Tuesday, 31 May 2022

VIJANA 200 WAPATIWA MAFUNZO YA KILIMO KIDIJITALI


Wadau mbalimbali wa Westerwelle Startup Haus Arusha wakijadili jambo wiki iliyopita kwenye uzinduzi wa kituo hicho Jijini Arusha, (picha na Queen Lema).

Na Queen Lema, Arusha.

Westerwelle Foundation kutoka Ujerumani imeungana na Obuntu Hub kutoka Tanzania kufungua kituo kipya kwa ajili ya kuwainua vijana wajasiriamali (Innovation Hub).


Mbali na kufungua kituo hicho Jijini Arusha, pia mpaka sasa vijana zaidi ya 200 wameshanufaika na mafunzo kwenye kituo hicho.


Akiongea mwishoni mwa wiki na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kituo hicho, Meneja mkuu wa Westerwelle Startup Haus Arusha Bw. Collins Kimaro amesema kuwa uwepo wa kituo hicho ni msaada mkubwa sana kwa vijana


Kimaro amesema kuwa vijana hao 200 walipatiwa ujuzi wa kidigitali kutoka katika sekta ya kilimo.


Kimaro amesema kuwa vijana hao kutoka Arusha na Iringa walipewa ujuzi wa kidigitali.


"Ni fursa kubwa sasa kwa vijana kunufaika na kituo hiki maana hata hao vijana 200 ambao tumewafikia toka mwezi Juni tayari matokeo yameshaonekana kwaiyo tuseme kuwa kila kijana mjasiriamali sasa atumie kituo hiki" ameongeza


Akiongea kituo hicho amesema kuwa ni muungano wa Obuntu Hub na Westerwelle Foundation,ambapo sasa kwa umoja huo wamefungua Westerwelle Startup Haus Arusha(WSHA) ambapo kituo hicho kitatoa nafasi za kisasa za kufanyia kazi yaani co working space,


Ameongeza kuwa programu ya mafunzo mbalimbali na kuwakutanisha wajasiriamali wa kitanzania na mtandao kimataifa.


Kimaro amebainisha kuwa anawashukuru wafadhili mbalimbali ambao wamejitolea kuwasaidia vijana ambapo mpaka sasa matunda yameshaonekana


Akahitimisha kwa kusema kuwa kwa sasa vijana wanakabiliwa na changamoto Kama vile ukosefu wa mitaji,na masoko lakini sasa wanatakiwa kujiunga na kituo hicho,lakini pia wanatakiwa kuchangamkia fursa pamoja na mashindano ya kimataifa ambayo yanatangazwa.


Naye mkurugenzi wa Westerwelle foundation Bw Oliver Reisner amesema kuwa wamefurahi sana kufika Tanzania na wameona muamko wa vijana na wataungana na jitiada za Serikali ya Tanzania kuchochea maendeleo kupitia ubunifu na ujasiriamali.


George Akilimali ni mmoja wa wanufaika, amesema kuwa umoja huo umekuwa msaada kwa vijana wengi sana hapa nchini ambapo kwa yeye aliweza kupata msaada mbalimbali ikiwemo elimu,na mtaji


Amedai kuwa hapo awali hakuwa na uwezo wa kupata masoko ya kimataifa ila kwa sasa amekutanishwa na wadau wa kimataifa hivyo vijana wanatakiwa kutumia kituo hicho.

Share:

KIUWASA MSHINDI WA KANDA MAJI CUP

Afisa elimu taaluma mkoa Kigoma, David Mwamalasi (katikati mwenye suti) ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye akikagua na kusalimiana na wachezaji wa timu ya KIUAWASA ambao waliibuka mabingwa wa kanda wa maji Cup.
Afisa elimu taaluma mkoa Kigoma, David Mwamalasi (katikati mwenye suti) ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye akikagua na kusalimiana na wachezaji wa timu ya KIUAWASA ambao waliibuka mabingwa wa kanda wa maji Cup.
Afisa elimu taaluma mkoa Kigoma, David Mwamalasi (katikakati) ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye kwenye fainali za maji Cup zilizofanyika uwanja wa lake Tanganyika Mjini Kigoma akisalimiana na kukagua timu ya Kigoma Veteran.
Mkuu wa wilaya Kigoma Ester Mahawe (Mwenye kofia) akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kigoma Veteran wakati wa fainali ya maji Cup kwenye uwanja wa lake Tanganyika Mjini Kigoma.
Afisa elimu taaluma mkoa Kigoma, David Mwamalasi (wa pili kushoto) ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye kwenye fainali za Maji Cup zilizofanyika uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma akizungumza na wachezaji wa timu zilizoingia fainali muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo huo. (Picha zote na Fadhili Abdallah)

Na Fadhili Abdallah,Kigoma
TIMU ya soka ya Mamlaka ya maji safi na maji taka Kigoma imeibuka mabingwa wa wa kanda ya magharibi wa mashindano ya kombe la maji baada ya kuifunga timu ya Kigoma Veteren kwa jumla ya magoli 6 – 1.

Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma washindi walijihakikishia nafasi yao tangu kipindi cha kwanza ambapo walitoka mapumziko wakiwa wanaongoza kwa magoli 3-0.

Mashindano hayo yanaandaliwa na Wizara ya maji kwa kushirikiana na Taasisi inayojishughulisha na usimamizi wa usambazaji maji nchini (ATAWAS) kwa kushirikiana na mamlaka za maji za majiji na halmashauri.

Timu ya Maveteran watabidi wajilaumu kwa wachezaji wake kushindwa kufunga licha ya kupata nafasi nzuri ya kupata magoli na hivyo kuambulia goli moja la kufuta machozi huku timu ya Mamlaka ya maji ikizidi kuongeza magoli ambapo hadi mpira unamaliza Mamlaka ya maji Kigoma Ujiji ilikuwa mbele kwa magoli 6-1.

Ushindi huo unaifanya timu hiyo ya mamlaka ya Maji Kigoma Ujiji kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya Taifa ya kombe la maji linalohusisha mamlaka za maji za mikoa nchi njema na Mamlaka hiyo ilikuwa icheze mchezo huo na timu ya mamlaka ya maji Rukwa ambayo haikutokea uwanjani.

Akizungumzia mashindano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na maji taka Kigoma Ujiji, Jones Mbike alisema kuwa yanalenga kuhamasisha jamii kushiriki kutoa taarifa ya mivujo ya maji ili kuzuia kupotewa kwa maji ambayo yamesafisha.

Mbike alisema kuwa ujumbe wa mashindao hayo pamoja na kuwa ni burudani lakini yanatumika kuimarisha afya za watumishi wa mamlaka hiyo sambamba na kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na masuala ya maji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi inayosimamia usambazaji maji (ATAWAS) Constantine Chiwalo alisema kuwa kufanyika mashindani hayo kunalenga kuwakuwasanya wananchi na kupeleka ujumbe kushiriki kwenye mipango na utekelezaji wa miradi ya maji.

Chiwalo alisema kuwa mashindano hayo yanalenga pia kutoa ujumbe kwa jamii kuwa walinzi wa miundi mbinu ya maji dhidi ya wahujumu wa miundo mbinu hiyo sambamba na kusaidia kutoa taarifa kuhusu upotevu wa maji (mivujo) kwenye maeneo yao.

Afisa elimu taaluma mkoa Kigoma, David Mwamalasi akimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amezitaka mamlaka za mkoa huo kutumia michezo na burudani kufikisha ujumbe kwa wananchi kuhusu taarifa za utekelezaji wa miradi ya maji lakini pia kuhimiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji miradi, kulinda miundo mbinu na kutoa taarifa za mivujo ya maji.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 31,2022

Magazetini leo Jumanne May 31 2022
3931269_6294fd050594d

53919140_6294cda4f0bce

53927835_6294ef9b2d4f1

53943910_62952e66919b5

653923649_6294df41bec01

653931794_6294ff1213b23
653935824_62950ed0b7874

653936977_6295135127582

3939770_62951e3a052cd

653927780_6294ef644221e

53930192_6294f8d067bb6

53933015_629503d7a0670

653943126_62952b56e5c4c

Share:

MAMA MZAZI ASIMULIA MKASA MZIMA CHANZO BINTI YAKE KUUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MMEWE JIJINI MWANZA


Picha ya Marehemu Swalha akiwa na mume wake

Mama mzazi wa mwanamke aliyefahamika kwa jina la Swalha ambaye ameuawa kwa kupigwa risasi saba kichwani na mume wake kwa sababu ya wivu wa mapenzi amesimulia mkasa mzima kilichopelekea kifo cha mwanaye.


Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo huko Jijini Mwanza na ndoa yao ilidumu kwa muda wa miezi mitano.


Zaidi tazama hapa kwenye video Mama wa Swalha akizungumzia zaidi.


CHANZO: EATV
Share:

Monday, 30 May 2022

SHABIKI KINDAKINDAKI WA YANGA AFARIKI KWA FURAHA AKISHANGILIA USHINDI WALIVYOIBUTUA SIMBA SC


Feisal Salim ‘Fei Toto’ akishangilia bao alilofunga dhidi ya Simba SC
Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya Simba SC katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azama Sports
 ***

NI VILIO na Simanzi vikitawala nyumbani kwa James Mhamba mwenye umri wa miaka zaidi ya Sitini ambaye alikuwa shabiki wa timu ya Yanga na mkazi wa Rwamishenye iliyopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ambaye amepoteza maisha baada ya mechi ya simba na Yanga huku chanzo kikidaiwa kuwa ni furaha baada ya timu yake kuibuka na ushindi.


Mechi hiyo ilichezwa juzi Jumamosi, Mei 28, 2022 katika Dimba la CCM Kirumba Mwanza ambapo Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’ na kuipeleka Yanga Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.


Wakizungumza msibani hapo, majirani na marafiki wa mzee huyo wamesema;


“Mzee Mhamba alikuwa kiongozi kwenye umoja wetu wa Simba na Yanga (YASI), alikuwa shabiki mzuri wa Yanga, ni mtu aliyekuwa amehamasika na timu yake. Yanga ikishindwa alikuwa ananyong’onyea lakini ikishinda anachangamka sana.


Mimi nilionana naye jana kabla ya mechi alikuwa mzima tu, lakini leo nikapigiwa simu kuwa amekufa sikuamini kabisa, nimefika hapa nyumbani nikakuta kweli ameshafariki, basi tukafanya taratibu za kuupeleka mwili mochwari. Inasikitisha sana.

Alikuwa mcheshi sana na Sahabiki kindakindaki wa Yanga, ana rekodi za Yanga atakutajia wachezaji na rekodi za timu yake, sio shabiki lakini mpira alikuwa anaufahamu. Ilikuwa lazima avae jezi ya yanga, hivyo unaweza kuona alivyoipenda timu yake,” Hamidu Abdinul, mkazi wa eneo hilo.


Alikuwa na maradhi ya presha, baada ya mchezo wa jana (Simba vs Yanga), furaha ilizidi, huenda presha ilipanda ikasababisha kifo chake, amekuwa akinifundisha mengi ya kiuongozi katika chama chetu hiki, nilionana nae jana wakati wa mechi yeye akawa anaangalia kwake mimi nikaenda sehemu nyingine.


Wanasema baada ya mechi alitoka eneo alilokuwa akiangalia akaingia ndani, akavua shati lake akidai kuwa anahisi joto, akaenda kwenye bomba kujimwagia maji ya baridi, hapo hapo ndipo alianguka chini, wakaita majirani, lakini walipokuwa wakimuingiza ndani wakagundua tayari ameshakufa.
Share:

RAIS SAMIA ALIANDIKIA BARUA BUNGE LA TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) kutokana na mafanikio kwenye Ujenzi wa Barabara, mara baada ya kukabidhiwa Tuzo hiyo na Makamu wa Rais wa Sekta Binafsi, Miundombinu na Viwanda katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Solomon Quaynor tarehe 25 Mei 2022 Accra nchini Ghana.

**

Rais Samia Suluhu Hassan, ameliandikia Bunge barua ya salamu za shukrani kuwashukuru wabunge kwa kujadili na kutoa azimio la kumpongeza baada ya kupata tuzo ya Babacar Ndiaye nchini Ghana, ambayo hupatiwa Rais wa nchi za Afrika zinazofanya vizuri kwenye miundombinu ya barabara.

Barua hiyo imesomwa leo Mei 30, 2022, na Spika wa Bunge hilo Dkt. Tulia Ackson

"Kwa kipekee kabisa tuzo hiyo ni ya wabunge kwa kutambua mchango wenu katika kusimamia miradi, matumizi sahihi ya fedha za miradi na kupitisha na kusimamia bajeti ya serikali hivyo ninaomba Watanzania wote wafurahie tuzo huku tukiendelea kusimamia, kulinda na kuitunza miundombinu yetu," imeeleza sehemu ya barua ya Rais Samia kwa Bunge.
Share:

WAPENZI WALIOANZA UCHUMBA TANGU MWAKA 1956 WAFUNGA NDOA UZEENI 2022


Alex na Jane wakiwa na watoto wao watano
 **
Alex mwenye umri wa miaka 91 na Jane Hamilton mwenye miaka 89 kutokea nchini Uingereza wamefunga ndoa baada ya kudumu kwenye mahusiano kwa miaka 60 na kufanikiwa kupata watoto watano.


Alex na Jane walikutana mwaka 1956, ambapo kila mmoja alikuwa katika mahusiano na mtu mwingine. Baada ya miaka 6 walikutana na kuanza mahusiano yaliyodumu mpaka mwaka 2022, ndipo walipoamua kuwa mke na mume baada ya kudumu pamoja kwa miaka 60
Share:

BENKI YA EXIM YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 100 SHINYANGA



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Sophia Mjema (Kushoto), Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Bw Elias Ramadhani Masumbuko (Katikati) na Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Bi. Agnes Kaganda (Kulia) wakiwa wameketi kwenye moja ya madawati 100 yaliyotolewa na benki ya Exim Tanzania ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madawati mkoani humo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Afisa elimu wa Mkoa huo Bi Neema Mkanga (Kushoto) maofisa waandamizi mkoa pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Sophia Mjema (Kushoto) akipokea msaada wa madawati 100 kutoka kwa Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Bi. Agnes Kaganda (Kulia) ikiwa ni msaada kutoka benki ya Exim Tanzania katika kusaidia jitihada za mkoa huo kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madawati wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Meneja wa Benki ya Exim Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa Bw Amos Lyimo (Kulia) maofisa waandamizi mkoa pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Sophia Mjema (Kushoto) akikagua msaada wa madawati 100 yaliyotolewa na benki ya Exim Tanzania katika kusaidia jitihada za mkoa huo kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madawati wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa mwishoni mwa wiki.


Wakitoa shukrani zao kwa benki hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Bw Elias Ramadhani Masumbuko (Kulia) na Afisa elimu wa Mkoa huo Bi Neema Mkanga (Kushoto) walionyesha kuridhishwa na viwango vya ubora wa madawati hayo huku wakibainisha kuwa msaada huo utasaidia zaidi kuboresha mazingira ya kufundishia kwa shule zitakazonufaika na madawati hayo.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Sophia Mjema (wa pili kulia) akisalimiana na Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Bi. Agnes Kaganda (wa pili kushoto) wakati maofisa wa benki hiyo walipotembelea ofisi ya mkuu wa mkoa huyo ili kukabidhi msaada wa madawati 100 ikiwa ni msaada kutoka benki ya Exim Tanzania katika kusaidia jitihada za mkoa huo kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madawati mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Meneja wa Benki ya Exim Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa Bw Amos Lyimo (Kushoto) na Meneja wa Benki hiyo tawi la Shinyanga Bw Japhet Mazumira


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Sophia Mjema (katikati) Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Bw Elias Ramadhani Masumbuko (wa pili kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wa benki ya Exim walioongozwa na Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Bi. Agnes Kaganda (wa tatu kulia) wakati maofisa hao wa benki hiyo walipotembelea ofisi ya mkuu wa mkoa huyo ili kukabidhi msaada wa madawati 100 ikiwa ni msaada kutoka benki ya Exim Tanzania katika kusaidia jitihada za mkoa huo kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madawati mwishoni mwa wiki.

......................................

Na Mwandishi Wetu,Shinyanga

BENKI ya Exim Tanzania imekabidhi msaada wa madawati 100 yenye thamani ya Sh milioni 20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Sophia Mjema ili kuunga mkono jitihada za mkoa huo katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo kero ya uhaba wa madawati.


 Madawati hayo yatagawanywa miongoni mwa shule zinazokabiliwa zaidi na changamoto ya uhaba wa madawati mkoani humo.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi madawati hayo iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Bi. Agnes Kaganda alisema ni muendelezo wa mkakati wa benki hiyo unaofahamika kama Exim Cares unayolenga kugawa madawati zaidi ya 1000 katika mikoa mbalimbali hapa nchini na ni sehemu tu jitihada ambazo benki hiyo imekuwa ikifanya kusaidia jamii inayoizunguka.


Alisema kuwa benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na serikali katika kufanikisha mipango mbalimbali hususani katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini hatua aliyoilezea kuwa ndio chachu ya maendeleo kwa sekta zote ikiwemo ya benki pia.


“Msaada hu unatarajiwa kuwanufaisha wanafunzi zaidi ya 300 kwa mwaka katika kipindi cha makadilio ya miaka 10. Mkakati wetu huu wa kusaidia katika elimu unatokana na imani yetu kwamba bila kuwa na jamii iliyoelimika hata huduma za kibenki tunazozitoa lazima zitateteleka kutokana na ukweli kuwa biashara yetu hii inategemea sana mafanikio ya jamii inayotuzunguka…mafanikio ambayo tunaamini yataletwa na elimu,’’ alisema.


Alisema tangu kuanza kwa mkakati huo uliozinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mwishoni mwa mwaka jana, tayari jumla ya madawati 500 yameshakabidhiwa katika mikoa ya Lindi, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Shinyanga.


Akizungumza mara tu baada ya kupokea msaada huo, Mkuu Mkoa wa Shinyanga Bi Sophia Mjema pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa msaada huo alisema msaada huo umepatikana kwa wakati muafaka kwa kuwa mkoa huo unaendelea na mkakati wake wa kuboresha elimu kwa kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi.


“Katika kufanikisha hili Rais Samia Suluhu amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha sisi kama mkoa tunapata mahitaji yote muhimu katika elimu ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa na maslahi ya watumishi. Inapotokea wadau kama benki ya Exim wanatusaidia pia kwa msaada kama huu wa madawati wanakuwa wameunga mkono jitihada za serikali na hivyo kurahisisha ndoto za Mheshimiwa Rais ambazo ni kuboresha zaidi sekta ya elimu,’’ alisema.


Wakitoa shukrani zao kwa benki hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Bw Elias Ramadhani Masumbuko na Afisa elimu wa Mkoa huo Bi Neema Mkanga walionyesha kuridhishwa na viwango vya ubora wa madawati hayo huku wakibainisha kuwa msaada huo utasaidia zaidi kuboresha mazingira ya kufundishia kwa shule zitakazonufaika na madawati hayo.

“Tunawashukuru sana benki ya Exim kwa msaada huu na tunatarajia kwamba wadau wengine wataendelea kuiga mfano huu ili kwa pamoja tusaidiane kukabiliana na changamoto hii. 

Kwa sasa mkoa unakabiliwa na uhaba wa madawati 2500 huku jitihada za kutengeza madawati mengi zikiendelea kupitia VETA kupitia ofisi ya Mkurugenzi. 

Hivyo milango bado ipo wazi kwa wadau wengine kwa kuwa jitihada za pamoja ni muhimu zaidi,’’ alisema Bi Mkanga
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 30, 2022


Magazeti ya leo Jumatatu May 30 2022
















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger