Mapema leo Oktoba 11 2023 viongozi wa kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi kata ya kilimani pamoja na wajumbe wa secretariat ya kata ya kilimani Wamefanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa shule ya msingi unatekelezwa katika mtaa wa Chinyoyo kata ya Kilimani
Pamoja na kuona kasi ya ujenzi huo unavyokwenda viongozi hao wamesisitiza ujenzi huo uongeze kasi kulingana na mkataba unavyoelekeza licha ya kuwa na changamoto ndogo ndogo ambazo hazizuii mradi huo kusimama.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Kilimani Nathani Chibeye amesema ujenzi huo wa shule ya msingi hiyo utakuwa mkombozi kwa kata ya Kilimani kwa kuwa kata hiyo tangu ipate Uhuru haijawahi kuwa na shule ya msingi jambo ambalo hupelekea watoto wa mitaa minne ya Kilimani kusoma katika shule za kata nyingine na kusababisha kutembea umbali mrefu kuitafuta elimu.
"Hata hivi Sasa sisi kama viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Kilimani tunaishukuru SERIKALI YA AWAMU YA SITA INAYOONGOZWA NA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuweza kutupatia fedha za ujenzi wa shule hii ambayo itakuwa mkombozi kwa wananchi wa kata ya kilimani"amesema Chibeye.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kilimani Rotta Ndimbo ameitaka kamati ya ujenzi na mkandarasi kuhakikisha wanatanguliza uzalendo katika ujenzi wa shule hiyo ili thamani ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi huo zinatumika kama zilivyo kusudiwa.
Ziara hiyo ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Kilimani ni mwendelezo wa kugagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika kata ya Kilimani ili kuhakikisha utekelezaji wa ilani ya chama unafanikiwa.
0 comments:
Post a Comment