Wednesday 15 November 2023

VIJANA 224 WAHITIMU MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KISHAPU

...
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoania Shinyanga Bw. Joseph Mkude  akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya jeshi la akiba (Mgambo) Novemba 14,2023, katika viwanja vya shule ya Msingi Idukilo, kata ya Idukilo  mafunzo yaliyojumisha wahitimu  224 wanawake 17   na wanaume  207
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Bw.Emmanuel Johnson akizungumza kwenye sherehe za kufunga mafunzo ya jeshi la akiba (Mgambo) love Novemba 14,2023  katika viwanja vya shule ya Msingi Idukilo, kata ya Idukilo.

***************

Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Bw. Joseph Mkude  amefunga mafunzo ya jeshi la akiba (Mgambo) tarehe 14/11/2023, katika viwanja vya shule ya Msingi Idukilo, kata ya Idukilo  mafunzo yaliyojumisha wahitimu  224 wanawake 17   na wanaume  207

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo  Mkuu huyo ametoa pongezi na shukrani kwa viongozi wa kata ya Idukilo kwa kuhakikisha mafunzo ya  jeshi la akiba "Mgambo" yameanza na kumalizika salama, huku akiwashukuru Wakufunzi waliohusika kutoa mafunzo na kuwafanya wanafunzi kuhitimu mafunzo hayo kwa viwango vinavyohitajika.

" Ninawapongeza na kuwashukuru  sana wakufunzi wote mliotoa mafunzo haya ya viwango vinavyohitajika, wahitimu wote mkawe mstari wa mbele katika kuilinda, nchi yenu na kuwa mstari wa mbele  kujitolea kazi mbalimbali za ujenzi wa Taifa, 
Vilevile mafunzo mliyoyapata yakawe ni sehemu ya kupeleka elimu kwa jamii juu ya maadili mema, ikiwa ni pamoja na kushirikiana  na vyombo vya Ulinzi na usalama katika kutoa taarifa za uhalifu popote pale unapotokea." Alisema Mkude

Aidha  Mkude  ametoa wito kwa makampuni yote ya ulinzi wilayani kuajiri vijana waliopitia katika mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo) na kuwapa kipaumbele katika nafasi za Jeshinla Kujenga Taifa ( JKT ).

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kishapu Ndugu. Emmanuel Johnson  amewapogeza sana wahitimu pamoja na wakufunzi kwa kumaliza salama mafunzo pamoja na kuahidi kutenga bajeti kupitia Mapato ya ndani kwaajili ya sare za Jeshi la akiba 

Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Wilaya ya  Kishapu  Ocd .Esther Gesogwe Amewataka wahitimu wote kuhakikisha usalama maeneo yote amabayo watakuwepo na kushirikiana kwa ukaribu na Jeshi la Polisi  pamoja na kuimarisha Amani.

Aidha mafunzo hayo yaliyoanza tangia julai 10, 2023 na kumalizika November 15 ,2023 yenye lengo la  kuwajengea uwezo vijana hao ili kuimarisha ulinzi na usalama ndani na nje ya Wilaya hiyo.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger