Tuesday, 18 December 2018

VYAMA VYA UPINZANI VYAJILIPUA,VYATOA MAZIMIO HAYA YAKUPINGANA NA AGIZO LA JPM

NA KAROLI VINSENT VYAMA Sita vya Upinzani vilivyokutana Faragha kwa muda siku mbili,vimekuja na maazimio ya Mawili mazito, ikiwemo la kufanya mikutano ya Hadhara pamoja na kuwatangaza Viongozi wa Upinzani waliokuwa Gerezani kuwa ni wafungwa wa kisiasa. Maazimio hayo ambayo yanatajwa kama yakumjaribu Rais John Magufuli ,baada ya kupingana na Agizo alilotoa Rais la kuweka  utaratibu wa vyama hivyo juu ya ufanyikaji wa mikutano ya Hadhara baada ya kuelekeza waliochaguliwa na wananchi kwenye majimbo yao (Wabunge) na Madiwani (Kata) ndio wanaruhusiwa  kufanya mikutano hiyo. Mkutano huo wa Faragha ambao umeratibiwa…

Source

Share:

BEKI HUYU WA YANGA ATUMA UJUMBE HUU KUELEKEA MECHI YA AFRIKA LYON

LICHA ya Timu ya Yanga ambao ni Mabingwa historia kukumbana na sintofahamu kuhusu Kocha wa timu hiyo Mkongoman Mwinyi Zahare na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hussein Nyika ,Beki kinda wa timu hiyo, Paul Godfrey amesema wapo tayari kuvaana na African Lyon katika mchezo wao wa Ligi Kuu utakaopigwa mkoani Arusha siku ya alhamisi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Yanga wamefanikiwa kufanya vizuri kwenye michezo yao 16 waliyocheza mpaka sasa bila kupoteza hata mchezo mmoja. “Tupo sawa kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya African Lyon, hatuna mashaka kwa…

Source

Share:

SERIKALI YAMFUNGIA MSANII DIAMOND KWA MDA USIOJULIKANA,NI SIKU MOJA KUPITA BAADA YA KULIPONDA SHIRIKA LA NDEGE LA ATCL

NA mwandishi wetu NI mwaka wa shetani kwa wanamuziki Diamond Platnumz na Rayvanny ndivyo naweza kusema mara baada Baraza la Sanaa nchini (Basata) limewafungia kutojihusisha shughuli za sanaa kwa muda usiojulikana. Taarifa hii ya kufungiwa wimbo huu ,unakuja ikiwa ni siku moja kupita baada ya msanii Diamond ambaye anatwajwa kuwa na mafakikio makubwa kuirushia lawama Shirika la Ndege nchini la (ATCL) kusema linatoa huduma mbovu. Mara baada ya kutoa kauli hiyo ambayo ilileta taharuki kwa watanzania mpaka ikawafanya ATCL kupitia msemaji wake ,Josephat Kagirwa ,kuibuka na kupinga tuhuma alitoa Diamond…

Source

Share:

Picha : WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI ZANAKI WATEMBELEA HIFADHI ASILI YA MAGAMBA LUSHOTO, TANGA


Afisa Utalii wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga Samiji Mlemba (katikati) akitoa maelezo kwa wanafunzi wa Sekondari ya Zanaki jijini Dar es Salaam waliopata ufadhili wa kutembelea hifadhi hiyo waliopewa na Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kupitia mradi wa Uwezo Award uliendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la Great Hope Foundation. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG - Lushoto.

Afisa Utalii wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga Samiji Mlemba akiwa ameongozana na kuwapa maelezo wanafunzi na wanahabari waliokuwa katika ziara hiyo.
Moja ya bango linalowakaribisha wageni katika hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga na kuwapa maelezo machache.
Wanafunzi wakiendelea na safari ambayo iliwachukua saa 3 kufika katika kilele kwa km 2.2.
Wanafunzi wakifurahia katika kituo cha kwanza ambacho kilikuwa ni Chanzo cha Maji.
Pichani ni wanahabari wa vyombo mbali mbali Msungu wa ITV (kwanza kulia) na Said Makala (wa pili toka kulia) wakifurahia pamoja na maofisa wa GHF Noela na Maria wa TTB... Juu ni Mwanahabari Cathbert Kajuna -Kajunason/MMG akiwa na wanafunzi wakifurahia katika kituo cha pili ambacho ni Mshai.
Afisa Utalii wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga Samiji Mlemba akitoa maelezo machache wakati wanafunzi hao walipofika kituo cha Mshai wakielekea katika kilele cha mlima Kigulu Hakwewa.
Safari ya kuelekea katika kilele cha mlima wa Kigulu Hakwewa.
Safari ilikuwa ni ndefu ambapo wengine waliamua kupumzika ili kuweza kuvuta pumzi katika miti yenye umri wa miaka 40.
Muonekano wa miti mikubwa yenye kuvutia iliyoishi umri wa miaka 40 mpaka sasa.
Kila mmoja alikuwa na furaha kufika katika kituo cha tatu cha Kwesimu ambapo historia ya sehemu hiyo ilikuwa ni kupatikana kwa huduma za simu. Hapo ndipo mawasiliano ya simu yakipatikana yani namaanisha kila mtu mwenye simu alikuwa akifika hapo ili aweze kupata nawasiliamo (Network ilikuwa ikipatikana eneo hilo).
Eneo hilo la Kwesimu ndipo mkondo wa maji ulikuwa ukipita.
Wanafunzi wakifurahia katika mlango wa pango la Wajerumani walilolitumia katika vita vya kwanza vya dunia vilivyotokea mwaka 1914 - 1918.
Wanafunzi wakifurahia na mwalimu wao walieambatana nae katika mlango wa pango la Wajerumani walilolitumia katika vita vya kwanza vya dunia vilivyotokea mwaka 1914 - 1918.
Meneja Uhusiano wa Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) nae aliweza kupata wasaa katika lango la pango la Wajerumani lililotumika katika Vita vya kwanza vya Dunia 1914-1918.

Ndani ya pango la Wajerumani walilolitumia katika vita vya kwanza vya dunia vilivyotokea mwaka 1914 - 1918.

Wanafunzi wakifurahia na Afisa Utalii, Samiji Mlemba (katikati) wakiwa kwenye geti la kuingia kilele cha mlima Kigulu Hakwewa.

 Kilele cha Mlima Kigulu Hakwewa ambapo ni (1840 A.M.S.L) Usawa wa Juu wa Kiwango cha Bahari.
Kila mmoja akifurahia...
Makulaji kidogo!
Kila mmoja akiwa na uso wa furaha baada ya kutoka kilele cha Mlima Mgulu Hakwewa.
Baada ya wanafunzi kutembelea kilele cha mlima Kigulu Hakwewa waliweza kufika katika Msitu wa Asili wa Mkusu unaolimilikiwa na Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) ili kujionea maporomoko ya maji ya Mvueni.
Wanafunzi wakifurahia katika maporomoko ya maji ya Mvueni yaliyopo katika Msitu wa Asili wa Mkusu uliopo Lushoto, Tanga.
Maporomoko ya maji ya Mvueni yaliyopo katika Msitu wa Asili wa Mkusu uliopo Lushoto, Tanga.
Wanafunzi wakifurahia katika Maporomoko ya maji ya Mvueni.
---
Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga ni moja ya vivutio vya hifadhi 12 za mazingira asilia vinavyosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Watu wengi wamekuwa wakisahau kuwa utalii wa ikolojia nao unafaida kwa jamii yetu ili iweze kujifunza mambo mbali mbali kuhusu misitu na viumbe hai.

Wakizungumza kwa wakati tofauti mara baada ya kutembelea hifadhi ya mazingira ya Magamba, Mfaume Salehe Msasa amesema “Kuwa Coordinator wa ni bahati kwangu na furaha pia kwa kuwa nimejifunza vitu vingi sana tangia nimeaza kuvolunteer @greathopetz pia naendelea kujifunza kwamaana kuwa kujifunza hakunaga mwisho,"

Kwa kwaida kila mwaka @greathopetz hua tunatoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi pamoja na shule zinazofanya miradi bora zaidi. Mwaka huu tulikua na shule 100 ambazo zimefanya mradi na shule ambayo imefanya mradi bora zaidi nakuweza kuwa mshindi wa kwanza ni Shule ya Sekondari Zanaki. “Miradi ya mwaka huu imekua ni ya tofauti kubwa kwa mshindi wa mradi wa Uwezo Award kupata zawadi nyingi na wamepewa safari ya kitalii ya kwenda msitu wa Magamba kwa kudhaminiwa na Wakala wa huduma za misitu Tanzania na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Nae Meneja wa Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) ameshukuru jinsi wanafunzi walikuwa na moyo wa kujifunza kuhusu mazingira na kuomba shule pamoja na wazazi waweze kujitokeza kuwapeleka watoto wao katika vivutio mbali mbali vya utalii wa ikolojia ambao watu wengi wamekuwa wakiusahau.

"Unajua watu wengi wamekuwa wakikimbiali kuangalia wanyama ila huku napo ni zaidi ya kule maana wale wanaopenda kuona mazingira yanavyotunzwa basi hawana budi kufika bila kukosa, tunawakaribisha watanzania wote hasa kipindi hiki cha likizo kwa wawalete watoto wao wajionee vivutio mbali mbali mbali," amesema Tulizo Kilaga

Great Hope Foundation - GHF ni shirika lisilo la kiserikali lililojikita katika kuwasaidia vijana kutambua na Kuendelea uwezo wao katika maeneo mbalimbali. Shirika hubuni na kuendesha miradi katika muktaadha wa kuwajengea uwezo Vijana.
Share:

KILA KIJIJI KILICHOPITIWA NA MRADI WA REA KIPATE UMEME

Na Mwandishi wetu Ruvuma. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amewataka wataalam katika Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuwa makini katika kazi ya upangaji wa vijiji vinavyopaswa kupelekewa umeme kwenye wilaya zenye majimbo mawili ya uchaguzi ili kuepusha malalamiko ya kupendelea upande mmoja wa Wilaya. Aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akikagua miradi ya usambazaji umeme vijijini katika Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma ambapo Wilaya hiyo ina Jimbo la Tunduru Kusini na Tunduru Kaskazini. Naibu Waziri alitoa agizo hilo baada ya kupata malalamiko kuwa, Vijiji…

Source

Share:

MADIWANI SIMAMIENI MIRADI YA MAENDELEO ILI KUFIKIA MALENGO YA SERIKALI

Na Stephen Noel -Mpwapwa. Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wametakiwa kuweza kusimamia Halmashauri zao na kuisadia serikali kufikia Malengo yaliyo kusudiwa. Kauli Hiyo imetolewa na Kamanda wa Tasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa wilayani Mpwapwa Bi July Mtui alipo kuwa akiwasilisha Mada ya wajibu wa madiwani wa Halmashauri ya Mpwapwa dhidi ya nafasi ya madiwani Katika kupambana na Rushwa. Bi.Mtui amesema kuwa Madiwani wakiwa Kama wenye viti wa kamati za maendeleo ya Kata (WDC) wametakiwa kusimamia rasilimali, miradi ya maendeleo na ili kuepuka miradi Hiyo…

Source

Share:

MVUA YAUA WAWILI KANISANI KAHAMA, 10 WAJERUHIWA

Share:

MOURINHO 'OUT' MAN UNITED, MRITHI ATANGAZWA


Kocha Jose Mourinho amefutwa kazi na Manchester United ikiwa ni siku moja tu imepita tangu afungwe mabao 3-1 na Liverpool.
Kupitia taarifa yake leo, Man United imeeleza kuwa imefikia uamzi huo ili kunusuru mwenendo wa klabu katika michuano mbalimbali inayoshiriki ikiwemo EPL na klabu bingwa Ulaya.

"Klabu inamshukuru Jose kwa kazi yake nzuri wakati akiwa na Manchester United na tunamtakia mafanikio katika kazi yake hapo baadaye'', imeeleza taarifa ya klabu.

Kiungo wa zamani wa timu hiyo Michael Carrick ametangazwa kuchukua nafasi ya Jose Mourinho kama kocha wa muda wa Manchester United mpaka mwisho wa msimu huu wa 2018/19.

Mourinho alijiunga na Manchester United Juni 2016 akiwa kocha huru baada ya kufukuzwa na Chelsea. Amedumu na Man United kwa takribani miaka miwili na nusu.
Share:

TRA KUWASAJIRI WABADIRISHA FEDHA MIPAKANI

Na Kahinde Kamugisha , Ngara Wafanyabiashara  ya kubadilisha fedha  katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera  wameshauriwa   kujisajili na kutambulika kisha kuwa na leseni kwa mujibu wa sheria kupitia benki kuu  ya Tanzania BOT na  shirika la fedha duniani IMF. Kaimu afisa Mfawidhi wa kituo cha forodha Kabanga wilayani Ngara Seifu Mkilindi ametoa ushauri huo mbele ya  waandishi wa habari Ofisini kwake na kwamba usajili huo lazima uanze na mwenye kuwa na dola elfu  10 na kuendelea. Amesema  kwa upande wa Tanzania wanaofanya biashara ya kubadilisha fedha  ni wachache katika kituo…

Source

Share:

KERO YA USAFIRI WA MELI KUPUNGUA.

Ujio wa Meli mpya ya safari za Baharini umeleta matumaini mapya kwa wasafiri wanaofanya safari za Dar es salaam na Zanzibar Meli hiyo mpya ya Kampuni ya Sea Star, ina uwezo wa kubeba Mizigo tani 1,400 na Abiria 1,500, imewasili Bandarini Zanzibar kwa ajili ya kuongeza huduma za usafari wa Baharini katika mwambao wa Bahari ya Afrika Mashariki Hivi karibuni kumekua na ongezeko kubwa la wanaofanya safari za Baharini, hususani safari za Dar – ZNZ, ambapo awali ilikua unafika Bandarini kukata tiketi na kusafiri Siku hiyo hiyo. Hivi sasa hali…

Source

Share:

Form One Selection 2019 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2019 Lindi Region for 2019/2020 Lindi

Form One Selection 2019 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2019 Lindi Region for 2019/2020 Lindi

The List of Selected Candidates is available for each Ward Education Coordinator, Each Board’s Advertising Boards and the Office of the Regional Head Office, Check it here

Form one selection for the academic year 2019/2020 

The following students have been selected to join form one for Lindi Secondary schools for the academic year 2019/2020.

Click here to access Form One School Selection System for Lindi Schools

 

The post Form One Selection 2019 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2019 Lindi Region for 2019/2020 Lindi appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Monday, 17 December 2018

TANGAZO LA KUTEMBELEA MBUGA YA SADAN DISEMBA 24 2018

Share:

Thursday, 6 December 2018

ANGALIA NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO USINGOJE AJIRA IJE MLANGONI



               13 JOB OPORTNITIES AT SOKOINE UNIVESITY OF AGRICULTURE
                                  bofya hapa chini


                                    AJIRA


             JOB OPPORTUNITY AT SOS CHILDREN'SVILLAGES ZANZIBAR PROGRAM  COORDINATOR
                             Bofya hapa chini
    
                                    AJIRA


        
                JOB OPPORTUNITY AT BRITAM, BRANCH MANAGER
                                  bofya hapa chini
                                   
                                 AJIRA




                

                                           
                          










Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA VYIO VYA UFUNDI VETA 2019


The Vocational Educational and Training Authority (VETA) was established by an Act of Parliament No. 1 of 1994 charged with broad tasks of coordinating, regulating, financing, Promoting and providing vocational education and training in Tanzania. The history of VETA dates back to 1940 when the Apprenticeship Ordinance was enacted to guide training in the industry. The Vocational Training Act of 1974, which established the National Vocational Training Division was replaced by the Vocational Educational and Training Act. of 1994. 

Mission: To ensure provision of quality Vocational Education and Training that meets labour market needs, through effective regulation, coordination, financing, and promotion, in collaboration with stakeholders”.
Vision: An excellent Vocational Education and Training system that is capable of supporting national social economic development in a global context”. 

VETA: APPLICANTS SELECTION RESULTS 2019 INTAKE
When you see your name, please go to your centre of study to collect your JOINING INSTRUCTION and payment procedures
Please CLICK HERE to view centre address and location.
To view the selection Results click the link below:  

Kuyaona majina halo bonyeza hapo>>>>> Majina ya waliochaguliwa kujiunga na vyuo vinavyomilikiwa na VETA
Share:

Thursday, 30 August 2018

UTATA WATAWALA KIFO CHA MTAWA BUGANDO...MAPYA YAIBUKA

Suala kifo cha Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando (BMC), Mtawa Suzan Bartholomew, limechukua sura mpya baada ya taarifa kusambazwa zikieleza huenda aliuawa.

Juzi, baada ya taarifa kwamba Mtawa huyo alijiua kwa kujirusha kutoka ghorofa ya pili kusambaa, kwenye mitandao ya jamii ulianza kusambaa ujumbe uliokuwa ukieleza kuna uwezekano mtawa huyo aliuawa na kwamba huenda alisukumwa na mtu au watu ambao hawajajulikana.

Akizungumzia suala hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna, alisema jana kuwa ameusoma ujumbe huo na kuufanyia kazi.

Alisema ujumbe huo hauna ukweli wowote kwa kuwa vipo vielelezo vingi ukiwamo ushahidi wa maandalizi ya mtawa huyo kujiua.

Kamanda Shanna alisema kabla ya kujirusha, Mtawa huyo alifungasha vitu vyake katika nyumba aliyokuwa akikaa ikiwa ni pamoja na kumkabidhi mmoja wa ndugu zake gari lake na picha zake na baba yake mzazi akimueleza kuwa anakwenda eneo asilolijua.

“Kwenye uchunguzi kuna mambo mengi, picha ya kamera ya CCTV po wazi, inamuonesha mtawa huyo akiwa anapanda ngazi kwenda eneo husika na alipojirusha kuna baadhi ya wafanyakazi wengine na wagonjwa ambao walimuona hivyo hakuna taarifa za kusukumwa wala kurushwa.

“Kabla ya tukio hilo Mtawa huyo alijiandaa na kufunga vitu vyake, aligawa baadhi ya vitu kwa watu ikiwa ni pamoja na kumpatia gari mmoja wa ndugu zake na picha zake na wazazi wake.

“… aliziondoa line za simu zake kutoka ndani ya simu na kuweka simu juu ya kiyoyozi eneo ambalo alijirusha,” alifafanua.

Kamanda Shanna alisema yeye binafsi alitembelea eneo alikojirusha Mtawa huyo na kupata maelezo kwa watu mbalimbali.

Alisema aliyesambaza ujumbe kuwa Mtawa huyo kuuawa alikuwa na lengo ambalo litashindana na ushahidi na polisi wanaendelea kuchapa kazi kwa kuwa ukweli wote umebainika.

Mtawa huyo anadaiwa kujirusha usiku wa kuamkia Agosti 27, mwaka huu na kuokotwa.

Alilazwa katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) na kuendelea kupatiwa matibabu lakini alifariki dunia usiku wa Agosti 28, mwaka huu wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Wizi wa fedha ulivyotokea:

Habari za ndani zilizopatikana zimedai kuwa Mtawa huyo akiwa mkuu wa kitengo cha fedha katika Hopsitali ya Rufaa Bugando, alikuwa amesimishwa kazi ikiwa ni pamoja na kushushwa cheo na bodi ya hospitali hiyo kutokana na kubainika upotevu wa Sh milioni 380.

Kwa mujibu wa uchunguzi, fedha zilizotoweka ni zile ambazo zilikuwa hazilipiwi katika mfumo wa benki ikiwa ni pamoja na sehemu ya fedha zilizokuwa zikilipwa benki moja kwa moja ambazo zilikuwa zikiinigizwa katika akaunti tofauti na kiasi kingine kikidaiwa kutoroshwa kwa njia ya mtandao.

“Wizi huu wa zaidi ya Sh milioni 300 ni wa kipindi cha miezi miwili tu hivyo ulipogundulika uongozi ulilazimika kufanya ukaguzi maalum.

“Lakini ukaguzi huo ulionyesha kulikuwa na wizi hivyo jukumu la kufuatilia likikabidhiwa kwa maofisa wa Benki ya CRDB, watalaamu wa mtandao, polisi kitengo cha fraud (udanganyifu) na Takukuru.

“Wiki mbili zilizopita baada ya kubainika hali hiyo uongozi wa hospitali ulitutangazia kusimamishwa kazi kwa Mtawa huyo ikiwa ni pamoja na kushushwa cheo.

“Hivyo alitakiwa kukabidhi ofisi lakini alikabidhi na baadhi ya vitu na siku ya kukabidhi ofisi hakutokea na hakuwapo nyumbani na ofisini hakufika mpaka siku iliyofuata ambako alikabidhi na siku moja baadaye kutokoea tukio hilo,” alieleza mtoa taarifa.

Akizungumzia kifo hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Bugando (BMC), Dk. Abel Makubi alisema hajabahatika kuona ujumbe ambao umesambazwa katika mitandao ya jamii.

Hata hivyo baada ya kutumiwa na kuusoma alisema anachoamini ni kwamba ujumbe huo umeandaliwa na mmoja wa watu ambao walikuwa na nia ya kutaka kuvuruga upelelezi unaondelea.

“Sikua nimeusoma ujumbe huo, lakini kwa jinsi ulivyonisomea, nauona kama ujumbe huu una lengo fulani.

“Kwanza muandikaji amejificha kwa kutaka kuaminisha yupo ndani ya polisi na anaongea kama polisi, lakini unaona anataka kuhamisha tatizo lionekane kuwa kauawa na ananijua mkurugenzi… hebu tuwaachie polisi wafanye uchunguzi wa haya, hata juu ya ujumbe huu,” alisema.

Alikizungumzia suala la kamera za usalama hospitalini hapo, alieleza kuwa zipo lakini kutokana na ukubwa wa jengo hilo hazijawekwa jengo lote kwa asilimia 100 isipokuwa katika maeneo muhimu na yale ya njia za wanaoingia na kutoka.

“Kweli kuna kamera (CCTV camera), lakini hazitoshelezi jengo zima la hospitali, hivyo siyo rahisi kwa jengo lote kuwa nazo,” alisema.
Chanzo - Mtanzania
Share:

Friday, 13 July 2018

HAYA HAPA MATOKEO KIDTO CHA SITA 2018(ACSEE RESULTS 2018)

MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA ACSEE 2018 NA MITIHANI YA UALIMU 2018 YAMETANGAZWA

Link 1: CLICK HERE TO SEE  FORM SIX RESULTS 2018(ACSEE)

LINK 2: CLICK HERE
LINK 3: CLICK HERE

Link 2: CLICK HERE TO SEE THE TEACHERS COLLEGES RESULTS (MATOKEO UALIMU 2018)
Share:

Saturday, 16 June 2018

PDF:SELECTION KIDATO CHA 5 NA VYUO VYA UFUNDI 2018/2019

Tamisemi imetangaza rasmi majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano 2018/2019.

Kama kawaida yetu MASWAYETU BLOG hua hatupendi upate shida ya kuangalia majina.

Tunatoa huduma ya kuangalizia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kwa gharama ya tshs 1000 tu kwa jina moja

ili uangaliziwe shule unayokwenda,

1.tuma jina lako na shule utokayo kwenda namba 0768260834

2.tuma pesa kwenda namba 0768260834

3.utajibiwa ndani ya dk 1 tu baada yakutuma pesa

kuona majina hayo bonyeza hapo chini,

KUYAONA MAJINA HAYO (PDF) BONYEZA HAPO>>>>>https://drive.google.com/file/d/0B8PPfYFKgrYJMjlTZGttZ19ZdVNCbDRnZ01ieEVvTUgzdC1F/view
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger