Friday, 4 January 2019

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA JAN,4 2019, RAMSEY KUTIMKIA JUVENTUS

Ramsey ndiye mchezaji wa sasa aliyekaa muda mrefu zaidi Arsenal, alijiunga nao 2008

Kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey, 28, ametia saini makubaliano ya awali ya mkataba na Juventus na huenda akajiunga na klabu hiyo ya Italia mwezi huu. (Sport Mediaset kupitia Calciomercato)

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Sevilla Joaquin Caparros anasema klabu hiyo huenda ikawasilisha ofa kumtaka mshambuliaji wa Chelsea ambaye zamani alichezea Real Madrid na Juventus Alvaro Morata, 26. (Football.London)


Morata angependa kurejea Madrid iwapo ataondoka Stamford Bridge lakini anaweza tu kuruhusiwa kuondoka iwapo Chelsea watampata mshambuliaji mwingine wakati wa dirisha la kuhama wachezaji la Januari. (Sun)

Hatima ya Mesut Ozil Arsenal haitaamuliwa hadi mwisho wa msimu baada ya kiungo huyo wa miaka 30 na klabu hiyo kupuuzilia mbali uwezekano wake kuhama mwezi huu. (Evening Standard)

Chelsea watafanya uamuzi kumhusu mshambuliaji Tammy Abraham kufikia 14 Januari. Mchezaji huyo wa miaka 21 yupo Aston Villa kwa mkopo lakini anaweza kuitwa kurejea klabu yake wiki mbili baada ya dirisha la kuhama wachezaji kufunguliwa kutokana na maelezo kwenye mkataba wake. (Telegraph)Tammy Abraham

Chelsea wameamua kutomfuata mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain, 31, mwezi huu. Mchezaji huyo kwa sasa yupo AC Milan kwa mkopo kutoka Juventus. (Goal)

Cesc Fabregas hatakubaliwa kukamilisha uhamisho wake kwenda Monaco hadi Chelsea wapate kiungo wa kati wa kujaza nafasi ya Mhispania huyo wa miaka 31. (Calciomercato)Cesc Fabregas

Mlinda lango wa Real Madrid Keylor Navas, 32, ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia Arsenal wiki za hivi karibuni, ameongeza muda wa mkataba wake katika klabu hiyo kwa mwaka mwingine mmoja, hadi Juni 2021. (Marca)Kipa wa Costa Rica Keylor Navas

Bayern Munich wamewasilisha ofa ya tatu ya zaidi ya £30m wakimtaka kiungo mshambuliaji wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, 18. (Sky Sports)Callum Hudson-Odoi alijiunga na Chelsea mwaka 2007

Beki wa Chelsea mzaliwa wa England Gary Cahill, 33, anakaribia kuhamia Fulham kwa mkopo. Klabu hiyo ya London magharibi imemrejesha Timothy Fosu-Mensah kwa Manchester United ili kutoa nafasi ya mchezaji mwingine ndipo waweze kumchukua Cahill. (Love Sport Radio)Gary Cahill

Crystal Palace wamewasilisha ofa ya £6.5m kumtaka mchezaji wa Everton na Senegal Oumar Niasse, 28, baada yao kushindwa kumpata mshambuliaji wa Liverpool Dominic Solanke kwa mkopo. (Sun)


Paris St-Germain wamewasilisha ofa ambayo haiwezi kufikiwa na Barcelona kumtaka kiungo wa kati Frenkie de Jong, 21, na beki wa kati Matthijs de Ligt, 19, kutoka Ajax. (Marca)

Leicester wamepokea ofa kutoka kwa Villarreal ya Uhispania wanaomtaka Vicente Iborra, lakini klabu hizo bado hazijakamilisha mazungumzo kuhusu uhamisho wa Mhispania huyo mwenye miaka 30. (Leicester Mercury)nNathaniel Clyne

Chelsea wanapanga kutoa £36m kumtaka winga wa PSV Hirving Lozano, 23, anayetokea Mexico. (Calciomercato, kupitia Talksport)

Cardiff na Bournemouth wote wanamtaka beki wa Liverpool Nathaniel Clyne. Bournemouth wanamtaka mkabaji huyo wa miaka 27 kwa mkopo kwa kipindi kilichosalia cha msimu. (Mail)

Kiungo wa kati wa Liverpool Adam Lallana, 30, anatafutwa na klabu ya Fenerbahce ya Uturuki mwezi huu. (Caught Offside)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amekataa kufutilia mbali uwezekano wa kiungo wa kati wa Ubeligji Mousa Dembele, 31, kuihama klabu hiyo mwezi huu. (Football.London)

Pamoja na Dembele, Tottenham wanataka kuwauza pia Fernando Llorente, 33, Vincent Janssen, 24, Georges-Kevin Nkoudou, 23, na Victor Wanyama, 27. (Mirror)Victor Wanyama

Nottingham Forest wamehusishwa na kumnunua winga wa Portsmouth Jamal Lowe, 24. (Nottingham Post)

Meneja wa zamani wa Birmingham na Derby Gary Rowett huenda akalazimika kuzuia kushindwa mechi ya Kombe la FA ugenini Shrewsbury Jumamosi ili kunusuru kazi yake kama meneja wa Stoke. (Telegraph)
Share:

NewAUDIO-SAIDA KAROLI-MAGENYI

Msanii Saida Karoli anakukaribisha kuusikiliza wimbo wake mpya uitwao Magenyi. 
Sikiliza wimbo huo hapa chini
Share:

KATIBU MKUU CCM ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA BABA WA TAIFA J.K NYERERE


Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally amepokelewa Mkoa wa Mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera
Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally atafanya ziara ya siku mbili kuimarisha Chama Mkoa wa Mara ikiwa ni pamoja na kutembelea Wilaya ya Butiama alikozikwa mwasisi wetu Mwl. Julius kambarage Nyerere

Aidha, Ndg. Bashiru Ally amesema katika ziara yake hii ni kukijenga chama nakukiimarisha katika Misingi iliyowekwa na Mwasisi wetu Mwl.Nyerere

Ndg. Bashiru Ally ameyasema hayo Mbele ya wananchi na viongozi wa Chama na serikali wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Mkoa Ndg. Samweli Kiboye wakikagua kituo cha Afya jimbo la Bunda

Katika ziara hiyo ameshiriki kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Butiama.

Katika kikao hicho Dkt.Bashiru Ally ametoa salamu za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mh. John Pombe Magufuli kwa wana Mara na kuwambia anawahakikishia kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Mkoa na Uwanja wa ndege wa kisasa Musoma itatekelezwa.

Katibu Mkuu wa CCM amehitimisha kikao hicho kwa kusisitiza Umoja kwa watumishi wa Chama na Serikali, kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaendeleza misingi iliyo asisiwa na Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Share:

WAZIRI MKUU AFUNGUA SOKO LA MAZAO SONGEA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefungua mradi wa maghala ya kuhifadhi nafaka na soko la mazao la OTC-Lilambo katika Halmashauri ya Songea uliogharimu sh. bilioni 1.5.

Amesema Rais Dkt. John Magufuli ameazimia kuwawezesha wakulima kuwa na mahala pa uhakika pa kuhifadhia mazao yao na sehemu ya kufanyia biashara ili kuwaongezea tija.

Amefungua soko hilo jana (Alhamisi, Januari 3, 2019) akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku nne ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani Ruvuma.

Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na ujenzi wa soko hilo pamoja na maghala kwani umezingatia viwango. Maghala hayo mawili yana uwezo wa kuhifadhi tani 5,000 za nafaka.

“Licha ya soko hili kuwapa wakulima wetu fursa ya kupata masoko ya kuuzia mazao yao, pia watapata mafunzo ya namna ya kuhifadhi bidhaa zao pamoja na taarifa za masoko.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ameiagiza bodi ya soko hilo kuhakikisha inatoa matangazo katika vyombo mbalimbali vya habari ili wakulima waweze kupeleka mazao yao sokoni hapo.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewataka wananchi kutumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha nchini kuandaa mashamba, kupanda mazao mbalimbali ya chakula na biashara.

“Nawaagiza viongozi wa kata na vijiji hakikisheni wananchi katika maeneo yenu wanaandaa mashamba na kupanda kwa wakati, tunataka tuwe na chakula cha kutosha na ziada tuuze.”

Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Songea, Martin Mtani ameiomba Serikali iwapatie mashine itakayowawezesha kupanga madaraja ya mazao ya nafaka mbalimbali.

Mkurugenzi huyo ameomba soko hilo liwekwe kwenye mpango wa kujengewa vihenge vyenye uwezo wa kukausha mazao kwa viwango vya kimataifa ili kutatua tatizo la unyaufu.

Pia Mkurugenzi huyo ameiomba Serikali iwasaidie katika kuliunganisha soko hilo na TMX ili waweze kuuza mazao ya nafaka ndani na nje ya nchi .

Ufunguzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenister Mhagama na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga.

Wengine ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme na maafisa wengine wa Serikali.
Share:

VideoMPYA: PATORANKING -EVERYDAY

Msanii kutoka Nigeria Patoranking amefungua Mwaka 2019 kwa kuachia wimbo wake mpya unaitwa “EVERYDAY
tazama hapa chini


Share:

SOMA MAGAZETI YA LEO 04/01/2019.

Share:

WAFANYAKAZI DAR ES SALAAM WAMPONGEZA RAIS KUFUATIA KUFUTWA KWA KIKOKOTOO.

Na.Mwandishi wetu. Wafanyakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam jana wameandamana katika maandamano ya amani ya Kumpongeza Rais Magufuli kuhusiana na kusitisha kanuni mpya ya sheria ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Maandamano hayo yaliandaliwa na Shirikisho La Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA)yalipokelewa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva . Akizungumza katika sherehe hizo za Wafanyakazi wa mkoa huo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva alizitaka Halmashauri za Mkoa Dar es Salaam zote Watumishi watumie Walaka kwa ajili ya kuwahudumia…

Source

Share:

LIVERPOOL YAKUBALI YAISHE,YAGONGWA 2 - 1 NA MAN CITY


Liverpool imekubali kupoteza mchezo uliopigwa usiku huu dhidi ya Manchester City kwa kufungwa bao 2-1.

Mabao ya City yamewekwa kimiani na Sergio Kun Arguero na Leroy Sane huku Liverpool ikifuta machozi kupitia kwa Roberto Firmino.

Ushindi huo wa Liverpool unakuwa wa kwanza baada ya mechi tano mfululizo katika EPL kushindwa kupata matokeo mbele ya Liverpool.

Kupoteza kwa Liverpool kumeifanya ikubali kufungwa mabao mawili msimu huu EPL ndani ya mechi moja na ikipoteza mchezo wa kwanza.

Msimamo unaonesha hivi sasa Liverpool bado ipo kileleni ikiwa na pointi 54 kwa tofauti ya alama 4 na Man City iliyo na 50.
Share:

WAAMUZI WA MCHEZO WA SIMBA NA JS SAOURA WATANGAZWA.

Na. Mwandishi wetu. Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza waamuzi watakaochezesha mechi ya Klabu Bingwa Afrika kati ya Simba na JS Saoura. Waamuzi hao ni Joshua Bondo ambaye atasimama kama mwamuzi wa kati, waamuzi wasaidizi Oamogetse Godisamang, Moemedi Godfrey Monakwane na mwamuzi wa akiba, Kutlwano Leso, wote kutoka nchini Botswana. Kamishna wa mechi ni James Leonard Mwenda kutoka nchini Malawi, msimamizi mkuu wa mchezo huo ni Alexander Sakyi Asante kutoka nchini Ghana. Simba itawakaribisha JS Saoura katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya makundi ambao utapigwa Januari 12 Jijini Dar…

Source

Share:

Thursday, 3 January 2019

WATOTO WAOKOTWA UFUKWENI MTWARA WAKIWA WAMEFARIKI.

  Watoto wawili wakazi wa kijiji cha Mgao, Mkoni Mtwara wameokotwa wakiwa wamefariki Dunia pembezoni mwa mwambao wa Bahari ya Hindi. Uchunguzi wa Daktari imebainisha kuwa vifo hivyo vimetokana na watoto hao kukosa hewa baada ya kuzama kwenye maji. Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Blasius Chatanda amesema hii leo kuwa, tukio hilo la kuzama majini limetokea Januari Mosi katika kijiji cha Mgao ambapo uchunguzi wa awali unaonesha watoto hao hawakuwa na wasimamizi walipokwenda kuogelea. “Watoto hao tumeweza kuwatambua, wa kwanza alikuwa anaitwa Rajab Athman mwenye…

Source

Share:

MHE. MABULA AFADHILI VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA SH. 6 MILIONI KOMBE LA MHANDU.

Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula hivi leo amekabidhi Vifaa Vya michezo vikiwemo Jezi, Mipira pamoja na Vitini Vya waamuzi vyenye thamani ya shilingi 6,000,000 kwa vikosi 11 kutoa Mitaa 11 ya Kata ya Mhandu vitakavyoshiriki michuano Kombe la Mhandu lililoandaliwa na Diwani Kata ya Mhandu Mhe. Constantine Sima litakalo anza mnamo tarehe 05.01.2019. Mhe. Mabula akikabidhi Vifaa hivyo amewaasa wana Mhandu kutumia michuano hiyo kama fursa ya kufahamiana vyema na kuwa na umoja katika kuijenga Mhandu, sanjari uibuaji wa Vipaji itakayochochea Mpira wa mguu kuwa ajira na msingi…

Source

Share:

MZEE MWINGINE ATENGENEZA HISTORIA TANZANIA AGUSA 2019 MIAKA 140

Na mwandishi wetu Mufindi Ni hali isiyo kuwa ya kawaida kwa binadamu kufika umri mrefu akiwa hai, lakini leo linathibitika kwa mara nyingine Nchini Tanzania katika kitongoji cha Ing’enyango nje kidogo ya kijiji cha Kilosa wilayani Mufindi mkoani Iringa kilomita 70 kutoka mji wa Mafinga ambapo mtandao huu umempata Mzee  Silyamgoda Kalinga mwenye umri wa miaka 140 huku akiitaka jamii kuwaenzi wazee wenye umri mkubwa na kuhitaji msaada kutokana na umri alio nao. Akizungumza na mtandao huu mtoto wa mzee huyo bwana PaskalKalinga amesema kuwa mzee wake alizaliwa mwaka 1879…

Source

Share:

WAFANYAKAZI WAANDAMANA KISA MAGUFULI


Wafanyakazi wakiwa wameshika mabango yenye maneno ya kumpongeza Rais, Magufuli.

Wafanyakazi jijini Dar es salaam wameandamana kwa lengo la kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa uamuzi wake wa kufuta kikokotoo kipya cha mifuko ya hifadhi za jamii na kurejesha cha zamani.

Maandamano hayo yamefanyika leo, Januari 3,2019 ambapo yameanzia ofisi za Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Mnazi Mmoja jijini humo hadi viwanja vya Mnazi Mmoja wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kumpongeza Rais Magufuli, yamepokewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva.

Akizungumza na waandamanaji hao, Lyaviva ametoa rai kwa wafanyakazi wa umma nchini kufanya kazi kwa uadilifu na kuwahudumia wananchi bila upendeleo. Amesema wapo baadhi ya watumishi wa serikali wanaochelewesha huduma kwa wananchi kwa makusudi hali inayosababisha malalamiko.

“Zingatieni nidhamu ya utumishi na utendaji, bahati nzuri kila taasisi ina mfumo wake wa utendaji kazi zingatieni hiyo mifumo, furaha hii ya kikokotoo haimanishi mjisahau katika kuwahudumia wananchi,” amesema.

Akizungumzia kuhusu tamko la Rais Magufuli la kusitisha kikokotoo walichokiita kandamizi amesema uamuzi huo uwe chachu ndani ya mioyo ya wafanyakazi hao kwa kufanya kazi kwa bidii na kujituma zaidi.

Akisoma risala iliyoandaliwa na wafanyakazi hao, Katibu wa kamati za wanawake wa TUCTA, Jenijely James amesema kikokotoo hicho kilichorejeshwa kina mafao bora katika sekta ya umma.

Desema 28, 2018, Rais Magufuli alikutana na TUCTA, viongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na wadau wengine Ikulu jijini Dar es salaam na kusitisha kikokotoo kipya na kurudisha cha zamani ambacho kitatumika hadi 2023.
Chanzo - EATV
Share:

HAWA NDIYO WAAMUZI MCHEZO WA SIMBA NA JS SAOURA


Wachezaji wa Simba na JS Saoura

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza waamuzi watakaochezesha mechi ya Klabu Bingwa Afrika kati ya Simba na JS Saoura. 

Waamuzi hao ni Joshua Bondo ambaye atasimama kama mwamuzi wa kati, waamuzi wasaidizi Oamogetse Godisamang, Moemedi Godfrey Monakwane na mwamuzi wa akiba, Kutlwano Leso, wote kutoka nchini Botswana.

Kamishna wa mechi ni James Leonard Mwenda kutoka nchini Malawi, msimamizi mkuu wa mchezo huo ni Alexander Sakyi Asante kutoka nchini Ghana.

Simba itawakaribisha JS Saoura katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya makundi ambao utapigwa Januari 12 Jijini Dar es salaam.

Ikumbukwe Simba ipo katika kundi D pamoja na vigogo wawili ambao ni Al Ahly ya Misri na AS Vita Club ya Congo DRC pamoja na JS Saoura ya Algeria ambayo haina uzoefu mkubwa katika michuano hiyo.
Share:

WAKATI MBOWE NA MATIKO WAKISOTA GEREZANI,PROFESA SAFARI AISHANGAA SERIKALI

  Wakati Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wakiendelea kusota mahabusu yapata mwezi mmoja na nusu sasa, Wakili anyewatetea Profesa Abdallah Safari amehoji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusu rufaa iliyokatwa na upande wa mashtaka katika Mahakama ya Rufani. Mbowe na Matiko wanasota mahabusu baada ya Mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana yao November 26,2018 kwa kukiuka masharti ya dhamana, ambapo waliamua kukata rufaa Mahakama Kuu lakini iliwekewa pingamizi baada ya upande wa mashtaka kukata rufaa Mahakama ya Rufani. Profesa Safari alihoji swali moja…

Source

Share:

JUMLA YA MASHAURI 118 YAMEPOKELEWA NA MAHAKAMA YA WATOTO KISUTU NA KUFANYIWA KAZI 2018

Mahakama ya watoto ya Kisutu imepokea jumla ya mashauri 118 ya jinai na makosa 295 ya madai yalipokelewa na kufanyiwa kazi kwa mwaka 2018. Hayo yamebainishwa na hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu Bi. Agness Mchome wakati akimpa maelezo katibu mkuu wizara ya Afya ,maendeleo ya jamii,Jinsia,wazee na watoto  idara kuu maendeleo ya jamii Dkt John Jingu alipotembea mahakama ya watoto kisutu. Hakimu Mchome amewataka wazazi kutimiza wajibu wao wa malezi kwa watoto ili kuwaepusha na mashitaka yanayozuilika kwani watoto wengi wanaofikishwa mahakamani hapo ni wale ambao wazazi…

Source

Share:

BINTI AJINYONGA KISA KAZUIWA KWENDA KWENYE MKESHA WA MWAKA MPYA


Mwaka Mpya wa 2019 umeanza na visa vya watu wawili wilayani Tarime mkoani Mara kufariki dunia kwa nyakati tofauti akiwemo msichana mkazi wa Mtaa wa Nkende, Elizabeth Magige (14) aliyejinyonga kwa kamba kwa madai ya kuzuiliwa na bibi yake kwenda kwenye sherehe za Mwaka Mpya.

Aidha, mkazi wa Kijiji cha Kembwi, Kata ya Manga Tarafa ya Inano, Mariba Nyaronyo (59) amefariki duniani kwa kunywa pombe haramu ya gongo kupita kiasi. Polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya na madiwani wa kata hizo mbili, walithibitisha vifo vya wananchi wao hao kwa sababu hizo tajwa.

Diwani wa Kata ya Nkende, Daniel Komote alisema “Tukio la msichana Elizabeth Mwita Magige wa miaka 14 kujinyonga nyumbani kwao lilitokea usiku wa kuamkia Januari mosi mwaka huu ambapo kulikuwa na sherehe za disko mjini Tarime ya kuamkia mkesha wa Mwaka Mpya na kuzuiliwa kwenda kuhudhuria mkesha huo. 

“Kitendo kilichomfanya binti huyo kushikwa na hasira na hatimaye kujitia kitanzi na mwili wake kukutwa asubuhi ukiwa unaning’inia ndani ya nyumba jirani na kwa bibi yake huyo aliyemkataza kwenda disko.”

Diwani wa Kata ya Manga, Stephen Gibai alisema, “Mariba Sasi alikuwa mnywaji pombe kali aina ya gongo ambapo ilidaiwa na watu walio karibu naye marafiki zake, siku ya mkesha wa Mwaka Mpya alikunywa pombe nyingi kupita kiasi aina ya gongo kusherehekea mwaka mpya ambayo pombe hiyo ilimdhuru na kufariki dunia.”

Kamanda wa Polisi Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe alithibitisha vifo hivyo viwili.

“Matukio ya watu kujinyonga katika Kata ya Nkende yamekuwa yakijitokeza viongozi wa dini, jamii ikiwemo familia zinatakiwa kuishi kwa amani na kumcha Mwenyezi Mungu huku vijana wakihimizwa kuacha kujichukulia maamuzi mabaya ya kujitoa uhai badala yake kusikiliza maneno ya wazee ya kubadilika kuacha vitendo vya pombe na dawa za kulevya ambayo yameathiri vijana wengi ambao wamekuwa wakijiingiza kwenye vitendo viovu vikiwemo vya kujitoa uhai,” alisema Mwaibambe. 

Miili ya marehemu hao, ipo chumba cha maiti Hospitali ya Wilaya Tarime kwa uchunguzi zaidi kabla ya kuchukuliwa na ndugu zao kwa mazishi.

Samson Chacha  - Habarileo Tarime 
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger