Friday, 31 January 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI FEBRUARI 1, 2025

Share:

Video Mpya : MJUKUU WA MWANAMALONDE - MAITI



Hii hapa ngoma mpya ya Mjukuu wa Mwanamalonde inaitwa Maiti
Share:

Video Mpya : SHINJE ORIGINAL - LENTUMBA


Hii hapa video mpya ya Shinje Original inaitwa Lentumba
Share:

Thursday, 30 January 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 31, 2025



 
Magazeti

Share:

ATCL YATANGAZA NAFASI 59 ZA AJIRA KWA WATANZANIA


DAR ES SALAAM – Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) imetangaza nafasi 59 za ajira kwa Watanzania wenye sifa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ufanisi wa uendeshaji na kuendana na kasi ya upanuzi wa huduma zake.

Nafasi hizi zinahusisha idara mbalimbali, ikiwemo Uendeshaji wa Ndege, Upangaji wa Ratiba za Wahudumu, Mauzo na Masoko, Usaidizi wa Rampu, na Udereva, kwa lengo la kuongeza nguvu kazi inayohitajika katika kipindi hiki cha ukuaji wa ATCL.

Nafasi za ajira zilizotangazwa ni:

✈ Afisa Uendeshaji wa Ndege (5) – Wenye leseni ya Flight Dispatcher kutoka TCAA au ICAO.

✈ Afisa Upangaji wa Ratiba za Wahudumu wa Ndege (2) – Wenye Shahada na cheti cha usafiri wa anga.

✈ Madereva (37) – Wenye Cheti cha Kidato cha Nne, leseni ya daraja C1 au E, na uzoefu wa mwaka mmoja.

✈ Afisa Mauzo na Masoko Msaidizi (1)

✈ Afisa Mauzo na Masoko (2) – Wenye Shahada na cheti cha masuala ya anga, kama Cheti cha Usimamizi wa Huduma za Ndege.

✈ Msaidizi wa Rampu (12) – Wenye Cheti cha Elimu ya Sekondari na cheti cha masuala ya anga.

Hii ni fursa muhimu kwa wale wanaohitaji kuwa sehemu ya Kampuni hii inayoendelea kukua kwa kasi kwa kutanua mtandao wake wa safari za ndani na kimataifa.

Aidha, Waombaji wenye sifa watapaswa kutuma maombi kupitia link ya ajira iliyo kwenye tovuti ya ATCL:https://ift.tt/zhO7YES ndani ya siku 14 tangu kutolewa kwa tangazo hilo.
Share:

Wednesday, 29 January 2025

ELIMU YA URAIA, UTAWALA BORA YAWAFIKIA NEWALA




Na Mwandishi Maalum, MTWARA

Mkoa wa Mtwara unatarajiwa kuwa na mafanikio makubwa kupitia mafunzo ya Elimu ya Uraia na Utawala Bora yanayoendelea kutolewa kwa menejmenti za Wilaya,kamati za usalama za wilaya ya Newala na watendaji wa kata.

Leo January 29 ,2025 Mafunzo hayo yameendeshwa kwa kujumuisha Halmashauri ya Wilaya ya Mji Newala na Halmashauri ya Wilaya ya Newala,lengo likiwa ni kuimarisha ufanisi katika utendaji wa viongozi na watendaji wa serikali.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo ,Wakili wa Serikali Mkuu na Mratibu wa Mafunzo ya Elimu ya Uraia na Utawala Bora kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Prosper Alexander Kisinini, amesisitiza kwamba lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo viongozi na watendaji ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Ameeleza kuwa ni muhimu kwa viongozi hao kukumbushana mara kwa mara kuhusu majukumu yao, ili kuongeza umakini na ufanisi katika utendaji wao.

Kisinini ameeleza matarajio ya Wizara kuwa baada ya mafunzo haya, viongozi hao wataweza kuzingatia haki za binadamu na utawala bora, huku masuala ya ulinzi na usalama yakipewa kipaumbele katika jamii.

"Huu ni mwanzo wa kujenga nchi salama kupitia kuongeza uzingatiaji wa masuala ya haki na usalama,Wizara ya Katiba na Sheria ina matumaini makubwa na mafanikio ya mafunzo haya," amesema.

Aidha, ametumia nafasi hiyo kuwashukuru viongozi wa Mkoa wa Mtwara, wakiwemo Mkurugenzi na Mkuu wa Mkoa, kwa msaada wao mkubwa katika kuhakikisha kwamba mafunzo hayo yanaenda vizuri bila changamoto yoyote.
Kisinini amethibitisha kuwa ushirikiano huo umeleta mafanikio kwa kiwango kikubwa.

Kwa upande wa washiriki, Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Mkunya, Bashiru Panali, ameonesha imani yake kwa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan na kuiomba Wizara hiyo kuendelea kutoa mafunzo hayo mara kwa mara ili kuongeza ufanisi katika kazi za utendaji na kuboresha huduma kwa Watanzania.

Panali amesema, "Mafunzo haya yanatufundisha kuhusu majukumu yetu na kutufanya tuwe na umakini zaidi katika utendaji wetu."
Naye Kassim Salim Butindwa, mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, ameeleza kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kutambua na kuboresha majukumu yao katika majukumu yao ya kila siku.

Amesema kuwa ni imani yake kuwa mafunzo yataleta mafanikio na mabadiliko chanya katika utendaji wa Serikali katika wilaya ya Newala.

Pamoja na mambo mengine Mafunzo hayo yanatoa matumaini kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara na Wilaya zake kwa ujumla ambapo viongozi na watendaji wa serikali wanatarajiwa kutumia elimu waliyoipata kuboresha utawala bora, haki za binadamu, na usalama katika jamii.













Share:

WATUMISHI THBUB WATAKIWA KUTUMIA MIKUTANO YA BARAZA LA WAFANYAKAZI KUJADILI MAMBO YANAYOLETA TIJA



Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) wametakiwa kutumia mikutano ya Baraza la wafanyakazi kujadili mambo yanayoleta tija katika kuongeza ufanisi wa kazi. 

Kauli hiyo imetolewa Januari 28, 2025 na Afisa Elimu Kazi Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Bi. Tulia Msemwa wakati wa kikao cha kuchagua Wajumbe Wapya  wa Baraza la wafanyakazi la THBUB baada ya wajumbe waliokuwepo kumaliza muda wao.

Bi. Msemwa amesema kuwa Baraza la Wafanyakazi  ni sehemu sahihi ya kujadili, kushauri na kutoa mapendekezo juu ya njia sahihi ya kuongeza ufanisi wa kazi  utakaosaidia kuweka mazingira mazuri kwa Wafanyakazi na Taasisi kwa ujumla.

“hivyo niwaombe wajumbe mtakaochaguliwa hakikisheni mnatumia vyema nafasi hiyo kwa kujadili yale yatakayokuwa na tija kwa watumishi wote.”amesema Bi.Msemwa

Naye, Mwenyekiti wa kikao hicho Bw. Fraksed Mushi ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu THBUB, amesema kuwa kila mjumbe aliyechaguliwa  anawajibu wa kutumia nafasi hiyo kushauri na kutoa maoni yatakayo saidia kujenga Mazingira bora kwa wafanyakazi katika  utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

“Tumieni Baraza hili katika kujadili mambo muhimu na kutoa mapendekezo sahihi juu ya kuboresha mazingira ya kazi, Idara na Vitengo ili kuongeza tija na ufanisi katika kutekeleza majukumu ya kuendeleza taasisi” amesema Bw. Mushi.

Jumla ya wajumbe tisa (9) walichaguliwa katika kikao hicho ambapo watatumikia nafasi hizo kwa muda wa miaka mitatu.




Share:

WANAHABARI KAGERA WANOLEWA DHIDI YA UGONJWA WA MURBURG




Na Mbuke Shilagi Kagera.

Waandishi wa habari wa mkoa wa kagera wamehudhuria semina ya siku moja waliopewa juu ya ugonjwa hatari wa Murburg iliyofanyika katika ukumbi wa ELCT Bukoba Manispaa.

Semina hiyo imeongozwa na mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa ambaye ameambatana na Katibu tawala wa Mkoa Bw. Steven Ndaki pamoja na viongozi na wataalamu kutoka wizara ya Afya pamoja na wadau wa Afya Unicef.

Akizungumza katika semina hiyo Mkurugenzi wa Kinga kutoka wizara ya Afya Dkt. Ntuli Kapolongwe amesema kuwa lengo ni kuhakikisha waandishi wa habari wanapata uelewa juu ya ugonjwa huo na kushirikiana kwa pamoja ambapo watasaidia kuondoa zana na imani potofu kwenye jamii kupitia vyombo vya habari.

‘’na tunaamini kama mwandishi atapata elimu na kufahamu wa kutosha juu ya ugonjwa wa Murburg basi kutakuwa hakuna taarifa maana watapata nafasi ya kuuliza na wapate elimu ili waweze kufahamu na vita hii tutaenda kuishinda kwa ufupi’’ Amesema Dkt. Ntuli.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amemtaka Mkurugenzi asisite kutoa matamko ambayo yatakuwa ya kutahadharisha watu.

Huku akiwataka watu kuachana na mazoea ya kuendele kushika marehemu au kuosha mwili wa marehemu bila kujua ugojwa ulio muua ni upi na kusema kuwa maswala yote yasiyo ya lazima na yaliyopitwa na wakati kutoyafanya.

‘’tuoshe mikutano kwa maji tiririka mara kwa mara, tutumie vitakasa mikono na tukikutana kwenye mikutano ya kukutanisha watu wengi tuvae barakoa kwasababu inaambukizwa kwa mate pia na tufate yote yanayoelekezwa na wataalamu wa afya’’

Aidha Mkuu wa Mkoa Fatma Mwassa amewataka waandishi wa habari kutumia elimu hiyo kwa weledi walioupata kuhakikisha inawafikia watu na wanaielewa.
Ikumbukwe kuwa ugonjwa wa Murburg umejirudia mara yaa pili katika Mkoa wa Kagera Nchini Tanzania ambapo mripuko wa kwanza ulitokea 2023 Machi katika Wilaya ya Bukoba Vijijini na mara ya pili mlipuko umetokea Januari 2025 katika Wilaya ya Biharamulo.

Ugonjwa wa Murburg ni homa ya virusi ambapo huambukizwa kwa kugusa majimaji ya mwili kutoka kwa mtu aliyeambukizwa au mizoga ya wanyama walioambukizwa.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, maumivu ya kichwa maumivu ya misuli, kutapika damu, kuhara damu au kutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili.
Share:

Tuesday, 28 January 2025

NI ZAMU YA TANDAHIMBA,WIZARA YA KATIBA NA SHERIA HAKUNA KULALA



Na Dotto Kwilasa, MTWARA

Leo tarehe 28 Januari 2025, timu ya utoaji Mafunzo ya Elimu ya Uraia na Utawala Bora kwa viongozi imeendesha mafunzo hayo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kwa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya.

Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi kubwa zinazofanywa na Wizara ya Katiba na Sheria katika kuboresha utawala bora na kuimarisha elimu ya uraia kwa viongozi wa ngazi mbalimbali.

Wizara ya Katiba na Sheria imeweka kambi katika Mkoa wa Mtwara ikiwa ni utaratibu wake wa kutoa mafunzo ya uraia na utawala bora kwa viongozi kuanzia ngazi ya mkoa, wilaya, kata, hadi vijiji.

Aidha, mafunzo haya yanatoa fursa kwa viongozi hao kuelewa vyema majukumu yao katika kuongoza jamii na kuhakikisha wanatekeleza haki na sheria kwa manufaa ya wananchi.
Pia, mafunzo haya yanahusiana na kampeni ya msaada wa kisheria inayoendeshwa kwa ushirikiano na kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia  kwa kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi katika halmashauri zote za Mkoa wa Mtwara, ikilenga kuondoa vikwazo vya kisheria na kuhakikisha haki za raia zinatambulika na kutekelezwa ipasavyo.

Kampeni hii ina manufaa makubwa kwa wananchi kwani inawawezesha kupata huduma za kisheria bure, hivyo kuimarisha ufahamu wa sheria na haki zao.

Faida za mafunzo haya ni nyingi, ikiwemo kuimarisha utawala bora, kuleta uwazi katika utendaji wa serikali, na kusaidia viongozi kutoa huduma bora kwa wananchi.
Kutokana na hayo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Tandahimba, Hamidu Shaban, ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kwa mafunzo hayo na kueleza kuwa kupitia elimu ya uraia, wananchi wanapata ufahamu wa haki na wajibu wao, jambo ambalo linasaidia katika kudumisha amani na usalama.

Shaban amesema mafunzo hayo ni muhimu hasa kwenye kamati ya ulinzi na usalama, ikiwa ni pamoja na kuendeleza demokrasia, kwani yanaimarisha ushiriki wa wananchi katika utawala, na kuwapa uwezo wa kushiriki katika michakato ya kisheria na ya utawala katika maeneo yao.

"Kwa ujumla, mafunzo haya yana umuhimu mkubwa katika kuendeleza utawala bora, kuboresha usalama, na kutoa fursa kwa wananchi kupata haki zao kwa njia ya kisheria, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila kiongozi anatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na haki za raia," ameeleza.

Licha ya hayo, amesisitiza kuwa mafunzo haya ni muhimu kwa kuboresha ushirikiano kati ya viongozi na wananchi, na kuimarisha usalama na utulivu katika maeneo yao.

Share:

MKUU WA MKOA WA RUVUMA ATAKA MRADI WA MAJI WA MIJI 28 KUKAMILIKA OKTOBA 2025

Mkuu wa Mkoa Kanali Ahmed Abbas akikagua mradi wa maji katika eneo la Chandamali Manispaa ya Songea wenye gharama ya Sh.bilioni 145.
Msimamizi wa mradi wa maji katika eneo la Chandamali Manispaa ya Songea Mhandisi Vicent Bahemana akitoa taarifa ya ujenzi kwa Mkuu wa Mkoa Kanali Ahmed Abbas kushoto, katikati mkurugenz Mtendaji wa maji na usafi wa mazingira Manispaa ya Songea Mhandisi Patrick Kibasa
Msimamizi wa mradi Mhandisi Vincent Bahemana akimuonyesha mchoro wa mradi huo wa maji unaotekelezwa katika eneo la Chandamali Manispaa ya Songea kwa gharama ya Sh.bilioni 145.

Na Regina Ndumbaro Ruvuma. 


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas, ameagiza Mkandarasi Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) kuhakikisha ujenzi wa Mradi wa Maji wa Miji 28 unakamilika kabla ya Oktoba 2025. 

Mradi huo unaotekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Maji, unalenga kuboresha huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Manispaa ya Songea na maeneo jirani.


Kanali Abbas ametoa agizo hilo wakati akikagua mradi huo unaogharimu Shilingi bilioni 145 katika eneo la Chandamali, Manispaa ya Songea. 

Amesisitiza kuwa Serikali inalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na si kugeuza miradi kuwa mapambo. 

Amewataka wakandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha wananchi wanapata maji kwa wakati.


Akizungumza kwa njia ya simu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, ameeleza kuwa ucheleweshaji wa mradi huo umetokana na madai ya malipo ya Mkandarasi. 

Hata hivyo, amesema Serikali imeshaanza kulipa madeni ya wakandarasi na ndani ya wiki mbili fedha za mradi huo zitapatikana.


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Songea (SOUWASA), Mhandisi Patrick Kibasa, amesema mradi huo ulianza kutekelezwa Januari 2024 na unatarajiwa kukamilika Septemba 2026. 

Amesema tayari Serikali imemlipa mkandarasi Shilingi bilioni 21.87 kama malipo ya awali kati ya Shilingi bilioni 145.77 zinazotarajiwa kutumika kutekeleza mradi huo.


Mhandisi Kibasa ameeleza kuwa kazi zitakazofanyika katika mradi huo ni pamoja na kujenga chanzo cha maji katika Mto Njuga chenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 17 kwa siku, kujenga mtambo wa kutibu maji wenye uwezo wa kuchuja lita milioni 16 kwa siku, na kujenga matenki matatu yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 9.

Hadi sasa, matenki mawili kati ya matatu yamekamilika, likiwemo tanki la Chandamali na tanki la Milaya, kila moja likiwa na uwezo wa kuhifadhi lita milioni 2. Tanki la Mahilo, lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 5, lipo katika hatua za uchimbaji wa msingi. 

Mradi pia unahusisha ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji urefu wa kilomita 30.2 na upanuzi wa mtandao wa mabomba kwa kilomita 34.7.


Hadi tarehe 30 Novemba 2024, utekelezaji wa mradi huo ulikuwa umefikia asilimia 5.

 Mradi huo unatarajiwa kuboresha huduma za maji safi na usafi wa mazingira kwa wakazi wa Manispaa ya Songea mara utakapokamilika.
Share:

TANESCO YAJITOKEZA KUTOA ELIMU KUHUSU MATUMIZI BORA YA NISHATI YA UMEME KATIKA MKUTANO WA NISHATI AFRIKA


Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO, linashiriki katika Maonesho kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi wa Afrika (African Energy Summit) unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).

Mkutano huo umeanza leo Januari 27, 2025 unawakutanisha Wakuu wa Nchi Barani Afrika kujadili mikakati ya upatikanaji wa nishati ambapo lengo kuu ni kuwafikishia nishati ya umeme Waafrika milioni 300 ifikapo mwaka 2030.

TANESCO kama mdau muhimu wa nishati ya umeme hapa nchini imeendelea kutumia maonesho hayo kutoa elimu kwa wadau juu ya matumizi ya nishati ya umeme ikiwa ni pamoja na maendeleo ya miradi ya umeme na matumizi ya nishati safi ya umeme kupikia.

Mkutano huo utamalizika kesho Januari 28, 2025 ambapo unatarajiwa kuonyesha mwelekeo wa mpya nishati katika bara la Afrika.
Share:

ORYX GAS YAWAKUTANA NA MAWAKALA MIKOA YOTE KUWEKA MIKAKATI YA 2025


Na Mwandishi Wetu,Arusha

KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imewakutanisha mawakala wake kutoka mikoa yote nchini katika mkutano mkuu wa mwaka 2025 kwa ajili ya kuweka dira ya kutekeleza majukumu yao ya kuendelea kutoa huduma bora kwa Watanzania sambamba na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Kikao kazi hicho cha mawakala wa Oryx kimefanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa pia na viongozi mbambali wa kampuni hiyo akiwemo Mkurugenzi Mkuu Araman Benoit.

Akizungumza kuhusu kikao hicho Shaban Fundi ambaye ni Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania amesema mkutano unajumuisha Mawakala wote wa nchi nzima.

“Oryx Oryx tunamawakala mikoani na wilayani pamoja na maeneo mengine ya vijijini na Mawakala hawa ndio wanatuwezesha kufika maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kuwahudumia wananchi kupata nishati safi ya kupikia.

“Na tunajivunia kuwa na Mawakala kila Mkoa ambao wanauwezo na ndio maana tunajidhatiti na kujipambanua tunauwezo wa kufikisha nishati safi katika maeneo yote nchi Tanzania ikiwemo Zanzibar.

“Kwahiyo mkutano huu ni mkubwa kwetu sisi kwani unatoa dira ya mwaka 2025 lakini tunatumiq mkutano huu wa mawakala wetu kutoa mwito kwa wananchi waendelee kupokea matumizi ya nishati safi ya kupikia na sisi Oryx Gas tumejipanga kisawasawa kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa kila Mtanzania.”

Aidha amesema katika kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia wamefika katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuzungumzia umuhimu wa kutumia nishati safi ambayo ni salama kiafya na inasaidia kutunza mazingira.

Kwa upande wake Meneja wa Oryx Gas Zanzibar Shuea Omar Khamisi ameongeza kwa kawaida mkutano huo unafanyika kila mwaka kwa ajili ya kukutana kuzungumza wapi wamefika kwa mwaka uliopita na nini wamefanya pamoja na kupanga safari ya mwaka 2025 jinsi gani watafikia malengo yao.

“Mawakala wakubwa waliopo katika mikoa ndio wawakilishi wetu katika soko na ndio wanaotuwakilisha kwa wateja sokoni,”amesema huku akitumia nafasi hiyo kuelezea matumizi ya nishati safi Zanzibar ambapo yameongezeka ndani ya miaka mitano.

“Mwaka 2020 matumizi ya nishati safi Zanzibar yalikuwa asilimia 7.7 ya usambazaji wa nishati safi na mwaka 2024 imeongezeka na kufikia asilimia 26.5.Hii inamaanisha tokea mwaka 2020 matumizi yetu Zanzibar ilikuwa tani 3600 lakini mwaka 2024 matumizi yameongezeka mpaka tani 12400,”amesema.

Ameongeza kuwa hiyo imeonesha Wakazi wa Zanzibar wamebadilika,wameamka kutoka katika nishati chafu na kuingia katika nishati safi na kwamba Oryx Gas wamefanya jitihada kubwa katika kuwabadilisha wananchi wa Zanzibar kutoka katika nishati chafu kwenda kwenye nishati safi.

“Nawaomba sana wananchi wa Zanzibar waondokane na matumizi ya kuni na mkaa ambayo sio salama kwa afya yetu na mazingira.Wengi wetu tunapata madhara yanayotokana na matumizi ya kuni na mkaa na tunatumia gharama kubwa kujitibu,”amesema Shuea Omar Khamisi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger