INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mume
aliyejulikana kwa jina moja la Ngosha, mkazi wa Mabibo jijini Dar,
amemfumania rafiki yake aitwaye Jazira akiwa chumbani na mkewe Jack
wakiivunja amri ya sita ya Mwenyezi Mungu.Tukio
hilo lilitokea Jumanne iliyopita saa 12 alfajiri ambapo ilidaiwa kuwa
Jack alikuwa chumbani na mwanaume huyo ambaye ni mpangaji, wenzake
wakipeana maraha.
Imedaiwa
kuwa, wawili hao walikuwa wakimtegea Ngosha akitoka kwenda katika
shughuli zake, Jazira alikuwa akizama katika chumba cha rafiki yake na
kufanya mchezo wa kikubwa.











