Sunday, 20 January 2019

Waziri Jafo atoa siku 68 kwa halmashauri kurejesha fedha

Waziri  wa nchi,Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo ametoa siku 68 kwa halmashauri 4 za Kigoma Ujiji, Butiama, Liwale na Bahi kurejesha fedha za mradi wa elimu (Equip)zilizotumika kinyume na utaratibu.

Aidha ameelekeza mamlaka ya nidhamu kumchukulia hatua za kumuondoa kwenye nafasi yake afisa mipango wa halmashauri ya Bahi kutokana na kushindwa kutimiza wajibu wake.

Halmashauri hizo ni kati ya halmashauri 8 zilizotumia fedha  kinyume kiasi cha milioni 912.7 ambapo halmashauri 4 zilitekeleza agizo lake na kurejesha fedha.

"Halmashauri hizi wamenihuzunisha sana kwa kutotii maelekezo, naziagiza mpaka machi 28 mwaka huu wawe wamerejesha ili fedha hizo zitekeleze miradi iliyokusudiwa, "amesema Jafo

Mbali na hayo  amemuagiza  Naibu Waziri wake Mwita Waitara  kuwa mkali katika kusimamia miradi ya elimu agizo ambalo Waitara  ameahidi kulishughulikia.


from MPEKUZI http://bit.ly/2MjfYTD
via Malunde
Share:

Makonda Amwandikia WARAKA Mzito Tundu Lissu

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  ameandika waraka mzito akimponda Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu,  ambaye kwa sasa yupo ziarani barani Ulaya baada ya kupata nafuu kufuatia shambulizi la kupigwa risasi alilofanyiwa Septemba 7, 2017 nyumbani kwake Dodoma.
 
Makonda ameandika; ACHA NISEME NAWE KIDOGO KAKA YANGU TUNDU LISSU HASA NIKIANZA NA Shukran kwake muumba wa mbingu na ardhi kwa kumpa kaka yetu Tundu Lissu afya na siha njema.
 
Wengi walioko jimboni Singida na wa Tanzania wote walihangaika kwa sala na maombi, usiku na mchana, Wengine wakichanga pesa zao na Hatimaye Mola akajibu maombi yao.
 
Kwa heshima na kuonyesha uzalendo, nakushauri Kaka yangu Tundu Lissu rudi nyumbani utoe shukrani zako kwao. Watu wako wamekumiss zaidi ya hao unaowakimbilia hivi sasa.
 
Ziara yako huko haina tija kwa yoyote, na kuichafua Serikali si kumchafua Mh. Rais ni kuichafua TANZANIA yetu sote na wewe ukiwemo. Jimboni kwako haujakuwepo muda mrefu, ni vizuri kwa kuwa Mungu kakujaalia afya basi ukaitumia kuwasikiliza na kuwasaidia watu wa jimboni kwako ambao ni Watanzania.
 
Huko uliko wanamatatizo yao na hawajawahi kuja TANZANIA kutueleza matatizo yao. Zaidi wanakuona kama kituko japokua hawawezi kukuambia.
 
Ikiwa ni lazima sana kuisema Tanzania dhidi ya kile unachokiita ubaya, na ni lazima useme kwa hao waliowatesa na kuwauwa Babu zetu basi Naomba usiache kuwaambia na haya; Shirika letu ya ATCL sasa limefufuka, sasa tuna ndege mpya sita (6), na ndege mbili (2) zikiwa njiani.
 
Ikiwa Lazima sana uwaambie pia ya kwamba ile mikataba mibovu iliyokuwa inapelekea shirika la Tanesco kufa na kufikia hata umeme kukatika katika, gharama kubwa na usiotabirika, sasa Rais Magufuli anajenga “Stiegler’s Gorge” yenye uwezo wa kuzalisha Megawatts zaidi 2,100 kwa wakati mmoja.
 
Ikiwa Lazima sana useme, basi waeleze kwamba mafisadi mwisho wao ulishafika, tulikuwa hatuna mahakama ya mafisadi, sasa tuna mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi. Mafisadi na wahujumu uchumi sasa wanafikishwa mahakamani.
 
Ikiwa ni lazima sana waeleze, naomba usisite pia kuwaambia Watoto wa masikini na wanyonge sasa wanasoma bure kuanzia darasa la kwanza mpaka Kidato cha nne.
 
Ndugu yangu na kaka yangu mpendwa Tundu Lissu, kama Lazima sana ukae na hao wazungu uwaeleze, Naomba uwaambie pia ya kwamba sasa miundo mbinu na barabara zinajengwa kila kona ya nchi ya Tanzania, hata utakaporudi Tanzania utapita kwa Flyover ya Mfugale.
 
Ikiwa ni Lazima sana waambie, basi usiache pia kuwaambia ya kwamba mashirika ya umma pamoja na mikataba iliyokuwa imeingiwa ya makampuni,  sasa hivi serikali inapata dividend.
 
Ikiwa ni Lazima sana waambie, wale Wanyama Tembo na Twiga waliokuwa wakisafirishwa na kuuwawa sasa hawasafirishwi tena kwenye ndege, wala hawauwawi na wapo salama hivyo waje kutembelea Tanzania tunahitaji watalii.
 
Ikiwa ni Lazima sana waambie basi Tanzanite inapatikana Tanzania tu, tena Arusha pale na duniani kote ni kwetu tu Tanzania. Tumejenga ukuta sasa kuhakikisha Tanzanite inalindwa na sasa thamani ya Tanzanite inaonekana kwenye mchango wa pato la Taifa.
 
Ndugu yangu na kaka yangu Mpendwa, Kama ni lazima sana waambie, yale madini waliyokuwa wanayasafirisha kwenye makontena na kutuambia ni mchanga tu, sasa yanabaki ndani ya nchi yetu na tayari taifa limeanza kunufaika. Na wale wajanja wanaosafirisha kwa kutorosha wanakamatwa, juzi tu hapa wamepelekwa mahakamani.
 
Ndugu yangu Tundu Lissu, Kama ni lazima saana waambie, waambie basi miradi ya maji kutoka ziwa Victoria, Miradi ya maji Dar es salaam, Miradi ya maji Mbeya, sasa hivi maji yanapatikana na kadri siku zinavyokwenda Raisi anazidi kutenga fedha kuhakikisha wananchi wanapata maji.
 
Kama ni lazima sana uwaambie, waambie basi migogoro ya wafugaji na wakulima imepungua sana na hawachinjani tena watanzania, wanakaa mezani wanayamaliza.
 
Lakini kama ni lazima sana uwaambie, waambie basi kwamba Raisi Magufuli anapanua tena bandari ya Dar es salaam kuhakikisha kwamba zile meli kubwa zenye mizigo mikubwa au mizigo mingi zinakuja kwenye bandari ya Dar es salaam.
 
Kama ni Lazima sana uwaambie, basi naomba uendelee kuwaambia ya kwamba Tanzania mpya inakuja, Tanzania mpya inajengwa, na Tanzania mpya ni ya watanzania wote.
 
Ndugu yangu Tundu Lissu, nakukaribisha tena, unaporejea tena katika taifa letu, taifa hili la Tanzania utakuta tayari terminal 3 Airport imeishaanza kufanya kazi na usisahau kupiga selfie maana nyumbani kumenoga.
 
Kama ni lazima sana uwaambie, waambie tangu mwaka 1909 ilipokuwa inajengwa reli ya kati kwa ajili ya kusafirisha mpira kutoka congo kuleta bandari ya Dar es salaam na wajerumani, sasa awamu hii raisi Magufuli anajenga reli ya Standard Gauge tena kwa fedha zetu za ndani.
 
Kama ni lazima sana uwaambie, waambie wafanyakazi sasa wanafurahia mifuko ya hifadhi na mafao yao. Misharaha ya wafanyakazi haicheleweshwi tena.
 
Kama ni Lazima sana uwaambie, waambie Viwanja vya ndege vinajengwa na Rada kulinda anga letu zinajengwa na usalama wa nchi unazidi kuhimarishwa
 
Usisahau tena kuwaambie bujeti ya Afya imeongezwa sana, Hospital na vituo vya afya vinajengwa, huduma za mama na mtoto pamoja na wazee zimeboreshwa, madawa yanapatikana sasa mahospitalini.
 
Wakati unakaribia kuwaaga na unataka kuwaambia la mwisho, basi waambie wamachinga wana vitambulisho vya kuwafanya wafanye kazi bila kubugudhiwa wala kusumbuliwa na yeyote. Waambie pia wamachinga wana pia bima za afya.
 
Ndugu yangu Tundu Lissu, kama ni lazima sana ukae na hao wazungu uwaeleze, waeleze basi habari za bomba la mafuta linajengwa kutoka Uganda kuelekea Kwetu Tanga kuimarisha uchumi wetu kwa ujumla.
 
Kama ni Lazima sana uwaambie, waambie serikali ya Tanzania ni ya Viwanda, viwanda vinajengwa na watanzania wana pata Ajira .
 
Kama ni lazima sana uwaambie, basi waambie kwamba sasa hivi Tanzania mfumuko wa bei umeshuka ( inflation).
 
Kama ni lazima sana uwaambie, waambie basi ndugu yangu, usisite basi na unapokuwa unataka kusema hayo unayotaka kuyasema naomba na mimi nikuongezee mengine ya kwangu na ya watanzania tulioko huku tunaojua kinachoendelea. Kama lazima sana useme waambie Interest rate imeshushwa na watanzania wanaendelea kukopa.
 
Kama ni lazima sana uwaambie, waambie hakuna njaa tena Tanzania, chakula kipo cha kutosha mpaka tunawauzia umoja wa mataifa wakasaidie makambi ya wakimbizi. Watu wanalima na wanavuna.
 
Kama ni lazima sana uwaambie, waambie pia Tanzania ni miongoni mwa nchi tano (5) za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi.
 
Kama ni lazima sana uwaambie, waambie waje wawekeze Tanzania, hakuna tena Rushwa, hakuna tena “ten percent” mambo yamenyooka.
 
Namalizia kwakushangaa leo watu waliochukua madini yetu, waliotutawala na kuwafanya watu weusi kuwa watumwa leo unawaomba wakuunge mkono ili uwe Rais, utakuwa Rais wetu au wa watu weupe, tutakua tumekuchangua sisi au umechaguliwa na wazungu. Hivi unapitishwa na wazungu kugombea Uraisi au na wanachama wa chama chako? Ni vikao vingapi vya chama haujahudhuria?
 
Mbaya Zaidi unajua mwenyekiti wa chama ambaye kimsingi ndiye aliyekupigania kutafuta fedha, kukaa na wewe Nairobi na kuja mpaka Ubeligiji umeamua kumwacha ateseke  na kutumia nafasi yako ya Urais ustaafu TLS kuwashawishi Mawakili wajitoe Ili aendelee kuteseka huku wewe ukitumia fursa hii kutafuta uraisi. Hauangaiki wala hata haufikirii kwamba ni wakati muafaka kurudi kuja kumpa moyo kama ambavyo alifanya yeye.
 
Kweli hayo ndio malipo unayompa Mbowe kwa kukuangaikia wewe upate matibabu bora. Tulitegemea wewe kama mwanasheria ungekuwa umerejea nchini na kumsaidia mbowe lakini uroho wa madaraka umekufanya kutumia matatizo yake kujiimarisha kisiasa na kutafuta uraisi.
 
Ni mimi Mdogo wako Paul Makonda.


from MPEKUZI http://bit.ly/2FLiwIV
via Malunde
Share:

MAHAKAMA YAMTANGAZA TSHISEKEDI MSHINDI WA UCHAGUZI WA RAIS DRC

Mahakama ya kikatiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumapili imemtangaza Felix Tshisekedi kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais na kutupilia mbali madai ya Fayulu kwamba uchaguzi huo ulikuwa na udanganyifu.

Uamuzi huo wa kuthibitisha kuwa Tshisekedi ndiye aliibuka mshindi wa kinyang'anyiro hicho cha urais unakuja baada ya mahakama kupinga kesi iliyowasilishwa na kiongozi wa muungano wa upinzani wa LAMUKA Martin Fayulu, licha ya kuwa na mashaka makubwa ya kuwepo udanganyifu wa kura.

Fayulu anadai kwamba Tshisekedi na Rais Joseph Kabila walifanya mpango wa kisiri siri baada ya matokeo ya awali kuonesha kwamba mgombea ambaye alikuwa akiungwa mkono na Kabila, Emmanuel Ramazani Shadary, ameshika nafasi ya tatu katika uchaguzi huo.

Uamuzi huo wa mahakama unamaanisha kuwa sasa Tshisekedi anaweza kuapishwa kuwa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ifikapo Jumanne wiki ijayo.

Fayulu ameitaka jumuiya ya kimataifa kupinga ushindi huo wa Tshisekedi kwa kutotambua mamlaka yake aliyoyataja yasiyoungwa mkono na Wacongo. Fayulu amejitangaza kuwa Rais halali wa Congo.

Vyombo kadhaa vya habari vya kimataifa siku ya Jumanne viliripoti kuwa data zilizovujishwa za uchaguzi wa Congo zilionesha kuwa Fayulu ndiye aliyeshinda na sio Tshisekedi.

Kanisa lenye ushawishi mkubwa nchini Congo la Kikatoliki pia limeunga mkono hoja ya Fayulu kuwa Tshisekedi hakushinda katika uchaguzi huo wa Desemba 30 na Umoja wa Afrika ulitaka matokeo kamili ya uchaguzi huo wa Rais kucheleweshwa.

Nchi za magharibi bado hazikumpongeza Tshisekedi
Nchi za magharibi bado hazikumtumia pongezi Tshisekedi, na Ufaransa imeeleza wasiwasi wake juu ya matokeo rasmi ya uchaguzi, ambayo yamempatia ushindi Tshisekedi kwa asilimia 38.57 ya kura zote zilopigwa na Fayulu kupata asilimia 34.8.

Gazeti la Financial Times na vyombo vengine vya habari vya kimataifa vimethibitisha kuona nyaraka zinazosema kuwa Fayulu ndiye mshindi wa uchaguzi huo.

"Iwapo mahakama itamtangaza Tshisekedi mshindi, hatari ya taifa hilo kutengwa ni kubwa kwa taifa mabalo lipo katikati ya bara la Afrika," Adeline Van Houtte wa kampuni ya utafiti wa kiuchumi ya Economist Intelligence Unit, ameandika katika ukurasa wa Twitter.

Kambi ya Fayulu iliusifu Umoja wa Afrika kwa kutoa ombi la kutaka matokea ya mwisho yaahirishwe, lakini kambi ya Tshisekedi ilisema ni ombi litakaloleta kashfa.

Mvutano huo umezua wasiwasi kwamba mgogoro wa kisiasa ulioanza mara baada ya Rais Joseph Kabila kukataa kuachia madaraka mwishoni mwa muhula anaoruhusiwa kikatiba kumalizika miaka miwili iliyopita unaweza kusababisha umwagaji damu mkubwa.

Taifa hilo kubwa barani Afrika na ambalo limekosa utulivu kwa muda mrefu, lilitumbukia katika vita vya kikanda 1996-97 na 1998-2003, na chaguzi mbili zilizopita, 2006 na 2011 zilighubikwa na mapigano ya umwagaji damu.

Umoja wa Afrika umechukua msimamao mkali miongoni mwa mashirika yote ya kimataifa kuhusu fujo zinazoweza kuzuka kufuatia uchaguzi nchini humo.

Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika-SADC, ambayo inajumuisha Angola na Afrika Kusini awali ilitoa wito wa kura kuhesabiwa tena pamoja na kuundwa kwa serikali ya umoja wa muungano.

Lakini taarifa yake ya baadaye, haikutaja madai hayo, badala yake iliwatolea wito wanasiasa wa Congo "kushughulikia malalamiko yoyote ya uchaguzi kulingana na Katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na sheria husika za uchaguzi".

Credit:DW

Share:

LUKAKU MAMBO YOTE UNITED

Romelu Lukaku ana jukumu kubwa katika kikosi cha Manchester United, asema meneja wa muda wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer.

Lukaku ameanza mechi mara moja tangu Jose Mourinho afutwe kazi kama meneja wa klabu hiyo.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Everton aliyejiunga na Man Utd kwa kima cha pauni milioni 75 amecheza mechi sita za ligi kuu ya England chini ya uongozi wa Solskjaer.

Solskjaer amesifia umahiri wa Rashford, Jesse Lingard na Anthony Martial.

Lakini raia huyo raia huyo wa Norway amesema Lukaku, 25, anasalia kuwa kiungo mhimu wa kikosi chake.

Rashford na Paul Pogba ambao wamefunga zaidi ya mabao matatu yaliyotiwa kimyani na Lukaku tangu Mourinho alipotimuliwa Disemaba 18 mwaka jana.

Chanzo:Bbc
Share:

MWANAUME ALIYEMUUA MKEWE NA WAKILI WAKE NAYE AJIUA

Mwanamume aliyeshtakiwa kwa kumuua mke wake miaka kadhaa iliyopita nchini Uhispania sasa anadaiwa kumuua wakili wake na kisha naye kujiua.

Jose Javier Salvador Calvo, 50, aliruka kutoka kwenye daraja la mji wa mashariki wa Teruel polisi walipojaribu kumkamata.

Kisa hicho kimewagutusha watu nchini Uhispania na kuzua mjadala mkali kuhusu sheria ya mzozo wa kinyumbani nchini humo.

Akizungumzia vifo hivyo waziri mkuu wa Uhispania, Pedro Sánchez ameapa kuendeleza juhudi za kukabiliana na visa vya unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Ikumbukwe kwamba Jose Javier Salvador Calvo alimpiga risasi na kumuua mke wake, Patricia Maurel Conte, 29, mwezi Mei mwaka 2003 katika eneo la Aragon kaskazini mashariki mwa Uhispani.

Baada ya kuachilia chini ya sheria maalum mwaka 2017, muuaji huyo alijiingiza katika uhusiano wa kimapenzi na Rebeca Santamalia Cáncer, 47,wakili aliyemtetea mahakamani aliposhtakiwa kwa mauaji,kwa kujibu wa vyombo vya habari vya Uhispania.

Polisi ilimpata wakili huyoakiwa ameuawa kwa kudungwa kisu katika nyumba ya Salvador Calvo iliyopo eneo la Aragon siku ya ijumaa baada ya mume wake kupiga ripoti kuwa ametoweka.

Muda mfupi kabla ya saa sita usiku mwili wa mshukiwa aliyejirusha kutoka daraja la Teruel, mji uliyopo kilo mita 150 kutoka eneo la tukio, ulipatikana na polisi waliyokuwa kazini.

Mwakilishi wa mamlaka ya mtaa huo Carmen Sánchez amewaambia wanahabari kuwa wakili huyo alikua mhasiriwa wa "unyanyasaji wa kijinsia".
Chanzo : Bbc
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya January 20




from MPEKUZI http://bit.ly/2FDMv6u
via Malunde
Share:

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA LEO JANUARI 20,2019.

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 20, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:

Saturday, 19 January 2019

NewAudio : FID Q FT BARAKAH THE PRINCE-MAFANIKIO

Share:

SIMBA YAPEWA KICHAPO CHA MBWA KOKO...YASHINDILIWA 5 - 0, AS VITA NOMA SANA


Dakika 90 za mchezo kati ya Simba na AS Vita zimemalizika kwa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wkufungwa mabao 5-0 katika mchezo wa pili wa Hatua ya Makundi Afrika uliochezwa Uwanja wa Martrys.
Share:

AS VITA YAGONGESHA SIMBA 3 - 0 DAKIKA 45 ZA KWANZA

Dakika 45 za mwanzo mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika,Simba SC dhidi ya AS Vita ya Congo,Simba wanachapwa bao 3-0
Share:

Halmashauri 33 Zavuka Malengo Ya Ukusanyaji Wa Mapato

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Halmashauri 33  kati ya halmashauri 185 zimeweza kukusanya mapato ya ndani kwa kiwango cha asilimia 50 na zaidi ya makisio ya mwaka wa fedha 2018/19 huku  halmashauri 21 zikiwa zimefanya vibaya kwa kusanya chini ya asilimi 20 ya makisio yake kwa mwaka.



Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemeni Jafo alipokuwa  akitoa taarifa ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa robo ya pili ya mwaka.

Alisema katika Halmashauri 33 zilizokusanya asilimia 50 na zaidi zimo Halmashauri za  Majiji tatu zikiongozwa na Jiji la Dodoma, Manispaa ni mbili zikiongozwa na manispaa ya Iringa, Halmashauri za Miji nane zikizongozwa na Mji wa Geita na Halmashauri za Wilaya ni ishirini zikiongozwa na Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

“Uchambuzi unaonyesha kuwa Katika Majiji 6, Jiji la Dodoma linaongoza kwa kukusanya asilimia 59 ya makisio na Jiji la Tanga limekuwa la mwisho kwa kukusanya asilimia 33 ya makisio” alisema.

Aidha Manispaa ya Iringa imeongoza katika kundi la Manispaa kwa kukusanya asilimia 64 ya makisio ambapo Manispaa ya Lindi imekuwa ya mwisho katika kundi hili kwa kukusanya asilimia 20 ya makisio.

Jafo aliongeza kuwa kwa upande wa Halmashauri za Miji, Halmashauri ya Mji wa Geita imeongoza kwa kukusanya asilimia 84 ya makisio na Halmashauri ya Mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho katika kundi hili kwa kukusanya asilimia 9 tu ya makisio,

Alisema Katika kundi la Halmashauri za Wilaya, Halmashauri ya Wilaya ya Geita imeongoza kwa kukusanya asilimia 78 ya makisio ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 6 tu ya makisio.

Kwa kuzingatia wingi wa makusanyo ya mapato ya  Halmashauri Jafo alibainisha Halmashauri iliyoongoza kwa kuwa ni Jiji la Dodoma ambalo limekusanya Shilingi Bilioni 40.12 na halmashauri iliyokusanya kiasi kidogo cha fedha ni halmashauri ya Wilaya ya Momba ambayo imekusanya shilingi milioni 105.04.

Waziri Jafo pia alibainisha Mkoa ambao Halmashauri zake zimekusanya mapato kwa kuzingatia wingi wa mapato kuwa ni Mkoa wa Dar es salaam ambao kwa jumla halmashauri zake zimekusanya shilingi bilioni 77.4 na Mkoa wa Mwisho ni Katavi ambao halmashauri zake zimekusanya shilingi bilioni 2.4 tu.

Alisema katika Mkoa uliokusanya vizuri kwa kuzingatia asilimia ya makusanyo ni  Mkoa wa Geita Halmashauri zake zimekusanya asilimia 56.4 ya makisio ya mwaka ukifuatiwa kwa karibu na Mkoa wa Dodoma uliokusanya asilimia 55.9 ya makisio yake na Mkoa wa mwisho kwa kigezo hicho ni Mkoa wa Mtwara ambao umekusanya asilimia 15 ya makisio yake ya mwaka.

Wakati huo huo Waziri Jafo amewataka wakurugenzi wote ambao Halmashauri zao hazikufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato kwa kukusanya chini ya asilimia kumi ya makisio yake kwa kipindi cha nusu mwaka kujieleza na kujitathimini na kuhakikisha wanaongeza bidii katika suala la ukusanyaji wa mapato.

“Halmashauri 9 kati ya 10 zilizofanya vibaya katika mwaka wa fedha uliopita zimefanikiwa kufanya vizuri katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2018/19 kwa kukusanya zaidi ya asilimia 20 ya makisio yake” alisema .

Waziri Jafo pia aliwaagiza Wakurugenzi wote kuhakikisha takwimu zote za mapato katika mfumo wa LGRCIS zinafanyiwa usuluhisho na kutumwa katika mfumo wa IFMS(Epicor)  kwani taarifa zote za mapato na matumizi ya fedha zinatakiwa kutolewa kupitia mfumo huo.

Ulinganifu huu wa taarifa za mapato umelenga kuonesha jinsi kazi za ukusanyaji wa mapato ya ndani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa inavyoendelea kusimamiwa vyema na takwimu hizi zinazotolewa ni kwa mujibu wa taarifa zilizofanywiwa usuluhisho na kutumwa katika mfumo wa IFMS(Epicor).

Katika mwaka wa fedha 2018/19 Halmashaurti zilipangiwa kukusanya shilingi bilioni 735.6 kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani na hadi kufikia Disemba 31,2018 Halmashauri zimekusanya shilingi bilioni 300 sawa na asilimia 41 ya makisio.

Kwa kipindi cha kwa mwaka 2017/18 halmashauri zilipanga kukusanya shilingi bilioni 687.3 na hadi  kufikia Disemba,2017 halmashauri hizo zilikuwa zimekusanya sh bilioni 281.3 sawa na asilimia 41 ya makisio.

Takwimu hizi zinabainisha kuwa kuna ongezeko la Shilingi bilioni 18.7 kwa mwaka wa fedha 2018/19 ikilinganishwa na makusanyo kwa kipindi kama hiki kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Share:

Waziri Mkuu Kuwapokea Watalii 300 Kutoka China

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameahidi kupokea kundi la watalii wasiopungua 300 ambao wanatarajiwa kuwasili nchini Machi, mwaka huu.

Watalii hao ni kundi la kwanza miongoni mwa watalii 10,000 wanaotarajiwa kuwasili nchini katika mwaka 2019 chini ya mpango unaosimamiwa baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi ya Utalii Tanzania na kampuni ya TouchRoad International Holding Group ya China.

Ametoa ahadi hiyo leo (Jumamosi, Januari 19, 2019) alipokutana na Mwenyekiti wa Touchroad Group, Bw. Liehui He na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Jaji Thomas Mihayo ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo baada ya kuelezwa na Bw. He huyo kwamba kundi hilo la watalii likiwa Djibouti litapokelewa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo na likienda Zimbabwe, litapokelewa na Rais wa nchi hiyo.

“Tanzania imeamua kuweka mkakati wa kuongeza idadi ya watalii nchini kwa kuboresha miundombinu ya usafiri na kukuza utalii kupitia vivutio vya vyakula vya asili, mavazi ya asili, wanyama, fukwe za bahari na milima. Kwa hiyo, ujio wa kundi hili kubwa, unatoa fursa mpya ya kutangaza vivutio vya nchi yetu,” amesema.

“Nitoe wito kwa Watanzania wanaoishi maeneo ya jirani na vivutio vyetu, wachangamkie fursa ya ujio wa watalii hawa katika maeneo mbalimbali. Wakifika Dar es Salaam, wanaweza kwenda Kigoma kuona Ziwa Tanganyika, mbuga zilizoko Nyanda za Juu Kusini, Arusha au vivutio vya Zanzibar. Tujiandae, tuwe tayari kuwauzia bidhaa mbalimbali,” amesema.

Pia amesema amefurahishwa na wazo lao la kuifanya Dar es Salaam iwe kitovu cha utalii (tourist hub) kwa makundi ya watalii ambayo yatakuja Tanzania na baadaye kutoka Tanzania kwenda Lusaka, Harare, Johannesburg na Djibouti.

Mwenyekiti huyo ambaye aliwasili nchini juzi, ameambatana na ujumbe wa watu 31 ambao unajumuisha waandishi wa habari, wasanii, wanamuziki na watu mashuhuri.

Akiwa Beijing, China, wakati akishiriki mkutano wa Jukwaa la Biashara baina ya Tanzania na China lililofanyika Septemba mwaka jana, Waziri Mkuu alikutana na uongozi wa kampuni ya TouchRoad ambayo ilionesha nia ya kutangaza fursa za utalii zilizopo hapa nchini.

Ziara ya Bw. He ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano yaliyoingiwa kati ya kampuni ya TouchRoad na Bodi ya Utalii ya Tanzania, Novemba 2018.

Mapema, Bw. He alimweleza Waziri Mkuu nia ya kampuni hiyo kutekeleza makubaliano yao ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania katika soko la China ili kuvutia watalii wapatao 10,000 waitembelee Tanzania katika mwaka 2019.

“Tumepanga kuleta watalii 10,000 kwa mwaka huu wa 2019 na tumeweka lengo la kuongeza idadi hiyo kwa asilimia 20 kila mwaka kwa muda wa miaka mitano. Pia tuna lengo la kuitumia ndege ya ATCL ili ilete watalii moja kwa moja kutoka Shanghai, China,” alisema.

Akielezea ujio wa kundi la kwanza la watalii, Bw. He alisema kundi hilo litakaa Djibouti kwa siku moja, Tanzania siku nne (tatu za kulala) na Zimbabwe siku tatu (mbili za kulala) na kisha kurejea China.

Alisema wanapanga kila mwezi wawe na kundi kubwa la watalii ambao watakuwa wanafikia Tanzania na kupelekwa nchi nyingine kwa sababu Wachina wengi hupenda kufanya utalii kwa siku walau 10, lakini wapelekwe maeneo matatu au manne tofauti kuona vivutio vya aina nyingine badala ya kukaa sehemu moja kwa kipindi chote hicho.

“Watalii hawa wakija kwa siku tatu au nne, wana uhakika wa kutumia dola za Marekani zaidi 2,000, wakienda eneo jingine watatumia fedha pia, namna hiyo tuna uhakika wa kuongeza pato la Taifa, lakini pia tuna uhakika wa kutengeneza ajira kwa Watanzania,” alisema.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


from MPEKUZI http://bit.ly/2TZWENW
via Malunde
Share:

YANGA YATOBOLEWA SHINYANGA....STAND UNITED HAWANA MASIHARA

Yanga SC imepoteza mechi ya kwanza ya msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuchapwa bao 1-0 na wenyeji, Stand United Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Safari ya kucheza bila kufungwa kwa Yanga katika msimu imeishia katika mechi ya 20 na sasa wanabaki na pointi zao 53, ingawa wanaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 12 zaidi ya Azam FC wanaofuatia katika nafasi ya pili, wakati mabingwa watetezi, Simba SC wana pointi 33 za mechi 14.

Bao lililoizamisha Yanga SC limefungwa na Nahodha wa Stand United, Jacok Massawe dakika ya 88 akimtungua kwa kichwa kipa Klaus Kindoki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kufuatia krosi ya Mwinyi Elias kutoa upande wa kulia. 

Kama lawama kwa bao hilo, basi ni za mabeki wa Yanga, ambao leo wamechezeshwa wengi zaidi ili kuongeza imara wa safu ya ulinzi, lakini wakamruhusu Massawe kuchomoka katikati yao na kuiunganishia nyavuni krosi ya Mwinyi aliyepasiwa na Six Mwakasega.

Yanga SC ilicheza vizuri leo tangu mwanzo, lakini ilikuwa hovyo katika eneo moja, kwenye umaliziaji, kwani pamoja na kufika mara nyingi kwenye eneo la hatari la Stand walishindwa kufunga.

Na mabadiliko yaliyofanywa na mwalimu Mwinyi Zahera leo, akimtoa Haruna Moshi ‘Boban’ na Mrisho Ngassa na kuwaingiza Mkongo mwenzake, Heritier Makambo na Pius Buswita nayo hayakuwana tija pia.

Siku ya kufa nyani, miti yote huteleza, wachezaji wa Yanga walimlalamikia mara mbili refa kuwanyima penalti baada ya wachezaji wa Stand United kuonkana kuunawa mpira kwenye boksi.

Kikosi cha Stand United kilikuwa; Mohammed Makaka, Mhando Washa, Majaliwa Shaaban, Jisendi Maganda, Ahmed Tajuden, Majjid Kimbondile, Datius Peter/Mwinyi Elias dk51, Hafidh Mussa, Six Mwasekaga, William Kimanzi/Maurice Mahela dk77 na Jacob Massawe.

Yanga SC; Klasu Kindoki, Paul Godfrey, Gardiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondan, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Mrisho Ngassa/Pius Buswita dk64, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Amissi Tambwe, Haruna Moshi/Heritier Makambo dk46 na Ibrahim Ajibu.

Via Binzubeiry blog
Share:

Picha : TGNP MTANDAO YAENDESHA WARSHA KWA WAHARIRI KUHUSU BAJETI YA MRENGO WA KIJINSIA

TGNP Mtandao imeendesha warsha kwa Wahariri na baadhi ya waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchini kuhusu bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa ajili ya kuwaongezea uelewa na uwezo kuhariri na kuripoti masuala ya kijinsia.

Warsha hiyo ya siku moja imefanyika leo Jumamosi Januari 19,2019 katika ofisi za TGNP Mtandao zilizopo jijini Dar es salaam.

Akifungua warsha,Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi alisema mafunzo hayo yawawezesha wahariri na waandishi wa habari kuhamasisha uingizwaji wa masuala ya kijinsia katika mipango,miongozo na sera za serikali.

"Tumekutana hapa kwa ajili ya kukumbushana dhana kuu za jinsia na umuhimu wa kuzingatia masuala ya jinsia kwa maendeleo lakini pia kuweka mikakati ya namna ya kuongeza kasi ya kuripoti masuala ya kijinsia katika vyombo vya habari kwani tunaamini vyombo vya habari ni muhimu kwa maendeleo ya jamii",alisema Liundi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akizungumza wakati akifungua warsha ya wahariri kuhusu bajeti yenye mrengo wa kijinsia katika ukumbi wa ofisi za TGNP Mtandao jijini Dar es salaam. Picha zote na Kadama Malunde - na Frankius Cleophace Malunde1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akielezea kuhusu dhana nzima ua bajeti yenye mrengo wa kijinsia.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John akisoma mwongozo kwa washiriki wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.
Regina Mziwanda wa BBC Swahili akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
Warsha inaendelea..
Mhariri wa gazeti la Majira,Imma Mbuguni akichangia hoja ukumbini.
Afisa Habari Msaidizi wa TGNP, Jackson Malangalila akitoa mada kuhusu mawasilisho ya uchambuzi wa kijinsia wa bajeti kwa mwaka 2018/2019.
Afisa Habari Msaidizi wa TGNP, Jackson Malangalila akiendelea kutoa mada ukumbini.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Joyce Shebe kutoka Clouds Media akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Mwandishi wa Habari Frankius Cleophace kutoka mkoa wa Mara akichukua matukio muhimu wakati wa warsha hiyo.
Jane Mihanji kutoka gazeti la Uhuru akiwa ukumbini
Warsha inaendelea.
 Picha zote na Kadama Malunde - na Frankius Cleophace Malunde1 blog
Share:

WANAFUNZI WALIOFAULU KIDATO CHA KWANZA LAKINI HAWAJUI KUSOMA, KUANDIKA KUCHUNGUZWA

Halmashauri ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya inakusudia kufanya uchunguzi juu ya madai ya kuwapo kwa wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu licha ya kuwa hawajui kusoma wala kuandika.

Madai hayo yameibuliwa na diwani wa Rujewa, Mkude Msasi katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika leo katika ofisi za maji bonde la Rufiji wilayani humo.

Msasi amedai wapo wanafunzi wengi waliofaulu pasi kujua kusoma wala kuandika huku akieleza anao ushahidi wa wanafunzi hao.

"Mimi shuleni kwangu nina wanafunzi 536 lakini kuna wanafunzi zaidi ya mia na kitu hawajui kusoma wamechaguliwa wako pale," amesema Msasi.


Na Yonathan Kossam, mwananchi
Share:

KAMANDA WA POLISI ALIYETUMBULIWA NA WAZIRI LUGOLA AKAMATA PESA BANDIA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Ramadhani Ng’anzi akionesha waandishi wa habari jana noti za fedha bandia zilizokamatwa kwenye operesheni za kutokomeza uhalifu jijini Arusha. Picha na Filbert Rweyemamu 
***
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Ramadhan Ng’anzi, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ameonekana kuendelea na wadhifa wake na jana alizungumzia kukamatwa kwa watuhumiwa wanaojihusisha na utengenezaji wa noti bandia.

Januari 16, Lugola alitengua uteuzi wa makamanda wa polisi wa mikoa mitatu; Salum Hamduni (Ilala), Emmannuel Lukula (Temeke) na Ramadhan Ng’anzi (Arusha).

Lakini, jana Kamanda Ng’anzi alionekana akiendelea na kazi yake kama kawaida na alizungumzia ukamataji wa noti bandia mkoani Arusha.

Huku makamanda hao watatu wakiendelea na kazi licha ya uteuzi wao kutenguliwa, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amesema atafanya mabadiliko wakati wowote wa makamanda wa polisi wa mikoa ya Ilala, Temeke na Arusha.

Kwa mujibu wa Lugola, sababu za kutengua uteuzi wa makamanda wa Ilala na Temeke ni kushindwa kusimamia mianya ya rushwa na utoaji wa dhamana kwa watuhumiwa, huku Ng’anzi akidaiwa kumwadhibu askari aliyetoa orodha ya polisi wanaojihusisha na biashara haramu ya bangi na mirugi wakati wa ziara ya naibu waziri wa wizara hiyo, Hamad Masauni.

IGP Sirro jana alizungumza na Mwananchi kuhusu utekelezaji wa agizo hilo la Lugola. “Bado nalifanyia kazi agizo lake na wakati wowote nitafanya mabadiliko ya makamanda wa mikoa hiyo kama ilivyoagizwa.”

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha jana, Ng’anzi alisema polisi iliwakamata watuhumiwa sita kwa makosa mbalimbali, kati yao wanne ambao hakuwataja majina wanajihusisha na utengenezaji wa fedha bandia.

Alisema mtuhumiwa wa kwanza alikutwa na idadi ya noti bandia za Dola za Marekani 50 ambazo zingekuwa halali zingekuwa na thamani ya dola 500.

Alisema mtuhumiwa huyo alipohojiwa aliwapeleka polisi nyumbani kwake zilipokutwa fedha hizo na watuhumiwa wenzake wakakamatwa.

“Huyu mtuhumiwa wa kwanza aliwapeleka askari wetu nyumbani kwake eneo la Daraja Mbili ambako zilikutwa fedha bandia za mataifa mbalimbali, tunaendelea kuwahoji ili tung’oe mtandao mzima wa uhalifu huu,” alisema Ng’anzi

Alitaja noti hizo bandia kuwa ni dola za Marekani, fedha za Umoja wa Ulaya (Euro), Kenya, Malawi, Zambia, Rwanda, Afrika Kusini, Angola na Sudan.

Kati ya fedha hizo bandia zipo Dola za Marekani 120,000 na Euro 10,700.

Alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa mahojiano na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Ng’anzi alisema watuhumiwa wengine wawili, Kennedy Mbilinyi na Richard Loishiye wamekamatwa kwa kuiba gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 241 DKC na kujaribu kulivusha mpaka wa Namanga kuingia Kenya.

Alisema mmiliki wa gari hilo alikuwa akitafuta mnunuzi na siku ya tukio alikuwa ameliegesha kwenye maduka ya TFA wakati akifanya manunuzi na alipotoka nje hakulikuta.

Na  Bakari Kiango na Filbert Rweyemamu mwananchi
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger