitiza kuwa ZPDC bado ni changa na hivyo basi kupitia ushirikiano huo wanahitaji kujifunza mengi na kufanya kazi kwa bidii ili kufikia viwango ikiwa bado wapo kwenye maboresho ya mfumo wa shirika.
“Tumesema tuje na kitu cha kuonyesha alama ya kufungua milango ya ushirikiano” alisema Bi Mwanamkaa huku akikabidhi alama ya mlango ikiwa ni ishara ya kufungua milango ya ushirikiano.
Naye Meneja mipango wa TPDC Lwaga Kibona aliungana na viongozi hao wa Zanzibar pamoja na wataalamu wa miradi ya gesi katika kutembelea miradi mbalimbali ya TPDC ikiwemo inayosambaza gesi asilia kwa matumizi ya viwandani, majumbani pamoja na kituo cha kujaza gesi kwenye magari (CNG) cha Ubungo na kituo cha kupokea gesi asilia Kinyerezi.
Katika kituo cha kupokelea gesi cha Kinyerezi, Mhandisi Baltazari Thomas ambaye ni Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni tanzu ya TPDC ijulikanayo kama GASCO alifafanua mambo mbalimbali yanayohusiana na gesi asilia ikiwemo upatikanaji wake na jinsi inavyopokelewa na kusambazwa kwa wateja mbalimbali ikiwemo Tanesco kwa ajili ya kuzalisha umeme. Baada ya kupokea maelezo hayo waliungana na wataalamu wengine kutembelea eneo hili kujionea namna kazi zinavyofanyika.
Ujumbe kutoka Zanzibar ulionekana kuwa na maswali mengi yote yakiwa na lengo la kuwaongezea uelewa katika sekta hii ya mafuta na gesi pamoja na usimamizi wake.
Kupitia wataalam wabobezi wa TPDC wageni hawa walipata fursa ya kujifunza na kujiongezea uelewa ambapo mwishoni kabisa walilishukuru shirika kwa maelezo ambayo wameyatoa na kuweka ahadi ya kwenda kuwajibika katika njia hizo hizo na zaidi ili kuleta manufaa kwa nchi.
--
WAKAZI DODOMA WAISHUKURU TBA KWA KUWAPA VIBARUA UJENZI MJI WA KISERIKALI
Shughuli za ujenzi wa Wizara ya Ofisi ya Rais ,Utumishi na Utawala Bora inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika mji wa Kiserikali uliopo Mtumba Jijini Dodoma.
Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dodoma Herman Tanguye akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Wizara ya Ofisi ya Rais ,Utumishi na Utawala Bora inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika mji wa Kiserikali uliopo Mtumba Jijini Dodoma.
Bi.Suzana Michael anayefanya kibarua katika ujenzi wa Wizara ya Ofisi ya Rais ,Utumishi na Utawala Bora inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) akitoa pongezi kwa majiri wake ambaye ni TBA katika mji wa Kiserikali uliopo Mtumba Jijini Dodoma.
Bw.Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ujenzi kutoka Wakala wa Majengo (TBA) Humprey Killo akitoa tathimini ya ujenzi wa Wizara ya Ofisi ya Rais ,Utumishi na Utawala Bora inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika Mji wa Kiserikali uliopo Mtumba jijini Dodoma
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Wizara ya Ofisi ya Rais ,Utumishi na Utawala Bora inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)katika Mji wa Kiserikali uliopo Mtumba jijini Dodoma.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
Wakati ujenzi wa Wizara ishirini na tatu ukiendelea katika mji wa kiserikali uliopo katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma wakazi wa mji huo wamesema kuwa wameweza kunufaika kwa kupata vibarua na kujiongezea ujuzi kufuatia shughuli ya ujenzi inayoendelea.
wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya vibarua wanaofanya shughuli za ujenzi katika Wizara ya Ofisi ya Rais ,Utumishi na Utawala Bora inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wamesema kuwa wamenufaika kutokana na ujenzi huo kwani wanaweza kuendesha maisha yao na familia zao.
Akizungumza mmoja wa vibarua hao Suzana Michael amesema kuwa amekuwa akipata ushirikianao mkubwa kutoka kwa wafanyakazi wengine wakiwemo TBA jambo ambalo hapo awali hakulitarajia.
“Nawashukuru sana TBA kwa kuweza kutujali na kuona umuhimu wanawake kuweza kufanya kazi ya ujenzi jambo ambalo kwa wengine imekuwa ni kama ndoto”amesema Suzana.
Naye Maimuna Chilemile ambaye ni mkazi wa kata ya Ipagala amesema kuwa kupitia ujenzi huo ameweza kunufaika kwa kuweza kuwasomesha watoto wake huku akiwataka wanawake wengine kuchangamkia fursa zinazoendelea za ujenzi wa mji wa kiserikali.
kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dodoma Herman Tanguye amesema kuwa hadi sasa wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za ujenzi.
“Changamoto zilikuwepo lakini hazikutuzuia kuendelea na ujenzi hivyo tulipambana mpaka sasa kila kitu kinaenda vizuri,pia vifaa vyote vinavyohitajika kwaajili ya kukamilisha ujenzi vimeshapatikana.”amesema Tanguye,
Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ujenzi kutoka Wakala wa Majengo (TBA) Humprey Killo amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha ndani ya muda waliopewa wa kukamilisha majengo hayo ifikapo Januari 31 wawe wamekaamilisha.