Wednesday 4 September 2024

WAZEE NCHINI WALAANI VITENDO VYA UKATILI VINAVYOENDELEA

...

CHAMA Cha Wazee Wanaume Nchini kinasikitishwa na kulaani vitendo vya ukatili vinayoendelea kufanywa na baadhi ya watu wasio na hofu ya Mungu, katika maeneo mbalimbali.

Kiongozi mkuu wa chama hicho Tadei Mchena amesema vitendo vinayoendelea havipaswi kabisa kufanywa na binadamu wenye akili timamu na wengine wakiwa ni watu wa makamo na wazee.

Mchena ametoa kauli hiyo kufuatia tukio la Septemba 2 mwaka huu katika Kijiji cha Kifuni, kata ya Kibosho, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo, Wenseslaus Olomi, miaka (50) alikuwa akimbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka 6.

"Kama chama cha wazee tunaendelea kulaani sana na kunakemea vikali kwa matukio haya yanayoendelea nchini, ukatili huu haukubaliki, tunaiomba serikali kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuangalia na kupitia upya Sheria hii ya ubakaji na ulawiti kwa watoto,

"Ikiwezekana Sheria itamke bayana ikibainika mtu anyongwe kabisa ili iwe fundisho la Wazee na watu wote wenye tabia hii mbaya ambayo inakithiri kila kukicha, watu hawa wasioogopa hata hofu ya Mungu", amesema Mchena.

Imeelezwa kwamba Olomi baada ya kukutwa akifanya kitendo cha ubakaji, alichukua hatua ya kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia shuka.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger