Friday, 21 February 2025

MBUNGE WA MADABA ATEMBELEA KATA YA MKONGOTEMA, AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

...

Mbunge Joseph Kizito Mhagama akicheza ngoma iliyoandaliwa na wananchi wa kijiji cha Lutukira na Ndelenyuma
Wananchi wakimshangilia  Mbunge Joseph Kizito Mhagama
Mbunge Joseph Kizito Mhagama akisalimiana na wananchi kata ya Mkongotema

Na Regina Ndumbaro -  Madaba

Mbunge wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Joseph Kizito Mhagama, ametembelea kata ya Mkongotema kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika eneo hilo. 

Ziara hiyo imewapa wananchi nafasi ya kueleza mafanikio yaliyopatikana kupitia utekelezaji wa miradi hiyo.

Katika hotuba yake, Mbunge Mhagama ameishukuru Serikali kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 

Ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa shule, zahanati, miradi ya maji safi na salama, pamoja na usambazaji wa umeme katika vijiji mbalimbali.

Akitolea mfano wa mafanikio hayo, Mhagama amekitaja kijiji cha Lutukila kama moja ya maeneo yaliyopokea huduma hizo kwa ufanisi mkubwa. Pia, ameongeza kuwa kijiji cha Ndelenyuma hapo awali kilikuwa na changamoto kubwa, lakini kwa sasa huduma muhimu kama maji, elimu, umeme, ujenzi wa ofisi za kijiji, na miundombinu ya barabara zimeboreshwa kwa kiwango kikubwa kwa bajeti kiasi cha shilingi bilion na milioni moja na ishirini .

Mwenyekiti wa kijiji cha Ndelenyuma Stanley Ngailo amepongeza juhudi za Mbunge Mhagama kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kijiji chao. 

Ameeleza kuwa wananchi wana imani kubwa naye na wanahitaji aendelee kuwaongoza kutokana na mchango wake mkubwa katika kuwaletea maendeleo.

Wananchi wa vijiji vya Lutukila na Ndelenyuma wameeleza kuridhishwa kwao na juhudi za Mbunge wao, wakisema kuwa kupitia uongozi wake, wamepata huduma bora za elimu, maji safi na miundombinu ya barabara inayorahisisha shughuli zao za kila siku.

Katika kata ya Mkongotema, wananchi wameonyesha furaha yao kwa maendeleo yaliyopatikana. 

Wamesema kuwa hawana deni lolote kwa Mbunge wao kwani ametekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa.

Baadhi ya wananchi wameeleza kuwa wanampenda sana Mhagama na wanatamani hata kumbeba kwa furaha ili kusherehekea mafanikio hayo pamoja naye. 

Hii ni ishara ya mapenzi yao kwa Mbunge wao na kuthamini kazi anayoifanya kwa ajili ya jamii.

Kwa ujumla, ziara hii imedhihirisha jinsi Ilani ya CCM inavyotekelezwa kwa vitendo katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma zote za msingi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger