MWANANCHI “Anakatwa, hakatwi” ndilo swali lililokuwa
linaulizwa nchi nzima jana, lakini hatimaye Kamati Kuu ya CCM
iliyokutana hadi usiku wa manane iliibuka na jibu kwamba Edward Lowassa amekatwa, huku kukiwa na wingu zito baada ya wajumbe watatu kupingana na uamuzi huo.