Saturday, 7 October 2023

DKT. RWEZIMULA ATOA MAELEKEZO KWA MENEJIMENTI YA DIT- MWANZA KATIKA USIMAMIZI WA MRADI WA EASTRIP

...

Na Mwandishi wetu - Mwanza

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayehusika na Elimu, Dkt. Franklin Jasson Rwezimula Leo tarehe 7/10/2023 ametembelea Taasisi ya Dar es Salaam (DIT) Kampasi ya Mwanza kuona Maendeleo ya Shughuli za ujenzi wa kituo Cha Umahiri wa Teknolojia ya Ngozi (Center of Excellence).


Ujenzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa ujuzi kwa maendeleo na uingiliano wa kikanda katika ukanda wa Afrika Mashariki(EASTRIP),unaotekelezwa na serikali kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia.


Dkt. Franklin amesema kituo hiki Cha Umahiri wa Teknolojia ya Ngozi kitakapokamilika kitakuwa msaada mkubwa ndani na nje yaTanzania kwa kuwa kitaongeza wataalam wa masuala ya Ngozi, kufundisha wakulima na wafugaji pamoja na kuchakata mazao ya ngozi (Leather Product Processing).

Kwa upande wake, Mhandisi Mshauri na msimamizi wa mradi upande wa serikali 
Silvester Francis  amesema hadi sasa mradi huu umekamilika kwa asilimia 60% na amebainisha maeneo hayo ambayo ni jengo la taaluma, utawala, mabweni ya kiume na kike, jengo la ngozi ( Leather Building) na uzio.


Aidha, Kaimu Mkurugenzi wa DIT-Mwanza ambaye pia ni Kaimu Mratibu wa mradi wa EASTRIP Mhandisi Issa Mwangosi amefurahia ujio huu.

"Tumepokea maelekezo na ushauri wa Naibu Katibu Mkuu (Elimu) na tupo tayari kutekeleza ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita katika kuleta mapinduzi ya Elimu ya Teknolojia kwa maslahi mapana ya nchi",amesema Mhandisi Mwangosi.

Mradi Huu ulianza kutekelezwa Mwaka 2019 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2024 ambapo utagharimu kiasi cha shillingi za kitanzania Billioni 37.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger