Thursday 19 September 2024

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA 11 WA TAASISI YA MERCK FOUNDATION AFRIKA ASIA LUMINARY

...

Dar es Salaam, 18 Septemba 2024

TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 11 wa Taasisi ya Merck Foundation utakaofanyika Oktoba 29 na 30, 2024 Jijini Dar es Salaam ambapo mkutano huo utafunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salam Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum amesema Mkutano huo utahudhuriwa na wenza wa Marais kutoka nchi 15 za Botswana; Burundi; Cape Verde; Jamhuri ya Afrika ya Kati; Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC); Gambia; Ghana, Liberia; Malawi; São Tomé; Zambia, Zimbabwe

Amesema kwa mwenyeji Tanzania itawakilishwa pia na mwenza wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Mama Mariam Mwinyi.

Aidha amesema nchi nyingine ambazo zitashiriki mkutano huo ni Angola; Kenya; Mauritania. Nyingine ni Msumbiji; Nigeria; Rwanda; Afrika Kusini; Comoros; Eswatini; na Sierra Leone.

Amesema washiriki wengine ni Mawaziri wa Afya, Jinsia, Mawasiliano, Elimu, Ustawi wa Jamii kutoka nchihizo, Wajumbe 45 wataalam watakaoambatana na wenza wa Marais kutoka nchi hizo, Wataalamu wa huduma za afya 500, wasomi, watunga sera na waandishi wa habari, Mabalozi wanaowakilisha nchi ambazo wenza wa Marais wamealikwa, Mabalozi wa Tanzania kutoka nchi hizo; na Wajumbe wengine wapatao 500 kutoka sehemu mbalimbali duniani watashiriki kwenye Mkutano huo kwa njia ya mtandao.

Pamoja na hayo amesema washiriki wa mikutano hiyo hunufaika na mijadala kutoka kwa Wataalam wa Kimataifa katika masuala ya maendeleo ya jamii, huduma za afya na udhibiti wa magonjwa mbalimbali yakiwemo Kisukari, Uzazi, Embriolojia, Afya ya Uzazi, Dharura za Watoto, Saratani, Afya ya Wanawake, Huduma za kuzuia Magonjwa ya Moyo, Endokrinolojia, Huduma za wagonjwa mahututi na wenye changamoto za Upumuaji, Afya ya Akili na Tiba ya Ndani. Mijadala hii inalenga kuchangia jitihada za bara la Afrika kwenye kuboresha usimamizi, uzuiaji na ugunduzi wa mapema wa magonjwa sugu, kujenga uwezo na upatikanaji wa huduma bora za afya za usawa.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger