Thursday, 17 January 2019

WAFANYAKAZI WA AIRTEL WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUINGILIA MFUMO WA MTANDAO

Wafanyakazi wawili wa kampuni ya simu ya Airtel na wengine tisa wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya kuingilia mifumo ya mawasiliano ya kampuni hiyo.
Akiwasomea mashtaka, Wakili wa Serikali, Ester Martin akisaidiana na Erick Shija, alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Kelvin Mhina kuwa kati ya Septemba 9 na Desemba 24 mwaka jana, jijini Dar es Salaam washtakiwa walikula njama ya kutenda kosa la wizi.

Katika shtaka la pili alidai siku na mahali hapo, washtakiwa hao huku wakijua kuwa ni kinyume cha sheria walijaribu kutenda kosa la wizi.

Katika shtaka la tatu, washtakiwa Laizer na Mwenda kwa makusudi na kinyume cha sheria walisababisha kuingilia mfumo wa mawasiliano wa kampuni ya Airtel bila ya kuwa na kibali.

Shtaka la nne alidai kuwa washtakiwa wote walitoa taarifa za mfumo wa mawasiliano wa kampuni hiyo kinyume cha sheria.

Waliofikishwa mahakamani ni Rodgers Laizer na Nancy Mwenda ambao ni wafanyakazi wa Airtel, Erick Fidelisi, Zephaniah Maduhu, Anthony Masaki, Lumuli Stanford, Ndeshiwonasiya Malle, Davis Waseda, Goodluck Nyakira, Michael Onyango na Sylvester Onyango.


Washtakiwa walikana kutenda makosa hayo na mshtakiwa Masaki, Stanford, Eased na Mwenda walipata dhamana na wengine wamepelekwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Kesi ime iatatajwa Januari 29, mwaka huu kwa kuwa upelelezi haujakamilika.

Chanzo:Mpekuzi
Share:

ALI KIBA AFIWA NA BABA YAKE MZEE SALEH KIBA

Hali ya simanzi na huzuni imegubika familia ya msanii wa bongo Fleva Ali Kiba baada ya babake kufariki dunia mapema leo.

Mzee Saleh Kiba alifariki katika hospitali ya Muhimbili ambapo alikuwa amelazwa.

Kulingana taarifa za  mdogo wa mwanamuziki huyo ambaye pia ni msanii Abdu Kiba alithibitisha habari hizo.

Msanii huyo amesema kuwa msiba unafanyika katika mtaa wa Kariakoo eneo la Muheza ambapo ndio nyumbani kwao.

Kulingana na afisa wa Uhisiano mwema katika hospitali ya Muhimbili Neema Mwangomo amesema kuwa Mzee Saleh alifikwa na mauti yake saa kumi na mbili alfajiri.

Aliongezea kuwa marehemu alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo tangu tarehe 27 mwezi Disemba.

Chanzo:Bbc
Share:

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO ALHAMISI 17.01.2019 HIGUAIN KUTUA DARAJANI

Chelsea wameamua kumsajili Gonzalo Higuain baada ya Juventus kukubali ofa yao. Mshambuliaji huyo raia wa Argentina alikuwa akichezea AC Milan kwa mkopo. (Telegraph)

Atletico Madrid wanakaribia kumsaini mshambuliaji wa Chelsea lvaro Morata, 26, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa euro milioni45. (Sky Sports)

Arsenal wako tayari kutumia sehemu ya mshahara wa Mesut Ozil endapo watafanikiwa kumuuza ili kumsajili mchezaji mwingine.

Ozil ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika klabu hiyo. (Mirror)

West Ham wanapania kumnunua mshambuliaji wa Celta Vigo na Uruguay Maxi Gomez, 22, kujaza pengo litakaloachwa na Marko Arnautovic. (Sky Sports)

Manchester City huenda wakapoteza nafasi ya kumsajili Frenkie De Jong kutoka Ajax baada ya Paris St-Germain kuonyesha azma ya kutaka kumununua kiungo huyo.

Chanzo:Bbc
Share:

RIPOTI YA HAKI ZA BINADAMU ZAIMULIKA SAUDIA NA CHINA

Saudia na China zamulikwa katika ripoti ya dunia ya haki za binadamu

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch limekosoa ukiukaji wa haki za binadamu nchini Saudi Arabia na China katika ripoti yake ya dunia ya mwaka 2019, yenye kurasa 400.

Ripoti hiyo pia inazikosoa nchi za Ulaya, lakini Mkurugenzi wa shirika hilo nchini Ujerumani Wenzel Michalski anasema licha ya yote hayo kuna sababu ya kuwa na matumaini kidogo.

Shirika la Human Rights Watch limekuwa likichapisha ripoti hiyo kila mwaka tangu mwaka 1989, mataifa yenye uongozi wa kidikteta ambayo haki za watoto, wanawake na wanaume zinakiukwa ndiyo yanayolengwa.

 Mwaka huu kama anavyosema Wenzel Michalski wanaharakati wa haki za binadamu hawajajikita tu katika baadhi ya nchi kwa ujumla bali kwa watu binafsi.

China inajaribu kuiuza sera yake ya ukiukaji wa haki za binadamu duniani

Chanzo:Dw
Share:

ZITTO KABWE AITAKA CHADEMA KUTOA TAARIFA ZA UGONJWA WA MBOWE

Share:

IDADI YA WALIOUAWA KENYA YAFIKIA 21,WENGINE 50 HAWAJULIKANI WALIPO

Inspekta Jenerali wa Kenya Joseph Boinnet

Idadi ya waliouawa katika shambulizi la kigaidi nchini Kenya imefikia 21, baada ya serikali ya Kenya kutangaza kuwa miili mingine 6 imepatikana kutoka katika kifusi kilicho kuwa katika eneo hilo.
Pia taarifa iliyotolewa inasema kuwa afisa polisi mmoja alifariki kutokana na majeraha wakati akipewa matibabu maalum.

Akizungumza na vyombo vya habari Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Kenya Joseph Boinnet ametoa taarifa hiyo Jumatano jioni.

Amefafanua kuwa kati ya waliouwawa kuna Wakenya 16, Muingereza moja, Mmarekani mmoja na wengine wa mataifa mbalimbali.

Hata hivyo IGP ametahadharisha vyombo vya habari kujiepusha kutoa ripoti ambazo zinaweza kuhatarisha uchunguzi ambao unaendelea baada ya shambulizi hilo.

Mapema Jumatano asubuhi Rais Uhuru Kenyatta amesema alisema kuwa watu wenye silaha waliovamia eneo la biashara la hoteli na kuuwa watu 14, “wameuwawa” baada ya takriban masaa ishirini ya mapambano ambapo mamia ya raia waliokolewa na wengine wanaokadiriwa kuwa 50 bado hawajulikani walipo.

Kikundi cha Al-Qaeda chenye mafungamano na kundi la Al-Shabaab kimedai kuhusika na shambulio hilo. Kikundi hicho kimekuwa kikilenga kuishambulia Kenya tangu ilipopeleka jeshi lake nchini Somalia Octoba 2011 kupambana na kikundi hicho cha wanajihadi.

Chanzo:Voa
Share:

FAINALI 7 ZA KIBABE ZILIZOAMULIWA NA RONALDO


Cristiano Ronaldo katika matukio mbalimbali.

Baada ya kufunga bao la ushindi jana katika fainali ya Kombe la Italia, mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronalado sasa amefunga mabao 8 katika fainali 7 zilizopita.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 33, jana usiku aliiwezesha timu yake kutwaa taji la Copa Italia kupitia bao lake alilofunga dakika ya 61 dhidi ya AC Milan huku Juventus ikifikisha makombe 8 ya Italia na kuwa ndio klabu iliyoshinda mara nyingi zaidi ikiipiku AC Milan yenye mataji 7.

Fainali ambazo Ronaldo amefunga mabao

Ronaldo alifunga mabao mawili kwenye fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya msimu wa 2016/17 Real Madrid ikishinda 4-0 dhidi ya Juventus.

Ronaldo pia alifunga bao 1 kwenye ushindi wa 2-1 iliopata Real Madrid dhidi ya Barcelona kwenye fainali ya 'Spanish Super Cup'.

Ronaldo pia amefunga jumla ya mabao 4 katika fainali mbili tofauti za Klabu bingwa ya Dunia. Alifunga mabao mawili dhidi ya Kashima Antlers mwaka 2016. Pia akafunga mabao mawili dhidi ya Gremio mwaka 2017.

Bao lake la jana limekuwa bao la nane katika fainali 7 zilizopita huku fainali zote timu alizokuwa akizichezea yaani Real Madrid na Juventus zimetwa ubingwa.
Share:

Maajabu : KUTANA NA MTU HUYU ANAMALIZA MARA 50 BILA KUFANYA TENDO LA NDOA


Msichana Amanda Gryce, mkazi wa Florida nchini Marekani, anasumbuliwa na ugonjwa ambao sio wa kawaida, unaomfanya afikie mshindo takriban mara 50 kwa siku, bila ya kufanya tendo la ndoa na mtu yeyote.

Msichana huyo mwenye miaka 22, anasema alianza kugundua ana tatizo hilo akiwa na miaka 6, na amekuwa akikabiliana nalo bila kujua hatma yake ni nini, na amekuwa akikutwa na hali hiyo muda wowote na mahali popote bila kufanya tendo la ndoa.

“Ilitakiwa iwe ni kitu kizuri kama ambavyo inatakiwa, imekuwa maumivu kwangu, kwa sababu inatokea sana, inaweza ikatokea hata mara 50 kwa siku au mara tano mpaka kumi kwa saa moja, inatokea nikiwa na rafiki zangu, au nikiwa sehemu tu na watu wengine, nikipanda gari ndio inazidi kutokana na mtikisiko wake, ni aibu sana”, amesema Amanda.

Tatizo hilo ambalo mwenyewe anadai limekuwa likimtesa maisha yake yote na kumfanya asifurahie maisha ya kimapenzi, kilimfanya awahi kuwaza kujiua, lakini mpenzi wake Stuart Triplett, amekuwa akimpa ushirikiano sana wa kutafuta tiba na kumfanya awe na tumaini.

Kutokana na hali hiyo, Amanda ameshakutana na baadhi ya madaktari kujaribu kupata tiba, lakini mpaka sasa hajapata ufumbuzi kutokana na ugonjwa huo kutokuwa na tiba ya moja kwa moja, hivyo kumpa njia mbadala za kukabliana nao, ikiwemo kufanya mazoezi.

Tatizo hilo kitaalamu linajulikana kama 'Persistent Genital Arousal Disorder'ambalo hutokea mara chache sana kwa binadamu. Mpaka sasa haujajulikana tiba sahihi ya kuweza kumaliza tatizo hilo, lakini madaktari wa masuala hayo wameshauri iwapo mtu atagundulika kuwa na tatizo hilo, atatakiwa kuhudhuruia tiba ya mwili 'Physiotherapy'.
Amanda akiwa na mpenzi wake Stuart Triplett
Share:

TUNDU LISSU : NIPO TAYARI KUGOMBEA URAIS...SINA MPAMBANO NA LOWASA

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu ameendelea kusimamia msimamo wake kuwa yupo tayari kugombea urais mwaka 2020 endapo chama chake kitaona anatosha kusimama katika nafasi hiyo.

Akihojiwa na Shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) Lissu amesema kauli hiyo haina maana yoyote kwamba anapambana na Edward Lowassa ambaye alisimamishwa na Chadema mwaka 2015 kuwania nafasi hiyo.

“Kama chama changu pamoja na vyama tunavyoshirikiana navyo na Watanzania wanaotuunga mkono watasema kwamba mimi nafaa kuwawakilisha nitakuwa tayari kufanya hivyo.

Alisema, “Sina mpambano na Lowassa uamuzi wa kugombea urais sio wangu wala Lowassa wala Mbowe ni vikao vya chama. Inaweza kwenye vikao viongozi nikaambiwa sitoshi nitakubali na inawezekana vikao vikamwambia Lowassa aniachie mimi nipambane kwa sababu mapambano ya sasa yanahitaji nguvu inawezekana kabisa”.

Kuhusu kwamba ni lini atarejea nchini alieleza, “Daktari wagu atakaposema sasa una uwezo wa kurudi kwenu nitarudi Tanzania.

Lissu alieleza kuwa licha ya kwamba hadi sasa Serikali imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwabaini waliomshambulia atarudi na itawajibika kumlinda kwa saa 24.


Na Elizabeth Edward,Mwananchi
Share:

RADI YAJERUHI WANAFUNZI 14 MULEBA

Wanafunzi 14 wa shule ya sekondari Rulongo wilayani Muleba Mkoa wa Kagera wamelazwa katika hospitali ya Lubya wilayani humo baada ya kujeruhiwa na radi.

Akizungumza jana Jumatano Januari 16, 2019 mganga mkuu wa hospitali hiyo, George Kasibante amesema tukio hilo limetokea leo na kwamba kati ya wanafunzi hao, watatu wana hali mbaya baada ya kuungua sehemu kubwa mwilini.

Amesema mwanafunzi mmoja amepoteza fahamu na madaktari wanajitahidi kuhakikisha anarejea katika hali yake ya kawaida, kwamba wengine walipata zaidi mshtuko.

Amesema radi hiyo ilipiga vyumba vya madarasa ya kidato cha pili na tatu, kwamba shule hiyo ipo mlimani eneo ambalo radi hupiga zaidi na kuwashauri wanafunzi kutojikinga na mvua katika maeneo yenye miti mirefu.


Na Shaaban Ndyamukama, Mwananchi
Share:

MWILI WAOKOTWA UKIWA UMEFUNGWA KWENYE KIROBA

Mwili wa mtu mmoja umeokotwa eneo la sayansi jirani na Chuo cha Ustawi wa jamii ukiwa umefungwa kwenye kiroba.

Kwa mujibu wa ITV, Mjumbe wa mtaa huo Bi Fortunata Mshindo amesema jana mchana yeye na wananchi wengine walipita katika eneo hilo na hakukua na kitu chochote huku pia akisisitizia uongozi wa manispaa kuweka taa katika eneo hilo ili kupunguza matukio ya kihalifu.


Maafisa wa Jeshi la Polisi walifika eneo la tukio wakauchukua mwili huo kwa uchunguzi zaidi


Chanzo ITV

Share:

MAWASILIANO YA BARABARA YA MOROGORO - DODOMA YAREJEA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, amewahakikishia wananchi na watumiaji wa barabara ya Morogoro-Dodoma kuwa mawasiliano ya barabara hiyo sehemu ya maingilio ya daraja la Dumila yamerudi kama ilivyokuwa awali.


Kauli hiyo ameitoa jana mkoani Morogoro, alipofika darajani hapo kujionea athari za mvua zilizosababisha kubomoka kwa daraja hilo na wananchi kushindwa kutumia barabara hiyo kwa takriban masaa saba.


“Kama mlivyoshuhudia tangu asubuhi tumeanza kazi za kurudisha mawasiliano katika barabara hii, matengenezo yamekamilika na wananchi tayari wameshaanza kutumia barabara”, alisema Naibu Waziri Kwandikwa.


Aidha, ameupaongeza Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Morogoro, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kampuni ya ujenzi ya Yapi Merkez na wadau wote waliojitokeza katika kuhakikisha wanashirikiana bega kwa bega ili kurudisha mawasiliano katika eneo hilo.


Aliongeza kuwa katika kuhakikisha mawasiliano ya barabara yanakuwa imara, Serikali ipo katika mpango wa kuboresha barabara hiyo ambapo kwa sasa wataalam wanafanya usanifu wa barabara hiyo na pindi usanifu huo utakapokamilika basi ujenzi wake utaanza mara moja na wataanza na sehemu korofi.


Awali akitoa taarifa kwa Naibu Waziri huyo, Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe, alisema kuwa uongozi wa mkoa ulifika eneo la tukio na kuanza kushirikiana na TANROADS mkoa kuhakikisha miundombinu hiyo inarejea mapema.


Aliwataka wananchi kujitolea kupanda matete na magugu maji katika eneo hilo ili kuelekeza maji yanayopita katika mto huo kuelekea sehemu husika.


Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dorothy Ntenga, alisema kuwa kazi zilizokuwa zikifanyika katika maingilio ya daraja hilo ilikuwa ni kuweka mawe makubwa na kokoto sehemu iliyobomoka.


Alifafanua kuwa kutokana na sehemu hiyo kuwa na maji mengi na mchanga mwingi, wamefikiria kufanya usanifu wa daraja hilo utakaoleta suluhisho la kudumu.

Share:

Tanzia : BABA MZAZI WA ALIKIBA AFARIKI DUNIA

Baba mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Alikiba Mzee Saleh amefariki dunia alfajiri ya leo Januari 17, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu..

Inaelezwa kuwa, Mzee Kiba ambaye pia ni baba mzazi wa msanii Abdu Kiba na Zabibu Kiba amekua akiugua kwa muda sasa huku akiendelea kutibiwa.
Share:

SERIKALI YAANIKA MAENEO VIPAUMBELE KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

Na. WAMJW-DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imebainisha maeneo muhimu yaliyowekewa kipaumbele katika bajeti ili kuboresha miundombinu na hali ya upatikanaji wa Huduma za afya nchini.

Akieleza taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya wizara kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia Julai hadi Desemba, 2018 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma, Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee Mh. Ummy Mwalimu amesema wizara hiyo iliidhinishiwa na Bunge kupokea na kutumia bajeti ya jumla ya shilingi bilioni 866.24 ambapo Kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni 304.44 ilikua ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambapo shilingi 88.47 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi 216.7 kwa ajili ya Mishahara ya watumishi walio makao makuu ya Wizara pamoja na Watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara.


Waziri Ummy amesema fedha zilizopokelewa katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2018 zimeainishwa katika utekelezaji wa majukumu ya wizara katika kipindi hicho ambapo maeneo muhimu kama Chanjo, afya ya mzazi na mtoto, mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba, upatikanaji wa damu salama, uimarishaji wa huduma za kibingwa, Utoaji wa huduma za Afya katika Hospitali za Kanda, Maalum, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali za Rufaa za Mikoa pamoja na uhakiki ubora wa huduma za afya yalipewa kipaumbele.


Aidha, Waziri Ummy amesema Wizara imeendelea kusimamia na kuratibu shughuli zilizokuwa zimepangwa kutekelezwa na Taasisi zilizopo chini yake. Taasisi hizo ni pamoja na Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Mabaraza ya Kitaaluma.


Hata hivyo, pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika utekelezaji wa Majukumu ya Wizara (Idara Kuu ya Afya), Waziri Ummy amebainisha changamoto mbalimbali zikiwemo Vituo vya kutolea huduma za Afya kutowasilisha mahitaji ya dawa, Vifaa, Vifaa tiba na Vitendanishi kwa wakati, Upatikanaji wa Huduma Bora na za Uhakika za Uzazi Mama na Mtoto, Upungufu wa watumishi wenye taaluma ya kutoa huduma za afya ikilinganishwa na mahitaji, Wigo mdogo wa wananchi walio katika mifumo ya Bima za Afya pamoja na Kuongezeka kwa watu wenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Share:

KIDATO CHA KWANZA WARUHUSIWA KUVAA SARE ZA SHULE YA MSINGI

Na Amiri kilagalila Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth msafiri ametoa ruhusa kuvaa sare za elimu ya msingi kwa wanafunzi ambao wamefanikiwa kufaulu elimu ya msingi na kushindwa kujiunga na elimu ya sekondari kutokana na wazazi kushindwa kukamilisha mahitaji hayo. Mkuu huyo wa wilaya alitoa ruhusa hiyo alipotembelea katika shule ya secondary Maheve iliyopo katika kata ya Ramadhani pamoja na shule ya secondari Joseph mbeyela zilizopo halmashauri ya mji wa Njombe na kupata taarifa ya baadhi ya wanafunzi kushindwa kufika shuleni kutokana na kukosa baadhi ya mahitaji. “Hawa wanafunzi si…

Source

Share:

HABARI ZA MAGAZETI YA TANZANIA LEO JANUARI 17,2019.

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 17, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:

SIMBA NJIANI KUWAVAA WAKONGO AS VITA CLUB

Emmanuel Okwi kushoto na Meddie Kagere.

Taarifa ya Simba jana jumatano imeeleza kuwa maandalizi kwaajili ya safari hiyo yamekamilika na timu itasafiri kwa ndege ikipitia Nairobi hadi Kinshasa ambapo utapigwa mchezo huo.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa mchezo huo utaanza saa 11:00 jioni kwa saa za DRC ambapo itakuwa ni saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika mashariki.

Klabu inatarajiwa kurejea nchini siku ya Jumapili tayari kwa ratiba nyingine ikiwemo michezo ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara pamoja na maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Al Ahly 1, 2, 2019 nchini Misri.

Mpaka sasa Meddie Kagere ndio mfungaji bora wa ligi ya mabingwa akiwa na mabao matano katika mechi 5 hiyo ni baada ya Moataz Al-Mehdi mwenye mabao 7 timu yake ya Al Nasr kutolewa.

 Emmanuel Okwi ndiye mchezaji aliyetengeneza mabao mengi zaidi ambayo ni matano.

Simba pia ndo timu iliyofunga mabao mengi zaidi kwenye michuano hiyo msimu huu ikiwa imefunga mabao 15 katika mechi 5 ilizocheza.

Chanzo:Eatv
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger