Na Elizabeth John, NJOMBE.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi, Dk. Pindi Chana ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Njombe na mikoa mingine wanaoshiriki kwenye maadhimisho ya kilele cha Siku ya Misitu Duniani kushiriki kwenye mdahalo kuhusu Sekta ya Misitu unaoendelea kwenye viwanja vya Saba Saba mjini Njombe ili kupata elimu ya uhifadhi kutoka kwa wataalam waliobobea katika sekta hiyo.
Dk. Chana ametoa kauli hiyo leo wakati akikagua maandalizi ya Siku ya Misitu Duniani na hatimaye kuongea na washiriki wa mdahalo unaoendelea kwa siku ya tatu sasa katika viwanja hivyo mjini Njombe ikiwa ni miongoni mwa shughuli zinazoendelea.
"Ndugu zangu nawasihi kupokea heshima hii tuliyopewa na Rais wetu kipenzi, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutuletea maadhimisho haya ili yafanyike katika mkoa wa Njombe" ,amefafanua Dk. Chana.
0 comments:
Post a Comment