Wednesday, 16 January 2019

TFF KUBURUZWA MAHAKAMANI SHINYANGA SAKATA LA UCHAGUZI WA VIONGOZI YANGA

Mwanachama wa Yanga Chibura Makorongo mkazi wa wilaya na mkoa wa Shinyanga mwenye kadi ya uanachama wa Yanga namba 0015249 amehitaji ufafanuzi kutoka kwa kamati ya shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) inayosimamia uchaguzi wa viongozi wa Yanga, kuhusu tafsiri ya uhalali wa uanachama wa Yanga kupitia Benki ya Posta, pia suala la viongozi wa klabu hiyo kuikacha mikoa mingine kuomba kura za kuiongoza klabu hiyo. 

Chibura amesema hayo wakati akizungumza na www.malunde.com kuhusu sintofahamu ya mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa klabu ya Yanga na kusema kuwa endapo mambo hayo hayatatolewa ufafanuzi yupo tayari kwenda mahakamani kusitisha zoezi la uchaguzi ambalo linasimamiwa na shirikisho la mpira wa miguu nchini(TFF). 

“Wanachama wa Yanga waliopitia mfumo wa kujiunga kupitia Benki ya Posta ni wanachama halali au la! Na kama ni la! Ni nani aliyepitisha suala hilo?” Aliuliza Chibura. 

“Na hao viongozi wanaowania nafasi mbona wameitenga mikoa mingine? Wakipata dhamana ya uongozi watakuwa wanawaongoza wanachama wa Dar es salaam ama wanachama wa nchi nzima? Tunapokwenda kwenye uchaguzi tutakwenda mahakamani hasa mimi nimeshaanza kuwasiliana na mwanasheria wangu,” Aliongeza Chibura.

Klabu ya Yanga licha ya kukabiliwa na misukosuko ya makundi mawili yanayosigana lakini klabu hiyo inakalia nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara ikiwa na alama 53,ikiwa imecheza mechi 19 bila ya kupoteza mchezo hata mmoja,ikifuatiwa na timu ya Azam fc yenye alama 40 baada ya kucheza michezo 17,huku Simba Sc ikishikilia nafasi ya tatu ikiwa na alama 33 baada ya kuchez mechi 14.


Na Malaki Philipo - Malunde1 blog
Share:

Picha : MIGODI YA BUZWAGI , BULYANHULU YATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI WA SHULE KAHAMA


Kampuni ya Uchimbaji madini ya dhahabu ya Acacia kupitia migodi yake ya Buzwagi na Bulyanhulu imetoa msaada wa mabati 2347 yenye thamani ya shilingi milioni 70 kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu katika shule za msingi na sekondari kwenye halmashauri za wilaya ya Msalala na Kahama Mji mkoani Shinyanga. 

Mabati hayo yenye geji 28  yamekabidhiwa leo Januari 16,2019 kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha Meneja Mwendeshaji mgodi wa Buzwagi, Arthur Mgongo akimwakilisha Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu. 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mgongo alisema Acacia inaunga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha kila mtoto anapata elimu kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Maendelo ya Taifa ya mwaka 2025. 

"Katika muitikio wa ombi la msaada wa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya madarasa na nyumba za walimu,migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu imechangia vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 150,mpaka sasa tumechangia mifuko ya saruji 3200 ambapo halmashauri ya Kahama Mji imepokea mifuko 1600 ya saruji na Msalala mifuko 1600 jumla ina thamani ya shilingi milioni 80",alieleza Mgongo.  

"Kiasi cha ziada ya fedha iliyobaki ambacho ni sh. Milioni 70 kimetumika kununua mabati haya 2347 yaani mabati 1173 kwa Halmashauri ya Kahama Mji na mabati 1174 Msalala",aliongeza Mgongo. 

Alisema msaada huo utasaidia kuongeza miundo mbinu katika shule ili kukidhi ongezeko la wanafunzi kwani tangu serikali ianze utekelezaji wa mpango wa kutoa elimu bure,uandikishaji wa wanafunzi shuleni umeongezeka na uhitaji wa miundombinu umeongezeka. 

Mgongo alielezea kuwa, kupitia mpango wake wa maendeleo ya jamii,Acacia imeendelea kuboresha upatikanaji wa elimu katika jamii zinazozunguka migodi yake na kuleta mapinduzi ya kijamii na kiuchumi nchini sambamba na ajenda kuu ya viwanda. 

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha aliishukuru Acacia kwa kuwa sehemu ya jamii kuchangia sekta ya elimu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Macha alisema wilaya yake ina uhitaji wa madarasa 250 na kubainisha kuwa mabati yaliyotolewa na Acacia yatatumika kwenye ujenzi wa madarasa 50 huku akitaja kipaumbele ni kwenye shule ambazo tayari wazazi wamejenga maboma. 

Aidha aliwataka wadau kushirikiana na serikali kuchangia kwenye elimu kwani kila mmoja ni sehemu ya jamii hivyo anatakiwa kuchangia badala ya kuiachia serikali pekee.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mwendeshaji mgodi wa Buzwagi, Arthur Mgongo akizungumza kwa niaba ya Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu wakati akikabidhi mabati  2347 yaliyotolewa na Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya Kahama Mji na Ushetu leo katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kahama.Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Mgongo akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha (kulia) wakati akikabidhi mabati  2347 (pichani nyuma) yaliyotolewa na Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya Kahama Mji na Ushetu. Kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji, Abel Shija.
Mgongo akielezea shughuli zinazofanywa na Acacia katika jamii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa maktaba mjini Kahama,Nyang'hwale na Tarime lakini pia maboresho na utanuzi wa shule za msingi na sekondari ikiwemo ujenzi wa maabara na mabweni.
Awali Mkurugenzi wa halmashauri ya Kahama Mji, Underson Msumba akiangalia mabati matatu kati ya 2347 ambapo 1173 ni kwa ajili ya Kahama Mji yaliyotolewa na migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akizungumza wakati akipokea mabati yaliyotolewa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia kupitia migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akiishukuru Acacia kwa kuendelea kuwa mdau muhimu wilayani Kahama kwa kuchangia shughuli za maendeleo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kahama Mji, Abel Shija akielezea jinsi Acacia wanavyoshirikiana na halmashauri hiyo kuwaletea maendeleo wananchi.
Katibu wa CCM wilaya ya Kahama (kwanza kushoto) akizungumza wakati wa makabidhiano ya mabati ambapo alisema mchango wa Acacia ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
Viongozi mbalimbali wa halmashauri  ya wilaya ya Kahama Mji na Msalala na waandishi wa habari wakiwa katika hafla fupi ya makabidhiano ya mabati.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

CCM YAUNGA MKONO SHERIA MPYA YA VYAMA VYA SIASA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amesema sheria vya vyama vya siasa iliyopo sasa haimpi nguvu Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya kazi kwa ufanisi hivyo mabadiliko ya muswada mpya yatasaidia uimara wa vyama vya siasa na Ofisi ya Msajili kufanya kazi kwa ufanisi.

Polepole ameyasema hayo leo Jumatano Januari 16 katika mkutano wa chama hicho wa kujadili mabadiliko ya muswada kabla ya kupelekwa Bungeni uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

“Mabadiliko hayo yatampa nguvu msajili wa vyama vya siasa kutazama kwa jicho la upole endapo chama kimefanya vizuri na jicho la ukali kwa mambo ya ovyo ambayo chama kitafanya,” amesema.

Aidha, amesema mabadiliko hayo yatampa nguvu Msajili kuhusika kwenye usajili wa vyama vya siasa, kusimamia chaguzi za vyama vya ndani, kutoa na kufuatilia uwajibikaji wa ruzuku.

“Sheria tunayoitumia sasa ni sheria ya mwaka 2010 ni miaka 10 imepita tangu kufanya mabadiliko ya sheria, sisi ni vijana tunatakiwa tutoe maoni na mabadiliko ya sheria mpya ili sheria mpya itakayokuja kutumika isiweze kumbana msajili wa vyama vya siasa pamoja na sisi wanachama,” amesema Polepole.


Awali katibu wa siasa na mahusiano ya kimataifa wa CCM, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga amewataka wanachana wa chama hicho kutoa maoni yao bila wasiwasi kuhusu muswada huo.

Amesema kusudi kubwa la muswada huo ni kutengeneza mazingira ya kuwaongoza Watanzania kulingana na mazingira yaliyopo.

Amesema muswada huo unapiga marufuku kuanzishwa kwa vikundi vya ulinzi na usalama ndani ya vyama vya siasa jambo ambalo ni sahihi
Share:

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA KWA MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF KUHUSU UCHAGUZI WA YANGA

Ndugu Wana-habari, Ijumaa iliyopita niliwatangazia kusogezwa mbele kwa muda uchaguzi mdogo wa klabu ya Yanga kufuatia taarifa za wimbi la (tulioamini kuwa wana-Yanga) kufungua kesi sehemu mbalimbali nchini kuzuia uchaguzi huo usifanyike na kwamba baadhi ya Mahakama zilishatoa amri hiyo. 

Kwa kuheshimu mamlaka ya ki-Katiba ya Mahakama nchini na kwamba nchi yetu inaheshimu na kufuata utawala wa sheria, Kamati yangu ya Uchaguzi haikuwa na njia nyingine ya kufanya bali kuusogeza mbele kwa muda uchaguzi wa Klabu ya Yanga uliopangwa ufanyike siku mbili baadaye, yaani Jumapili ya tarehe 13/01/2018. 

Kwa upande wa pili, Kamati ilijikuta na deni kubwa kwa wana-Yanga, deni la kuelezea kilichojiri, kuelezea msingi wa kesi hizo mahakamani zilizosababisha kusogezwa mbele kwa muda uchaguzi katika klabu yao. 

Hivyo kuanzia Ijumaa jioni, yaani mara tu baada ya kutangaza kusogezwa mbele kwa muda kwa uchaguzi huo, Kamati ilitumia njia mbalimbali kuwafikia wale wote waliofungua kesi ili kujua msingi wa malalamiko yao na uhalali wao kusimama mahakamani dhidi ya Klabu hiyo ya Yanga kwa mujibu wa Katiba ya Yanga. 

Tumejiridhisha kuwa malalamiko yote yamejikita kwenye maeneo makuu matatu: (i) mosi, uhalali wa wanachama wenye kadi za zamani, kadi za CRDB na kadi za Benki ya Posta kupiga kura; (ii) pili, kukataliwa majina ya wanachama katika baadhi ya matawi ya Yanga kuingizwa kwenye rejista ya wanachama wa Yanga; na (iii) tatu, sintofahamu ya nafasi ya Mwenyekiti wa Yanga hivyo kusababisha baadhi ya wanachama wenye sifa za uongozi, kuwa na mashaka kujitokeza. 

Kamati ya Uchaguzi, mbali na kuchambua sifa ya uanachama ya walalamikaji hao (ambapo Kamati imebaini kuwa walalamikaji wote kasoro mmoja, si wanachama hai wa Yanga), imepitia malalamiko yote hayo kwa kina na kuwapelekea ujumbe ufuatao walalamikaji wote kwamba: (i) uanachama wao Yanga una hitilafu ki-Katiba, hivyo hawakuwa na sifa (locus) kupeleka malamamiko yao popote pale kwa kivuli cha uanachama wa klabu hiyo; (ii) Katiba za Yanga, TFF, CAF na FIFA haziruhusu wanachama wao kupeleka malalamiko mahakamani, hivyo utaratibu huo hauna tija mbali na kuiondolea klabu sifa ya kuheshimu taratibu (compliance); (iii) malalamiko yao yote waliyoainisha yanatatulika kwa taratibu zilizopo ndani ya shirikisho, hivyo hawana budi kuondoa kesi hizo mahakamani mara moja. 

Napenda kuwataarifu kuwa walalamikaji wote wametuelewa na wamekubali kuondoa kesi zao zote mahakamami na hivyo, kuruhusu Kamati yangu kuwasilisha TFF malalamiko yote tuliyoainisha ili yafanyiwe kazi ndani ya siku 7 kuanzia jana na baada ya hapo Kamati itatangaza ratiba ya kukamilisha uchaguzi mdogo wa Yanga. 

Naomba vilevile nisisitize kwamba uchaguzi huu ni uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi zilizoachwa wazi. 

Hivyo viongozi wa Yanga tunaowachagua sasa ni wa kipindi kifupi kilichobaki cha takriban mwaka mmoja, kabla ya mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Yanga kuanza. 

Nihitimishe taarifa yangu kwa kuwashukuru Watanzania na wana-Yanga wote kwa utulivu na uvumilivu mkubwa mliouonesha baada ya uchaguzi wenu mdogo kusogezwa mbele kwa muda. 

Aidha nawaomba wana-Yanga wote wakiongozwa na Wajumbe wa Baraza la Wadhamini, Sekreterieti na Wajumbe waliobaki wa Kamati ya Utendaji, wasichoke maana tumekaribia mwisho wa zoezi hili lenye afya kwa ustawi na maendeleo ya klabu hii kongwe Afrika ya Mashariki na Kati. Timu bora inategemea uongozi bora unaowajibika kwa wanachama. 

AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA
Malangwe Ally Mchungahela
Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi ya TFF
Share:

LUGOLA AUNDA KAMATI YA KUCHUNGA MALALAMIKO YA RUSHWA KWA POLISI WA USALAMA BARABARANI

Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo aunde kamati ya kuchunguza vitendo na mianya ya rushwa kwa jeshi la polisi na msisitizo mkubwa kwenye kitengo cha usalama wa barabarani.

Akizungumza leo Jumatano Januari 16 2019, Lugola pia amemtaka kamanda wa kikosi cha usalama wa barabarani kujitafakari, kujipima kama anatosha katika nafasi hiyo.


"Nimemwelekeza katibu mkuu aunde timu ambayo itapewa miezi mitatu kuchunguza vitendo na mianya ya rushwa na msisitizo mkubwa kwenye usalama wa barabarani na tume hiyo itanipa hatua za kuchukua," amesema.


Amesema kumekuwa na malalamiko mengi yanayohusu ubambikiaji wa makosa ya barabarani kwa madhumuni ya kutaka rushwa na unyanyasaji wa madereva bodaboda.


Ameongeza kwamba licha ya kuwapo makamanda wa trafiki wa mikoa lakini bado kumekuwa na malalamiko juu ya utendaji wa polisi na hivyo ameamua kuchukua hatua dhidi ya vitendo hivyo.


Amesema tume itachunguza kitengo hicho na kumpelekea majibu ili aweze kuchukua hatua.
Share:

WAZIRI MKUU UINGEREZA ASHINDWA KUJITOA UMOJA WA ULAYA 'BREXIT'

Waziri Mkuu wa Uingereza ameshindwa vibaya katika kura ya kujitoa katika Umoja wa Ulaya – maarufu kama Brexit – katika bunge la Uingereza baada ya wabunge kupinga mswaada wake kwa kura 432 kwa 202.

Mara baada ya kipigo hicho, May amesema kuwa kutokana na wingi wa kura za kupinga mswaada huo serikali yake itaruhusu mswaada wa kutokuwa na imani kujadiliwa bungeni.

Aidha, wakati anarudi kukaa chini, kiongozi wa chama cha upinzani cha Leba, Jeremy Corbyn mara moja alithibitisha kuwa amewasilisha kura ya kutokuwa na imani na serikali ya May, mswaada ambao utajadiliwa Jumatano.


Hata hivyo, May alikuwa amewasilisha mbele ya bunge mpango mzima wa jinsi Uingereza itakavyojitoa katika Umoja wa Ulaya suala ambalo liliidhihirishwa katika kura ya maoni mwaka 2016.
Share:

BUNGE LASITISHA KUFANYA KAZI NA CAG

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema kwa sasa Bunge limesitisha kufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad. Aidha Ndugai amewatawanya wajumbe wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Tawala za Mikoa na Mitaa (LAAC) kufanya kazi katika kamati nyingine. Hatua ya usitishaji huo inatokana na kauli ya Profesa Assad aliyoitoa Desemba mwaka jana katika mahojiano na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Arnold Kayanda. Mtangazaji huyo alimuuliza CAG kuwa ni…

Source

Share:

BUNGE LASITISHA KAZI NA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema kwa sasa Bunge limesitisha kufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.
Kutokana na hali hiyo, amewatawanya wajumbe wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Tawala za Mikoa na Mitaa (LAAC) kufanya kazi katika kamati nyingine.

Hatua ya usitishaji huo inatokana na kauli ya Profesa Assad aliyoitoa Desemba mwaka jana katika mahojiano na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Arnold Kayanda.

Mtangazaji huyo alimuuliza CAG kuwa ni vipi ofisi yake imekuwa ikijitahidi kila mwaka kufanya ukaguzi na kutoa ripoti zenye kuonesha kuna ubadhirifu, lakini baada ya hapo wananchi hawaoni kinachoendelea.


Katika majibu yake CAG alisema; “Hilo ni jambo ambalo kimsingi ni kazi ya Bunge. Kama tunatoa ripoti zinazoonyesha kuna ubadhirifu halafu hatua hazichukuliwi, huo kwangu ni udhaifu wa Bunge".

“Bunge linatakiwa kusimamia na kuhakikisha pale panapoonekana kuna matatizo basi hatua zinachukuliwa",Aliongeza Profesa Assad.

Spika Ndugai jana alisema suala hilo si la utani kama baadhi ya wanasiasa wanavyolichukulia.

Chanzo:Mpekuzi
Share:

WAZIRI MKUU UINGEREZA KUKABILIWA NA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NAYE

Wabunge wa Uingereza Jumanne waliyakataa pakubwa makubaliano ya Waziri Mkuu Theresa May na Umoja wa Ulaya kuhusu Uingereza kujiondoa kutoka kwenye Umoja huo, jambo lililouvuruga mchakato wa Brexit.

Hatua hiyo imepelekea kura isiyokuwa na imani kuwasilishwa, hatua ambayo inaweza kuiangusha serikali ya May. Wabunge walioyapinga makubaliano hayo ni 432 huku walioyaunga mkono wakiwa 202 pekee.

 Kushindwa kwa Waziri Mkuu huyo kulitarajiwa na wengi ingawa kiasi cha kura alizoshindwa nazo ni jambo ambalo limeuharibu uongozi wake unaosuwasuwa.

Kushindwa huku ni kwa kihistoria kwa kuwa ndiyo mara ya kwanza kwa serikali kushindwa kwa kiasi kikubwa cha kura katika bunge la Uingereza na kunafuatia msukosuko wa kisiasa wa zaidi ya miaka miwili ambapo May alijiwekea hadhi ya kisiasa kwa kuhakikisha amepata makubaliano ya Brexit. 

Jeremy Corbyn aliwasilisha mswada wa kutokuwa na imani na serikali ya May

Muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa na spika John Bercow Waziri Mkuu May, alizungumza.

Chanzo:Dw
Share:

MAGAIDI WALIOSHAMBULIA NAIROBI WAUAWA

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema  oparesheni ya kukabiliana na washukiwa wa ugaidi waliovamia hoteli ya Dusit2 mjini Nairobi imekamilika na kwamba washambuliaji wote wameangamizwa.

Watu waliyokuwa wamejihami kwa silaha siku ya Jumanne walivamia jengo la hoteli ya kifahari ya Dusir2 katika eneo la Westlands katika jiji kuu la Nairobi nchini Kenya na kuwaua watu 14.

Awali maafisa walitangaza kuwa oparesheni hiyo ilikamilika saa kadhaa baada ya shambulio hilo lakini mlilio ya risasi na milipuko ilisikika mapema alfajiri ya leo (Jumatano)


Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la al-Shabab, limedai kuhusika na shambulio.

Haijabainika ni washambuliaji wangapi walihusika na shambulio hilo.

Akihutubia taifa kwa moja kwa moja kupitia televisheni kutoka Ikulu, rais Kenyatta amesema kuwa watu 14 waliuawa katika shambulio hilo na wengine 700 kuokolewa kutoka jengo hilo.

Shirika la msalaba mwekundu hata hivyo limeripoti kuwa waliyofariki katika mkasa huo ni watu 24.

Raia wa Marekani ni miongoni mwa waliyofariki, imesema wizara ya mambo ya nje ya Marekani.

Raia mmoja wa Uingereza pia anahofiwa kufariki dunia.

Chanzo:Bbc
Share:

DC NJOMBE AAGIZA KUSHUSHWA VYEO AFISA ELIMU,MRATIBU ELIMU KATA YA RAMADHANI

Na Amiri kilagalila Mkuu wa Wilaya ya NJOMBE RUTH MSAFIRI ameagiza kushushwa vyeo afisa elimu kata ya Ramadhani ESTER MJUJULU, Mratibu Elimu wa kata hiyo HURUMA MGEYEKWA pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari MAHEVE, VALENO KITALIKA kwa Tuhuma za kuwatoza wazazi michango ya madawati kiasi cha shilingi Elfu Thelathini. Hayo yameibuka wakati Mkuu wa wilaya ya Njombe alipokuwa akikagua ujenzi wa madarasa yanayojengwa kwa ajili ya kidato cha kwanza Katika Shule hiyo ambapo amesema kitendo hicho ni kinyume na maelekezo ya Rais JOHN MAGUFULI ya kukataza watendaji kuchangisha michango…

Source

Share:

MAKAMANDA WA POLISI MIKOA MITATU WATENGULIWA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametengua uteuzi wa makamanda wa polisi wa mikoa mitatu; Salum Hamduni (Ilala), Emmanuel Lukula (Temeke) na Ramadhani Ng’azi (Arusha). Ametangaza uamuzi huo leo Jumatano Januari 16, 2019, katika mkutano na waandishi wa habari akibainisha kuwa amefanya hivyo baada ya kushauriana na vyombo anavyoviongoza. Amesema sababu za kutengua uteuzi wa kamanda wa Ilala na Temeke ni kushindwa kusimamia mianya ya rushwa na utoaji wa dhamana kwa watuhumiwa. Pia, amemuagiza katibu mkuu wa wizara yake kuunda kamati ambayo itapewa miezi mitatu kuchunguza vitendo…

Source

Share:

MAKAMBA AITA NEMC KUIGA UTENDAJI WA TFS

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira ) Mhe. January Makamba ameitaka bodi ya NEMC kuiga utendaji kazi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Makamba aliyasema hayo wakati akimkabidhi rasmi vitendea kazi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo mara baada ya kuzindua Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere mapema siku ya jana Prof. Silayo ni miongoni mwa wajumbe nane walioteuliwa kuunda bodi…

Source

Share:

UMOJA WA AFRIKA NA MAREKANI WALAANI SHAMBULIZI LA NAIROBI

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat amelaani vikali shambulio la Hoteli ya kifahari ya DusitD2 jijini Nairobi.


Katika taarifa yake, Faki amevisifu vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya kwa kuchukua hatua za uokozi wa raia na kupambana na wahalifu mapema iwezekanavyo. Pia amesema tukio hilo linaonesha umuhimu wa kupitia upya mipango ya kuongeza nguvu ya kupambana na vikundi vya kigaidi barani Afrika.

Mwenyekiti wa Kamisheni anathibitisha utayari wa AU kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na Nchi Wanachama katika kupambana na visa vya ugaidi pamoja na harakati za kutuliza hali nchini Somalia na mapambano dhidi ya kundi al-Shabaab kupitia vikosi vyake vya AMISOM.

Balozi wa Marekani anayemaliza muda wake nchini Kenya Bw Robert Godec ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa Marekani inashutumu vikali shambulio hilo.


Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha kuwa raia wake mmoja ni kati ya watu waliopoteza maisha kwenya mkasa huo.

Chanzo:Bbc
Share:

KANGI LUGOLA ATUMBUA MAKAMANDA WA POLISI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametengua uteuzi wa makamanda wa polisi wa mikoa mitatu; Salum Hamduni (Ilala), Emmanuel Lukula (Temeke) na Ramadhani Ng'azi (Arusha).

Ametangaza uamuzi wake huo leo Jumatano Januari 16, 2019, katika mkutano na waandishi wa habari akibainisha kuwa amefanya hivyo baada ya kushauriana na vyombo anavyoviongoza.

Amesema sababu za kutengua uteuzi wa kamanda wa Ilala na Temeke ni kushindwa kusimamia mianya ya rushwa na utoaji wa dhamana kwa watuhumiwa.

Pia, amemuagiza katibu mkuu wa wizara yake kuunda kamati ambayo itapewa miezi mitatu kuchunguza vitendo vya rushwa akitaka mkazo uwekwe zaidi kwa askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani.

Waziri huyo amemtaka Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslimukujitafakari na kujipima kama anatosha katika nafasi hiyo.


Na Sharon Sauwa, Mwananchi
Share:

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMATANO 16.01.2019

Manchester United wamekubali kumuuza kiungo wao wa kati, mbelgiji Marouane Fellaini, 31, kwa kima cha euro milioni 15 mwezi huu.

Tayari vilabu vya AC Milan, Porto na Guangzhou Evergrande ya Uchina vimeonesha nia ya kutaka kumsajili. (Mirror)

Chelsea wanatarajiwa kuendelea mbeli na mpango wao wa kumsajili mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, ambaye yuko kwa mkopo AC Milan, kufikia mwisho wa wiki hii. (Telegraph)

Meneja wa AC Milan Gennaro Gattuso amesema kuwa Higuain hajamwambia kuwa anataka kuondoka klabu hiyo. (Evening Standard)

Christian Eriksen, 26,huenda akatia saini mkataba mpya na Tottenham, wakati ambapo Real Madrid pia inapigiwa upatu kumsajili kiungo huyo wa kati raia wa Denmark. (AS)

Chanzo:Bbc
Share:

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO JANUARI 16,2019.

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 16, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger