Chuo cha Uhasibu Arusha [IAA] Kimeanza kutoa Masomo ya Ujasiriamali Kwa Vijana wanaojiunga na chuo hicho kwa lengo la kuwajengea uwezo ili kuweza kujiajiri pindi wanapo hitimu masomo katika chuo hicho.
Akizungumza katika Wiki ya vijana inayoadhimishwa kitaifa mkoani Manyara Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha [INSTITUTE OF ACCOUNCY ARUSHA -IAA] Prof.Eliamani Sedoyeka amesema kwasasa chuo hicho kimeweka nguvu katika kuwawezesha vijana kwa kuwaelimisha hususani katika maswala ya ujasiriamali ili kuongeza wigo mpana kwa vijana hao kujiajiri na kuacha dhana ya kuajiriwa.
Aidha Prof.Sedoyekaa ameongeza Kuwa pamoja na kuwepo kwa wingo mpana wa kuajiriwa hasa kwa wanafunzi wanaohitimu katika chuo cha uhasibu Arusha [IAA] lakini masomo ya ujasiriamali yameongeza fursa zaidi kwa vijana hao katika kujiongezea kipato katika kujiajiri ili kuongeza uchumi wao na kujikwamua na wimbi la umaskini.
Baadhi ya Wanafunzi wa chuo cha Uhasibu Arusha [IAA] Bwa.Ruben Abeli na Bi Spensiaodha Mongo Wamepongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuweka msisitizo katika maswala ya Ujasiriamali kwani mpaka sasa wamefanikiwa kuzalisha bidhaa mbalimbali na kushiriki na vijana wengine katika Wiki ya vijana ambayo imefanyika kitaifa katika mkoa wa Manyara ambayo imehudhuriwa na vijana kutoka Mikoa mbalimbali hapa nchni.
Hata hivyo Masomo ya ujasiriamali yanayotolewa na chuo cha Uhasibu Arusha -IAA yameonekana Kuwa na toka kwa vijana wanaojiunga na chuo hicho kwani yamekuwa yakiwaandaa katika kujiajiri wenyewe pindi wanapo hitimu Masomo yao.
0 comments:
Post a Comment