Thursday, 10 July 2014

HIZI NDO SABABU ZA MUME KUMCHINJA MKEWE,KUBWA NI KUTOKANA NA "WIVU WA MAPENZI"

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linamsaka kwa udi na uvumba, muuza nyama jijini hapa, Lucas Lomayany Molel (37) mkazi wa Ilboru kwa madai ya kumuua mkewe wa ndoa, Agnes Lucas (24) kwa kumcharanga na sime kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.
Share:

KOMBE LA DUNIA:HATIMAE FAINALI NI GERMANY(TEAM MULLER) VS ARGENTINA(TEAM MESSI)

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Kipa wa Argentina Sergio Romero alikuwa Nyota wa mechi hiyo
Argentina imejukatia tikiti ya kufuzu kwa fainali yake ya kwanza tangu mwaka wa 1990 ambapo itachuana Ujerumani.
Argentina ilikuwa imetoka sare tasa baada ya muda wa kawaida na ule wa Ziada na hivyo kulazimu mechi hiyo kuamulia kwa mikwaju ya penalti.
Kipa wa Argentina Sergio Romero ndiye aliyekuwa nyota katika mechi hiyo baada ya kuokoa mikwaju miwili na kuipa Argentina Ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Uholanzi.
Share:

BABA KANUMBA AMCHANA MKEWE,AMWAMBIA AACHE NJAA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
“Namshangaa mama Kanumba…
BABA wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba ameibuka na kumtaka mama Kanumba, Flora Mtegoa kuacha tabia ya kuombaomba michango mbalimbali.
Share:

40 YA MSANII TYSON MAMA AKE AUGUA GHAFLA,SOMA HAPA NINI KIMETOKEA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Na Mwandishi Wetu
WAKATI jana, Julai 9, 2014 George Otieno Okumu ‘Tyson ametimiza siku 40 tangu kifo chake kilichotokea kwa ajali mbaya ya gari mkoani Dodoma, mama mzazi wa marehemu, Gladys Okumu ameripotiwa kuugua ghafla nchini Kenya anakoishi.
Share:

DIAMOND PLATNUM AMLIZA MAMA AKE MZAZI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Stori: Waandishi Wetu
STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amefanya tukio la kihistoria kiasi cha kumliza mama yake mzazi, Sanura Kassim ambaye alimwaga machozi kama mtoto mbele za watu.
Tukio la mama Diamond kumwaga machozi lilishuhudiwa na kamera za Amani, juzi Jumatatu, mishale ya saa mbili usiku nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na ‘bethidei’ ya mama huyo.
Share:

SEKREATIETI YA AJIRA:MATOKEO YA MCHUJO ULIOFANYIKA TAREHE 8 JULAI 2014

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
        MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO WA TAREHE 8
                                      JULAI 2014



EXAMINATION RESULTS FOR RESEARCH ASSISTANTNCC
Usaili wa mahojiano utafanyika tarehe 9/7/2014 SAA MOJA KAMILI ASUBUHI. 
katika OFISI ZA NATIONAL CONSTRUCTION COUNCIL (NCC)
NB: WASAILIWA WANATAKIWA KUZINGATIA MUDA NA SEHEMU ILIYOTAJWA KWA AJILI YA USAILI NA KUJA NA VYETI HALISI (ORIGINAL CERTIFICATES).
Na.    EXAMINATION NUMBER      SCORE   REMARKS
1       PSRS RESE ASS NCC - 121         80     SELECTED
2       PSRS RESE ASS NCC - 118         73     SELECTED
3       PSRS RESE ASS NCC - 124         73     SELECTED
4       PSRS RESE ASS NCC - 128         66     SELECTED
Share:

Wednesday, 9 July 2014

WANAFUNZI MKOANI MBEYA WAANDAMANA HADI KWA MKUU WA MKOA KWA KUKOSA NAFASI KIDATO CHA TANO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

WAHITIMU 39 wa kidato cha nne mwaka jana katika Shule ya Sekondari Karobe jijini hapa wakiwa na wazazi wao, jana waliandamana hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa ili kujua hatma yao baada Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kushindwa kuwapangia nafasi za kujiunga kidato cha tano licha ya kufanya vizuri katika mitihani yao.
Share:

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AFUNGUA BWENI LA WASICHANA-NAMTUMBO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Kiongozi wa mbio za mwenge RACHEL KASSANDA
Kiongozi wa mbio za mwenge RACHEL KASSANDA, amefungua bweni la wasichana la shule ya sekondari MSINDO na kuweka jiwe la Msingi katika majengo ya vyumba vinne vya madarasa na Maabara moja katika shule ya Sekondari RWINGA wilayani NAMTUMBO mkoani RUVUMA.
Share:

MASHABIKI WA BRAZIL WACHOMA BASI MOTO BAADA YA KIPIGO CHA 7-1

Basi lililochomwa na mashabiki wa Brazil waliokuwa na hasira likiteketea kwa moto.
Share:

WANAFUNZI WAFUNGWA JELA MIAKA 6 KWA MAUAJI YA MWALIMU WAO MKOANI SINGIDA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Vijana wawili waliokuwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chemchem wilayani Mkalama katika Mkoa wa Singida, wamehukumiwa kifungo cha miaka sita kila mmoja baada ya Mahakama kuwatia hatiani kwa kosa la mauaji ya mwalimu wao.
Share:

UJERUMANI YAWEKA HISTORIA:NI BAADA YA KUIFUNGA BRAZIL GOLI 7-1 NUSU FAINALI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
André Horst Schürrle (katikati) akifurahia na wachezaji wenzake wa Ujerumani baada ya kufunga bao la saba dhidi ya Brazil.
Share:

MASTAA WA BONGO MOVE WASUSA 40 YA JAPANESE

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Stori: Mwandishi wetu
MWANAMUZIKI aliyefariki dunia, Amina Ngaluma maarufu kama Japanese alifikisha siku 40 tokea azikwe Jumamosi iliyopita, lakini katika kisomo kilichosomwa nyumbani kwao Kitunda, hakuna staa yoyote wa muziki wa dansi aliyehudhuria.
Share:

WASANII Masogange, Wema, AuntEzekiel,Nagris, Hamisa, Dj Fetty Wakiwa Ndani Ya Hijabu Angalia Picha Zao

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Share:

MCHEZAJI WA UJERUMANI MIROSLAV KLOSE AWEKA HISTORIA KOMBE LA DUNIA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Miroslav Josef Klose akishangilia baada ya kutupia bao la pili kwa Ujerumani usiku huu na kuvunja rekodi ya kupachika mabao.
Klose wakati akifunga bao lake la 16 katika michuano ya kombe la dunia.
Mkali wa mabao Miroslav Josef Klose.
MSHAMBULIAJI wa Ujerumani na timu ya Lazio ya Italia, Miroslav Josef Klose, ameweka historia usiku huu baada ya kutupia bao lake la 16 na kuwa mfungaji wa mabao mengi katika michuano ya Kombe la Dunia iliyoanza mwaka 1930 ambayo kwa sasa inaendelea nchini Brazil.
Klose ameifungia Ujerumani bao la pili wakati ikitoa kichapo cha mabao 7-1 dhidi ya Brazil katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2014.
Klose alifunga mabao matano katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2002 na 2006, akatupia manne huko Afrika Kusini mwaka  2010 na mpaka sasa huko Brazil tayari amefunga mabao mawili moja dhidi ya timu yake na Ghana wakati la pili dhidi ya Brazil leo.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36 amempiku mshambuliaji wa Brazil, Ronaldo Luís Nazário de Lima aliyekuwa na mabao 15.
Wachezaji wengine waliowahi kufunga mabao zaidi ya 11 kwenye michuano hiyo ni: Gerd Muller wa Ujerumani 14, Just Fontaine wa Ufaransa 13, Pele wa Brazil 12, Jurgen Klinsmann wa Ujerumani 11 na Sandor Kocsis wa Hungary 11.
Share:

Tuesday, 8 July 2014

WATU WAWILI WAMEKUFA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA MKOANI PWANI LEO HII

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Watu wawili wamekufa katika ajali ya barabarani iliyotokea leo katika kijiji cha kwang’andu kata ya mbwewe mkoani PWANI.
Share:

KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA ALGERIA VAHID HALILHODZIC AJIUZULU

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Vahid Halilhodzic
Kocha wa Algeria Vahid Halilhodzic amejiuzulu licha ya ombi la binafsi kutoka kwa rais Abdelaziz Bouteflika akimsihi asijiuzulu.
Share:

NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA-BRAZIL KUMKOSA SILVA NA NEYMAR

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Mlinzi wa Brazil Thiago Silva (Kushoto) na Mshambuliaji Neymar(kulia)
Mlinzi wa Brazil Thiago Silva hatocheza katika mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani Jumanne .

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger