Monday, 14 June 2021

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA SGR MWANZA-ISAKA KM 341

...



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitembea kwenye mfano wa Reli ya Kisasa itakayojengwa kutoka Mwanza hadi Isaka mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa kuhusu ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha kutoka Mwanza hadi Isaka km 341 mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho, Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa pamoja na viongozi wengine wa Chama, Serikali na Bunge, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha kutoka Mwanza hadi Isaka km 341
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa Jiwe la Msingi jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi mradi huo mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR ambao utagharimu kiasi cha Shilingi za Kitanzania Trilioni 3.1
Baadhi ya mawaziri na viongozi wengine wa taasisi
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi mradi huo mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR ambao utagharimu kiasi cha Shilingi za Kitanzania Trilioni 3.1. 
Msanii wa Singeli Barobaro akitumbuiza huku viongozi mbalimbali wakimtunza katika Sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi mradi huo mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR katika eneo la Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.

(PICHA NA IKULU).
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger