Saturday, 5 January 2019

HABARI KWENYE MAGAZETI YA LEO 05/01/2019.

Habari za Asubuhi, Nakukaribisha kusoma Vichwa vya magazeti ya Tanzania leo Januari 05,2019.  ­

Source

Share:

Friday, 4 January 2019

NECTA YAFUTA MATOKEO YA WANAFUNZI WALIOANDIKA MATUSI KWENYE MITIHANI...ANGALIA MATOKEO HAPA

Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) leo Ijumaa Januari 4, 2019 limetangaza matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 2018, kueleza kuwa ufaulu umeongezeka ikilinganishwa na matokeo ya 2017.

Hata hivyo matukio ya wanafunzi kuandika matusi limeendelea  kujitokeza ambapo  Baraza la mitihani Tanzania limeyafuta matokeo yote ya watahiniwa tisa wa kidato cha pili walioandika matusi kwenye script zao katika na tumeelekeza bodi za shule kuwachukulia hatua za kinidhamu ili kukomesha tabia hii ya wanafunzi.

Akizungumza leo mjini Dodoma katibu mtendaji wa baraza hilo, Dk, Charles Msonde amesema kati ya watahiniwa 1,302,461 wa darasa la nne waliofanya mtihani huo sawa na asilimia 95.58, waliofaulu kwa kupata daraja A, B, C, na D ni 1,213,132 sawa na asilimia 93.16.

Hata hivyo wanafunzi 89,093 sawa na asilimia 6.84 wamepata alama za daraja E ambalo ni ufaulu usioridhisha.

“151 walishindwa kufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa na utoro,” amesema.

Dk Msonde amesema mwaka 2018 takwimu za matokeo zinaonyesha kuwa ufaulu wa watahiniwa kwa masomo yote uko juu ya wastani.


“Ubora wa ufaulu umezidi kuimarika kwa kuwa watahiniwa waliofaulu kwa daraja A, B na C umeongezeka kwa asilimia 0.03 ikilinganishwa na mwaka 2017,”amesema Dk Msonde.

Kuhusu kidato cha pili, Dk Msonde amesema watahiniwa 506,235 walisajiliwa kufanya mtihani huo sawa na asilimia 92.87, kwamba wanafunzi 38,842 sawa na asilimia 7.13 hawakufanya mtihani kutokana na ugonjwa na utoro.

Amesema wanafunzi 452,273 sawa na asilimia 89.68 wamepata alama za ufaulu zitakazowawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tatu.

Amesema wanafunzi 52,073 sawa na asilimia 10.32 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tatu.

Amesema mwaka 2017 wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 89.32 walipata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu, kwamba ikilinganishwa na 2018, ufaulu wa mwaka jana umeongezeka kwa asilimia 0.36.

Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa ya Kidato cha Pili (FTNA) 2018 Na Darasa la nne (SFNA) 2018 yametangazwa..Yaangalie hapa na pia mpangilio wa ufaulu ngazi ya mikoa na halmashauri

Share:

SABABU ZA YONDANI KUVULIWA UNAHODHA YANGA....AJIBU ARITHI


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amemvua unahodha, Kelvin Yondani kutokana na mchezaji huyo kutofika mazoezini bila taarifa yoyote, nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahim Ajibu. 

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, imeeleza kikosi cha wachezaji wasioenda kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kuendelea na mazoezi pamoja na kuondolewa kwa Yondani katika nafasi hiyo.

“Wachezaji waliobaki Dar es Salaam, wanaendelea na mazoezi leo katika viwanja vya polisi ufundi kurasini jijini Dar es Salaam baada ya mapumziko ya siku nne kwa baadhi ya wachezaji ambao hawakusafiri na timu visiwani Zanzibar kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi.” Ilienda sehemu ya taarifa hiyo.

Siyo mara ya kwanza kocha huyo kuchukua maamuzi magumu kwa baadhi ya wachezaji ndani ya kikosi hicho kutokana kuhitaji usawa na nidhamu kwa wachezaji wote ndani ya klabu hiyo kiasi cha hivi karibuni kumuondoa katika kikosi kipa namba moja wa timu hiyo, Beno Kakolanya baada ya kuondoka kambini bila taarifa kwa kushinikiza alipwe madai yake.

Mazoezi hayo yaliongozwa na kocha huyo yalikuwa ya utimamu wa mwili pia kwa upande wa uwanjani kulikuwa na mafunzo maalumu juu ya umakni uwanjani (Concentration) pamoja na umaliziaji kwenye safu ya ushambuliaji.
Share:

WAZIRI UMMY ATOA MABATI 100 KATA YA KIRARE JIJINI TANGA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WANANCHI


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi mabati 100 Diwani wa Kata ya Kirare Jijini Tanga Mwagilo ambazo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa zahanati za Mapojoni na Ujenzi wa Bweni la Wasichana Shule ya Sekondari Kirare wanaoshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudu Mayeji kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mganga wa Mfawidhi wa Zahanati ya Mapojoni mara baada ya kukabidhi mabati hayo wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya kukabidhi mabati hayo kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na
 Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kulia akimsikiliza kwa umakini Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mapojoni wakati alipokwenda kukabidhi mabati 100
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kushoto akikagua dawa kwenye zanhanati ya Mapojoni wakati alipokwenda kuwakabidhi mabati 100 
 ***
Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) na
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo amekabidhi mabati 100 katika Kata ya Kirare Jijini Tanga kwa ajili ya zahanati za Mapojoni na Ujenzi wa Bweni la Wasichana Shule ya Sekondari Kirare.

Ujenzi huo wa Bweni la Wasichana kwenye shule hiyo litasaidia kuondosha changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu umbali wa kilomita 15 jambo ambalo linaweza kupelekea kukumbana na vishawishi ambavyo vinaweza kukwamisha ndoto zao. 

Halfa ya makabidhiano hayo yamefanyika leo kwenye Kata hiyo ikiwa ni juhudi zinazoonyeshwa na Mbunge huyo
kwa ajili ya kuhakikisha changamoto mbalimbali zinazowakabili wananachi anashirikiana nao kuweza kuzipatia ufumbuzi. 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi mabati hayo Waziri Ummy alisema serikali ya awamu ya tano itaendelea kuchapa kazi kwa ufanisi mkubwa ili kuweza kutatua changamoto wa wananchi ili ziweze kupata ufumbuzi.

Sambamba na Waziri huyo kuchangia mabati hayo wakati huo
huo Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imeguswa na changamoto hiyo na kuchangia mabati 50 na saruji 70 katika ujenzi wa bweni la wasichana la shule ya Sekondari Kirare na kushiriki kwenye shughuli za ujenzi. 

Alisema kwani wao watahakikisha wanashirikiana na wananchi kwenye maeneo mbalimbali kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi changamoto za Afya ambazo zinaweza kuwa kikwazo kwenye kujiletea maendeleo. 

“Labda niwaambie tu kwamba Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu Dkt John Magufuli imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha changamoto mbalimbali zinbapatiwa ufumbuzi
hivyo endeleeni kushirikiana nayo kuweza kupata mafanikio ",alisema Waziri Ummy. 

Aidha Waziri huyo alisisitiza umuhimu wa wananchi kuhakikisha wanakata bima za Afya ili ziweze kuwasaidia kunufaika na huduma za matibabu wanapokuwa wakiugua. 

“Niwasisitize kwamba kateni bima ya Afya mkiumwa muweza kupata huduma za matibabu kwani wengine fedha zenu ni za msimu hivyo mkiwa na bima mnaweza kupata matibabu bure”,alisema. 

Waziri huyo alisema gharama za matibabu zimekuwa kubwa hivyo iwapo wakijiunga na bima hususani iliyoboreshwa ukitoa elfu thelathini kwa kaya ya watu sita unaweza kupata huduma za matibabu kwenye maeneo mbalimbali. 

“Bima kubwa ya kitaifa ya NHIF wana bima ya mtoto wameona badala ya kusema mtoto aishie elfu thelathini tu kwa hiyo ukimliptia mtoto 50400 atapata huduma mzuri”,alisema. 


Alisema sababu ya kusaidia juhudi hizo za wananchi ni kutokana na kuguswa namna walivyojitahidi kuhakikisha wanajenga jengo hilo wakishirikiana na viongozi wenu namna hivyo kuamua kuwaunga mkono. 

Aidha alisema anaamini mabati hayo yatakuwa chachu katika
 kutatua changamoto iliyopo kwenye jengo hilo ili kuweza kuzimaliza na kutoa fursa kwa wananchi kuweza kupata huduma bila kuwepo vikwazo. 

“Lakini hapa nimeambiwa mnachangamoto ya vifaa hivyo
 nitashirikiana nanyi kuweza kuzipatia ufumbuzi vifaa vyote
vinavyoihitaji kwenye zanahati hii”,alisema 

Awali akizungumza,Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) Isango Isubiri alisema wanamshukuru Rais John Magufuli kwa kutoa fedha za ukarabati za vituo vya afya kwenye Jiji ambavyo ni Makorora,Ngamiani,Mikanjuni na Duga ambao kwa sasa unaendelea. 

Alisema kwenye zahanati ya Mapojoni Jijini Tanga kulikuwa na uhaba wa chumba cha maabara na daktari hivyo kilichofanywa na Waziri huyo ni kutambua umuhimu kuunga mkono nguvu
za wananchi katika ujenzi wa jengo hilo lenye uhitaji mkubwa ambalo baada ya kulijenga walikosa mabato na saruji ili kuweza kulikamilisha.

Mganga huyo wa Jiji alisema ujenzi wa Jengo hilo ulianza mwaka 2016 ambapo litakapokamilika litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi ambao wanakwenda kupata huduma za matibabu kwenye zahanati hiyo. 

Aidha alisema pia suala lingine ni ujenzi wa hospitali ya
wilaya ya Tanga ambapo zilitolewa Bilioni 3.6 katika kipindi cha mwaka 2018 jambo ambalo limesaidia kuweza kuondosha changamoto ya afya. 

Share:

BITEKO AFUNGUA MAFUNZO KWA WACHIMBAJI MADINI MKOANI MARA


Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (pichani) amefungua mafunzo ya siku mbili kuanzia leo Januari 04, 2018 kwa wachimbaji wadogo wa madini/ dhahabu yaliyofanyika katika Kijiji cha Byatika Kata ya Buhemba Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Mafunzo kama hayo yanaendelea kwa nyakati tofauti katika maeneo mbalimbali nchini ambapo juzi Januari 02, 2018 Biteko alifungua mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu/ madini katika Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

Mafunzo hayo yanatolewa na Serikali kupitia taasisi zake ikiwemo Tume ya Madini pamoja na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ombi la wachimbaji wadogo wa madini hapa nchini ambao waliomba kupatiwa mafunzo ili kufanya shughuli zao kwa weledi bila kubahatisha.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Afisa Madini mkoani Mara, Nyaisara Mgaya akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
Godson Kamihanda kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini hapa nchini (GST) akizungumza wakati wa mafunzo hayo ambapo katika mafunzo hayo taasisi hiyo itatoa taarifa ya utafiti wa madini hapa nchi ili uwasaidie wachimbaji kufanya kazi zao bila kubahatisha.
Wachimbaji wadogo wa dhahabu wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (aliyekaa kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika wilaya ya Butiama mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (aliyekaa kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika wilaya ya Butiama mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (aliyekaa kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika wilaya ya Butiama mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (aliyekaa kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika wilaya ya Butiama mkoani Mara.
Awali Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko alipita katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya Butiama, Anna Rose Nyambi (pichani) na kupokea taarifa ya hali ya uchimbaji madini katika wilaya hiyo.
Tazama BMG Online TV hapa chini


Share:

DAWASA YAKABIDHIWA JENGO, WATAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo akizungumza na wanahabari na wageni waalikwa wakati wa utilianaji wa saini wa usimamizi wa jengo la Maji lililokuwa likijengwa na Wizara ya maji na Umwagiliaji na sasa wamekabidhiwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa ajili ya kulimalizia na kuhamishia ofisi. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage akizungumza na wanahabari na wageni waalikwa wakati wa utilianaji wa saini wa usimamizi wa jengo la Maji lililokuwa likijengwa na Wizara ya maji na Umwagiliaji na sasa wamekabidhiwa DAWASA kwa ajili ya kulimalizia na kuhamishia ofisi. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa machache.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto) akisaini mkataba na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) wa kusimimia jengo la Maji House linalotarajiwa kumalizika Februari 2020. Pambeni kulia ni mmoja ya wajenzi wa kampuni ya CCECC ambao ndiyo wakandarasi. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto) akisaini mkataba na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) wa kusimimia jengo la Maji House linalotarajiwa kumalizika Februari 2020. Pambeni kulia ni mmoja ya mkandarasi msahauri wa jengo hilo. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) akimkabidhi makataba wa kusimimia jengo la Maji House linalotarajiwa kumalizika Februari 2020. Pambeni anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto).
Wafanyakazi wa DAWASA na wageni waalikwa wakifuatiliwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage (anayefuata kushoto) wakifurahi pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) mara baada ya kuzindua picha ya jengo la Maji linalotarajiwa kumalizika Februari 2020.
Muonekano wa jengo la Maji litakalohamishiwa ofisi za DAWASA mara baada ya kumalizika.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kusimamia miradi ya maji kwa umakini mkubwa.

Amewataka DAWASA kuhakikisha kufikia 2020 asilimia 85 ya vijijini na asilimia 95 ya mijini inapata maji safi na salama.

Mkumbo amesema hayo wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya jengo la Maji lililopo Ubungo jijini Dar es Salaama na linalotarajiwa kumalizaika Februari 2020.

Utiaji wa saini hiyo ulihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Akizungumza baada ya utiaji wa saini, Mkumbo amesema DAWASA lazima wahakikishe wanasimamia mapato ili kuweza kuendeleza miradi ya maji ili wananchi waweze kufaidika.

Amesema, hafla ya leo sio ya kukabidhiwa jengo tu ila wanatakiwa kusimamia mradi wa Kidunda, visima vya Kimbiji Mpera pamoja na kuwaunganishia wateja wapya.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi Mwamunyage amesema changamoto kubwa iliyokuwepo katika mamlaka hiyo ni maeneo ya kufanyia kazi ila baada ya kukabidhiwa jengo hilo wanaamini kwa sasa kazi zitafanyika kwa wakati.

Amesema, kwa sasa DAWASA wanajiendesha wenyewe kwa mapato ya ndani na watasimamia mpaka kumalizika Februari 2020.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Luhemeja amewashukuru Wizara kwa kuwakabidhi jengo hilo lenye ghorofa 15 kwa ajili ya kuweka ofisi na itawasadia kufanya kazi kwa uharaka zaidi na ameahidi kuwa jengo hilo litakamilika kwa wakati kwani tayari ameshamuagiza Mkurugenzi wa Fedha kuanza kufanya malipo.

Pia ameeleza kuwa kwa sasa DAWASA ndani ya miezi mitatu wameweza kufikia malengo ya kufikia Bilioni 10 kwa mwezi katika ukusanyaji wa maji ila wamejizatiti kwa mwaka huu kufikia malengo ya serikali ya upatikanaji wa maji mijini na vijijini kabla ya 2020 ikiwemo na kupunguza mivujo kwa asilimia 25.
Share:

WAWILI WAFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI LA POLISI ARUSHA

Watu wawili wamefariki dunia baada ya pikipiki waliyokuwa wamepanda kugongwa na gari la polisi wilayani Monduli mkoani Arusha.

Tukio hilo limetokea jana jioni Januari 3, 2019 eneo la Meserani Duka Bovu wilayani Monduli.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'azi alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

"Ni kweli kuna hiyo ajali lakini mkuu wa upelelezi mkoa amekwenda eneo la tukio ndio atatupa taarifa sahihi ya kilichotokea,” amesema.


Kamanda Ng'azi amesema taarifa sahihi za tukio hilo ikiwepo majina ya marehemu zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.


Pikipiki hiyo ilikuwa ikitoka kuweka mafuta katika kituo cha mafuta kilichopo pembezoni mwa barabarani ya Arusha- Dodoma na kukutana na gari hilo lililokuwa likipita barabara kuu.
Share:

WANAFUNZI 38,842 HAWAKUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA PILI 2018...ANGALIA MATOKEO HAPA

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dk Charles Msonde, amesema watahiniwa 506,235 walisajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha pili kati yao wanafunzi 38,842 sawa na asilimia 7.13 hawakufanya mtihani kutokana na ugonjwa na utoro.

Dkt. Msonde ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza matokeo ya kidato cha pili na darasa la nne kwa mwaka 2018, ambapo amesema wanafunzi katika mtihani huo 452,273 sawa na asilimia 89.68 wamefaulu.

Aidha amesema wanafunzi 52,073 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tatu.

Kuhusiana na matokeo ya darasa la nne kati ya watahiniwa 1,302,461 wa darasa la nne waliofanya mtihani huo sawa na asilimia 95.58, waliofaulu kwa kupata daraja A, B, C, na D ni 1,213,132 sawa na asilimia 93.16.

"Ubora wa ufaulu umezidi kuimarika kwa kuwa watahiniwa waliofaulu kwa daraja A,B na C umeongezeka kwa asilimia 0.03 ikilinganishwa na mwaka 2017,”amesema Dkt. Msonde."

Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa ya Kidato cha Pili (FTNA) 2018 Na Darasa la nne (SFNA) 2018 yametangazwa..Yaangalie hapa

Share:

SERIKALI YAPEWA SIKU 7 KUJIELEZA SAKATA LA MUSWADA WA VYAMA VYA SIASA

Mahakama Kuu Tanzania imeipa siku saba Serikali kuwasilisha utetezi wake katika shauri la maombi ya kupinga muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, tofauti na muda uliowekwa kisheria wa siku 14.


Kesi hiyo imefunguliwa na Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe na wenzake wawili, Joran Bashange na Salim Biman wa CUF kwa niaba ya muungano wa wanachama wa vyama 10 vya upinzani, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).


Uamuzi huo umetolewa leo mchana Ijumaa Januari 4, 2019 na kiongozi wa jopo la majaji watatu wanaosikiliza shauri hilo, Jaji Barke Sahel.


Ametoa uamuzi huo baada ya kukubaliana na maombi ya waombaji katika shauri hilo la kupunguza muda wa Serikali kuwasilisha utetezi wake kutoka siku 14 zinazoelekezwa kisheria.


Awali Serikali kupitia kwa mwanasheria wa Serikali mkuu, Mark Mulwambo iliomba kuongezewa muda kutoka siku 14 za kisheria mpaka siku 21 kwa madai ya kufanya mashauriano baina ya Serikali na taasisi zake nyingine.


Akisoma uamuzi huo, Jaji Sahel amesema mahakama haikushawishika na maombi ya Serikali ya kuongezewa muda kwa lengo la kushaurina.


“Kwa kuzingatia kwamba shauri hili limewasilishwa chini ya hati ya dharura na kwa kuwa lina maslahi kwa umma na kwa kuzingatia kwamba muswada huu umepangwa kusomwa bungeni kwa mara ya pili Januari 15, 2019 mahakama inatoa amri zifuatazo,” amesema.


“Mjibu maombi atawasilisha majibu yake akiambatanisha na hati ya kiapo ndani ya siku saba tangu siku ya kupewa nyaraka za shauri hili, yaani atawasilisha utetezi wake kabla au Januari 9, 2019. Usikilizwaji wa shauri hili utafanyika Januari 11 saa 3 asubuhi.”


Katika shauri hilo la Kikatiba namba 31 la mwaka 2018, waombaji wanapinga kifungu cha 8 (3) cha Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi kinachoeleza kuwa muswada wowote hauwezi kupingwa mahakamani.


Zitto na wenzake wanapinga muswada huo pamoja na mambo mengine wakidai kuwa unakiuka haki za kisiasa za binadamu kwa kuwa unaharamisha shughuli za kisiasa na kumpa mamlaka makubwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuingilia mambo ya ndani ya vyama vya siasa, yakiwemo ya uongozi.
Share:

KIJANA MATATANI KWA KUBAKA MBUZI..MWENYEWE ASEMA ALIKUBALIANA NA MBUZI


Pichani, Kennedy Kambani pamoja na mbuzi anayetuhumiwa kumbaka.

Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Kennedy Kambani (21) huko Machinji, Malawi, ameshtakiwa kwa kumbaka mbuzi kwa madai kwamba aliomba ruhusa ya kufanya jambo hilo kwa mnyama huyo kabla ya kumuingilia.

Kamanda wa polisi, Lubrino Kaitano ameeleza kwamba kwa mujibu wa mmiliki wa mnyama huyo Pemphero Mwakhulika, alifikiri Kambani alikuwa akitaka kuiba mbuzi huyo alipomuona awali, lakini alipokwenda kuita watu ndipo alimkuta akifanya ngono na mbuzi wake.

Aidha ameeleza kwamba Kambani alikamatwa na kupelekwa kwenye kituo cha polisi na kushtakiwa kwa kitendo hicho lakini amedai kwamba yeye alimwomba ruhusa mnyama huyo kwanza.

Imeelezwa kwamba Mbuzi huyo alikuwa sehemu ya kundi la malisho kando ya Mchinji lakini jinsia yake haijatajwa.

Matukio ya binadamu kubaka wanyama yamekuwa yakitokea mara kwa mara ambapo Zambia, Sicko Reuben Mwaba,(22), alihukumiwa miaka 15 kwa kubaka mbuzi huku, Feselani Mcube ( 33), wa Afrika Kusini naye akituhumiwa kubaka mbuzi wa jirani yake aliyekuwa mjamzito.
Share:

Standard Four mpangilio wa ufaulu-Kitaifa & Mikoa 2018/19

NECTA-FORM TWO AND STANDARD FOUR NATIONAL ASSESSMENT RESULTS

 

The National Examinations Council of Tanzania (NECTA) is Government Institution which was established by the Parliamentary Act No. 21 of 1973. NECTA is responsible for the administration of all National Examinations in Tanzania.

National Level

http://41.59.85.99/files/HALMASHAURI_UFAULU_SFNA.pdf

Halmashauri/Manispaa Level

http://41.59.85.99/files/HALMASHAURI_UFAULU_SFNA.pdf

 

The post Standard Four mpangilio wa ufaulu-Kitaifa & Mikoa 2018/19 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Form two mpangilio wa ufaulu-Kitaifa & Mikoa 2018/19

NECTA-FORM TWO AND STANDARD FOUR NATIONAL ASSESSMENT RESULTS

 

The National Examinations Council of Tanzania (NECTA) is Government Institution which was established by the Parliamentary Act No. 21 of 1973. NECTA is responsible for the administration of all National Examinations in Tanzania.

National Level

http://41.59.85.99/files/HALMASHAURI_UFAULU_FTNA_2018.pdf

Regional level

http://41.59.85.99/files/HALMASHAURI_UFAULU_FTNA_2018.pdf

 

The post Form two mpangilio wa ufaulu-Kitaifa & Mikoa 2018/19 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

SFNA Results 2018/19 | Matokeo ya darasa la nne 2018

Share:

NECTA Form Two National Assessment (FTNA) Result 2018/19

Share:

UPEPO MKALI NA MAWIMBI YAVIKUMBA VIJIJI VYA THAILAND.

  Na. Jovine Sosthenes Mvua, upepo mkali na mawimbi vimelikumba eneo la kusini mwa Thailand hususani katika maeneo ya vijiji vilivyo jirani na fukwe ikiwemo maeneo ya utalii yaliyokumbwa na kimbunga kikali cha Papuk. Hakuna taarifa ya vifo lakini tayari mamlaka ya hali ya hewa nchini humo imetoa tahadhari huku ikishuhudiwa mamia ya watalii wakiondoka katika maeneo waliyokuwepo. Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini humo imesema kimbunga kingine kikubwa kinatarajiwa kupiga jioni ya leo na kitakua kina kasi ya kilomita 80 kwa saa. Kimbunga hicho kinatarajiwa kupiga zaidi eneo la Nakhon…

Source

Share:

BITEKO AKERWA NA AJALI MAENEO YA WACHIMBAJI WA MADINI MKOANI MARA.

  Na. Augustine Richard. Naibu Waziri wa Madini, Doto Mashaka Biteko leo Januari 4, 2019 amewataka wachimbaji wadogo katika eneo la uchimbaji mji wa Buhemba wilayani Butiama mkoani Mara kuzingatia uchimbaji salama ili kuepusha ajali zinazotokea mara kwa mara katika maeneo ya migodi. Biteko ameyasema hayo wakati wa mafunzo kwa wachimbaji wadogo yaliyofanyika wilayani Butiama mkoani Mara yenye lengo la kuwafundisha wachimbaji wadogo masuala ya uchimbaji salama, uchenjuaji, afya,umhimu wa kulipa kodi na tozo mbalimbali na mazingira ya uchimbaji katika mkoa wa Mara. “Akifa mtanzania mmoja huyo Mtanzania ni muhimu…

Source

Share:

WANAFUNZI 463 WAKOSA NAFASI KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA WILAYANI NJOMBE,UHABA WA MADARASA WACHANGIA

Na Amiri kilagalila-Njombe Halmashauri ya wilaya ya Njombe imefanikiwa kutafuta muarobaini wa wanafunzi zaidi ya 400 waliokosa nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza kutokana na ukosefu wa vyumba vya madarasa kwa kuchukua hatua za haraka katika ujenzi wa vyumba vilivyokuwa pungufu katika halmashauri hiyo. Kwa mujibu wa afisa elimu taaluma sekondari Christopher haule katika halmashauri hiyo amesema licha ya wanafunzi 1953 kufaulu vyema mtihani wa darasa la saba lakini wanafunzi 1230 ambapo wavulana wakiwa 710 na wasichana 983 pekee huku wanafunzi 463 wakikosa nafasi kutokana na upunfungufu wa vyumba tisa…

Source

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger