Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh.Hassan Bomboko ameelekeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kumaliza changamoto ya upotevu wa maji katika kata ya Makuburi, Wilaya ya Ubungo ila wananchi waweze kupata huduma ya maji kwa uhakika.
Mheshimiwa Bomboko ameeleza hayo katika siku ya pili ya ziara ya Mtaa kwa mtaa aliyoifanya katika Kata ya Makuburi kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.
"Maji ni huduma muhimu, tumepata changamoto kuwa maji yanapotea na muda mwingine kupelekea barabara kuharibika na kujaa maji, DAWASA mtatue changamoto hii na nitafatilia kuona imekwisha ili wananchi waendelee kupata huduma ya uhakika" ameeleza Mh.Bomboko
Bomboko ameongeza kuwa maeneo yote yanayopata huduma ya maji kwa mgao, yasimamiwe vyema na wananchi waweze kupata maji kupitia mgao husika na zaidi maji yatoke muda wa mchana ambapo kila mwananchi atakua na uwezo wa kutumia huduma hiyo.
Kwa upande wake Mhandisi wa DAWASA Mkoa wa kihuduma Tabata, Daniel Sabuni ameeleza kuwa wameyapokea maelekezo ya Mkuu wa Wilaya na kazi inaanza mara moja kutatua changamoto hiyo, lakini zaidi kutoa wito kwa Wananchi kutoa taarifa pindi wanapopata changamoto yeyote ya huduma ya maji katika Ofisi za Kihuduma DAWASA
0 comments:
Post a Comment