Friday, 6 October 2023

DK.MPANGO AYAONYA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

...


Na Dotto Kwilasa, Dodoma

MAKAMU wa Rais Dk Philip Mpango amezindua ramani ya kidigitali ya utambuzi wa mashirika yasiyo ya kiserikali huku akiyataka mashirika hayo kulinda na kutunza  maadili ya kitanzania kwa kutokubali kutumiwa na baadhi ya watu wasioitakia mema nchi.

Katika hilo ametoa maelekezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Ustawi na Maendeleo ya Jamii kufanya uchambuzi wa mchango wa mashirika hayo na kuishauri serikali juu ya mwenendo na ufanisi wake.

Dokta Mpango ametoa msisitizo huo jana Jijini Dodoma wakati akifunga Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya kiserikali na kuyashauri mashirika hayo kupeleka changamoto zote za kikodi zilizopo wizara ya fedha nayeye apewe taarifa.

Aidha amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili NGOs ziendelee kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu.

"Serikali inaahidi kuendelea na jitihada za kuondoa baadhi ya  changamoto zinazoathiri ufanisi wa NGOs nchini lakini NGOs zinapaswa kuwa na uwazi  jinsi ya uendeshaji wa shughuli zake, " alisema na kuongeza, "amesema na kuongeza;

Nazipongeza NGOs zote kwa kazi zinazofanya kwani zinawagusa wananchi katika nyanja mbalimbali za maisha na kuiunga Serikali mkono katika kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla, " Amesema Dk. Mpango

Kuhusu mabadiliko ya tabia nchi,Dk.Mpango amesema Serikali inaendelea na kuhimiza kupanda miti na shughuli za maendeleo katika kukabiliana na athari hiyo na kuzipongeza NGOs ambazo zinapambana na suala hilo .

"Natoa wito kwa mashirika yote kuendelea kutoa elimu kwa wanachi kuhusu kutunza mazingira,nimeridhia pia ombi la Mwenyekiti wa Bodi ya NaCoNGO kwa kuelekeza mamlaka za mikoa na wilaya kufanya kazi kwa karibu na NGOs kwa kufuatilia kazi zao na kuziwekea mazingira mazuri ili ziendelee kufanya kazi vema, "alisema

Pamoja na hayo Makamu huyo wa Rais ametaka NGOs zote  kuimarisha ushirikiano na NGOs za nchi zingine ili kuweza kujenga ufanisi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali na kuwasisitiza wendaji wa Serikali kujibu haraka wanapoandikiwa barua na NGOs,  ili wapate majibu kwa lengo husika.

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dokta Dorothy Gwajima amesema wizara yake kupitia ofisi ya msajili wa NGOs ina jukumu la kuratibu shughuli za mashirika hayo kwa upande wa Tanznaia Bara ili kuhakikisha yanaleta tija kwa jamii.

Awali,Mwenyekiti wa Uratibu wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Mwantumu Mahiza ameziomba mamlaka za mikoa na wilaya kufanya kazi kwa karibu na mashirika yasiyo ya kiserikali huku Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO),Lilian ametaja changamoto zilizopo ikiwemo mfumo wa mamlaka ya kodi kutokuwa rafiki.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO), Dkt. Lilian Badi amesema sekta ya mashirika yasiyo ya Kiserikali inaendelea kukua mwaka hadi mwaka siyo tu kwa idadi inavyoongezeka bali utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ameitaja baadhi ya miradi inayotekelezwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo afya, mazingira, ulinzi wa jamii, uwezeshaji wa wananchi, elimu, kilimo, jinsia, maji, utawala bora na haki za binadamu.

"Tunaahidi kuendelea kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya mashirika yasiyo ya Kiserikali ili kutekeleza majukumu yetu kwa ajili ya maslahi ya Watanzania na Taifa kwa ujumla, " Amesema


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger