Wednesday, 9 January 2019

RAIS MAGUFULI AMPOTEZEA SPIKA NDUGAI OMBI LA MAWAZIRI KUCHOKA WAPEWE LIKIZO


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewaombea likizo mawaziri na manaibu waziri kwa Rais John Magufuli. 

Spika Ndugai ametoa maombi hayo kwa Rais Magufuli wakati akitoa salamu katika hafla ya uapisho wa viongozi wa serikali iliyofanyika leo tarehe 9 Januari 2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

“Nikiwaangalia mawaziri nawaona mmechoka hivi mnakwenda likizo kweli?, ninawaombea kwa rais likizo hata ya mara moja kwa mwezi,” amesema na kuongeza Spika Ndugai.

“Mawaziri wetu wamekuwa wakifanya kazi kubwa, namalizia kwa kuwahakikishia ushirikiano, bunge letu litakuwa pamoja nanyi na kama mtahitaji msaada wetu kwa jambo lolote lile wakati wowote ofisi ziko wazi.”

Katika hatua nyingine, Spika Ndugai amewapongeza viongozi walioapishwa leo na kuwapa pole kutokana na kasi ya utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano huku akiwataka kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi hiyo.

Akijibu maombi ya Spika Ndugai, Rais Magufuli amesema mawaziri hawana likizo kwa kuwa wananchi wanaowaongoza hawana likizo, na kuwataka kukubali kuteseka katika kipindi hiki cha miaka mitano ya awamu ya kwanza ya uongozi wake ili kuwaletea maendeleo watanzania.

“Kwa makatibu wakuu na wizara, najua mna majukumu makubwa ndio maana mheshimiwa spika anazungumza hamjachukua likizo lakini na mimi sijachukua likizo, wananchi unaowaongoza hawana likizo watanzania hawa wote milioni 55 hawana likizo katika shughuli zao kwa hiyo wakati mwingine inakuwa vigumu kuchukua likizo sababu tunaowaongoza hawana likizo,” amesema na kuongeza Rais Magufuli.

“Leo sijalala nilikuwa nazungumza na waliokwenda kuchukua ndege ya ‘Air Bus’, kujua kama wamechukua spea na kui ‘test’ ndege (kuijaribu ndege), wakaniambia tumekaa angani masaa manne ndege inazunguka, kwa hiyo tukichukua likizo, angalau hii miaka mitano tuteseke kuwatumikia watanzania.”
Share:

POLEPOLE : HAKUNA MWINGINE ATAKAYEPEWA RIDHAA YA KUGOMBEA URAIS CCM ZAIDI YA JPM


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa alichokifanya Rais Magufuli kwa kipindi hiki kifupi alichokaa madarakani, ni dhahiri kuwa hakuna mwingine atakayepewa ridhaa na chama zaidi yake kugombea 2020.

Polepole ametoa kauli hiyo leo katika kipindi cha East Africa BreakFast cha East Africa Radio ambapo amesema CCM haina sababu ya kupitisha mgombea mwingine ikiwa Rais Magufuli amefanya vitu vikubwa na bado uwezo na nguvu ya kulitumikia taifa bado anao.

"Mwaka 2020 hatuna shaka katika nafasi ya Urais mgombea wetu ni Rais Magufuli hatuna wasiwasi kabisa na kiongozi wetu kwa aliyofanya kwa kipindi hiki njia ni nyeupe, lakini hatujakataza wengine kuchukua fomu wao wachukue tu", amesema Polepole.

Akizungumzia kupunguzwa kwa wanachama wanaotakiwa kupiga kura za maoni amesema kuwa, "Sisi hatuukatai ubaya ambao ulikuwepo zamani, tunakiri na kufuta kwa kufanya mema, CCM tuna kadi za kielektroniki hivyo huwezi kupiga kura ya maoni, kama huna kadi ile na sio kwamba tumewapunguza bali ni mabadiliko ya teknolojia hivyo wahakikishe wanakubaliana na mabadiliko na hakuna aliyefukuzwa".

Aidha Polepole amesema kuwa chama chake, hakipokei tena watu wanaotoka upinzani wao wabaki hukohuko usajili umeshafungwa, na kudai kuwa waliobaki hawana vigezo na wajiandae kuachia majimbo 2020.
Share:

MO SALAH ATAWAZWA MCHEZAJI BORA WA MWAKA AFRIKA

Mohamed Salah alikabidhiwa tuzo hiyo na rais wa Caf Ahmad Ahmad (kushoto) na rais wa Liberia George Weah (kulia)

Mshambuliaji wa Misri na klabu ya Liverpool ya England Mohamed Salah ndiye Mchezaji Bora wa Mwaka wa Shirikisho la Soka Barani Afrika kwa mwaka 2018 - hii ikiwa ni mara yake ya pili kushinda tuzo hiyo.

Salah, 26, alimshinda mwenzake wa Liverpool Sadio Mane kutoka Senegal na mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang.

Alikabidhiwa tuzo hiyo katika sherehe iliyofanyika nchini Senegal Jumanne januari 8,2019.

"Nimekuwa na ndoto ya kushinda tuzo hii tangu nilipokuwa mdogo na sasa nimefanya hivyo mara mbili mtawalia," Salah alisema.

Salah amefunga mabao 16 katika mechi 29 alizoichezea Liverpool mashindano yote msimu huu.

Salah, Mane na Aubameyang wamo kwenye Kikosi Bora cha Mwaka Afrika pamoja na beki wa Manchester United Eric Bailly, kiungo wa kati wa Manchester City Riyad Mahrez, kiungo wa kati wa Liverpool Naby Keita na beki wa kushoto wa Tottenham Serge Aurier.

Chanzo:Bbc
Share:

KATIBU MKUU WA CCM AMUONYA DIALLO NA MECK SADICK KUENDELEZA MGOGORO


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amemwonya aliyekuwa mgombea wa uenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mwanza, Said Meck Sadiki kuacha kuendeleza fitina na badala yake ashirikiane na mshindi halali wa kiti hicho, Anthony Diallo kujenga chama.

Onyo hilo alilitoa jana wakati akizungumza na wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, Mkoa wa Mwanza ambacho kiliwahusisha pia watendaji wa serikali ngazi ya mkoa, wilaya na halmashauri kuangalia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi.

Baada ya hotuba yake hiyo, Dk. Bashiru aliwaita Diallo na Sadick mbele ya wanachama na kuwataka kupeana mikono ya heri na kukumbatiana ikiwa ni ishara ya kuondoa tofauti zao na kuwa kitu kimoja ili mkoa uweze kuwa imara na kushinda uchaguzi ujao. 

Dk Bashiru alisema, Sadick alifikisha malalamiko ya kumpinga Dk Diallo ambapo kila mmoja alisikilizwa na uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM iliamuru aliyeshinda uchaguzi wa mwaka jana awaongoze.

Alisema viongozi hao walielezwa kuwaunganisha wanachama kukiimarisha chama na kukinadi kwa wananchi wazidi kukiunga mkono lakini Meck Sadiki ameendeleza fitina za chini chini, jambao ambalo ni hatari kwa ustawi wa chama hicho.


Alisema anatambua Meck Sadik na Dk Dialo ni marafiki lakini wanagawanywa na wanachama na makada ambao dhamira yao washindwe kushirikiana na viongozi kusimamia maendeleo ya wananchi, hivyo aliwaonya kwa pamoja kuachana na tofauti hizo.


“Tukiendekeza migogoro na makundi ya watu hatutafika salama maana tutatoa mwanya kwa watu kufanya ubinafsi kwa maslahi yao.


“Kwanza kinachoendelea kati ya Dk Diallo na Sadick ni sawa na kukidhalilisha chama na wananchi, hali ambayo husababisha kukichukia na kukiadhibu kwenye baadhi ya maeneo,” alisisitiza katibu mkuu huyo.


Aidha Dk Bashiru aliwataka viongozi wa chama ngazi ya mkoa na wilaya kutowapokea na kuungana nao kwenye ziara zao mawaziri ambao hawapiti na kujitambulisha kwenye ofisi za chama hicho na pengine hata kuelezwa kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.


Awali Dk Bashiru alitembelea na kukagua shamba la ekari 29.23 la CCM lililopo Kijiji na Kata ya Katunguru Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza ambapo alipendekeza kijengwe chuo cha uongozi cha chama ili kusaidia kuelimisha viongozi wa CCM wa mikoa ya Kanda ya Ziwa.


Kwa upande wake, Dk Diallo alisema kwamba wamepokea kwa mikono miwili ushauri na maelekezo ya katibu mkuu huyo na watayafanyia kazi ili chama kiwe imara.
Share:

UPINZANI WAONYA MATOKEO YA UCHAGUZI NCHINI DRC

Mgombea wa urais wa upinzani nchini Congo DRC Martin Fayulu amewaonya maafisa wa uchaguzi dhidi ya ''kuficha ukweli'' huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda baada ya matokeo ya uchaguzi kucheleweshwa.

Bwana Fayulu amesema watu wa Congo tayari wanajua  matokeo ya uchaguzi uliyofanyika Desemba 30 kuahirishwa kwa wiki moja.

Matokeo ya awali ya uchaguzi huo yalitarajiwa kutangazwa siku ya Jumapili ya Januari 6 lakini yakaahirishwa.

Uchaguzi huo ulikuwa wa kumtafuta mrithi wa rais Joseph Kabila, ambaye anaachia madaraka baada ya kuongoza nchi hiyo ya maziwa makuu kwa miaka 18.

Kabila ameahidi kwamba uchaguzi huo ambao ulikuwa umepangwa ufanyike miaka miwili uliyopita utakuwa wa kwanza wa kupokezana madaraka kwa njia ya kidemokrasia nchini DR Congo tangu taifa hilo lilipojinyakulia uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji mwaka 1960.

Mrithi wake anayempendelea ambaye pia ni waziri wa zamani wa mambo ya ndani Emmanuel Shadary,anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wagombea wa upinzani Martin Fayulu,tajiri mkubwa wa mafuta na Felix Tshisekedi, mwana wa kiume wa kigogo wa upinzani.

Chanzo:Bbc
Share:

Good News : Pakua Upya App ya Malunde 1 blog ...Imeboreshwa Kukupa Raha zaidi ...Bonyeza HAPA SASA

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Share:

KUZIONA SIMBA NA JS SOUARA LAKI MOJA


Klabu ya soka ya Simba imetangaza viingilio vya mchezo wao wa klabu bingwa Afrika Jumamosi hii dhidi ya JS Souara kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam.

Simba kupitia kwa msemaji wake Haji Manara imesema kiingilio cha chini ni shilingi 5,000 huku cha juu kikiwa ni laki moja.

''Viingilio vya mchezo mzunguko ni 5,000 huku VIP B ikiwa ni 10,000 lakini tutakuwa na tiketi za Platinums ambayo ni 100,000 itajumuisha kuchukuliwa na 'Luxury bus' kutoka Serena Hotel na kusindikizwa na polisi, jezi mpya ya Simba, 'Bites na soft drinks' muda wote utakaokuwa uwanjani pamoja na kurejeshwa Serena'', - Manara.

''Tunawasihi sana wanasimba na washabiki wote tujae kama kawaida yetu Jumamosi, na tuje kuhanikiza, tuje tukijua ujaji wetu ndio silaha yetu'', ameongeza Manara.
Share:

MAHAKAMA YAAMURU MWILI WA MAREHEMU UFUKULIWE ILI UCHUNGUZWE

Na Stephen Noel Mpwapwa . Mahakama ya Hakimu mkazi wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imeamuru kufukufukuliwa kwa mwili wa marehemu Cosmas Msote aliye fariki miezi mitano ili ufanyiwe uchunguzi wa chanzo cha kifo chake. Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kuwapo na ubishani Kati ya taarifa zilizo andikwa na Mganga wa hospital ya wilaya ya Mpwapwa juu chanzo cha kifo cha bwana Cosmas Msote aliye fariki dunia tarehe 5 October 2018. Kwa mujibu wa Hakimu mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Mpwapwa bwana Pascal Mayumba amesema aliamua kutoa…

Source

Share:

HALMASHAURI ZA WILAYA KOTE NCHINI ZIMEAGIZWA KUTENGA FEDHA KUTOKA MAPATO YA NDANI,KWA KUSHIRIKIANA NA WANAINCHI KUJENGA NYUMBA ZA WATUMISHI WA JESHI LA POLISI.

MULEBA, KAGERA. Na Mwandishi wetu. Waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola ametoa agizo hilo jana Januari 8,2019 kwenye mkutano wa hadhara, uliofanyika uwanja wa Fatuma Muleba mjini mkoani Kagera na kwamba nyumba hizo zijengwe palipo na kituo cha polisi Lugola amesema askari wanatakiwa kuishi kambini kwenye makazi ya pamoja na kulinda maadiliyao ya kiutendaji wakiwa na familia zao badala ya kuishi mitaani na kukiuka misingi ya utumishi wa Umma na wengine kushawishiwa na rushwa Amesema halmashauri nyingi nchini kwa kutumia kamati za ulinzi na usalama zikijipanga zitaweza kuanzisha maboma…

Source

Share:

MAHAKAMA YAAMURU MWILI WA MAREHEMU UFUKULIWE ILI UCHUNGUZWE.

Na, Stephen Noel Mpwapwa . Mahakama ya Hakimu mkazi wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imeamuru kufukufukuliwa kwa mwili wa marehemu Cosmas Msote aliye fariki miezi mitano ili ufanyiwe uchunguzi wa chanzo cha kifo chake. Mahakama hiyo imefikia waamuzi huo baada ya kuwapo na ubishani Kati ya taarifa zilizo andikwa na Mganga wa hospital ya wilaya ya Mpwapwa juu chanzo cha kifo cha bwana Cosmas Msote aliye fariki dunia tarehe 5 October 2018. Kwa mujibu wa Hakimu mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Mpwapwa bwana Pascal Mayumba amesema aliamua kutoa…

Source

Share:

TIZAMA VICHWA VYA HABARI VYA MAGAZETI YA LEO YA TANZANIA JANUARI 9,2019.

Share:

Tuesday, 8 January 2019

BENKI KUU YA TANZANIA YATOA MAAGIZO

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imetoa tangazo kwa umma kupitia tovuti yake (www.bot.go.tz) likiwataka watu na taasisi zote zinazofanya biashara ya huduma ndogo za fedha zilizoko Tanzania Bara (isipokuwa vyama vya ushirika vya akiba na mikopo – SACCOS) kutoa taarifa zitakazotumika katika utayarishaji wa Kanuni za Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha. “Bali ni kukusanya taarifa za awali kuhusu huduma hizo, kama amnavyo ilivyoainishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kupitisha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, lengo la sheria hiyo ni kuwalinda wadau…

Source

Share:

Picha : WAZIRI WA MAJI AMSWEKA RUMANDE MHANDISI WA MAJI SHINYANGA, AAGIZA WAHANDISI KUTEMBELEA MIRADI

Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso ameliagiza jeshi la polisi mkoani Shinyanga kumkamata mhandisi wa maji Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba  kushindwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi wa maji uliogharimu serikali kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja.


Agizo hilo amelitoa leo Januari 8,2019 wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mwakitolyo kwenye mkutano wa hadhara ambapo wananchi waliopewa nafasi ya kuuliza maswali walijikita na changamoto ya upatikanaji wa maji kutokana na mradi uliopo kushindwa kutoa maji.

Hata hivyo majibu ya mhandisi wa maji Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba yalishindwa kujitosheleza licha ya serikali kutoa fedha kiasi cha shilingi bilioni moja,milioni mia nne na sitini na mbili.

Kufuatia kukosekana kwa majibu kuhusu namna pesa hizo zilivyotumika,Aweso alieleza kusikitishwa na ucheleweshwaji wa mradi huo akidai kuna uzembe wa Mhandisi huo hivyo kumwagiza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko na jeshi la polisi kumkamata mhandisi huyo.

“Mradi wa maji Mwakitolyo gharama yake ni shilingi bilioni 1.482 mpaka sasa serikali ya imelipa kiasi cha bilioni 1.462, sisi tunaumia sana wakati mwingine huyu angekuwa daktari si angeshaua watu, mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ita polisi peleka ndani mtu huyu” ,alisema Aweso.

Waziri Aweso pia alimuagiza kaimu mhandisi wa maji mkoa wa Shinyanga Julieth Payovela kuandika barua ya kujitathmini katika utendaji kazi wake,na kuwaagiza wahandisi wa maji nchini kutembelea na kukagua miradi ya maji iliyopo kwenye maeneo yao na kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo ili kufikia azma ya kumtua mama ndoo kichwani.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum alisema wakazi wa jimbo hilo bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za miundombinu ya barabara, elimu, umeme na huduma za afya na kuiomba serikali kuwatazama wakazi wa jimbo hilo kwani wanajihisi kutengwa licha ya baadhi ya wataalamu kukwamisha juhudi za serikali kuwapatia wananchi wake huduma bora za kijamii.

“Jimbo la Solwa ni miongoni mwa majimbo nchini yanayokabiliwa na changamoto lukuki hasa katika sekta ya afya,elimu na miundombinu ya barabara, wananchi hawa hawana pa kukimbilia zaidi ya serikalini kutokana na mapato wanayoichangia serikali katika huduma za kimaendeleo” ,alisema Ahmed.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI

Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso  akizungumza na wakazi wa kata ya Mwakitolyo kwenye mkutano wa hadhara ili kusikiliza kero zinazowakabili - Picha zote na Malaki Philipo- Malunde1 blog
Mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba(kushoto) akihojiwa na Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso (kulia) kuhusu kushindwa kusimamia mradi wa maji kata ya Mwakitolyo.
Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akizungumza na kuagiza Mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba akamatwe na polisi .
Polisi wakitekeleza agizo la kumshikilia na kumuweka chini ya ulinzi mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba.

Mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba akiwa chini ya ulinzi.
Wakazi wa kata ya Mwakitolyo wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Tenki la maji Mwakitolyo,mradi wa maji ambao umeigharimu serikali kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja na mradi haujawanufaisha wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na wakazi wa kata ya Mwakitolyo.
Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Naibu waziri wa maji Mwakitolyo.
Wakazi wa Mwakitolyo wakiwa kwenye mkutano.
Awali Sada Khamis mkazi wa kijiji cha Mwakitolyo akieleza kero ya maji katika eneo hilo mbele ya Naibu waziri wa maji Juma Aweso.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mwakitolyo Nuhu Nshomi akieleza changamoto za elimu,maji na umeme wakati wa mkutano.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (wa kwanza kushoto), Naibu waziri wa maji Juma Aweso(katikati), Mbunge jimbo la Solwa Ahmed Salum(kulia) wakisikiliza kero za wananchi.
Mkutano ukiendelea...
Kaimu mhandisi maji Mkoa wa Shinyanga Julieth Pyovela akichota maji ya kunywa yanayopatikana Mwakitolyo baada ya kutakiwa anywe mbele ya Naibu waziri wa maji Juma Aweso.
Kaimu mhandisi maji Julieth Payovela akitekeleza agizo la kunywa maji alilopewa na Naibu waziri wa maji Juma Aweso.
Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akinywa maji yanayopatikana Mwakitolyo.
Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum akishiriki zoezi la kunywa maji ya Mwakitolyo.
Naibu waziri wa maji Juma Aweso akiwapigia simu wataalamu kutoka wizara ya maji kwa lengo la kuja kujiridhisha na majibu yaliyotolewa na Mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba kuhusu ucheleweshwaji wa huduma ya maji Mwakitolyo.
Mkutano ukiendelea
Afisa elimu kata ya Mwakitolyo Adam Lanja akieleza changamoto za elimu.
Awali Afisa tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela (mbele kulia) akitoa taarifa ya mkoa kwa Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza ofisini kwake wakati Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akipokea taarifa ya mkoa wa Shinyanga.
Mhandisi wa maji Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba akielezea kuhusu miradi ya maji katika wilaya ya Shinyanga mbele ya Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso.
Maafisa kutoka SHUWASA NA KASHUWASA wakiwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso. 

Picha zote na Malaki Philipo - Malunde1 blog

Share:

HUYU NDIO KOCHA ZAHERA AJA NA MPANGO HUU WA KUONDOA NJAA KWA WACHEZAJI WAKE WA YANGA

HUKU mashabiki wa Yanga wakiiona timu yao haina fedha na masikini kumbe wanajidanganya  baada ya kocha mkuu wao kipenzi, Mwinyi Zahera, kutamka wazi kwamba anaweza kuifanya klabu hiyo kumaliza ukata wa kifedha ndani ya miezi miwili kutokana na hazina kubwa ya wanachama na mashabiki iliyonayo. Yanga ni klabu kongwe nchini, lakini imekuwa ikishindwa kutumia rasilimali ilizonazo katika kujiletea maendeleo, huku baadhi ya wadau wakidai tatizo hilo linasababishwa na viongozi wanaojali masilahi yao binafsi na si ya klabu. Pamoja na kuwa na majengo mawili katika ya Jiji la Dar es Salaam,…

Source

Share:

SIMBA YAMUAANDAA BEKI HUYO KISIKI KUBEBA MIKOBA YA NYONI KWENYE MECHI NA WAARABU ,KOCHA MBELGIJI AFUMUA KIKOSI CHAKE

KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems, ameanza kumwandaa beki wake, Jjuuko Murushid, kuchukua nafasi ya Erasto Nyoni, ambaye hatakuwepo katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. katika Mechi hiyo Simba wanahitaji kila aina ya njia kuwakalisha waarabu ambapo Nyoni ameondolewa katika mipango ya  kocha huyo katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuumia goti wakati wa mechi ya juzi ya Kombe la Mapinduzi…

Source

Share:

SHAMBULIO LA AIBU LAMFIKISHA MAHAKAMANI MWINGINE ASHITAKIWA KWA KUJARIBU KUBAKA

Watu wawili wamefikishwa mahakama ya wilaya ya Serengeti kujibu mashtaka katika kesi mbili tofauti mmoja akijaribu kubaka na mwingine akifanya shambulio la Aibu Mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile mwendesha mashtaka wa Jamhuri Renatus Zakeo alisema katika shauri la jinai namba 2/2019 mshitakiwa Manyama Machota(36) mkazi wa kijiji cha Robanda wilayani hapa anashitakiwa kwa kosa moja la Shambulio la aibu Zakeo alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo Juni 9 mwaka 2018 katika kijiji cha Robanda baada ya kumshika binti aitwaye Zawadi Peter(16) sehemu mbalimbali za mwili wake bila…

Source

Share:

YANGA WAANZA MIPANGO YA KUMTAFUTA MRITHI WA MANJI,WANACHAMA WAPEWA NENO HILI

WAKATI suala la Uchaguzi wa Yanga likiwa bado kizungumkuti huku ikitajwa uwenda siku ya uchaguzi kukatokea fujo ya kupinga uchaguzi,wanachama wa Yanga wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni za uchaguzi ambazo zimezinduliwa rasmi leo katika Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na viongozi wa Yanga pamoja na wale wa TFF kwa ajili ya kujaza nafasi zilizo wazi kuanzia ile ya Mwenyekiti iliyokuwa wazi baada ya Yusuf Manji kujiuzulu pamoja na Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine. Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Januari 13 katika ukumbi wa Polisi Messi Oysterbay kuanzia…

Source

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger