Friday, 7 March 2025

BUWSSA NA MIKAKATI YA KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAJI KUTOKA ASILIMIA 64 HADI 32

...


Na Deborah Lemmubi-Dodoma.

MKURUGENZI Mtendaji Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda Bi. Ester Gilyoma ameeleza Mikakati ya kupunguza Upotevu wa maji katika mjinhuo ambapo amesema mwaka 2021 upotevu ulikuwa asilimia 64 lakini kwasasa ni asilimia 32 kutokana na maboresho ya bomba chakavu na ubadilishaji wa mita goi goi.

Bi Ester ameyasema hayo mapema Leo hii Jijini Dodoma Machi 6,2025 wakati akizungumza na Wanahabari akielezea mafanikio ya Mamlaka hiyo kuelekea Maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan.

Na kuongeza kuwa upotevu wa maji wa asilimia 64 ulitokana na mtandao wa bomba chakavu uliojengwa kutoka mwaka 1972 lakini Serikali ya awamu ya sita ilitoa fedha na kufanya matengenezo ya bomba hizo pamoja na mita.

"Upotevu wa maji kwa 2021 ulikuwa wastani wa asilimia 64 kutokana na mtandao wa bomba chakavu uliojengwa kuanzia mwaka 1972,baada ya jitihada za Serikali ya awamu ya sita za kutoa fedha na kubadili bomba chakavu na mita goi goi upotevu wa maji kwasasa ni asilimia 32 na unaendelea kushuka kutokana na jitihada zinazoendelea kufanyika".

Aidha amesema kuwa tangu awamu ya sita kuingia Madarakani Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Bunda imepitishiwa
miradi ya thamani ya TShs 28,180,572,033.71 na Tshs 11,894,976,776.81 taryari zimepokelewa
na baadhi ya miradi imekamilika na mingine utekelezaji unaendelea.


Mamlaka hiyo pia imenufaisha wakazi 195,848 mwaka 2024 kati ya hao Asilimia 85 yenye sawa na wakazi 165,613 wamepata huduma ya maji ya bomba Kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Dkt samia.

Ambapo amebainisha chanzo cha maji hayo kuwa ni ziwa vikitoria ambapo kuna umbali wa kilomita 24.8 kutoka katika kijiji cha Nyabehu na uzalishwaji wake ni wastani wa mita za ujazo 2976m3 kwa siku.

Pamoja na kupambana na usafi wa mazingira kwa sasa Mamlaka ya maji safi Bunda inaujenzi wa mradi wa miundombinu ya majitaka katika eneo la Butakale ,kwa ajili ya usafi wa mazingira na mradi utakamika ndani ya mwaka huu wa fedha 2024/2025.

Vile vile Mwenyekiti wa bodi ya maji safi bunda Bwana Jushua chacha Merumbe, ameeleza kuwa hali iliyopo sasa hivi bunda ni bora kuliku hapo awali pia amesema kwa kata 13 zilizopatiwa maji zinaendelea kutumia na kufurahia huduma hiyo ambayo awali ilikuwa ni changamoto kwa wakazi wa mji wa Bunda.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger