Wednesday, 29 January 2025

WANAHABARI KAGERA WANOLEWA DHIDI YA UGONJWA WA MURBURG

...



Na Mbuke Shilagi Kagera.

Waandishi wa habari wa mkoa wa kagera wamehudhuria semina ya siku moja waliopewa juu ya ugonjwa hatari wa Murburg iliyofanyika katika ukumbi wa ELCT Bukoba Manispaa.

Semina hiyo imeongozwa na mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa ambaye ameambatana na Katibu tawala wa Mkoa Bw. Steven Ndaki pamoja na viongozi na wataalamu kutoka wizara ya Afya pamoja na wadau wa Afya Unicef.

Akizungumza katika semina hiyo Mkurugenzi wa Kinga kutoka wizara ya Afya Dkt. Ntuli Kapolongwe amesema kuwa lengo ni kuhakikisha waandishi wa habari wanapata uelewa juu ya ugonjwa huo na kushirikiana kwa pamoja ambapo watasaidia kuondoa zana na imani potofu kwenye jamii kupitia vyombo vya habari.

‘’na tunaamini kama mwandishi atapata elimu na kufahamu wa kutosha juu ya ugonjwa wa Murburg basi kutakuwa hakuna taarifa maana watapata nafasi ya kuuliza na wapate elimu ili waweze kufahamu na vita hii tutaenda kuishinda kwa ufupi’’ Amesema Dkt. Ntuli.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amemtaka Mkurugenzi asisite kutoa matamko ambayo yatakuwa ya kutahadharisha watu.

Huku akiwataka watu kuachana na mazoea ya kuendele kushika marehemu au kuosha mwili wa marehemu bila kujua ugojwa ulio muua ni upi na kusema kuwa maswala yote yasiyo ya lazima na yaliyopitwa na wakati kutoyafanya.

‘’tuoshe mikutano kwa maji tiririka mara kwa mara, tutumie vitakasa mikono na tukikutana kwenye mikutano ya kukutanisha watu wengi tuvae barakoa kwasababu inaambukizwa kwa mate pia na tufate yote yanayoelekezwa na wataalamu wa afya’’

Aidha Mkuu wa Mkoa Fatma Mwassa amewataka waandishi wa habari kutumia elimu hiyo kwa weledi walioupata kuhakikisha inawafikia watu na wanaielewa.
Ikumbukwe kuwa ugonjwa wa Murburg umejirudia mara yaa pili katika Mkoa wa Kagera Nchini Tanzania ambapo mripuko wa kwanza ulitokea 2023 Machi katika Wilaya ya Bukoba Vijijini na mara ya pili mlipuko umetokea Januari 2025 katika Wilaya ya Biharamulo.

Ugonjwa wa Murburg ni homa ya virusi ambapo huambukizwa kwa kugusa majimaji ya mwili kutoka kwa mtu aliyeambukizwa au mizoga ya wanyama walioambukizwa.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, maumivu ya kichwa maumivu ya misuli, kutapika damu, kuhara damu au kutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger